Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KUMI NA SABA (17).





Riwaya:THE TRUE LOVE.

SEHEMU YA KUMI NA SABA (17).
Walitulia tuli pale mafichoni na kwa maana hiyo tayari Wanjera nae alikuwa ameshajiunga moja kwa moja na kundi hilo la kigaidi akiwa na dada Jack yaani Recho.Walikuwa bize katika kuyaangaza macho yao huku na huko,na waliambizana hakuna kupiga kelele zaidi ya kubaki kimya na vitendo vitumike zaidi kuliko maneno.Baadae Mr Makalai ile hali akairidhia akaona ni muda sasa wa kuanza kulizingira lile jumba haraka iwezekanavyo.Kwa kuwa pale jumla yao walikuwa saba ukijumlisha Recho na Wanje inakuwa tisa,walianza kusimama mmoja baada ya mwingine maana wakati wakiwa pale mafichoni walikuwa wamechuchumaa.Alianza Mr Makalai mwenyewe na wa mwisho akawa ni Wanjera na kwa kipindi hicho hata yeye tayari alikuwa amekabidhiwa bastora .Kimya kimya jumba lote wakawa wamemaliza kulizingira,,,s
iraha zao wakaziweka sawa !!.Huku hayo yakiendelea,Imma,Minza pamoja na Jack wao walikuwa ndani ya jumba hilo hilo maana kitambo walitoka kule jikoni baada ya Wanjera kutimua mbio.Ghafla Minza akachezwa na machale akatambua kwa hapa mambo yameshaanza kuharibika,aliyazungusha macho yake juu juu baadae akasimama na kuanza kwa kuwasihi Imma na Jack waingie ndani ya chumba kimoja kilichokuwepo kunako upande wa kulia wa ile sebule.....Imma na Jack wakawa wanatapa tapa tu kwani wao walikuwa gizani kabisa na hawakuwa wakifahamu chochote kile ,siri yote ilikuwa ndani ya binti machachali Minza......binti mwenye akili za ziada kuwahi kutokea chini ya mbingu.
"Mbona kama sielewi shemeji kwani kuna nini?" Aliuliza Imma mara hii aking'aa ng'aa macho.Minza akamshika juu ya lipsi zake."Shemeji jambo usilolijua ni kama usiku wa giza,kuna maadui wengi sana wanawawinda bila ya nyinyi kujua!!! Wengine ni ndugu zenu wa karibu,ukweli wote nitawaambieni baadae".Alisema Minza,ikawabidi Imma na mpenzi wake Jack wasimame kuanza kuondoka pale sebuleni ili waingie ndani ya kile chumba.Waliingia,,Minza akachukua kufuli moja na kisha kukifunga kile chumba.Alipomaliza kukifunga alianza kuzipiga hatua za mwendo wa kunyata kuusogelea mlango wa sebuleni,mlango wa kutokea nje.Aliufikia akawa anaufungua kwa umakini wa hali ya juu,ukafunguka akaunyoosha mguu wake wa kulia ili atoke nje,,,,tayari binti alikuwa amefahamu fika kwamba huko nje kuna hatari,,maadui wametamalaki kila mahali.Sasa ile anaunyanyua tu huo mguu wake vishindo vikasikika."Simama hapo ulipo,ukidhubutu kutembea tu hata kuweweseka tuna kunyofoa kichwa".Mr Makalai alizungumza,na magaidi wote wakaanza kukusanyika mbele ya Minza wakiwa na siraha zao.Minza yeye alikuwa mikono tu lakini moto wake si wa kitoto!! Ukisikia komandoo asilia wa kike ndo huyu sasa mbali na kwamba ana miaka kumi na tisa tu.Kwa kumwangalia alivyo hasa mwili wake hata kidogo usingeamini kama anauwezo hata ule wa kumuua nyoka."Kwani nyie ni kina nani na hapa mmekuja kufanya nini?" Aliuliza Minza,Mr Makalai akacheka sana,,,wakati akicheka kumbe ile sauti Recho aliitambua na akamtambua msichana huyo kuwa ni Minza hivyo kutoka pale alipokuwa amesimamia aliamua kusogea hadi kwa Minza akawa amefanikiwa kumfikia na akisha kumfikia alisimama mbele yake.
"Kumbe yale maneno niliyokuwa nikiambiwa na watu kwamba wewe ni mnafiki,muongo na mmbeya kumbe ni ya kweli ee!! Bila shaka wewe ndo unayenicheleweshea mipango yangu....Sasa leo huu ndo utakuwa mwisho wako!! Siku zote dawa ya mnafiki ni kumripua tu maana ukimuacha atakuripua yeye".Alisema Recho kisha akarudi kinyume nyume hadi pale alipokuwa ametokea.Kwa upande wa Wanjera huo muda ulikuwa ni wa full vicheko tu "Hahahahaha!! Ahahahahaha!! Si unajifanyaga panya,unatawala pindi paka akiwa matembezini,onyesha sasa jeuri yako Mpumbavu mkubwa wewe". Aliongea Wanje,Minza akabaki kimya kwa muda huo.....alibaki kimya kama dakika tano hivi,baadae akasema.
"Mimi sinaga maneno mengi kwenye vipindi vitukufu kama hivi.....najua mnamtafuta Jack,Ila niwaambie tu ukweli,Jack yupo na Imma yupo humu humu ndani ya hili jumba mtamchukua endapo mtafanikiwa kunishinda". Aliongea kwa kujiamini sana Minza kitendo ambacho kilipelekea magaidi wote waanze kucheka pamoja na kina Recho .
"Ahahahahaha!! Mr Makalai huyu binti anaongea nini sasa? Au hot ya sex imemkamata hadi kwenye ubongo? Yaani anazungumza utadhani anaongea na kina Malaya wenzake!! Watu kama sisi anaupatia wapi ujasiri wa kuyaongea hayo mbele yetu,watu wenye PhD za ugaidi?".Hayo aliyaongea jamaa mmoja mwenye ndevu za mduara huku akimalizia kwa kucheka kicheko cha dharau maana Minza walimchukulia poa.
"Mr Ndundukiro,nadhani huyu binti alambwe mtama mmoja tu kisha akaning'inizwe juu ya ule mti,ili tuingie moja kwa moja humu ndani tuwachomoe hao watu,mmoja tumuue na mwingine tuondoke nae".Alisema Mr Makalai,Mr Ndundukiro ndo akawa wa kwanza kumfuata Minza ili akayatekeleze hayo bila kukawia.Wakati akianza kumsogelea.....Minza nae alianza kusogea sogea nyuma,Mr Ndundukiro akaongeza kasi ya kumsogelea,Minza akasimama.Na jamaa huyo akawa amemfikia!! Mr Ndundukiro alijaribu kumshika Minza akaishia kushika upepo maana binti tayari alikuwa amesogea kidogo tu upande wa kushoto akatulia zake.Kwa hasira Mr Ndundukiro alirusha teke ,Minza akalidaka na bin vuu akamkamata hadi kwenye zile pukuchu zake mbili akazifanyia kitu kibaya sana kisha akamtandika teke moja la maana,jamaa akadondoka umbali wa mita tano akaanza kulia tu huku akijishika kwa uchungu katikati ya mapaja yake hayo,na akiamka hapo basi atakuwa mwanaume.
"Mr Ndundukiro kulikoni tena? Huyu binti mdogo amekupiga,acha masihara jamaa angu!!". Aliongea jamaa mwingine aliyekuwa akijulikana kwa jina la Mr Mtacha!!.Maneno yale yalimkera sana Mr Ndundukiro wakati akiuguzia maumivu yake pale chini hapo hapo akachomoa bastora yake na kumtandika risasi tano mfululizo za kifuani Mr Mtacha akaanguka na kufa hapo hapo.Alishtuka Mr Makalai hasira ikawaka juu yake akaamua kumfuata kwa kasi Mr Ndundukiro pale chini akatoa SMG yake na kumteketeza muda huo huo bila kungoja.Magaidi wakawa wanafarakana wao kwa wao,,,, kitendo kile kiliwafanya washindwe kuifanya kazi yao iliyowapeleka pale wakaondoka magaidi wanne wakatokomea zao ,,eneo lile akabaki Mr Makalai pamoja na kina Recho.
********************************
Ndani ya kile chumba alionekana Imma na Jack wakiwa wamekaa kitandani wakitetemeka tu kwani ile milio ya risasi waliisikia vizuri mno na bila kipingamizi chochote wakajua huenda Minza tayari ameshauliwa,hivyo hofu juu yao ikawa kubwa kupita maelezo.Alisimama Imma kwa ushujaa akajiandaa kutoka....Jack akamvuta na kumrudishia pale kitandani akawa anambusu na kumriwadha hatimaye Imma akatulia.
"Baby!! Mpenzi wangu Imma bila shaka tukitoka salama humu inatakiwa haya majumba uyauze tu tukaishi kwa amani kwingine na ikiwezekana tukishafunga pingu za maisha tuuhame huu mji tukaishi mji mwingine maana najua rafiki yangu Minza wameshamuua". Aliongea Jack kwa uchungu sana huku akijua fika Minza ameshauawa tu.
"Nitafanya hivyo Jack wangu ila....ila nimeumia sana,bora Minza angebaki humu humu". Aliongea Imma baadae wakaacha kuzungumza wakakaa kimya.Huku nje baada ya wale magaidi kuondoka na kubakiwa na gaidi mmoja Mr Makalai na ile miili ya magaidi wengine wawili.Hasira iliwaka kwa Mr Makalai akazipakata SMG mbili,moja upande wa kulia na nyingine upande wa kushoto akaanza kumfuata Minza maana alitambua huyo ndiye aliyevuruga kila kitu hivyo akaona ni bora ammalize hapo hapo.
"We malaya umetuharibia mipango yetu hivyo naanza na wewe kabla ya yule aliyemo ndani".Alisema Mr Makalai!! Kisha akaanza kuziseti kwa pamoja siraha zake hizo."Sa...?" Alitaka aseme sali kwa mara ya mwisho lakini akashindwa kwani Minza aliruka sarakasi tatu mfululizo za juu juu akaenda na kutua nyuma ya mabega yake na kuyakalia akazipangua SMG ,zote zikadondoka chini,,,,akampiga na kiwiko cha kichwani......mawenge yakamkamata Mr Makalai!! .Minza aliruka kulia akatua na kusimama akimuacha Mr Makalai akiweweseka huku akiwa amekishika kichwa chake.Akawa anamngoja amfuate,,,Alichomoka Recho kumfuata Minza akafika na kujaribu kumsogelea msichana huyo kwa lengo la kumshambulia ,,,kabla hajafanya chochote kumbe Wanjera huku nyuma aliinyoosha ile bastora kwa lengo la kumpiga Minza,,,purukushani za hapa na pale mara Wanje akaruhusu risasi.....risasi ikatembea na kuja kutua moja kwa moja shingoni kwa Recho,binti huyo akadondoka chini na kuanza kuruka ruka chini kwa chini kama kuku aliyemaliza kuchinjwa,Wanjera kuona hivyo ile bastora aliinyoosha kunako upande mmoja wa kichwa chake akajipiga risasi.....ubongo ukatoka nae akaanguka na kisha kufa hapo hapo.
ITAENDELEA............................................



No comments: