Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KUMI NA SITA (16).
Riwaya:THE TRUE LOVE.
SEHEMU YA KUMI NA SITA (16).
Alirudi kwenye hiyo kona ili aendelee kumchunguza Wanjera kwa uzuri zaidi aone ni nini atafanya,,,Minza alichuchumaa akawa makini zaidi na anachokifanya.Muda mfupi baadae alionekana Wanjera akitoka ndani ya ile nyumba kubwa huku macho yake akiyapepesa kila upande na usoni alikuwa akitabasamu kwani aliamini hiyo itakuwa ni siku nyingine tena ya kumkomesha Kaka yake Imma.Alianza kutembea kwa mwendo wa taratibu baadae haraka akawa amefanikiwa kuufikia mlango wa jiko,akasimama na kisha kujitizama mikononi kama mara mbili hivi kwa zamu akaingia rasmi ndani ya jiko ile iliyokuwa kwa nje au nje ya nyumba.Wakati anaingia hakuwa akijua kama kile kijimfuko kimeshachukuliwa yeye alijua tu kitakuwepo hivyo wala hakuwa na wasiwasi na alitambua yupo peke yake hakuna anayemuona.Ghafla akayaangaza macho na kuyaelekeza eneo lile ambalo alikuwa amekiweka kile kijimfuko,akashtuka ikambidi asimame.
"Mh? Nani?...nani amechukua kijimfuko changu tena? Au wachawi nini? Aise hapana!!". Alijisemesha na akawa hana cha kusubiri zaidi ya kuanza kukisaka kijimfuko chake,alikisaka wee lakini akaambulia patupu.Sasa wakati akiendelea kukitafuta huku jasho likimtoka usoni na makwapani,mara Minza akajitokeza na kusimama mbele ya ule mlango,,,Wanjera almanusura azimie maana alikurupushwa sana akahisi mzuka umemvamia.Minza akakaa kimya ili amtegeshee Wanjera atasema nini.... ikumbukwe tayari kile kijimfuko alikuwa nacho na hilo Wanje hakulifahamu."Dada Minza umenikurupusha,karibu dada".Alisema Wanje lakini Minza akakaa kimya pasipo kumuongelesha hadi binti huyo akashtuka na kuanza kuogopa sana."Vipi Minza mbona upo kimya kulikoni tena?" Aliuliza Wanjera,Muda huo huo Minza akakitoa kile kijimfuko na kuanza kumuonyesha ili kama atakitambua akitambue,Wanje akakitazama kwa makini sana akawa amekitambua.
"Samahani dada Minza hicho kijimfuko ni changu na humo kuna sukari nyeupe,tafadhari nakiomba maana nilichanganyikiwa baada ya kukikosa,mpaka nikajiuliza ni nani amekitwaa?" Alizungumza Wanje bila ya kujua kama Minza alimgundua na alitambua kila kitu ambacho alikuwa akitaka kukifanya.
"Sukari ? Ngoja niingie humo humo tuzungumze vizuri".Alisema Minza,akawa anazipiga hatua kuingia ndani ya jiko akafika na kusimama wala hakuwa na muda wa kusema akae."Umesema hiki kijimfuko kina sukari ndani yake au masikio yangu yamenidanganya?" Aliuliza Minza,Wanje akabadiri gia angani."Hapana nimesema hicho kijimfuko kina chumvi ndani yake wala si sukari hapa dada utakuwa umesikia vibaya".Alitamka Wanje,Minza akacheka sana mara hii akimkazia macho usoni,binti huyu alikuwa strong kotekote,ukimuijia kwa kumchamba nae ni mchambaji tena moto wa kuotea mbali na ukimuijia kwa ugomvi hapo ndo balaa kwani alikuwa akipiga hata kisichopigika."Sawa nimekuelewa,kama hii ndo chumvi basi usiku wa leo utakuwa wa kwanza kuionja kwa kuiweka kwenye chakula chako ambacho utakitumia".Man
eno hayo yalimchanganya mno Wanje akatambua kwa vyovyote vile siri imeshafichuka,,, Alishindwa ajieleze vipi ili Minza amuelewe ,binti akaanza kutetemeka tu mithili ya mtu aliyemwagiwa maji ya barafu."Hapana dada,hiyo siyo chumvi ni dawa inayotibu magonjwa ya tumbo".Aliropoka Wanje huku mikono yake yote ikitetemeka.
"Hujanishawishi bibie!! Dawa ya tumbo,mara hii ni sukari mara hoo hii siyo sukari hii ni chumvi,kwa taarifa yako kila kitu ambacho ulikuwa ukikipanga nilikisikia,ulikuwa na mpango wa kumuwekea sumu Jack aliyemo mule ndani,sasa una kipi cha kuniambia?" Aliuliza Minza,maneno yale yakasikika hadi ndani.....Jack akatoka haraka na alipofika akamkuta Minza akashangaa sana maana alijiuliza pale amefika saa ngapi au amefika muda gani,swali hilo akaliweka kapuni ."Vipi kuna nini hapa?" Aliuliza Jack huku akijisogeza hadi ndani."Tazama hiki kitu Jack,huyu wifi yako hata siku moja hakutakii mema.....kuna mpango alikuwa akiupanga ili Usiku huu wa leo akuondoe duniani,hiki kijimfuko kina sumu ndani yake na hii sumu ndiyo ambayo ilitumika kumuulia mama mkwe wako ambaye ni mama Imma,,sasa nimembamba harafu anajiropokea tu,eti humu kuna sukari,mara humu kuna chumvi mara hoo humu kuna dawa inayotibu magonjwa ya tumbo.Nakuambia huyu dada siyo mtu mzuri na hakutakii mema wewe pamoja na mpenzi wako Imma".Alisema Minza,Jack akacharuka mpaka akajishika kichwani kwa huzuni .
"Wifi kwa nini huna fadhira? Kwa nini hufadhiriki wifi? Unataka kuniuwa wifi kwa kosa gani ambalo nimelifanya,au ni kitu gani kilicho kibaya ambacho nimekitenda kwako? Au kukuombea msamaha kwa Kaka yako hilo ndo kosa nililolifanya? Basi wifi kwa sasa mimi nachukua maji kabisa,nanawa".Alisema Jack na bila kupoteza muda akarudi ndani.Baada ya Jack kurudi ndani....Minza alitoa simu yake akampigia Imma haraka iwezekanavyo.
"Haloo shemu,nakuomba mara Moja uje huku nyumbani kwenu.....jiwe ulilolithamini leo hii linataka kuumwaga unga wako,njoo haraka shemeji ".Alitamka Minza baadae akakata simu na kukaa kabisa pale mlangoni akiwa na suruali yake ile ile ya kijeshi.Zilipita dakika kumi na saba na sekunde kadhaa,Imma akawa amewasiri eneo lile akiwa na gari yake.....akafika na kisha kuipaki pembeni akashuka na kuanza kuzipiga hatua huku akiita"shemeji..... Shemeji!!".Aliita Imma,Minza akajitokeza na kuitika "Abe shemeji nipo huku ".Imma akamuona kwa pamoja wakaongozana hadi jikoni.
Kunako upande mwingine alionekana Recho akitembea haraka haraka kwenda nyumbani kwa kina Jane usiku ule ule wa saa mbili na robo tena akiwa kwa miguu maana aliona haina haja ya kutumia gari ni kujichosha tu.Alitembea akawa amefika akawakuta wazazi wake na Jane huko akawasalimia na baadae akawaulizia kuhusu Jane."Binti ,,huyo Jane,hebu sogea kwenye ule mlango maana humo ndimo huwa analala".Baba Jane aliyaongea hayo baada ya Recho kuuliza.Recho hakujibu chochote alinyoosha hadi kwenye ule mlango akawa amefika na kuanza kuugonga...kama kwenye dakika mbili hivi,mlango huo ulifunguliwa na aliyeonekana akitoka ni Jane mwenyewe na mkononi yaani kwenye mkono wake wa kulia alikuwa ameshikilia counter book kuashiria kwamba alikuwa akijisomea."Karibu dada Recho,karibu ndani ".Alisema Jane na Recho akaingia moja kwa moja humo ndani.Alikaa kitandani akawaza kitu baadae akajisachi na kuchomoa noti zenye thamani ya shilingi laki tano akazinyoosha kumpa Jane.
"Za nini hizi dada Recho?" Aliuliza Jane maana hakujua ni kwa nini ama sababu ipi ilimfanya Recho hadi akaamua kumpa zile pesa."We chukua tu wala usiogope".Alisema Recho,Jane akawa anasita sita baadae akazipokea zile pesa."Sasa nisikilize Jane,nataka nikutume ikiwezekana kesho ukaongee na Jack umshawishi hadi akubali uje nae hapa kwenu". Aliongea Recho akatulia na kuanza kujisachi akachomoa kijimfuko cheusi kama kile cha Rambo."Humu kuna sumu inaitwa methacholine huwa inakuaga na muonekano wa unga mweupe ila ina kazi moja tu ya kukatakata maini yote tumboni ndani ya dakika moja,,,sasa utaichukua hii harafu, halafu ukija na Jack hapa hakikisha unamwekea kwenye kinywaji chochote,ukifanikiwa kwa hilo nitakupa zaidi ya billion moja pamoja na kukununulia gari nzuri ya kutembelea". Aliongea Recho,Jane akakataa.
"Kama ni hivyo dada,hiyo kazi mimi siiwezi,mimi siyo muuaji dada!! Chukua tu hizi pesa zako na hiyo billion yako baki nayo tu.....siwezi kuishi kwa raha duniani halafu nikawe makuti ya kuchomelea moto jehanamu,baki nazo tu hizo pesa zako,na ninadhani humu ndani tayari umeshapoteza sifa ya kukaa,kama vipi simama tu dada angu uondoke".Alisema Jane akamrudishia zile pesa zake,Recho akazipokea akamtazama sana binti huyo.
"Mdogo wangu kwenye hii dunia ni pesa na pesa ni dunia.....Sasa kwa mtindo huu wa kizwazwa ulio nao hakika utakufa masikini".Alisema Recho mara hii zile pesa akizirudishia mfukoni."Acha niwe zwazwa au nife maskini nikaipate neema akhera kuliko kuwa na pesa za damu zitakazonipeleka jehanamu,,,dada we nenda tu". Aliongea Jane,Recho akatoka na kuanza kuondoka eneo hilo.Wakati akitembea mara simu yake ya mkononi ikaanza kuita.. .haraka Recho akaitoa mfukoni akaitazama na juu ya kioo cha simu hiyo akaona jina la Mr Makalai,akajua hapa kuna cha maana,kwa maana huyu Mr Makalai alikuwa ni miongoni mwa wale Magaidi waliokuwa wakimuwinda Jack wamuue,hivyo bila kujihoji aliipokea hapo hapo.
"Boss fanya haraka.....wahi kwenye nyumba moja yenye rangi ya kaki pamoja na michirizi ya ya bluu yule binti yumo humo tumemchunguza kwa kutumia darubini yetu ile ya kivita ambayo tuliinunua siku ile".Maneno hayo yalisikika na kumfanya Recho aanze kuchomoka kama mwendawazimu kuelekea huko,ile nyumba kwa hayo maelezo tu alikuwa ameitambua vilivyo kama nyumba hiyo ndo kwa kina Imma.Alikimbia akawa ameanza kuyakaribia maeneo hayo.....kwa mbali karibu na barabara moja pana linalopakana na ile nyumba aliiona gari ya kina Mr Makalai imepakiwa,huku Makalai na wenzake saba wakiwa wamesimama kwa kuiegemea gari ile wakiwa na makoti yao marefu.Recho aliwasogelea hapo akawa amewafikia.
*********************************
"Nipatie bastora mbili,hatuna muda wa kupoteza hapa".Alisema Recho,Mr Makalai akampatia zile bastora wakaanza kutembelea kwa kujificha ficha huku wakiwa na lengo la kuanza kwanza kwa kulizingira jumba lote lile kimya kimya bila mtu kuwashtukia.Kwa upande wa Wanje baada ya kuhojiwa maswali magumu alichoka akachomoka kama risasi mule jikoni ili akimbie,kwa bahati wakati akikimbia alikimbilia eneo lile lile ambalo Recho na wale magaidi walikuwa wamejifichia.
"Nani yule...nani yulee? Just shut her".Alisema Mr Makalai,Recho akamwahi na kumkataza maana huyo binti alimfahamu kuwa ni Wanjera na wapo kundi moja,,,hivyo alisimama kimya kimya na kuanza kumfuata haraka Wanje akamfikia na kumshika."Shiiii! Wanje mimi Recho,tafadhari usipige kelele".Alisema Recho,Wanje akashusha pumzi,nao wakawa wanasogea kwa wale magaidi wenye siraha kali za moto ,walisogea hatimaye wakawa wamefika hapo."Tena dada Recho,Jack yupo humu humu,Minza yule mnafiki pamoja na Imma,naomba kama inawezekana wote wauwawe".Alisema Wanje,,,Recho akasema "Imma siwezi kumuua,mimi nataka huyu Jack ndo auawe".Alimaliza wakawa wametulia.
ITAENDELEA.................................................

No comments: