Riwaya:THE TRUE LOVE.SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12).
Riwaya:THE TRUE LOVE.SEHEMU YA KUMI NA MBILI (12).
"Sijaja kunywa chai hapa dada,kwa sababu chai tayari nimeshainywa tena ile ya maziwa ya ng'ombe wa kisasa hivyo labda uitunze tu kwa ajili ya matumizi yako ya baadae". Alizungumza Imma huku akiwa hamtazami dada yake Wanjera na wakati akiyaongea maneno hayo hakuonekana kuwa na masihara hata kidogo,Sasa baada ya Wanje kuyasikia vyema maneno hayo kutoka katika kinywa cha Kaka yake hakuweza kumuelewa akawa anadhani huo ni utani tu wa Kaka yake kama ambavyo alikuwa akimfahamu tangia siku za nyuma sana wakiwa watoto wadogo."Aaa!! Kaka ina maana ndo umekataa kunywa chai iliyoandaliwa na dada yako?" Aliuliza Wanje mara hii akijichekesha chekesha,binafsi hakujua nia ya Imma kuwepo pale pamoja na wale watu,yeye kwa muda huo alijua tu huenda labda Kaka yake amekuja kwa ajili ya kukamilisha mambo furani .....alikuwa akiwatazama wale jamaa na suti zao akadhani ni wana sheria wa Serikali na amekuja kuziandikisha zile mali ili ziwe zake azimiliki yeye."Dada uwe mwelewa basi,nimeshakwambia hapa sijaja kunywa chai nimekuja kwa ajili ya mambo yangu na si vinginevyo".Aliongea Imma kisha akaanza kusogea sogea nyuma kuwafuata wale jamaa walipokuwa wamesimamia."Wanjera kuna story moja nataka nikusimulie sijui utakuwa tayari?" Aliuliza Imma."Story gani sasa Kaka bila shaka unaweza kunisimulia".Alijibu Wanje,Imma akatabasamu kidogo."Sasa story yenyewe ni hii hapa....Kuna mama mmoja kwa taabu sana alimzaa mtoto wake akawa anahangaika kumlea,baba wa mtoto huyo hakudumu sana kwani alifariki katika mazingira ya kutatanisha na hapo ndo mateso yalivyozidi kwa mama huyo pamoja na mwanae,shida na dhiki zilipozidi kuongezeka mama alikata shauri ya kuanza kufanya kazi ya kuponda kokoto ili mwanae ale,alale na aweze kusoma kwani aliamini elimu ndo ufunguo wa maisha ,mwanae akisoma basi hata yeye ataishi kwa furaha na kumfuta machozi.Basi mama akaanza kuifanya ile kazi...akaifanyaa hatimaye kipato akawa anakipata,pamoja na kipato hicho kuwa ni cha chini na hakitoshi lakini alikigawanya hivyo hivyo ili tu aweze kuishi na mwanae mpendwa .Kweli Mungu kupitia juhudi hizo za yule mama alimsaidia na mwanae akawa anazidi kupaa tu,mwisho wa siku mwanae akasoma hadi chuo kikuu na kupata kazi.Mama huyo alifurahi mno akaamini sasa matunda ya mwanae ataanza kuyala,na kweli alianza kuyala.Muda mfupi tu mama akiwa anafaidi matunda ya mwanae alikuja kutokea kijana mwingine sijui alitokea wapi akaja na kumuomba yule mama awe anamfanyia kazi za pale,mshahara wake akataka uwe ni chakula na maradhi tu basi,mambo mengine yatajipanga mbele ya safari.Ndani ya mwaka mmoja tu,yule kijana akaanza kuingiliwa na tamaa kuhusiana na zile mali za yule mama,shetani nae sijui akamshawishi kijana wa watu,si akaanza kumuwazia mabaya yule mama....akawaza wee mwisho akapata jibu la kumuua mama wa watu,alipanga mpango wa kumvamia mama huyo usiku wa manane akiwa amelala,amshukie mazima amchome kisu afe,huo mpango ulipokamilika na kweli yule kijana akamuua mama wa watu na hiyo ikabaki kuwa ni siri,akasingizia mama yule alivamiwa na watu Usiku wakati yeye akiwa dukani wakamuua mama yule.Basi maisha yakaendelea na jambo hilo likawa kama limesahaurika.Sasa kwa vile dunia haina siri,na kama unakikumbuka kile kitabu cha hadithi ya Mfalme ana masikio makubwa kama ya punda bila shaka utakuwa unaielewa story yangu hii.Kumbe bwana,yule kijana wakati analifanya lile tukio na kujiona yupo peke yake hakuna anayemuona kumbe kuna mtoto mdogo alimuona na haikujulikana yule mtoto alitokea wapi,na ndiye aliyekuja kuitoboa ile siri kwa mtoto wa mama yule baada ya siku nyingi kupita.Kijana yaani mtoto wa yule mama alikasirika sana akaja na ghadhabu ya kumkamata kijana yule muuaji akaenda kumfungulia mashtaka na mwisho wa siku,kijana muuaji akahukumiwa kifungo cha maisha jela,biashara yake ikawa imeishia hapo". Alizungumza Imma baadae akameza fundo moja la mate akamsogelea mtoto wake na Wanjera akambeba.Kunako upande mmoja wa mafichoni,, ilionekana gari ya Recho ikiwa imepakiwa na katika eneo hilo hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akionekana kuja au kurudi.Zilionek
ana nyasi tu zikitikisika kwa sababu ya upepo mdogo wa majira hayo ya asubuhi....vichaka navyo vilikuwa vikipepea kwa mtindo wa kustaajabisha mno.Kama kwenye dakika ishirini na kitu hivi kwa mbali walionekana wanaume saba wenye mbavu na six pack za kutisha wakija......walitembea wakaziacha hatua tatu nyuma wakasimama na kwa pamoja wakageuka kama vile kufumba na kufumbua.Wakiwa wamegeuka,mara binti mmoja aliyekuwa amevalia jinzi nyeusi iliyotoboka kwenye magoti alionekana akija mbele ya wale jamaa,alitembea haraka haraka kumbe wakati anasogea alikuwa ndiye Recho mwenyewe.Alifanikiwa kuwafikia hao jamaa akasimama katikati yao.....akaanza kuwatazama mmoja baada ya mwingine,akawapa ishara ya kwamba,sasa waendelee na safari.Waliifikia ile gari wakasimama tena.Recho akaivua ile miwani yake ya jua akajisachi mfukoni na hapo akatoa picha mbili,moja ilikuwa ni picha ya kijana Imma na nyingine ilikuwa ni picha ya mdogo wake Jack,akawa anawaonyesha na jamaa wakawa wanamsikiliza kwa umakini mkubwa mno."Mr Makangaros,,,sasa naomba myatege masikio yenu,tena myatege kwa makini sana.Bila shaka hawa watu mmeshawatambua kupitia hizi picha.Hawa watu mnamo tarehe ya Saba mwezi wa nane mwaka huu watafunga ndoa yaani harusi katika kanisa la Anglican hapa mjini,,,, Makangaros nisikilizeni sasa.....Siku hiyo mtaenda huko mkiwa mmevaa suti zenu mkaonekane kama wageni wengine tu.Mkae mbele kiasi na wengine wakae nyuma,,,lile tukio la viapo likianza wengine wakasimame sehemu furani ili kumtageti huyu binti na kabla hajazungumza chochote hakikisheni mnamshuti afe....narudia tena hakikisheni mnamshuti afe...afe...afe hakuna kumuonea huruma". Aliongea Recho huku akiwa amekunja ndita za hasira."Lakini dada mbona huyu ni dada yako na mtoto wa mwisho wa baba yako Mr Ludovic,sasa kwa nini unataka kumfanyia hivyo?" Aliuliza jamaa mmoja,Recho akamtazama kwa jicho baya sana."Hakuna cha ndugu hapa,,,kila mmoja akishatoka kwenye ule mfuko wa uzazi basi ameshakuwa kivyake,,,nyie si mnataka pesa bwana,,,,sasa hii kitu itekelezeni,kuhusu yule kijana yeye msimfanye chochote". Aliongea Recho kwa pamoja wakapanda ndani ya ile gari wakaondoka.Ile wanaondoka tu,alionekana Minza akitokelezea ndani ya nyasi ndefu zilizokuwa zimetengeneza kichaka mithili ya kile cha miti mifupi mifupi....na sikujua hapo alifika fikaje kwani kuna muda alikuwepo pale nyumbani kwa mama Imma.Sasa baada ya Minza kutoka ndani ya kile kichaka,alitembea kwa kuyaangaza macho yake huku na huko akawa amefika katikati ya barabara ile ya lami akasimama na kuanza kuipangusa pangusa suruali yake yenye rangi mithili ya magwanda ya kijeshi.Akamaliza na kutembea kwa mwendo wa haraka haraka akatoweka maeneo hayo na kurudi alipokuwa ametokea.Basi kwa upande wa Imma mara baada ya kumsimulia dada yake ile story na kumbeba mtoto Bahati mara hii hakuwa na cha kupoteza.
"Wanjera hapa duniani hakuna mtu yeyote yule mwenye thamani kama mama,katika familia hata iweje mama hawezi kuwakimbia watoto wake kwamba aende zake kama ambavyo mababa huwa wanafanya.Katika familia mambo yakiwa magumu kupita kiasi mtu wa kwanza kuikimbia familia bila kujali pale kuna watoto wenye umri gani ni baba....yeye kwa muda huo hayo yote atakuwa ameyasahau na hatojua chochote.Atakimbia kivyake na ataenda anakokujua lakini mama yeye hawezi hata siku moja kuwakimbia watoto wake na kuwaacha wakiwa hawajui pa kwenda.Mama atakuwa tayari kulala njaa na wanae pale itakapowezekana lakini yeye huyo huyo hatotaka kuwaona watoto wake wakilala njaa .Yupo radhi yeye asile lakini watoto wake wale....yupo radhi kufa na watoto wake pale inaposhindikana...huyo ndo mama na ndio maana nikasema hapa duniani hakuna kama mama.Mara nyingi,kina baba wao huwa wanamfariji na kuonekana kuwa na mama wakati wa neema tu ila mambo yakigeuka na yeye anageuka na kuwa mbogo tena mwenye mapembe......hivi umeshawahi kujiuliza ni kwa nini kina baba au wavulana hupenda kuwavua nguo mabinti na kufanya mambo yao kwa raha zao lakini binti huyo huyo akipata mimba tu,mvulana au mbaba anakimbia au kuikana ile mimba hata kama ni yake? Kwa hapo nakuachia home work japo sitopata muda wa kulitaka jibu lako". Aliongea Imma kisha akavuta pumzi ili aendelee kwa muda huo Wanjera alikuwa kimya kusikiliza na moyoni mwake hakuonekana kuwa na hofu wala wasiwasi,sasa baada ya Imma kuwa sawa alimuita Jack.....wakati Jack akimsogelea Imma hapo hapo akaonekana Minza akija,akafika na kusimama pale alipokuwa amesimamia Jack.Sasa Jack kwa mwendo wake ule alifanikiwa kumfikia Imma akaenda na kumuegemea kwenye bega lake moja la kushoto."Dada Wanjera,wewe ni dada yangu wa ukweli kabisa,tena tumezaliwa kutoka ndani ya tumbo moja.....Mama mmoja na baba mmoja,toka nitoke,,,nilitoka mimi ukatoka na wewe,,,sasa unamuona huyu binti? Huyu ni Jack kama ulikuwa humfahamu,kwa sasa huyu ni mama yangu na ni dada yangu na pia mke wangu mtarajiwa au kwa ufupi mke wangu ". Aliongea Imma,na kwa hapo Wanjera akaanza kuhisi kitu."Kaka mbona sikuelewi?" Wanjera aliuliza huku akianza kumsogelea Imma ili kama ni kumpigia magoti kwa kinachoendelea afanye hivyo.Imma alimkwepa akamsogelea Minza pale alipokuwa amesimamia akamuomba simu yake na Minza bila ubishi akamkabidhi.Imma akasogea hadi pale kwenye lile eneo lake la awali,Jack akaendelea kumuegemea kama kawaida maana kuna raha yake binti aliihisi kutoka hapo."Kaka unaongea maneno lakini sikuelewi Kaka? Una maanisha nini Kaka?" Hayo maswali aliyauliza Wanje,,,,Imma akatabasamu na kumkodolea macho akamsogeza Bahati karibu yake baada ya kumshusha kwa mara ile."Wanje utanielewa tu,sasa nataka nikuulize swali moja .......Wanjera inasemekana wewe ndiye uliidharau thamani ya mama ukaiona haifai pamoja na mama kuishi maisha yale ya taabu ,akapata neema ukaamua kumfanyia ukatili,,sasa swali langu ni hili,,,ni kweli mama ulimnywesha sumu akafa au hukumnywesha sumu ni bora uniambie ukweli kabla majumba haya sijayapiga mnada na wewe kukufukuza kama mbwa koko huku Bahati nikiondoka nae,sema ukweli nadhani hawa watu kama huwafahamu ni wafanyabiashara na ndio niliokuja nao kuifanya hiyo kazi,sasa naomba uniambie".Alisema Imma.
***************************
"Kaka,maskini mimi naanzaje kumuua mama yangu? Mama wala nisingeweza kumfanyia hivyo....Mama nilikuwa nikimpenda tena sana.Nasema kutoka ndani ya moyo wangu hata Mungu shahidi,sikumnywesha sumu mama,bali ile siku anatutoka hata Mimi sikujua chanzo cha kifo chake kilikuwa ni kipi,,,,hivyo Kaka,kama kuna watu wamekuambia hivyo naomba hizo taarifa uzipuuze Kaka,kwani hao watu wana mpango wao wa kutaka kutuvuruga mimi na wewe". Aliongea Wanjera mara hii akiwa amepiga magoti huku akilia kwa uchungu,,,Imma alimtazamaa,kisha akacheka kidogo."Wanje hakuna kitu ninachokichukia kama kudanganywa,kwa mara ya mwisho naomba uniambie ukweli,ulimuwekea mama Sumu kwenye chakula afe au hukumuwekea?". Aliuliza Imma kwa mara ya mwisho."Kaka huo ndo ukweli wangu sikumwekea mama sumu".Alizidi kukataa katakata Wanjera."Aha!! Kumbe sasa,subiri,,,,
kwa vile wewe umekataa basi ushahidi utakuumbua na hapa hutokaa tena".Alisema Imma kisha akajisachi mfukoni na kukitoa kile kijimfuko cha ile sumu nyeupe,muda huo akalisechi na lile faili lenye sauti yake wakati akiongea na Minza kipindi hicho,,,Kasi ya kutetemeka ikawa ni kubwa sana kwa Wanje."Samahani Kaka,kwa sasa nitaongea ukweli.........Acha niongee ukweli Kaka ..
ITAENDELEA....................................

No comments: