Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KUMI NA NNE (14).





Akisha kufika huko,kazi zote za ndani alianza kuzifanya yeye.....aliosha vyombo,kufua nguo za Imma pamoja na kupika.Majira ya mchana yalipowadia kila kitu kilikuwa sawa na hakuna ambacho hakikuwa sawa.Walipata chakula cha mchana mnamo majira ya saa saba na nusu hivi,,,,wakati wakiwa wanapata hicho chakula kuna muda kijana Imma alikuwa akimtazama mchumba wake Jack na kutengeneza maswali ya kumuuliza japo kwa huo muda kama kinywa chake kilikuwa kizito vile,,,hii ilitokana na kutomuelewa Jack ni kipi hasa kilichomfanya aende kwake kwani hakuwa na jingine binti huyo zaidi ya tabasamu tu na kumuangalia Imma bila kuchoka.Kijana alijikaza kukaa kimya mwisho uvumilivu wa kukaa kimya ukamshinda akaamua kumuuliza msichana huyo lengo lake kubwa lililompeleka pale kwa maana hiyo haikuwa kawaida yake."Mchumba.....tangu asubuhi nakuona ukifanya kazi zote za hapa na wakati mwingine kuniacha mdomo wazi pasipo kuniambia lengo lako la kuja hapa ni lipi....Sasa huenda kuna shida umekuja nayo,naomba uniambie maana ukibaki kimya utaniweka katika wakati mgumu sana,niambie usinifiche". Aliongea Imma huku macho yake mawili yakiwa usoni mwa Jack,,Sasa baada ya Jack kuulizwa hilo swali alianza kujinyonga nyonga mara ajing'ate ng'ate baadae kama kwenye dakika mbili hivi akaamua kufunguka .
"Hapana mpenzi nimekuja hapa kwa sababu nakupenda,na kama nakupenda wala sitoona haya kuzifanya kazi zote za humu ndani,,,nimekuja kukusaidia tu mpenzi wangu wala usihofu....Siku moja moja siyo mbaya". Aliongea Jack,lile jambo la kwamba ameenda kumtega aone kama atakubali kufanya nae mapenzi hilo hakumwambia.Basi muda ukazidi kusogea japo kwa taratibu hatimaye kama kufumba na kufumbua jioni hii hapa ikafika.Jack aliingia chumbani akamkuta Imma amejipumzikia kitandani akawa anamkodolea macho bila kuyapepesa lakini wakati akiendelea kumtazama,Imma yeye kwa upande wake wala hakuwa akitambua kama Jack anamtazama maana wakati akiwa amejilaza pale kitandani mikono yake alikuwa ameisogeza yote kunako upande wa macho yake.Ghafla akawa kama amekurupuka kutoka usingizini,akaamka na kumuona Jack amesimama mbele ya mboni za macho yake,akashangaa sana lakini moyoni akagundua jambo,na jambo jenyewe likawa ni huenda binti huyo aliyeumbika ameingia humo ili ajiandae kwa ajili ya kwenda kuoga bafuni.Hilo Imma aliligundua na akafahamu hivyo .Ili kujiridhisha kama anampenda kwa upendo ule wa dhati alitoka pale kitandani akawa anazipiga hatua kutoka nje ya chumba hicho ili amuachie nafasi,Jack avue aende akaoge.
"Mpenzi unaenda wapi sasa?" Aliuliza Jack baada ya kumuona Imma akiusogelea mlango ili aufungue atoke maana ulikuwa umefungwa tayari.Swali hilo lilimfanya Imma aanze kujikuna kuna kichwani.
"Nataka nitoke nikuachie nafasi,naona unataka ukaoge na ndio maana nimeamua kutoka pale kitandani".Alijibu Imma Jack akaachia tabasamu,tabasamu la haja huku macho yake akiyarembua na kuyalegeza kwa ufundi wa hali ya juu japo hakuwa na ujuzi wowote kwenye tasnia ya mapenzi maana binti alikuwa bado ni bikra.Jack aliunyoosha mkono wake wa kulia akawa anamzuia Imma ili asitoke nje ,,,Imma alikubali kishingo upande akawa amesimama kwenye kona moja ya ule mlango mara hii mapigo yake ya moyo yakianza kwenda kwa kasi.Ikumbukwe Imma tangia azaliwe na mama yake hadi anafikisha huo umri wa miaka ishirini na tisa hakuwa amewahi kulala na mwanamke yeyote yule wala msichana yeyote yule na siyo kwamba alikuwa ni mgonjwa hapana,kijana alikuwa ni mzima kabisa na jogoo lake lilikuwa na uwezo kuupanda mtungi kwa uzuri bila matatizo yoyote yale.Jack baada ya kumzuia alianza kuvua nguo zake alizokuwa amezivaa akianza kwa kuivua ile blauzi yake,,,wakati akizivua hizo nguo alikuwa akiendelea kumlegezea macho Imma na mara hii akiwa hazungumzi neno lolote lile zaidi ya kuwa kimya tu.Imma ile hali ilianza kumchanganya akaona hapa asipokuwa makini atajikuta akiingia majaribuni,aliyafumba macho yake ili asiuone mwili wa mchumba wake pindi atakapokuwa amemaliza kuzivua nguo zake.Kumbe wakati akiwa ameyafumba macho yake,Jack alimgundua akaamua kumsogelea na kuyafumbua hayo macho na akamsihi wala asione aibu kuyafumbua macho yake....hivyo Imma ikambidi ajikaze kisabuni tu kuyafumbua,aliy
afumbua akawa anamshuhudia binti huyo akivua nguo zake ili akaoge.Alimaliza kuivua ile blauzi akabakiwa na sidria nyeupe yenye maua ikawa inazionyesha chuchu za msichana huyo na kiukweli zilikuwa ni chuchu saa sita yaani zilikuwa zimesimama mithili ya misumari ukizisogelea zinaweza hata kukuchoma.Jack alitulia kidogo akamtazama Imma,na kumgundua alikuwa akitetemeka,aliacha kumtazama akaendelea kuvua.Aliichomoa na ile blauzi,hapo sasa ikawa balaa.Zile chuchu si zikawa zinaonekana na rangi yake ya chungwa.Imma akajitoa ufahamu akaamua kuufungua haraka ule mlango akatoka bila ya Jack kumuwahi....mara hii Jack alimuacha akamalizia kuvua nguo zake zote akamaliza na kisha kujifunga ile kanga yake.Baadae akatoka na kwenda kuoga......alioga wee akawa amelikamilisha zoezi hilo.Ile kanga aliitepesha na kweli ikawa imejichora mwilini mwake na kuyaonyesha vizuri maungo yake yote akatoka na kujipitisha mbele ya Imma lakini Imma alikuwa amemuona wakati akija hivyo macho yake aliyafumba kwa ujanja bila Jack kumgundua.Mpaka anaingia chumbani,Jack hakugundua kama mpenzi wake Imma alikuwa ameyafumba macho yake.Ile anafika humo alimuita Imma.
"Baby njoo basi humu chumbani mara moja".Aliita Jack,Imma akasimama kwa kujivuta vuta akawa anatembea kuusogelea ule mlango kama hataki,aliufikia huo mlango akaufungua na kuingia ndani.Akamkuta Jack akiwa ameiweka pembeni ile kanga yake na tayari alikuwa kama ambavyo alizaliwa,kidogo Imma atoke nje akajikaza tu.Huku chini jogoo nae alianza kudai haki yake na kwa muda wote huo Imma alikuwa ameshaichafua nguo yake ya ndani ,tangu azaliwe ile hali ya kuuona mwili wa mwanamke au msichana aliyepevuka katika huo muonekano hakuwa amewahi hata kule hospitalini tu nako hakuwahi kwani yeye japo alikuwa ni Daktari mkuu lakini taaluma yake ilikuwa ni ya kwenye masuala ya mifupa na ubongo.Daah!! Ule muonekano wa Jack,kusema ukweli kama ningekuwa mimi sidhani kama ningeweza kuvumilia,bila shaka shetani angenipitia tu.Jack mwili wake haukuwa na makovu,mwili ulikuwa ni mnyororo utadhani mwarabu sijui mvenezuera sijui mzungu wa south Africa sijui chotara wa kiarabu na kiafrika yaani ilikuwa ni hatari,,,unaweza kujiuliza haya niliyajuaje ni swaiba wangu Imma huyo huyo ndiye alinisimulia.Sasa Jack baada ya kumuona Imma tayari ameshafika alianza kudeka,mara anahisi baridi mara kuna mende amemuona mara mgongo wake unawasha anahitaji kukunwa mara anatamani Imma ampake mafuta ainjoy yaani ilikuwa ni shida."Baby naomba usogee unipake mafuta,I love you so much my bae". Aliongea Jack kwa sauti ndogo nyororo yenye uwezo wa kumtoa nyoka wa aina yoyote ile kutoka ndani ya pango.Imma kwa muda huo alikuwa kama bubu aliuacha ule msemo wa nifundishe kunyamaza uendelee kufanya kazi maana hakukuwa na namna.Alimsogelea mchumba wake Jack akachukua mafuta na kuanza kumpaka japo mikono yake ilikuwa ikionekana dhahiri ilikuwa ikitetemeka .Alimpaka hivyo hivyo akawa amemaliza na hapo hapo Jack,akajirusha kitandani na kisha akalala chali.Imma akawa anajiuliza hivi leo Jack amekuaje na huu ujasiri ameupatia wapi akakosa jibu.Jack baada ya kulala pale kitandani akaanza kumuita Imma aje amkumbatie anahisi baridi."Baby nahisi baridi,njoo unihag".Alitamka Jack,kwa hapa Imma akaamua kuutupilia mbali ule ububu.
"Jack....najua wewe ni mchumba wangu nakupenda na wewe unanipenda ......hilo unalolidai ni haki yako kabisa ila kwa hapa naomba unisamehe mchumba.Chukua hilo blanket ujifunike .Haya yote tutayafanya tukishafunga pingu za maisha na nadhani kwa pamoja siku hiyo hatutatamani iishe wala kupambazuke,maa
na tutainjoy sana ,hivyo Jack naomba unielewe katika hilo".Baada ya Imma kuyaongea hayo,Jack kwa hapo akaamini zaidi ya asilimia mia mbili kwamba Imma anampenda tena kwa upendo ule wa dhati,na yeye moyoni mwake akaapa hatomsaliti maishani,atampa vyote na kumriwadha kwa namna ile aipendayo.Aliny
anyuka pale kitandani akazichukua nguo zake za kuzivaa haraka haraka akamaliza na kumsogelea Imma akaenda kumkumbatia huku michirizi ya machozi ikimtoka."Imma leo hii nimeamini kama wewe ni mwanaume wa kweli na unanipenda kwa dhati,hakika upendo wako si bure na hautokufa kamwe.Hata mimi nakuahidi nitakupenda hadi mwisho wa uhai wangu hadi siku ile nitakaposhushwa kaburini,,,sitakuacha na ningekuwa na uwezo ningeomba hata kule peponi tukifa tukaoane na mapenzi yetu yadumu milele na milele,leo hii nakupa rasmi moyo wangu uumiliki wewe".Alisema Jack kisha wakashikana mikono na kutoka hadi sebuleni wakaenda kukaa kwenye sofa moja,baadae kama kwenye dakika tatu hivi Jack alitoka kwenye hilo sofa akaifata keki moja aliyokuwa ameiandaa akaja nayo na kuanza kumlisha Imma.
****************************
"Hii ni ishara ya upendo wangu Imma.....mtima wangu !! Mwanaume wa ndoto zangu,nitakupa zawadi nono siku ya harusi yetu".Maneno hayo,Jack aliyatamka wakati akimalizia kumlisha ile keki Imma.Baada ya kuona ametosheka,Imma nae aliipokea ile keki akaanza kumlisha mke wake mtarajiwa Jack."Nikifa mimi mchumba kule peponi nitakungoja,kwako nimetia nanga,,,,nitakupa zawadi nono siku ya harusi yetu".Imma nae aliyaongea maneno hayo.Jioni ilipowadia,,,Jack alisimama akaagana na Imma huku akimuahidi atakuja tena siku nyingine kumsalimia wakiwa wanaingoja kwa hamu siku ya harusi yao.
"Imma namuomba Mungu akulinde,na akulinde nakupenda sana Imma.....nitakuja tena kukusalimia,nikutakie jioni njema na usiku mwema pia".Baada ya Jack kumaliza kuyatamka hayo alianza kuzipiga hatua kutoka nje ili aondoke,Imma akawa anamfuata kwa nyuma.Wakiwa nje ,Imma alimuomba amsindikize kwa maana giza nalo lilikuwa limeshaanza kutanda,Jack akakataa na kusema atafika tu hivyo Imma wala asiwaze.
"Mpenzi sasa hivi bado ni mapema sana hivyo wala usihofu nyumbani nitafika tu,saa moja sasa hivi,nitafika tu mchumba".Alisema Jack,na Imma akawa amemtakia safari njema.Laiti kama angekuwa anajua ni kipi kitamkuta mbele ya safari asingekataa kuongozana na Imma kuelekea huko nyumbani kwao huenda labda hilo lingeepukika,lakini kama tujuavyo kila jambo hapa duniani huwa linapangwa na Mungu mwenyewe japo na shetani nae huwa anapanga.Recho dada yake akiwa na wale jamaa aliamua kumngoja chemba,na katika siku hiyo kabla hakujapambazuka aliapa atahakikisha anamuondoa duniani ."Oya....kaeni chonjo,huyoo anakuja,,,akifika tu mkamateni tuondoke nae hadi porini tukamuulie huko huko,baba nitachonga nae kimpango tu".Ni maneno ambayo aliyatamka Recho wakati akiwa amejificha mafichoni na wale magaidi.Jack akazidi kulisogelea eneo hilo.
ITAENDELEA...........................................



No comments: