Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KUMI (10).
Riwaya:THE TRUE LOVE.
SEHEMU YA KUMI (10).
Hakujua kama kwenye kile chakula mwanae Wanjera alimuwekea sumu kwa lengo la kumuua.Mama Imma akaanza kula hapo hapo,alikula ile sahani yote ya chakula akawa ameimaliza.Alisimama akajinyoosha baadae akayasema maneno haya "Mwanangu asante kwa chakula,hebu ngoja nikapumzike kidogo maana kwa sasa nimeshiba nikiamka tutaongea".Maneno hayo yakawa kama ndo maneno ya mwisho kutoka kinywani mwa mama huyo ambaye alipigana kwa jasho na damu kumfanya kijana wake mkubwa Imma kufika hapo alipo,,Wanjera baada ya kuyasikia vilivyo hayo maneno alitabasamu mpaka akasimama na kisha kumkumbatia mama yake,kumbatio moja la kinafiki huku moyoni akichekelea kwa kudhani sasa neema itamshukia katika maisha yake."Nawe pia mama asante kwa Shukrani yako,nakupenda sana mama yangu na pia nakutakia maisha marefu ya hapa duniani". Alizungumza Wanjera ,mama Imma akawa hana neno lolote la kuzungumza zaidi alianza kuzipiga hatua za mwendo wa taratibu kuingia chumbani kwake.Mama huyo alienda akakaa kitandani,ghafla kama kwenye dakika mbili hivi,alianza kuhisi maumivu makali ya kichwa,akawa analalama sana,hajakaa sawa mara tumbo kila kona nalo likaanza kuuma,mama akajikongoja akawa amesimama kwa kuegemea upande mmoja.Nguvu zilimuishia hapo hapo akaanguka chini kifudifudi,povu jingi jeupe likawa linamtoka mama wa watu,,,alianza kuipiga piga miguu yake pamoja na mikono yake mwisho akatulia na akawa amekata roho muda huo huo .Nje ya chumba cha mama Imma alionekana Wanjera akizipiga hatua za mwendo wa kunyata kuusogelea mlango wa chumba cha mama huyo,kwa vile mlango huo ulikuwa umefungwa alijaribu kuugonga akaugonga sana akaishia kupokelewa na ukimya.....akajua tayari mama yake ameshaenda na maji.Aliusukuma kwa nguvu ukafunguka hapo hapo akaingia.Alipoingia alimuona mama yake amelala chini kifudifudi akayaangaza macho huku na huko akaangua kilio cha kuekti."Jamani mama...Mamaa!! Njooni mumuone mama yangu,jamani mamaaa?" Alilia kwa nguvu sana huku akimlalia lalia mama yake pale chini,Dakika moja tu watu walianza kumiminika kwa wingi nyumbani kwa mama Imma,Huku Jack nae akiwasiri pale muda huo akiwa hajui chochote kinachoendelea eneo hilo."Mama,jamani mama,umefanyaje? Amka mama!!!" Wanjera aliendelea kulia kwa kuigiza,mpaka watu wakamshika na kutoka nae wakaelekea ndani ya chumba kimoja kwa ajili ya kumnyamazisha."Wanjera,nyamaza usilie huenda mama yako hajafa,nyamaza Wanjera".Mama Mmoja aliyazungumza maneno hayo."Siwezi kunyamaza mimi,siweziiii!! Mama uko wapi mama,inuka mama yanguuu!!".Wanj
era alizidi kulia mpaka Jack akatoka nje alipokuwa amesimamia akaingia ndani kujua ni kitu gani kimetokea maana bado alikuwa njia panda.Sasa alipoulizia ni kipi kimetokea na kuambiwa mama Imma amefariki dunia , alidondoka pale pale na kupoteza fahamu.Watu walimbeba wakampeleka chini ya ule mti wa Mkuyu kwa ajili ya kwenda kumhudumia.Taarifa zilimfikia Imma kule hospitalini akatoka mbio kwa miguu hadi nyumbani kwa mamaye,akafika na kuingia moja kwa moja chumbani kwa mama yake.Alipomuona mamaye amelazwa kitandani alimwangukia akawa analia mithili ya mtoto mdogo.Imma alilia mno "Sina baba,sina mama,faraja yangu kubwa ilibakia kwa mama yangu,mama...Mama hivi umekufa au naota? No.....no...hapana mama hujafa!! Hujafa mama yangu,kwa nini uende mapema kiasi hiki mama? Hapana mama!!! Mama....Hata hujayafaidi matunda yangu mama ndo unanitoka? Tumetoka mbali mama yangu,tumekula ugali wa mtama mama yangu,tumelala njaa mama yangu,tumedharauliwa mama yangu na kulala chini lakini busara yako isiyofifia ilisimama imara kunipa matumaini kwamba ipo siku nasi tutaishi kwa furaha ,,eti leo mama baada ya dhiki kupita ndo umekufa? Hapana mama,,,mama....
Mamaaa ....Mama,amka mama".Kijana Imma baada ya kulia vya kutosha marafiki zake ambao pia ni madaktari wenzake walikuja eneo hilo la tukio wakamshikilia Imma hadi kwenye kibalaza kimoja wakaenda kumtuliza huko.Siku tano zilimalizika hatimaye siku ya msiba yaani siku ya kumzika mama Imma ikawadia.Siku hiyo ilihudhuriwa na watu wengi sana,,,sasa baada ya mambo yote kumalizika muda wa kuuaga mwili wa mama huyo ukafika.....vilio vilitamalaki mno,Jack alikuwa akilia kupita maelezo huku Imma akiwa hoi hajitambui kwa kilio na uchungu aliokuwa nao kwa kuondokewa na mamaye ambaye bado alikuwa akimhitaji,ila ilimbidi ajikaze tu kwani kama ni maji tayari yalikuwa yameshamwagika hivyo kuzoleka ingekuwa ni vigumu sana....binafsi hakuwa akitambua ni kipi kimemuua mama yake hadi siku hiyo ya msiba na hata kabla ya msiba hakuwa na wazo kabisa la kusema akamchunguze mamaye kujua nini chanzo cha kifo chake,kumbuka damu ni nzito kuliko maji.Basi mnamo majira ya saa kumi na robo mama Imma akawa amezikwa na watu wakatawanyika maeneo hayo.Eneo hilo akabaki Imma pekee akiendelea kulitizama kaburi la mama yake kwa uchungu usiokuwa na kipimo.Akiwa amechuchumaa alisimama akairusha rusha mikono yake akisema "Nenda mama....ila..ila mama nitakumisi sana,kapumzike kwa amani mama!!! Najua umeniachia maswali magumu sana lakini yote kwa yote ipo siku tutaonana tena ,hata kama hatutaonana sehemu yoyote tutaonana pahala pema peponi amen!!".Wakati akimalizia kuyasema maneno hayo huku akiivua miwani yake nyeusi,kumbe kwa nyuma alionekana Recho akija akafika na kumshika mabega yake yote "Pole Imma,jikaze!! Wala usilie mama ameenda kupumzika cha msingi ni kuyaacha maisha yaendelee".Alisema Recho kisha akamshika mkono Imma wakaanza kuondoka....waliziacha kama hatua tano tu,Imma akageuka tena na kusimama akawa analitazama kaburi la mama yake,alitikisa kichwa kwa masononeko makubwa ,Recho akamvuta wakaendelea na safari na kwa muda wote huo Imma hakuwa akizungumza chochote pamoja na kwamba Recho yeye alikuwa akiongea ongea .Walifika nyumbani wakaungana na watu waliokuwepo pale kwa ajili ya kuyaanza matanga ya mama Imma.Matanga hayo yaliendelea kwa jumla ya siku arobaini ,mwisho siku zote hizo zikamalizika....maisha yakaendelea.Siku moja ya juma mosi,Mr Ludovic aliwaita Imma pamoja na dada yake Wanjera pale kwake wakaenda mnamo majira ya saa tisa alasiri kwani alitaka kwenda kuwafariji pamoja na kuwaandalia sherehe kuwapoza machungu yao.....Wanjera wakati anaondoka hakuondoka akiwa yeye kama yeye bali aliondoka pamoja na mwanae wa kiume Bahati mwenye umri wa miaka mitano.
"Kwanza kabisa nipende kutoa pole kwa kijana wangu Imma pamoja na dada yake Wanjera kwa kuondokewa na mama katika kipindi hicho cha kushtuza.Najua vijana hawa watakuwa na maumivu makali sana kwani uchungu wa msiba aujuaye ni mfiwa.Ila nawaomba tu wawe na mioyo ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na Mungu azidi kuwatia nguvu,,,,Kwa siku hii ya leo nimepanga kufanya kitu kimoja cha kihistoria".Mr Ludovic aliyazungumza hayo akanyamaza kidogo baadae akamgeukia Jack na kumtazama huku akiwa anaonyesha hali ya tabasamu nono usoni mwake."Mwanangu Jack kabla hajaondoka kwenda kujiunga na masomo yake ya chuo kikuu cha California kule nchini Marekani nitahakikisha nazitimiza ndoto zake zote kabla hajaenda huko,Jack kuna siku aliwahi kuniambia kwamba katika maisha yake tangu akiwa mdogo hakuna mwanaume aliyewahi kutokea kumpenda kama Imma na akaniambia hata siku moja hatakuja kuolewa na mwanaume yeyote zaidi ya Imma hivyo.....?" Kabla Mzee hayajaendelea,maneno yale yalimchoma sana Recho akasimama pale alipokuwa amekaa akatoka nje akiwa na hasira akatokomea kabisa.Mr Ludovic akamgeukia mkewe "Mama Recho,huyu binti kulikoni? Mbona amesimama na kutoka nje ?" Aliuliza Mr Ludovic mama Recho akakosa jibu la kumwambia ikambidi mzee aendelee tu atadili nae binti huyo baadae.Hivyo humo ndani wakabaki watu kumi na wawili mhimu huku Minza ,Jane pamoja na marafiki wengine wa Jack wakiwemo."Nami naridhia mwanangu Jack kuolewa na Imma,na gharama zote za harusi yao zitakuwa juu yangu tena Imma sitaki atoe mahali ya aina yoyote ile,nampa bure kabisa binti angu kwani nimegundua wawili hawa wanapendana sana,,,labda nikuulize swali moja kijana wangu Imma,je utakubali kumuoa mwanangu Jack?" Alizungumza Mr Ludovic,Imma akatabasamu huku akiyafumba fumba macho yake."Ndio Mzee nitamuoa kwani huyu ndiye mwanamke wa kwanza kabisa katika maisha yangu ukimweka kando mama yangu ambaye ndo hivyo tena.....kwa sasa Jack nampenda mno na ndiye aliyebakia kuufariji moyo wangu". Alizungumza Imma,shangwe zikasikika mule ndani."Na wewe Jack una cha kusema?" Aliuliza Mr Ludovic,Jack akasimama "Baba,Imma ni kama mboni ya macho yangu,nampenda kuliko hata ninavyofikiria,ni mwanaume mmoja wa thamani sana maishani mwangu na nitaolewa na yeye na kamwe sitakuja kumsaliti".Baada ya Jack kuyazungumza hayo,alimfuata Imma akamnyanyua kisha wakakumbatiana.Basi nyumbani kwa Mr Ludovic,Imma na dada yake Wanjera walibaki hadi majira ya saa moja za jioni baadae wakaagana na wote waliokuwepo pale wakaondoka kurudi kwao.Kina Minza nao wakaondoka,sasa mabinti hao wawili baada ya kufika ndani ya barabara kuu walisogea pembeni kwani kuna gumzo moja lilikuwa limeigubika mioyo yao."Minza,hivi ni kwa nini Recho alitoka nje baada ya baba yake kuyazungumza yale maneno?" Aliuliza Jane,Minza kabla ya kumjibu akacheka,kicheko kikali cha kuvuta."Sikia,J
ane,sababu iliyomfanya huyo danguro atoke nje ni hii,,,Huyo danguro alijua baba yake atamzungumzia yeye ili aolewe na Imma,sasa lilipobuma tu akaona isiwe tabu akasimama na kutoka nje.Recho ni malaya mzoefu,tena ameshakuwa sugu na ndio maana baada ya kuona umri unaenda na hapati wa kumuoa akawa analazimisha kwa nguvu ili yeye aolewe na Imma". Aliongea Minza."Duuh! Kumbe ila Imma ameshakuwa handsome jamani,daah!! Hadi namuonea wivu Jack". Aliongea Jane baadae wakaondoka kuendelea na safari ya kule walipokuwa wanaenda.
********************************
Kesho yake ilikuwa ni siku ya juma pili.....Siku hiyo Imma alienda kanisani kama ilivyo kawaida yake,sasa wakati anatoka huko kanisani kwenye mishale ya saa nne hivi hakwenda moja kwa moja nyumbani kwake bali alielekea nyumbani kwao .Huko akafika na kumkuta dada yake Wanjera akiwa jikoni akimalizia kuandaa chai.......mtoto wa Wanjera nae alikuwepo maeneo hayo na ndiye aliyemtolea kiti Imma ili akakae kwenye ule mti wake.Sasa pale Imma alikaa kama dakika tatu hivi,akaonekana tena Bahati akija akamfikia Imma na kuja kusimama katikati ya miguu yake."Mjomba,umependezaa!!" Aliongea mtoto huyo Imma akawa anacheka tu."Sikia Mjomba,mama kabla Bibi hajafa ile siku wakati nacheza nilikuja nikachungulia kwenye lile dirisha la jikoni nikamuona...........
ITAENDELEA..............................................

No comments: