Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA KWANZA (01)...
We
Riwaya:THE TRUE LOVE.
SEHEMU YA KWANZA (01)...
"Riwaya ya The True love ni moja ya simulizi pendwa zinazovuma sana duniani hususani katika maisha halisia ya wanadamu kwani huwa zinaongoza kwa kupendwa na wengi na husomwa na maelfu ya watu kutoka pande mbali mbali za dunia.Katika Riwaya hii tutamuona kijana mmoja mpole aliyepitia changamoto ngumu sana katika maisha yake......ni kijana Emma ambaye hakuwahi kuwa na bahati ya kupendwa na msichana yeyote yule tangia anapevuka na hata pale alipofanikiwa kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu katika mji wa Gilgali uliokuwa umejaliwa kuwa na wasichana wa kila aina na warembo kuliko mji wowote ule duniani.Katika majira asiyoyatarajia anabahatika kukutana na binti mmoja kigori mweupe,mrembo na mwenye umbo la kupendeza,anatokea kumpenda sana hatimaye wanaianza safari yao ya mahusiano....Mahusiano yao yanapitia misukosuko mingi sana ikiwemo Imma mwenyewe kukamatwa kwa kosa la kusingiziwa kwamba ameuwa ili hali hajafanya hivyo,anatupwa gerezani pia anafukuzwa kazi na matatizo mengine mengi ya kukatisha tamaa,,,msimamo wa binti kigori haukuteteleka alisimama na mpenzi wake katika tabu na dhiki akishirikiana na binti wa ajabu Minza rafiki yake kipenzi hatimaye anafanikiwa kuyashinda yote.Riwaya hii ni ya kubuni hivyo majina yote yatakayotumika humu hayatamlenga mtu moja kwa moja .....Basi nakuomba uungane na mimi mtunzi wako kuanzia mwanzo wa Riwaya hii hadi mwisho ili upate kujifunza mambo mengi yatakayoibadirisha tabia yako na mwenendo wako.ASANTENI".
*******************
Mnamo mishale ya asubuhi saa kumi na moja kamili alionekana kijana Emma akiamka kitandani kwake ndani ya kijumba chake cha matope....akakaa na kisha kuachia miayo akasimama na kuanza kujinyoosha kidogo ili kuuweka sawa mwili wake kwa ajili ya majukumu ya siku hiyo tulivu kabisa ya juma nne.Hakuwa na muda wa kupoteza kijana huyu katika suala zima la kuyasaka maisha akiwa anaisubiri hatima yake kama atafauru na kuendelea na masomo ama laa kwani kwa kipindi hicho tayari alikuwa kashahitimu masomo ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari ya Elinde iliyomo katika huo huo mji wao wa Gilgali.Huo ulikuwa ni mwaka wa 2009 mwezi wa pili.Basi baada ya kumaliza kujinyoosha alizipiga hatua mbili tatu akaufikia mlango na kuufungua,akatoka nje na kuanza kuyaangaza macho yake pande zote,,,hakuna cha zaidi alichokiona kwa muda huo zaidi ya kumuona tu paka wake mweupe akija mbele yake huku akimlilia kama ishara ya kumpongeza kwa kuiona tena siku hiyo mpya.Hapo nje hakusimama sana alirudi ndani akatoka kwa mara nyingine akiwa amebeba ndoo zake mbili ili awahi bustanini kule ambapo alikuwa amelima mazao mbali mbali ikiwemo zao la nyanya.Baada ya kuzichukua ndoo hizo aliona si vizuri kuondoka bila ya kuwajulia hali wazazi wake kabla hajaondoka asubuhi hiyo..... alielekea kwenye nyumba yao kubwa iliyokuwa imejengwa kwa tofali za tope na kuezekwa kwa nyasi akaifikia na kisha hapo hapo akaanza kuugonga mlango kwa utaratibu,,,aliugonga kama muda wa dakika tano hivi ukaja kufunguliwa akaonekana mama yake amesimama akawa anamtazama kwa macho ya huruma sana kijana wake huyo,Emma nae alimtazama mama yake akatabasamu hivyo hivyo pamoja na mambo mengi aliyokuwa akiyawaza kwa muda huo."Mama shikamoo?" Emma alimsalimia mamae muda huo akiitengeneza kaptura yake chakavu iliyokuwa imekaliwa na matope kila pande,mama Emma alitikisa kichwa chake kidogo kisha akamjibu na kumwambia mambo kadhaa ambayo yalimtia moyo sana kijana huyo aliyezaliwa katika maisha ya kimaskini,baadae akamuuliza kama baba yake ameshaamka au hajaamka,mamae akamjibu kwa kumwambia baba yake bado hajaamka hivyo hakuna haja ya kujisumbua kumwamsha na kama ni kumsalimia atakuja tu kumsalimia baadae .Kwa upande mwingine Emma alikuwa na dada yake aitwaye Wanje binti ambaye alikuwa akijiona sana bila ya kujua hali yao ya maisha ipoje....binti huyo katika kipindi hicho alikuwa akisoma shule ya Sekondari ya Nzansi na alikuwa kidato cha tatu .Basi kijana akamaliza kujuliana hali na mama yake akaanza kuondoka mbele yake ili aianze safari ya kuelekea shambani yaani bustanini kwake.Baada ya kuikamata njia moja iliyokuwa imezungukwa na kingo za nyasi ndefu alijikuta akikazana kutembea ili awahi haraka akaendelee na majukumu yake.Huko alifanikiwa kufika baada ya nusu saa kupita akaenda na kuanza mara Moja kazi ya kumwagilia mazao aliyokuwa akiyategemea sana.Alienda kama safari tano hivi akaja kwa ajili ya safari ya sita.Sasa ile anajiandaa tu kuanza kuchota maji ghafla aliteleza akadumbukia kisimani na kuzama muda huo huo,alipokuja kuibuka alikakamaa kwa nguvu akajishikiza kwenye mizizi ya miti pamoja na nyasi akaanza kupiga kelele kujaribu kuomba msaada maana kile kisima kilikuwa na kina kirefu sana.Alipiga sana kelele bila mafanikio baadae wakaja vijana wawili aliokuwa akifahamiana nao akawaomba kwa dhati wamsaidie lakini vijana hao kwa dharau walimcheka huku wakimdhihaki kwa kumwambia waziwazi kwamba wao hawawezi kumsaidia mtu mwenye asili ya sokwe kama yeye wakamwambia ajigange yeye mwenyewe,hivyo waliondoka wakamuacha peke yake .Emma aliendelea kujishikiza pale mpaka wakaja wababa wawili ndipo wakamsaidia na kumtoa mule kisimani,aliwashukuru sana baadae akaendelea na kazi yake hiyo mpaka jua likawa linaanza kuwa kali.Muda wa kutoka bustanini uliwadia,kijana Emma akatoka akiwa amechoka sana na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao.Alifika na kumkuta Wanje amekaa chini ya mti wa mkwaju akijitazama kwenye kioo huku akiwa amevaa kijisiketi kimoja kifupi sana ambacho hakikuwa na utofauti wowote na kimini,Emma akamsogelea ili amsalimie,alims
alimia kwa mara ya kwanza "Dada Wanje habari za mchana,sasa mbona dada yangu hujaenda shule kulikoni?" Alisalimia Imma lakini Wanje aliishia kuigeuza shingo yake kumtazama akamsonya kwa hasira na kuendelea na kazi yake ya kujipondoa."Dada si nakusalimia ina maana hunisikii?" Alirudia tena lakini Wanje hakumjibu wala kumsemesha neno lolote lile.Wanje alisimama akaondoka pale na kumuacha Kaka yake akiwa amegubikwa na mshangao wa hali ya juu.Hakujua ni nani aliyemfundisha jeuri hiyo dada yake kwani hakuwahi kumshuhudia akifanya vitu kama hivyo siku za nyuma,,,ina maana kwa hapa Imma alikuwa kama yupo gizani hakuwa akijua chochote kile kinachoendelea kwa dada yake Wanje.Alijitazama kwenye kaptura yake kisha akaondoka pale na kuanza kuelekea ndani,akaingia kwenye nyumba yao kubwa,akawa anamuita mama yake,kumbe kwa muda huo mama Imma alikuwa jikoni akiandaa chakula .Imma aliamua kumfuata huko huko ."Mama shikamoo,umeshi
ndaje?" ......"Marahaba mwanangu nimeshinda vizuri tu".Aliitikia mama Imma mara hii akionekana kama hayupo sawa pamoja na kujilazimisha kutabasamu ili kuificha huzuni yake.
*************************
"Mama yaani wewe unaandaa chakula halafu Wanje yeye amekaa tu akijipodoa? Mama huyu binti hii tabia ameitoa wapi?" Aliuliza Imma muda huu akichuchumaa,mama yake alimgeukia akawa anamtazama sana mpaka zikamalizika dakika tano nzima baadae ndo akazungumza "Acha tu mwanangu,hii ni dunia na kama hujazaa huwezi yajua haya yote".Aliongea mama Imma kwa sauti ya uchungu sana akatulia kidogo."Mdogo wako sijui amepatwa na nini tu siku hizi kwani tangia aingie kidato cha tatu mwaka huu amebadirika sana hadi nashindwa kumuelewa,kazi hataki kufanya na bila aibu huwa ananijibu kama mimi ndo mwanae".Kabla hata mama Imma hayamaliza kuzungumza mengine,Imma aliondoka akamfuata Wanje moja kwa moja akafika mlangoni na kuanza kubisha hodi,Wanje akaja kutoka baada ya dakika kumi na tano akasimama na kujishika kiunoni muda huo akicheza cheza."Hivi dada Wanje kwa nini lakini? Hivi wewe humhurumii mama? Yaani mama na uzee wake yupo jikoni anapika wewe upo upo tu bila hata aibu,na shule hujaenda kwa nini?" Aliuliza Imma ,Wanje akatabasamu kwa dharau kisha akatoka nje bila ya kumjibu neno lolote lile Kaka yake.Imma akajiuliza sijui amfuate akampige moyo wake ukasita akaamua kumuacha tu ila anachokitafuta atakipata .Sasa Wanje alitoka akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka haraka akaifikia barabara pana akanyoosha hadi nyumbani kwa kijana mmoja kutoka katika familia ya kitajiri akafika huko akaonana na kijana huyo wakakumbatiana na kupigana mabusu baadae wakapanda ndani ya gari na kuanza kutoka hapo.Safari yao ilikuwa ni ya kurudi nyumbani kwa kina Imma.Kwa upande wa kijana Imma mara hii akiwa amekaa kwenye ule mti aliona gari aina ya Range Rover ikija ikakata kona na kusimama karibu yake akashuka kijana mmoja ambaye hata kidogo hakuwa akimfahamu,kijana huyo mweupe na mwenye umbo kubwa akiwa na suti yake alisimama kibabe bila hata kumsalimia Imma akajishika kiunoni akaita "Sweet!! Sweet!! Shuka bwana".Wanje akaangua kicheko humo humo ndani ya gari na akamjibu kijana huyo "Nashuka Sweet".Hivyo binti akashuka akamsogelea yule kijana wakakumbatiana mbele ya Imma bila hata aibu....mapigo ya moyo wa Imma yalianza kwenda mbio akajaribu kusimama akashindwa ukizingatia na ule uchovu wa shamba aliokuwa nao."Sweet!! Huyu jamaa ndo Kaka yako ?" Aliuliza yule kijana huku akimtazama Imma kuanzia kwenye unyayo wa miguu yake hadi juu ya kichwa chake."Ah!! Ninaweza kusema huyu ni Kaka yangu lakini daah!! Hadi naona aibu".
"Pole sana sweet!! Unajua nini laiti kama kungekuwa na uwezekano ungemkataa huyu jamaa kwamba si Kaka yako......jamaa ana uso kama katapira la Kichina isitoshe niliposimama tu hapa nilianza kuhisi kichefuchefu maana kuna harufu furani hivi nilikuwa nikiisikia,,,kwa ufupi hufanani nae kabisa". Aliongea kwa dharau yule kijana na Wanje akamsapoti."Acha tu sweet!! Hili jamaa silipendi kama nini na sidhani kama litapata mke".
THE TRUE LOVE ITAKUJAJE KWA KIJANA EMMA

No comments: