Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11).




Riwaya:THE TRUE LOVE.

SEHEMU YA KUMI NA MOJA (11).
Anaweka vitu vyeupe kwenye sahani ambayo alikuja kuitumia Bibi,,na wakati anaweka vitu hivyo tayari hiyo sahani ilikuwa na chakula.Bibi alipokuja kula tu kile chakula na ndo hapo hapo akafa". Aliongea mtoto Bahati,Imma akashtuka sana ikambidi akae vizuri ili amsikilize mtoto huyo kwa umakini mkubwa kwani alijua huenda huo utakuwa ni ukweli usiopingika."Nisikilize Mjomba,kwa hiyo baada ya mama kuviweka vile vitu ile sahani alimpelekea Bibi yako au?" Aliuliza Imma mara hii mapigo yake ya moyo yakianza kwenda kasi muda huo macho akiyaangaza huku na huko."Ndio Mjomba baada ya mama kumaliza kuviweka alimpelekea Bibi akala na siku hiyo hiyo ndo akafa,,,tena baada ya Bibi kufa.... kwenye lile dirisha la kushoto la chumba chake nilichungulia nikamuona mama akiwa amesimama mbele yake pale chini akayaangaza macho kulia na kushoto baadae nikamuona akiinyoosha mikono yake juu kushangilia huku akicheka na kumzomea Bibi pale chini.Alipomaliza kufanya hivyo ndo akaanza kulia sasa na watu wakaja".Bahati alitema cheche zote na ukweli ukawa umefichuka hapo hapo."Wanjera kumbe wewe ndo uliyemuua mama sasa ndo nimejua". Aliongea Imma kimoyo moyo."Mjomba na wewe usije ukakubali kukaribishwa kula chakula na mama ,mama hua anauwa watu,alimuua hata baba akakimbia sijui wapi akiwa amenibeba mgongoni".Mtoto aliendelea kuzungumza mpaka Imma hasira ikaanza kuwaka ndani ya moyo wake japo alikuwa akijikaza kiume.Imma haraka alisimama akaanza kuondoka,Bahati akawa anamfuata kwa nyuma....Imma alidhamiria kufanya kitu na ndio maana hakuwa na muda tena wa kusema akamuage dada yake Wanjera kule jikoni.Alitembea kimya kimya akawa amezunguka kwenye ukuta wa nyuma wa nyumba kubwa ya marehemu mama yake akambeba Bahati akamuaga "Mjomba nitakuja siku moja nikuchukue twende wote ukapafahamu kwangu eti,najua hupafahamu". Aliongea Imma,Bahati akaitikia kwa ishara ya kutikisa kichwa chake,baadae Imma akamshusha chini akaondoka kuelekea kwake muda huo huo.Pale alibaki mtoto Bahati akimkodolea macho tu mjomba wake mpaka alipoishia kwenye kinjia kimoja chembamba kilichokuwa kimezungukwa na mtaro wa maji machafu.Alipoona mjomba ametoweka alirudi haraka hadi kwa mama yake kule jikoni."Mama nina njaa naomba unipe chai ninywe".Alisema Bahati huku akideka kwa jinsi apendayo,mama yake alimtazama usoni akacheka kidogo."Hahaa!! We nae yaani mara hii tu umeshapata na njaa? Ila haina shida fuata sahani na kikombe nikupatie sawa ee?" Aliuliza Wanjera.Bahati alitoka haraka kufuata sahani na kikombe....Sasa wakati mtoto huyo akiondoka tu,Wanjera haraka sana aliyanyanyua macho yake kukitafuta kile kijimfuko cha sumu kwani kwa mawazo yake alidhani Kaka yake yupo na lengo lake kuu kwa muda huo lilikuwa limehamia kwa Imma.Alikiona kile kijimfuko,akakitia kwenye mapaja yake ,hapo hapo Bahati nae akaingia."Mama nimeleta sasa naomba unipe chai yangu".Alisema Bahati,mamaye akatabasamu akaipokea ile sahani pamoja na kile kikombe ,,,kabla hata hajakaa sawa.Kile kijimfuko,Mtoto Bahati alikiona maana mtoto huyu alikuwa ni zaidi ya clever,alicheka kwa kejeli."Mama hicho kijimfuko hapo miguuni mwako ndo chenye majani ya chai au sukari?" Bahati aliuliza lakini moyoni akajua kuwa kile kijimfuko ndicho ambacho alikiona siku ile mama yake anamuwekea mama Imma sumu kwenye kile chakula ,aliamua kumtega tu mama yake ili aone atamjibuje."Hapana Bahati humu kuna...kuna...kuna kuna unga wa ngano kidogo ulibakia nikaamua kuutunza humu".Alijibu Wanjera akidhani kwa maneno hayo ,Bahati atampoteza na hatogundua chochote."Sasa mama kama huo ni unga wa ngano mbona naona kama una michirizi miekundu ,harafu naona kuna kitu kama kichwa na alama ya kuzidisha,mama huo sio unga wa ngano, na kama ni unga wa ngano nauomba nikauchanganye kwenye ule mfuko mkubwa wa unga wa ngano".Bahati alimuweka katika wakati mgumu sana mamaye,kijasho chembamba kikawa kinamtoka."Naomba ule kwanza mwanangu halafu leo jioni nitakununulia bigboom eti?" Alisema Wanjera japo kwa kubangaiza maana mtoto yule alikuwa amemshika pabaya akajua huyu atakuwa amegundua siri yote."Hahaha!! Mama siwezi kula ,nataka kwanza unipe hicho kijimfuko nikae nacho mimi hapa,sitaki hata uninunulie hiyo bigboom".Alisema Bahati,Wanjera akili yake ikawa imevurugika akaanza kumtukana mwanae huku akimtisha,Mtoto ikabidi atulie tu lakini moyoni akawa na moja kichwani.Bahati aliipokea ile sahani iliyokuwa na chapati tatu akakichukua na kile kikombe cha chai akaondoka zake.Wanjera alipoona mwanae ametoka,alisonya akakirudishia kile kijimfuko sehemu ambayo alikitolea awali.Baada ya kukiweka hapo alitoka humo jikoni akaja nje na kisha kuanza kuita "Kaka wa mie....Imma where are you? Kaka ,,chai tayari".Aliita,alipokuja kuyanyanyua juu macho yake hakuona mtu pale chini ya mti wa Mkuyu zaidi ya kuona kiti tu ambacho kilikuwa wazi.Kwa upande wa Imma,baada ya kuondoka na kurejea kwake alienda kufanya mpango mmoja mkubwa sana,huo mpango alikuja kuumaliza baada ya lisaa limoja kupita."Sasa huyu itabidi ale jeuri yake tu ,tangia zamani nimejaribu kuishi nae kwa kumvumilia sana lakini naona kama habebeki,mama,,,unamuua mama kwa kipi hasa? Kwa hili naomba Mungu anisamehe". Alijisemesha Imma maneno hayo wakati akiwa ameketi kwenye moja ya masofa yake pale sebuleni.Wakati akiwa amekaa hapo,zilikatika dakika tano,baadae mlango ukaanza kugongwa,,,,Imma alisimama na kwenda kuufungua mlango huo.Alikutana na binti mmoja sura yake akaitambua lakini jina akawa halitambui hata kidogo."Karibu dada,karibu ndani".Alisema Imma,binti huyo akaingia na kwenda kukaa ."Kaka Imma,mimi naitwa Minza ni rafiki yake na Jack".Alisema,k
umbe alikuwa ndo Minza mwenyewe."Aha!! Kumbe ndo Minza?? Shemu karibu sana,unajua sura niliielewa sana ila nikawa najiuliza huyu binti mbona kama namfahamuu!! Daah eneway sijui huwa unatumia kinywaji gani?" Alisema Imma,Minza akatabasamu huku akimkazia macho Imma,usoni."Acha tu shemu wala nisikusumbue sana".Minza alikataa."Basi haina shida,niambie sasa". Aliongea Imma,Minza akaonekana kama alienda pale akiwa na ubuyu wa kutosha Kama ilivyo kawaida yake."Shemu nataka nikupe habari moja japo itakushtua". Aliongea Minza.....Imma akakaa sawa kwa ajili ya kutaka kusikia ni habari gani itazungumzwa na binti huyo."Nakusikiliza shemu unaweza kusema tu wala usihofu". Aliongea Imma,hapo hapo Minza akaanza kufunguka neno moja baada ya jingine.
"Hivi shemu unajua mama yako alifariki kwa ugonjwa upi ?" Minza alianza kwa kumhoji swali hilo Imma."Daah!! Kwa kweli sifahamu ila kuna fununu ninazo japo kwa sasa sitaki kuziweka hadharani,mama hakuwa na ugonjwa wowote na wala hakuwahi kuwa na presha maana Mimi mwenyewe nilikuwa nimejiwekea utaratibu wa kumfanyia vipimo mama kila baada ya mwisho wa mwezi ,sasa sijui ni kipi kilimuua ,sijui".Alisema Imma ,Minza akazidi kumkazia macho."Sasa shemu nisikilize,naanza kwa kuyanukuu maneno haya ambayo dada yako Wanje aliwahi kuniambia siku moja,yaani siku tatu kabla ya mama yako hajafariki,,,Wanje alisema "Yaani shoga angu acha kabisa,unajua katika hii dunia ukiwa mjinga na mzubaifu utaishia kufa maskini....bina
fsi nimepanga mali zote alizonazo mama,kuanzia majumba mpaka maduka aliyojengewa na Kaka Imma nataka siku moja yawe yangu niyamiliki mimi,sasa naomba unitunzie siri moja,,,,kesho kutwa mchana nimepanga kumuwekea sumu mama kwenye chakula afe ili zile mali ziwe zangu kwani kuna siku nilijaribu ikashindikana".Mwisho wa kunukuu,,audio ya maneno yake ninayo kwani niliyarekodi kwenye hii simu yangu,,,,binafsi nilimkataza asifanye hivyo ila akakataa katakata nikamuacha nikawa napanga kabla hajafanya hilo tukio nije nikuambie sema tu nilisahau nisamehe kwa hilo,,,sasa shemu Imma huo ndo ukweli,kifo cha mama yako kimesababishwa na huyo huyo Wanjera unayemuita dada,shemu hapa sikai sana ngoja niondoke,nikutakie tu jioni njema".Minza alisimama akaanza kutoka huku Imma akimsindikiza kwa macho.Imma alitahaluki akawa anayakumbukia yale maneno aliyoambiwa na mtoto Bahati na hapo ndipo akaamini kuwa ni kweli Wanjera ndiye aliyemuua mama yake kwa kumuwekea sumu kwenye chakula . Aliendelea kumtazama Minza mpaka akatoweka mbele ya mboni za macho yake.Sasa Minza baada ya kuondoka nyumbani kwa Imma alifunga safari ya kuelekea nyumbani kwa marehemu mama Imma,,alifika huko kama kawaida akamkuta Wanje ,muda huo alikuwa akiosha vyombo ."Shoga angu nakuona ukiwa katika ubora wako,,,sasa Wanje nina shida moja naomba unisaidie". Alizungumza Minza."Shida gani hiyo?" Aliuliza Wanjera huku akisimama."Naom
ba unikopeshe laki moja juma tatu ijayo nitakurudishia maana nadaiwa ada kiasi furani na baba anazingua".Alijieleza Minza lakini huo haukuwa ukweli na hakuwa akidaiwa ada kama alivyozungumza."Sawa shoga angu,nitakupa tu hiyo hela wala usinirudishie maana Mimi na wewe tunajuana na tunaishi kama marafiki wa dhati".Baada ya Wanje kumaliza kuyaongea maneno hayo,Alisimama akaingia ndani haraka na punde si punde akatoka akiwa na hicho kiasi cha pesa akampa Minza.Minza alimshukuru akamuaga hapo hapo akaondoka kuendelea na safari zake.
******************************
Zilipita siku tano mfululizo bila ya Imma kukanyaga nyumbani kwao na hakwenda kabisa kumsalimia dada yake na hata kwa njia ya simu tu napo hakumjulia hali,wala hilo halikumpa tabu yoyote Wanjera zaidi aliona tu lengo lake tayari limeshatimia.Siku ya juma mosi asubuhi sana,,,Imma aliwapigia simu jamaa watano,wafanyabiashara wakubwa pale mjini akapanda gari na kuanza kuelekea kwao akiwa ameambatana na hao watu.Alifika huko baada ya nusu saa kukatika,,akamkuta Wanjera akicheza na mtoto wake Bahati,sasa Imma wala hakuwa na muda wa kumsalimia zaidi alikuwa akimtazama tu,,,muda huo huo Minza nae alionekana akija akiwa ameongozana na Jack.Sasa Imma alishusha briefcase yake aliyokuwa ameibeba akawa anaifungua ,baada ya kuifungua alitoa hati miliki zote za majumba yale pamoja na lile duka akaanza kuwatazama wale jamaa kwa zamu na hakutaka kusikia chochote kutoka kwa Wanje."Kaka shikamoo?" Kaka chai yako ipo jikoni nikufuatie unywe?".
ITAENDELEA.........................................



No comments: