Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KUMI NA NANE (18).




Riwaya:THE TRUE LOVE.

SEHEMU YA KUMI NA NANE (18).
Kifo cha binti huyo kilikuwa ni kibaya sana,ukimtazama mara Moja huwezi rudia tena kumtazama kwa mara ya pili,,,kichwa chake chote kuanzia usoni hadi kisogoni kilikuwa hakitamaniki.Minza aliyaangaza macho akawa anamtazama Mr Makalai baadae akaamua kumsogelea,alipomsogelea,jamaa huyo sijui nguvu alizipatia wapi kwani jamaa alitimua mbio akawa ametokomea gizani na hakuweza kurudi tena.Minza akasimama akatikisha kichwa kama mara mbili hivi ,na akisha kumaliza aliufuata mwili wa Wanjera pale chini akafanikiwa kuufikia nae akajishika kiunoni akitumia mikono yake miwili."Ndo malipo yako haya dada,ukizoea kuuwa wenzako basi jua na wewe utakufa tena kwa kifo kama hiki,,,nenda kapumzike mwanao tuachie tutamlea sisi".Alisema Minza akatoka hapo na kisha kumsogelea na Recho aliyekuwa akiendelea kujirusha rusha kama hatua za mwisho mwisho kabla hajakata roho.Alimfikia akasimama kwa mtindo wake ule ule wa kujishika kiunoni maana alikuwa amezoea."Dada Recho ,mapenzi katika hii dunia hayalazimishwi,waache wanao pendana wayajenge....kama huna bahati ya kupendwa basi muombe tu Mungu na si kutumia nguvu za pesa au za mwili kulazimisha kitu kisichowezekana".Akisha kumaliza kuyazungumza hayo maneno Minza,Recho alitulia tuli akawa amefariki huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu kila mahali.Alitikisa kichwa Minza kwa mara nyingine kisha akatoka mbele ya mwili wa Recho akakazana kuzipiga hatua kuelekea ndani ya lile jumba.Alipoziacha zipatazo hatua sita na kidogo aliingia humo ndani akaenda moja kwa moja hadi kunako ule mlango wa kile chumba ambacho alikuwa amewaweka kina Imma na mpenzi wake Jack.Alichukua ufunguo aliokuwa ameuficha sehemu akalifungua lile kufuli na kisha kumalizia kwa kuufungua mlango wenyewe .
"Shemeji Vita imemalizika nawaomba muwe na amani".Alisema Minza,Imma akashtuka na Jack nae akashtuka maana walijua Minza ameshauawa yaani ameuliwa .Walitoka haraka ndani ya kile chumba wakaja sebuleni na kwa pamoja wakamkumbatia Minza huku machozi ya furaha yakiwatoka.
"Minza mimi nilijua umekufa rafiki yangu,kumbe bado upo hai?" Aliuliza Jack huku akimtazama Minza zaidi ya mara tatu tatu usoni kuona kama ni yeye ama laa."Sijafa Jack,maana Mungu amekuja mwenyewe na kupigana zidi ya maadui wenu pia akaniokoa na mimi.Shemeji,dada yako yupo huko nje amekufa kwa kujipiga risasi mwenyewe baada ya kumpiga Recho risasi ya shingoni kwa bahati mbaya,,,Recho imekuwa kama amepigwa na Mungu kwani alikuwa ndo adui namba moja wa Jack mke wako mtarajiwa,mengine nitayazungumza baadae,twendeni mkawaone huko nje ". Aliongea Minza,gia ikabadirikia angani,Imma na Recho wakawa wanatetemeka tu huku taarifa ile wakiitafsiri kama ndoto ya alinacha ndani ya usiku mrefu wa giza.Jack alijikaza kaza kidogo tu mwisho machozi yakawa yanamtoka asiamini kama dada yake Recho amekufa mbali na kwamba alikuwa ni adui yake namba moja.Minza aliongoza wakati wakitoka nje huku Imma na Jack wakimfuata kwa nyuma hadi nje.Minza aliufuata mwili wa Wanje akaubeba na kuusogeza karibu kabisa na kina Imma."Huuu!! Huuu!! Wanje..Wanje....Wa?" Alitetemeka Imma akawa anayatamka hayo maneno kama kichaa vile lakini kulia hakulia alikuwa amejikaza sana,na kifo cha dada yake hakikumuuma kama ambavyo kifo cha mama yake kilimuuma.Baadae Minza aliufuata na mwili wa Recho uliokuwa umelala umbali wa mita saba kutoka eneo lile walilokuwa wamesimamia kina Imma akaufikia na kuubeba akauleta mbele yao.
"Huyu ndo dada Recho ama naota?" Aliuliza Jack,Minza akamkazia macho,kabla hajamjibu alimtuliza kwanza maana yeye siri yote ya Recho alikuwa akiifahamu."Ndo yeye Jack,wala usilie kwa maana kufa kwake ndo pona yako,,,,kila kitu nitakiweka hadharani ukweli mtaujua tu". Aliongea Minza,baadae Imma japo bado alikuwa akiendelea kutetemeka alipiga simu ili ije Ambulance pale iibebe ile miili ipelekwe haraka kunako hospitali ya Taifa.Gari hiyo ilikuja eneo hilo baada ya dakika thelasini kupita,Miili minne ikabebwa ikiwemo na ile ya magaidi...... Ambulance hiyo ikaondoka usiku huo huo kuelekea hospitalini ili miili ikahifadhiwe mochwari.
"Tunalala wapi Imma? Hapa au tunalala wapi?" Aliuliza Jack huku akionekana dhahiri alikuwa amechanganyikiwa.Minza hilo akaligundua akamuomba Imma amuachie yeye atamuweka sawa.Minza alimshika mkono binti huyo wakaanza kuondoka kuelekea nyumbani kwa kina Minza maana kwa Usiku huo Minza alitaka akalale na Jack ili amweke vizuri kisaikolojia.Hivyo wakaondoka na Imma akabaki peke yake asijue aisogeze wapi miguu yake,aisogeze kulia au kushoto,apande gari aondoke pale au afanye nini!! Imma hakujua akabaki njia panda.Eneo lile alilokuwa amesimamia alisimama kama nguzo ya umeme bila kupepesuka ,akafanya hivyo mpaka zikamalizika dakika nyingi ndo akaamua kuondoka hapo akaingia ndani.Usiku huo hakuondoka,alilala hadi kukapambazuka,,
,kulipopambazuka,mapema sana aliamka akamfuata mtoto wa marehemu dada yake yaani Bahati akambeba ili aondoke nae japo mtoto bado alikuwa usingizini.Baada ya kumbeba ile anatoka tu nje alikutana na umati wa watu wengi sana wakiwa wamesimama makundi makundi,ikumbukwe lile eneo lote lilikuwa limetapakaa damu,
"Ina maana huyu Daktari anafuga magaidi,,,usiku hili tukio nililishuhudia kwa macho yangu mawili!! Japo nilikuwa nimejificha,ona hii damu kuna mauaji yalitokea,,moja ya mauaji hayo ni binti mkubwa wa mfanyabiashara maarufu nchini Mr Ludovic,huyu ukweli anaujua wotee!!".Ilisikika sauti yenye ukakasi wa hali ya juu kutoka kinywani mwa kijana mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Dura.Minong'ono ikaanza kusikika na Imma akapigwa stop wakimsihi asimame hapo alipo,,,zile siraha zilizokuwa zimetapakaa chini zilikuwa ndo ushahidi tosha kabisa.
"Jamani siyo mimi,mimi si muuaji jamani". Aliongea Imma huku akimpakata vizuri mtoto Bahati."Kaa kimya kijana....wewe siyo muuaji? Na hizi siraha ni za kina nani,huyu atakuwa ni Daktari feki huyu na ni gaidi aliyejificha kwenye kivuli cha udakitari,cha msingi wapigiwe simu maaskari". Alizungumza Mzee mmoja aliyekuwa amevaa kanzu nyeusi,,,Wazo la Mzee likakubalika ikabidi wana mtaa wafanye hivyo.Binafsi Imma hakujua kama angekuwa na maadui wengi kiasi hicho,walio wengi walikuwa ni watu wake wa karibu sana na alikuwa akifurahi na kucheka nao lakini hiyo siku wote walimgeuka na kuanza kushabikia yeye ni gaidi tena muuaji.Baada ya simu kupigwa,Defender ilitia tairi eneo hilo,wakashuka maaskari na kuanza kusogea mbele.Walizikusanya siraha zote baadae Afisa mmoja akaamua kumfuata Imma,jamaa alianza kwa kumtazama kuanzia miguuni hadi juu ya kichwa chake.
"Kila siku tunahangaika kuwatafuta magaidi wa hii nchi tusiwaone kumbe mpo mnatuinjoy mmejificha kama hampo!! Kijana hizo pesa za mshahara wako hazitoshi ukaona uwe mkuu wa magaidi sivyo?". Alizungumza Afisa huyo kisha akaanza kurudi rudi nyuma bila kumruhusu Imma aongee au azungumze neno lolote lile...Imma akazidi kuchanganyikiwa maana kile kiwango chake cha kutetemeka kiliongezeka maradufu.Mr Ludovic nae alipigiwa akaambiwa kila kitu.
Mr Ludovic alikuja baada ya dakika arobaini na tano kupita akaambiwa Imma ameshirikiana na magaidi na usiku wa kuamkia hiyo siku amemuua mwanae mkubwa Recho.Mr Ludovic hakuamini alijikuta akilia kwa sauti ya juu kama mtoto mdogo,asiamini kabisa.
"Imma?.....Imma,yaani baada ya kukupa binti yangu Jack,uthamani wa binti yangu Recho ukautoa kabisa moyoni mwako!! Nikupe nini Imma nikupe nini!!" Alilia Mr Ludovic,Imma akajaribu kujitetea ikashindikana.Wale maaskari walimkamata akiwa na mtoto Bahati wakamweka ndani ya ile Defender.
Safari ikaanza......walielekea hospitalini kwanza kujiridhisha na kauli za kijana Dura alizokuwa akizitoa kwamba Imma kwa kushirikiana na magaidi wamemuua Recho pamoja na dada yake Wanjera na kisha kuwapeleka hospitalini kimya kimya usiku huo huo.Mr Ludovic nae akawa kwenye huo msafara.
Walifika hospitalini,na kweli baada ya kuelekea kwenye ile Mochwari waliikuta miili ya wale mabinti na kila mmoja akaamini Imma ni gaidi na hilo tukio amelifanya yeye hakuna ambaye hakuamini ukizingatia kila kitu kilitendeka nyumbani kwao.Maafisa mbali mbali walijurishwa na hizo taarifa zikamfikia hadi Rais wa nchi.Kila kona habari zikawa ni Daktari auwa dada yake,auwa binti wa mfanyabiashara maarufu kisa pesa.Siku hiyo hiyo Imma akasimamishwa kazi na ikabidi apelekwe sello siku hiyo hiyo ili baadae asomewe mashtaka.Sasa kabla hajafikishwa huko ,Mr Ludovic alimfuata Afisa mmoja akatoka nae pembeni na kuanza kuteta jambo.
"Unasikia,huyu kijana kumbe hafai....cha msingi naomba akishahukumiwa ahukumiwe kunyongwa maana tayari ameshautonesha moyo wangu,nilijua ni kijana mwema kumbe shetani? Fanya hima Afisa niko tayari kutumia hata Billion moja ili tu huyo kijana anyongwe". Aliyaongea maneno hayo Mr Ludovic kwa sauti ya chini baadae wakatoka eneo hilo na safari ya kumpeleka Imma sello ikaanza .Huku hayo yakiendelea,machale yalimcheza Minza binti wa ajabu akajua Imma yupo matatizoni tena matatizo makubwa,,
"Jack!! Imma wamemkamata!! Na kwa sasa wapo njiani wanampeleka Sello ,kuna kijana mmoja nimemuona na ndiye aliyetoa siri za uongo!! Huyo niachie mimi,nitampoteza ndani ya masaa ishirini na nne". Aliongea Minza,Maneno hayo yakamshtua sana Jack,akawa anajiuliza Minza ni mtu ama jini na zile taarifa ni nani ambaye alikuwa akimpatia,ni mtu wa namna gani huyu? Alijiuliza akakosa jibu ikambidi akae kimya tu japo alikuwa akitetemeka hatari kuhusiana na taarifa hiyo ukichanganya na kile kifo cha dada yake Recho.
*****************************
Imma alifikishwa Sello na huko likaibuka kundi moja kubwa sana la vijana waliokuwa wakiimba huku wakihimiza Imma afungwe haraka na idadi yao ilipata vijana kama hamsini hivi hatari sana!!.Kabla hajapelekwa rasmi Sello,watu wengi walikusanyika kwa ajili ya kulishuhudia tukio hilo ambalo waliamini ndo litakuwa ni la kihistoria.Tayari Jack na Minza nao walienda huko....Jack akawa analia tu
"Jamani naomba mmuachie Imma wanguuu!! Muachieni Imma wangu!! Amewakosea nini?" Alilia Jack baada ya kumuona Imma akiwa ametiwa pingu mikononi amevulishwa na shati kabisa.
"Afungweee!! Tunasema....na afungweee!! Ni gaidiii....ni gaidiii !!".Wale vijana huku wakikimbia kimbia kulizunguka eneo lile waliendelea kuimba kwa sauti ya kishindo.Alicho
moka Minza akaenda kumbeba mtoto Bahati akaja nae karibu na Jack aliyekuwa akiendelea kulia.Imma muda huo huo akashikiliwa na kuanza kuburuzwa kama gunia kupelekwa Sello.Watu eneo hilo baada ya Imma kupelekwa huko walianza kuangua vicheko.
"Alikuwa akijiona,eti Daktari mkuu wa hospitali ya Taifa,sasa wacha tuone Hahahaha!! Siye macho yetu tu"....."Acha kabisa shoga angu,hata kusalimia kijana alikuwa hasalimii,akipita na gari yake ni mwendo wa kuwarushia matope tu kama siyo vumbi".Sauti za wanawake wawili zilisikika zikiyaongea hayo."Jamani Imma,naomba mmuachie Imma wanguuu!!" Aliendelea kulalamika Jack kwenye huo umati mkubwa wa watu,Minza akamtuliza huku akimvuta kwa kutumia mkono wake wa kulia."Nyamaza Jack,naomba tuondoke,,Hili niachie mimi....na unipe siku tatu tu". Aliongea Minza huku akimbebe vizuri mtoto Bahati.
ITAENDELEA..........................................




No comments: