Riwaya:: NDOA NDOANO SEHEMU YA 17




Riwaya:: NDOA NDOANO
          SEHEMU YA 17

Endelea.......

Lile furushi lilobe lilitoka kwa Mwamvita ili liweze kumfikia Bwana Maposo, kweli kijana alifanya kama alivyoagizwa akaligikisha na yeye akarudi alikotokea. Maposo hakuwa na haraka sana ya kutaka kuufungua mzigo huo ambao hakutambua nini ambacho kililetwa pale. Aliamua kupanga jedhi lake vizuri kisha akaanza kulihutubia hata kabla hawajaingia katika mapambano.
'Haya nataka mutambue jambo moja tu, hawa vijana wamekimbia hapa na nadhani watakuwa wamekimbilia kijiji cha jirani pia tunafahamu kuwa hawa ndio kikwazo kikubwa sana kwetu ndio maana mzee Baba yetu kaenda kuongea na Mfalme wa kijiji hiko ili kama wapo watu wetu tukawakamate haraka inayotakiwa, kikubwa sisi kujiimarisha' hayo yalikuwa ni maneno ya bwana maposo akijiaminisha.
Aliyasema hayo bila kujua ni kitu gani ambacho kipo mbele yake. Siku ya kwanza, siku ya pili hadi ya tatu. Ndani kwa maposo kukaanza kutoa harufu mbaya. Palianza kutoa harufu kali ya uozo ambayo haikujulikana ni aina gani na inatokea wapi. Walinzi wliambiwa kuwa watafute mahali popote pale ambapo panahisiwa labda mzoga umewekwa. Maposo akiingia ndani ya chumba chake basi harufu inazifi kupita kiasi.
Hakuwa na hata kumbukumbu ya kuweza kukumbuka kufungua moja ya masanduku ambayo aliweka ile zawadi ambayo haikutambulika aina gani kwa kutokufunguliwa. Baada ya muda kidogo Mwanamke ambae alimuweka kwa lengo la kufanya usafi alivyoingia chumbani harufu hakuweza kuvumilia, wakati anajaribu kutoka anaona kwenye sanduku moja funza mkubwa akiwa anatoka. 'Haaaaa huyu mdudu anatokea humu aaah maposo atakuwa kamuua mtu kamuweka humu'
Akatoka haraka kwenda nje akaanza kuwauliza walinzi majina ya marafiki zake alihakikisha mpaka wote wametimia akajiuliza ni mtu gani ambae kapungua labda anaweza kuhisi kama kauliwa na Maposo. Akamtafuta mlinzi ambae huwa anaelewana nae akamuuliza kama wao wametimia jawabu ni kuwa wametimia wote.
Aliamua kwenda kulipeleka swala hilo kwa Maposo mwenyewe. Maposo alipopata taarifa hiyo akaamua kwenda kufungua lile sanduku haki ya nani alichokikuta alifurahi na roho yake. Aliona lile furushi likiwa limejaa funza alipochunguza ndani anakutana na kichwa cha baba yake ambacho kimeharibika sana. Makelele aliyoyapiga hapo hakuna ambae hakusikia ambae yuko karibu na hapo. Walisikia zile kelele ambazo zilipigwa ndipo watu wote wakawa karibu na hapo. Maposo hakuamini kabisa macho yake kama anayekiona mbele yake ni kichwa cha Baba yake Mzazi. Aliumiasana zaidi.
Zilipita siku kadhaa za majonzi, ambayo yaliombolezwa kwa muda mrefu kutokana na kuwa Mtu mkubwa wa kijiji. Maposo aliapa mbele ya umati wa watu kuwa atamkata shingo mtu huyo ambae kaua baba yake. Wanakijiji baadhi walifurahi sana kwani Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu, mateso ya kuuwa watu wa kijiji hiko hakukumbuka ila kilichomuuma sana cha kuchinjwa shingo baba yake. Walishuhudia majonzi ya Mtu mbaya na wakaamini kumbe hata yeye maumivu anayapata. Maposo aliamua jambo.
Alimtuma mtu aende kule ambako tukio hilo limefanyika. Lakini ajabu kila ambae alitumwa hakuweza kurudi salama. Basi wanakijiji wakaanza kutomheshimu sasa Maposo, lakini alikuwa anatumia nguvu zake kuwaongoza watu ambao hawampendi . Upande wa Malkia mwamvita akiwa na Mumqa wanapanga Swala la kuivamia ngome ya Maposo na ikiwezekana wakishike na kile kijiji ili kiwe mikononi yao na kuwafanya wananchi waishi kwa amani na upendo......

Itaendelea....



No comments: