Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KUMI NA TATU (13).
Riwaya:THE TRUE LOVE.
SEHEMU YA KUMI NA TATU (13).
Maneno hayo aliyazungumza Wanjera na kiukweli alianza kutia huruma sana kwani kuna muda alikuwa akitembelea magoti kama mlemavu.Imma yeye kwa muda huo alidhamiria kukifanya kile alichokuwa amekipanga na wala hakuonekana kumhurumia hata kidogo Wanje."Si umeusema ukweli wote kwamba hukumnywesha sumu mama,sasa unataka kuniambia ukweli upi ulio nao?" Kwa muda huu mimi nadhani sina hata dakika ya kukusikiliza...mlango wa neema umeshafungwa simama tu wala usijisumbue". Aliongea Imma na akisha kuyazungumza hayo alizidi kumchanganya Wanjera hadi akawa analia kwa uchungu mno ....Imma bado hakuwa na dalili zozote za kumsamehe na kijana huyu alikuwa na msimamo wa ajabu,akiamua kitu kumshawishi akiache labda utumie mbinu ambayo haipo duniani."Mwanasheria hii nyumba unayoiona hapa ndo ambayo imenunuliwa na huyu jamaa,yeye anaitwa Mr Mishimo,na ile nyingine pamoja na duka lake amenunua jamaa angu yule pale mwenye suti nyeusi na kwa taratibu nilizokuagiza nadhani utazikamilisha tu ndani ya siku mbili,hati za umiliki nadhikabidhi kama ifuatavyo". Alizungumza Imma baadae zile hati akaanza kuwakabidhi wale wanaume huku akimuacha Wanje akiendelea kulia kama hana akili nzuri."Kaka,naomba unisamehe nitaenda kuishi kwa nani mimi? Nisamehe Kaka,naomba unisamehe mimi dada yako,nisamehe".Wanjera aliomba msamaha zaidi ya mara tatu tatu lakini Imma hakuonekana kumsamehe kwani alikuwa ameamua na utani hakuwa nao kabisa,Minza yeye pale alipokuwa amesimamia alikuwa akichekelea tu huku akibadirisha mapozi kwa jinsi anavyojisikia."Wanjera sina muda wa kukusamehe wewe,nenda ukajifunze kwanza,dunia ikakufunze labda akili yako itakaa sawa,,,na humo ndani unatakiwa kutoa mizigo yako yote ndani ya dakika mbili tu,kwani ukichelewa tunatia makufuli milango yote,hatuna muda wa kupoteza hapaa".Imma alizidi kuwa mkali na alikuwa amebadirika utadhani siyo yeye maana hata mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda mbio sana."Kaka,nipo chini ya miguu yako,naomba unisamehe nimetenda kosa mimi,nisamehe Kaka,nitaenda kuishi kwa nani mimi?" Alilia sana Wanjera hadi huruma ikamwingia Jack....akaamua kumsogelea Imma ili akambembeleze aone kama ataipangua kauli yake ile ya kumfukuza Wanje."Imma,,,naomba unisikilize mimi,nisikilize mpenzi wangu!! Unajua hapa duniani kufanya kosa kwa mara ya kwanza siyo kosa ila kosa ni kurudia kosa kwa mara ya pili ....nipo chini yako naomba msamaha kwa niaba ya wifi yangu Wanjera.....ni kweli amekuumiza mno,ni kweli ameusononesha mno moyo wako,ila...ila yote haya ni maisha tu,hakuna asiyefanya kosa hapa duniani,,,kumbuka Mungu ndiye mwenye mamlaka ya kutoa hukumu wala si mwanadamu....Mama ameenda kwa sasa imebaki story tu,hata kama utamfukuza dada yako kwa kumkatilia mbali,ukweli utabaki kuwa ni ule ule kwamba mama amelala na hawezi kuamka tena,na hawezi kurudi tena....hivyo Imma naomba umsamehe sana dada yako...msamehe tu kama vile neno la Mungu linavyosema tunapaswa kusamehe saba mara sabini".Maneno hayo aliyaongea Jack kwa sauti ya upole na yenye hisia kali mno huku akiwa amepiga magoti mbele ya kijana Imma,kitendo ambacho kilipelekea hadi Imma akaanza kutokwa na machozi ,,Imma alimnyanyua Jack akamkumbatia baadae akamuachia na kujikuta akiirusha rusha mikono yake asijue hata cha kusema ......alimtizama Wanje pale chini akamsogelea na kumnyanyua akamkumbatia pale pale,,,hayo yakawa yamekwisha.Baadae alimgeukia mwanasheria wake pamoja na wale jamaa akawaambia."Ndu
gu zangu,nadhani damu ni nzito kuliko maji,,,ni...ni..bora tu tuiache kama ilivyo".Imma alitengua uamuzi wa kumfukuza dada yake kupitia yale maneno ya mpenzi wake Jack akaamua kughaili kuziuza zile mali akakata shauri ya kuwarudishia wale watu pesa zao ambazo walikuwa wamezitoa.Kwa hapa Jack ninaweza kusema ndiye aliyemshawishi Imma mpaka akautengea uamzi wake kwani bila yeye Imma hata kwa bahati mbaya asingeweza kumsamehe Wanjera.Walikubaliana vizuri,na kwa bahati wale watu wakakubali na biashara hiyo ikawa imeishia hapo.Imma alianza kuondoka kuelekea kwenye gari yake akaifikia na kisha kusimama akajiinamia kidogo,aliinama sana baadae akageuka nyuma ikawa kama kuna kitu amekisahau.Alirudi haraka hadi kwa Jack akaenda kumkumbatia kwa nguvu zake zote akaangua kilio kama mtoto mdogo."Jack ....Jack....Jack ,,,, nakupenda sana Jack sitaki nikupoteze,wewe ndo mke wangu wa maisha wa kufa na kuzikana hivyo kukuacha wewe siwezi".Aliyatamka maneno hayo akamuaga Jack wake akageuza tena kuifuata gari yake....baada ya kupanda,wale watu nao walimfuata wakapanda pamoja na yule mwanasheria wakawa wameondoka maeneo hayo .Sasa baada ya Imma kuondoka Wanjera alisimama alipokuwa amepiga magoti akamkimbilia Jack na kwenda kumkumbatia vicheko vikasikika pamoja na kwamba Minza yeye hakujishughulisha na vicheko hivyo,,,na kwa kumtazama tu alionekana kama amechukia mno."Wifi,,,wifi hakika sitokusahau ,umeniokoa wifi na hakika wewe unafaa". Aliongea Wanje huku akiwa anamtazama Jack mara kumi kumi usoni ."Usijali wifi....kama maji yalishamwagika kuyazoa ni vigumu sana,acha maisha yaendelee tu,kwani hata kama Imma angekufukuza isingekuwa na maana yoyote ya kusema labda sasa mama atarudi au atafufuka". Aliongea Jack,baadae wakapiga story mbili tatu,wakaagana ili Jack na Minza waondoke maana kuna sehemu walikuwa wakielekea ukizingatia tayari jua lilikuwa limeshaanza kuwa kali kuashiria majira ya mchana yameshawadia.Basi waliagana.....Jack na Minza rafiki yake wakaondoka muda huo huo.Kunako nyumbani kwa Mr Ludovic,mbele ya bustani moja ya maua mbali mbali huku kijiupepo cha mbali kikipunga.... alionekana Recho akiwa amekaa kwenye kiti kimoja kirefu cha plastic kinachofanana na benchi au kitanda chembamba,amekaa kwa mtindo wa kukiegemesha kichwa chake pamoja na kuinyoosha miguu yake.....kwa muda huo mikononi mwake alikuwa na simu aina ya iPhone akiichezea chezea huku akicheka na kutabasamu,,,,Sasa wakati akiwa amekaa hapo,,,kwa mbali kwenye ule mlango wa nyuma wa nyumba kubwa.Alionekana mama yake akija ,mama huyo akawa anazipiga hatua kumsogelea,ile anamfikia tu....Recho aliificha ile simu."Recho habari za mchana?" Alimsalimia mama Jack huku akimkazia macho usoni pamoja na kwenye kile kimini chake kifupi alichokuwa amekivaa.Sasa hiyo salamu,Recho akawa kama hajaisikia kwani hakuitikia.Mama yake alirudia zaidi na zaidi mpaka akachoka na kujiondokea maana alimsoma mwanae huyo akagundua hayupo sawa.Hivyo mama Jack akaondoka.Baada ya mama huyo kuondoka..... Zilipita dakika kumi na tano,geti la nje likafunguliwa akaonekana Jane akiingia.Recho alimuona vizuri akawa anamkazia macho kwa umakini mkubwa mno .Basi Jane alisogea.... akamsogeleaa!! Hadi akawa amemfikia akakaa kwenye zile nyasi fupi na zenye mvuto."Recho mambo?" Jane alisamilia,,,Recho akaachia tabasamu,akajip
angusa kidogo usoni mwake."Poa tu,mzima wewe?" Alijibu Recho mara hii akikaa vizuri."Mi mzima ,sijui wewe". Aliongea Jane."Kwa kweli mimi sipo poa kabisa".Alitamka Recho,Jane akamkazia macho ."Kwa nini umesema hivyo dada Recho?" Jane alimuuliza."Imma Jane....Imma". Alijibu Recho."Imma? Imma amefanyaje?" Aliuliza Jane."Nampenda sana Imma,na sipo tayari kumpoteza kwani...kwani ni mwanaume pekee niliyemchunguza nikambaini ananifaa na anafaa kuwa mume wangu". Aliongea Recho huku akiipunguza punguza sauti yake."Si huyo tayari ameshahalalishwa na baba yako kuwa ndiye mume mtarajiwa wa Jack mdogo wako?" Aliuliza Jane."Hilo nalijua....tena nalijua kabisa ila siwezi kukubali kumuona Jack akiolewa na Imma hata siku moja ,nitafanya lolote na nitafanya chochote ili hiyo ndoa niikwamishe.....Jane kuna kitu naomba unisaidie kama utakuwa tayari".Alisema Recho."Kitu gani hicho?" Aliuliza Jane."Nataka tufanye mpango mmoja wa siri sana kuhusiana na Jack". Aliongea Recho,Jane akawa hayupo tayari kuendelea kumsikiliza binti huyo kwani aliamini kwa vyovyote vile ni lazima huo mpango ungekuwa si mpango mzuri."Hapana Recho,mimi sipo tayari kwa kweli ,mimi siyo msaliti hivyo labda umtafute mwingine". Aliongea Jane kisha akasimama na kuondoka haraka.....na kwa muda huo huo akarejea nyumbani kwao na kumuacha Recho kwenye mataa akiendelea na mawazo yake aliyokuwa akiyawaza.
Ndani ya ukumbi mmoja wa starehe,,,,saa ya ukutani ilizunguka kwa kutumia mishale yake.....mshale unaoonyesha mfumo wa masaa ukasoma.Ilikuwa imewadia mida ya saa saba kamili za mchana,watu walikuwa wamekaa kwenye meza mbali mbali kwenye viti vyao wakifurahia maisha huku watu wengine wakizunguka na kupishana pishana.Upande wa nyuma ,,,,walionekana Jack na Minza wakizungumza kwa ishara huku wakiyakodoa kodoa macho yao.Kwenye ile meza iliyokuwako mbele yao zilionekana plate za maana zikiwa na vyakula vizuri pamoja na vinywaji na matunda mbali mbali."Jack hii ndo ofa yangu niliyokuambia kwamba nitakupatia,kukutoa lunch hii ndo ofa yangu kwako,,,Kwa hiyo jisikie amani.Ila ni siku nyingi nimekuwa nikijiuliza swali moja ambalo ni gumu sana,sasa leo hii naomba unisaidie kulijibu ".Alizungumza Minza,huku akilibeba paja moja la kuku na kulitia kinywani."Swali gani tena Minza?" Aliuliza Jack,,Minza,binti mwenye miaka kumi na tisa tu akacheka kwa sauti ya chini."Tangu uanzishe uhusiano wa kimapenzi na Imma hivi mmeshawahi kufanya mapenzi hata siku moja?" Aliuliza Minza huku akiendelea kulishughulikia lile paja lake la kuku .Jack alimtazamaa,baadae akatikisa kichwa chake."Mh!! Minza kusema ukweli mimi na Imma tangia tuanze uhusiano hatujawahi hata siku moja kushiriki tendo la ndoa,na kwa upande wangu siijui hiyo radha kwamba ina utamu gani au uchungu gani,hiyo siyo kwangu tu,hata kwa upande wa Imma nae hajawahi kushiriki tendo la ndoa tangia azaliwe tuna mpango wa kufanya hivyo tukishamaliza kufunga pingu za maisha yaani ndoa halali ".Alisema Jack,Minza akacheka sana."Unaibiwa Jack narudia kwa mara nyingine tena unaibiwaa!! Nimesema hivyo nikiwa na maana kwamba,wanaume hisia zao kwenye suala la mapenzi ni sawa na moto wa mabua,ukishawaka tu mpaka uzimike wenyewe japo utawaka kwa muda mfupi......Mimi nakataa Imma hawezi kuwa bikra wa kiume hata siku moja kwa umri wote huo alionao,haiwezekani mwanaume awe na miaka ishirini na tisa halafu awe hajawahi kushiriki tendo la ndoa labda kwa wanaume wanaoishi ndani ya sayari ya Pluto kama wapo,lakini kwa wanaoishi ndani ya hii dunia kwa kweli tutadanganyana".Alisema Minza mara hii akibeba ndizi moja kubwa na kisha kuanza kuimenya."Sawa ,kwa hiyo wewe unanishauri nini? Ila mimi mbona nina mwamini Imma!! Na hawezi kunidanganya wala kuniambia uwongo".Alisema Jack,yeye akiwa ametulia hali tena."Ushauli wangu ni huu.....tenga siku moja uende nyumbani kwa Imma mishale ya jioni jioni akiwa ametoka kazini,ukafanye kila mbinu kumtega kimapenzi,,,akitokwa na udenda tu jua huyo siyo bikra wa kiume na ukweli utajulikana". Aliongea Minza huku akiendelea kushambulia chakula kama kawaida yake."Sasa nitamtagaje kimapenzi si mimi nampenda? Na ndiye mpenzi wangu?" Aliuliza Jack,Minza akacheka."Simaa
nishi hivyo,namaanisha hivi,,,ukishaenda nyumbani kwake,ukifika tu fanya kama unaenda kuoga......vua nguo zako zote jifunge kanga moja ingia bafuni oga.Ukishamaliza itepeshe hiyo kanga iyaonyeshe maungo yako kama yote,pita mbele yake wakati ukirudi,ingia chumbani muite hata kama yupo sebuleni.Akija tu,mwambie yale maji akufute na ikiwezekana akupake na mafuta kabisa......akikubali kufanya hivyo hiyo ni hatua ya awali.Hatua inayofuata chomoa mazima hiyo kanga yako tupa kulee!! Jilaze chali kitandani halafu mwambie unahisi baridi unatamani akukumbatie.....akikubali kuja tu,nadhani jibu utakuwa umelipata vizuri". Alizungumza Minza,binti matata sana huyu Jack akawa anashangaa shangaa tu kwani yeye pamoja na kuwa na umri wote ule wa miaka ishirini na miwili hakuwa akifahamu chochote.Jack akakubali na akaamua kesho yake atafanya hivyo......wali
endelea kula....wakala mpaka wakashiba baadae wakasimama na kujiandaa kutoka ndani ya ukumbi huo.Walikuja kutoka baada ya dakika tano hivi,wakafika nje wakaagana kila mmoja akaondoka sasa kunyoosha kuelekea kwao.
***************************
Siku hiyo ilipita hatimaye kukawa kumepambazuka,,,,kulipopambazuka,siku hiyo ya juma pili ambayo Imma hakuwa ameenda kazini Jack wazo lake kubwa likawa ni lile lile tu,binti aliwaza sana kwamba itakuaje.Hakusubiria siku ya juma tatu wala juma nne alikuwa ameamua siku hiyo hiyo ya juma pili akamchallenge mpenzi wake Imma aone itakuaje.Siku hiyo pale kwao hakukaa sana aliondoka mapema mno akawa ameenda nyumbani kwa mpenzi wake Imma huku akiwa na vipodozi vyake vya hapa na pale,wakati anaondoka vyote kwa pamoja alikuwa amevitia ndani ya mkoba wake pamoja na kanga moja nyeupe.
Je kwa mara ya kwanza Imma na Jack watafanya yao??
ITAENDELEA...............................................

No comments: