Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KUMI NA TANO (15).
Alipokuwa akizidi kulisogelea lile eneo....kwa mbali karibu na kona moja alionekana Minza akija kwa mwendo wa haraka haraka huku akiwa makini katika kuyapepesa macho yake.Alikuwa amemuona kwa uzuri kabisa Jack na kwa wakati huo binti huyo alikuwa akielekea nyumbani kwa Imma kumpelekea ile taarifa aliyokuwa ameiona siku ile.Kutoka pale alipokuwa amejifichia Recho pamoja na wale magaidi ulikuwa ni umbali wa kama mita sitini hivi sema tu kulikuwa na kona nyingi nyingi pamoja na makolongo ya hapa na pale.Minza baada ya kuziacha hatua arobaini nyuma alianza kutimua mbio hadi akamfikia rafiki yake Jack akamshika mkono kwa nguvu bila kumuongelesha neno lolote akawa anatimua nae mbio kurudi walipokuwa wametoka."Shiiti ,nimemuona msichana mmoja sijui ni nani amemshika mkono na wameanza kukimbia,Mr Makongoros nakutuma uwafuatilie hadi watakapotia miguu yao.....chukua na hii bastoraa!! Chomoka harakaa!!".Alitamka Recho na Mr Makongoros hakuwa na cha kupoteza,jamaa alisimama muda huo huo akaanza kuwafuata Jack na Minza na ndo kwanza kutoka eneo lake alipoanzia hadi awafikie ulikuwa ni umbali usiopungua mita sitini .Kwa upande wa Minza,binti alichezwa na machale akazunguka mara tatu mfululizo huku akiwa amemshikilia Jack akakata kwenye kona nyingine karibu na kinjia cha maji machafu ya mtaro akawa anatimua mbio kuelekea mbele.Akili ya Minza ilimpoteza kabisa Mr Makongoros kwani baada ya kuzikamilisha zile mita alishindwa aelekee wapi maana mabinti wale hakuwaona tena.Alisimama kwenye ile njia panda yenye kona nyingi nyingi akajipiga kichwani kama mara saba hivi."Kudadadeki!! Wamekimbilia wapi,ila poa nitawapata tu". Alijisemesha Mr Makongoros baadae akaanza kurudi alipokuwa ametoka yaani kuwafuata kina Recho kwani wenyewe bado walikuwa wamejificha wakisubiri mrejesho wa jamaa huyo mwenye miraba ya kutisha mwilini mwake.Sasa Mr Makongoros nae akawa amechezwa na machale akasimama na kuamua kuahirisha kuwasogelea kina Recho akageuka na kuanza kurudi tena.Alizifikia zile kona akasimama,akahesabu mara tatu akababia njia ya kupita na kwa bahati akawa amepita njia ile ile ambayo kina Minza na Jack waliipitia.Akai
nyoosha na kisha kuanza kutimua mbio kwa vishindo,aliacha kukimbia akawa anatembea,,,ali
tembea hadi akasogea zaidi na zaidi.Minza na mwenzake Jack walikuwa wamejificha sehemu moja fixed sana ambayo jamaa huyo asingewaona kiurahisi.Jamaa akawa anazipiga hatua huku akiyazungusha macho yake kulia,kushoto.....akasimama,,,pale aliposimamia na eneo lile ambalo Minza na Jack walikuwa wamejifichia ulikuwa ni umbali wa kama hatua kumi na tano hivi miguu ya mtu mzima.Minza, huyo jamaa akawa amemuona vizuri sana ."Shiiii!! Jack unamuona yule jamaa ndiye anayeiwinda roho yako".
"Ila ni kwa nini jamani? Kwani mimi nina kosa gani?" Aliuliza Jack huku mapigo yake ya moyo yakienda kasi maana bado alikuwa njia panda .
"Nitakusimulia baadae,kwa sasa tulia hapa hapa niende nikapambane na yule jamaa". Aliongea Minza baadae akamtuliza zaidi Jack akasimama kama Ninja akaitengeneza vizuri suruali yake ya kijeshi aliyokuwa akipenda kuivaa hasa kwenye majira ya jioni jioni au usiku jua likizama.Tayari kwa wakati huo mishale ya saa mbili ilikuwa imeshawadia.Minza sasa akawa ametoka pale,akaanza kutembea kwa kunyata kumsogelea yule jamaa huku akijificha ficha gizani asionekane.Mr Makongoros bado macho yake alikuwa hajayageuza nyuma....na mara hii mikononi mwake alikuwa ametoa simu sijui alikuwa akichati sijui alikuwa akifanyaje kwa hapo mimi sijui kwa kweli.Hatimaye Minza akabakiza hatua tatu amfikie,alitembea kwa mwendo ule ule akawa amebakiza hatua moja.Hakupoteza muda,aliruka sarakasi ya juu juu na alivyo mwepesi akaenda kumkanyaga Mr Makongoros shingoni upande wa nyuma,jamaa akaenda chini na six pack zake bila kipingamizi chochote kile.Minza mara hii akawa ameenda na kusimama mbele yake na hakuwa na woga,kwa kumtazama tu,binti alikuwa akiyaweza sana mambo hayo.Huku hayo yakiendelea,Jack kila kitu alikuwa akikishuhudia kwa macho yake pamoja na kwamba sehemu hiyo ya mafichoni hakusogeza miguu yake kulia ama kushoto,kusini au Kaskazini.
"Hahahaha!! Binti ina maana wewe ndiye uliyenipiga na kunifanya nidondoke chini? Ahahaha!! Ngoja nikuonyeshe kazi".Maneno hayo aliyaongea Mr Makongoros baada ya kusimama na kumuona vilivyo Minza ,Minza hakuongea bali yeye macho yake yalikuwa chini akijaribu kumsoma jamaa huyo ."Binti chagua moja nikuue au nikubake maana wewe sioni hata pa kukupigia ama unataka kuwa kama story ya Daudi kumuua Goliati?" Aliuliza Mr Makongoros,Minza hakumjibu wala nini.Binti akaanza kumsogeleza ,Mr Makongoros nae akawa anamsogelea.Wakawa wanakaribiana,,,Haraka kama kufumba na kufumbua,Minza alirudi nyuma akaruka sarakati moja akasimama.Mr Makongoros kuona hivyo alimfuata akajaribu kumkamata kwa nguvu akaambulia kukamata upepo hasira ikawaka maana kitambo sana Minza alikuwa amerukia pembeni.Sasa cha kufanya ,,,,Ili kumaliza mchezo,Mr Makongoros alichomoa bastora yake akaanza kujiandaa kumshambulia binti huyo.Alirusha risasi mbili zote zikakwepwa na Minza kwa ustadi wa hali ya juu.Minza akaona huu sasa ndo muda wa kumuondoa duniani huyo jamaa.Alianza kutambaa chini chini kama nyoka akaruka bin vuu juu juu akaenda na kutua juu ya mabega ya jamaa huyo akamkalia na kisha kuikamata kwa nguvu shingo yake,Mr Makongoros akawa anafurukuta kwa kutumia nguvu zake zote lakini wapi,,Minza alikuwa amemng'angania kama kupe .Huku hayo yakiendelea ,Recho na wenzake walianza kuhaha sehemu ile walipokuwa wamejifichia .
"Oya!! Ina maana mpaka muda huu Mr Makongoros bado hajarudi tu? Maana zimepita dakika thelasini sasa".Alitamka Recho kila mmoja akawa anamtazama bila ya kuwa na jibu maana hata wao hawakuwa wakifahamu chochote.
"Dada mimi nina oni moja,unaonaje na sisi tukianza kumfatilia Mr Makongoros kwa nyuma?" Aliuliza jamaa mmoja,Recho akakubali kwa ishara ya kutikisa kichwa,hawakuzidi kuzungumza muda huo huo walielewana kwa pamoja wakaamua kuondoka eneo hilo.Mr Makongoros alijitahidi sana kujinasua kutoka katika mikono ya binti matata Minza lakini mwisho akashindwa maana nguvu zilianza kumwishia,,,,Minza akaona hapa kazi imemalizika.Aliruka akashuka mabegani kwa Mr Makongoros akasimama nyuma yake na hapo hapo akamtandika teke moja la maana kwa nyuma,jamaa akaanguka chini kama mti wa mbuyu.Minza akamfuata na kwenda kumkanyaga shingoni akitumia laba zake nyeupe alizokuwa amezivaa akamuua muda huo huo akamuacha.Alitoka hapo mbio akamfuata Jack na kwenda kumchukua wakaondoka eneo hilo na kuanza kukimbia kusogea mbele.Recho na wale magaidi wengine nao wakawa wameifikia ile njia panda wakasimama."Tupite wapi....tupite wapii? Oya hebu tupiteni hapa".Alisema Recho wakawa wameikamata ile njia ambayo ndo aliipitia Mr Makongoros wakati akiwafuatilia kina Jack,wakakimbia ,baada ya kuziacha hatua za kutosha nyuma kwa mbele walishangaa kumuona mtu mmoja amelala na hawakuweza kumtambua kwa maana giza nalo lilikuwa limeshatamalaki kila mahali.Walimsogelea huyo mtu wakawa wamemfikia.
"Haa!! Huyu si ndiye Mr Makongoros?" Aliuliza Recho huku akiwa ameshaanza kuchanganyikiwa maana alimtambua vilivyo."Ndiye yeye".Alijibu jamaa mmoja aliyekuwa amechuchumaa kunako upande wa kulia wa msichana huyo."Nani amemuua,nani amemuua?" Aliuliza Recho,magaidi wakakosa jibu la kumpa,,,Walimbe
ba Mr Makongoros huku wakiwa wamechanganyiki
wa wakaghaili kuwafuatia kina Recho wakaanza kurudi kule walikotoka.
Hivyo Minza akawa amemuokoa Jack na kumrudisha moja kwa moja hadi nyumbani kwao.Kabla hajaondoka,Jack alimsihi amweleze ni kipi kilitokea maana bado alikuwa njia panda haelewi chochote."Minza niambie basi ujue sielewi ina maana yule alikuwa anataka kuniuwa kwa kosa lipi nililolifanya ?" Aliuliza Jack."Nitakuamb
ia siku nyingine Jack,kwa sasa ingia tu ndani maana giza linazidi na usiku unazidi kuwa mrefu".Alisema Minza ikambidi Jack akubali tu kuingia japo bado alikuwa gizani hajui ni nini kinaendelea.Minza alimsubiria mpaka alipozama ndani ndipo na yeye akaondoka.......Usiku huo huo,Recho alirudi nyumbani kwao akiwa na ghadhabu ya hali ya juu na hakuongea na mtu alikuwa kimya tu na isitoshe alipitiliza moja kwa moja chumbani kwake kwenda kulala.Recho hakuelewa wala hakutambua ni nani ambaye alijitokeza akamuokoa Jack na kumpotezea lengo lake ambalo alikuwa amelipanga.
************************************
Zilipita siku mbili mfululizo bila ya Recho kuzungumza neno lolote la Shari wala shwari na mdogo wake Jack,walikuwa wakiangaliana tu.Siku hiyo ya pili yake ilikuwa ni ya juma tano,Baada ya Jack kukeleka kukaa pale kwao kutokana na uwepo wa dada yake Recho maana walikuwa hawaangaliani vizuri,kila mmoja alikuwa kivyake vyake tu,hivyo Jack aliondoka mchana huo huo akaenda nyumbani kwa kina Imma yaani kule ambako alikuwa akiishi Wanjera.Alishinda huko mpaka giza likaingia na Wanjera akaanza kuandaa chakula cha usiku kama ilivyo ada.Aliandaa akamaliza,akiwa anajiandaa kuanza kupakua kuna wazo lilimuijia "Huyu binti nae ni mnafiki,tu.....kuna haja na yeye ya kumuua kama ambavyo nilimuua mama". Alijiongelesha Wanjera,wakati akiwa jikoni na punde si punde akayaangaza macho yake kulia na kukichukua kijimfuko kimoja cha sumu ya kufisha!! ambacho alikuwa amekinunua kwa mara nyingine baada ya kile cha awali kuibiwa, Akakiweka juu ya kinu kidogo akatoka nje haraka kufuata zile sahani zake,,,alifika sebuleni akamkuta Jack amekaa ametulia zake bila kujua ni jambo lipi linapangwa na Wanjera kwa kipindi hicho."Wifi ngoja nikakupakulie chakula ule nahisi kama una njaa wifi angu".Alisema Wanjera ,Jack akakubali.Sasa kabla binti huyo hajarudi tena jikoni ...Kumbe binti matata Minza kwa muda wote ule ,wakati Wanje akijiongelesha peke yake mule jikoni yeye alikuwa amejificha karibu na kona yenye upenyo akimsikiliza.Minza akaanza kuingia kimya kimya mule jikoni kabla ya Wanje,akafika na kukichukua kile kijimfuko akaondoka nacho,akarudi tena kwenye ile kona.
ITAENDELEA......................................

No comments: