Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA PILI (02).
Riwaya:THE TRUE LOVE.
SEHEMU YA PILI (02).
Wanjera hakuona hata aibu kuyasema maneno hayo huku akijua fika yule alikuwa ndo Kaka yake pekee tena wa damu ila maisha tu ndo yamemfanya aonekane katika hali ile.Imma kwa muda huo hakuweza kuzungumza chochote alibakia kimya tu japo moyo wake ulifura kwa uchungu pamoja na hasira isiyokuwa na kifani iliyokuwa ikimnyemelea.Alijikaza kaza kidogo tu na uvumilivu nao ukawa umemshinda.....
alinyanyuka juu akaanza kumtazama yule kijana huku akihema juu juu."Brother sikujui hunijui ila nataka nikuulize swali moja tu,huyu dada unamfahamu kama nani yako?" Aliuliza Imma huku hasira ya kiwango cha juu ikizidi kumsakama,yule kijana baada ya kuulizwa lile swali alicheka kwa dharau akatikisa kichwa chake baadae akamshika kiunoni Wanjera na kumbusu kama mara mbili hivi,kitendo hicho kilimuumiza sana Imma akashindwa kujizuia na kurusha ngumi hapo hapo.....Sasa pamoja nakuirusha hiyo ngumi kwa kutumia mkono wake wa kushoto lakini haikuwa na manufaa yoyote kwani ilidakwa na yule kijana."Baby hebu simama pembeni nimwonyeshe huyu mpuuzi" alisema kijana yule na Wanjera akakubali akamuachia kisha yeye akasogea pembeni.Kijana yule alimkamata kwa nguvu sana Imma akamsogeza kifuani kwake kisha muda huo huo akampiga ngumi ya kifuani Imma iliyomfanya aende chini moja kwa moja,Imma akiwa chini alianza kujikongoja kunyanyuka lakini yule kijana akamwahi akampiga teke la nguvu kisha akamalizia kwa kumrukia kifuani akitumia miguu yake miwili,Imma akatulia kimya."Pumbavu mimi siyo type yako" alizungumza kijana yule muda huo akijisogeza pembeni,,,kumbe mama Imma zile purukushani alizisikia vizuri wakati akiwa jikoni,mama alitoka mbio humo jikoni na mwiko wake wa ugali wa mtama akafika lile eneo la tukio huku akihema sana."Mmemfanyaje mwanangu,mmemfanyaje? Wanjera huyu kijana ni nani?" Aliongea mama Imma huku akiinama kumtazama mwanae aliyekuwa amelala chini amezimia damu zikimtoka puani na mdomoni.Alichomoa kanga yake akawa anampepea mwanae bila mafanikio,,,Wanjera na yule mpenzi wake walinong'onezana wakakazana kuingia ndani ya ile gari,wakaingia ,yule jamaa akaiwasha muda ule ule wakaondoka.Mama Imma hakujua afanye nini,alichanganyikiwa sana akawa anayageuza macho yake huku na huko,katika eneo hilo alitoka mbio hadi ndani,akaenda kuushusha mkoba wake akaanza kuusachi sana kama kutakuwa na pesa....mwisho aliishia kupata shilingi mia mbili tu ya chenchi za mia mia,alimtazama mume wake pale kitandani akamuona amejilaza huku akiwa ameyafumba macho yake,alianza kumuita lakini mumewe hakuitika akajua labda atakuwa amekamatwa na usingizi mzito.Alitoka mbio akaelekea kwa majilani kuomba msaada...... alielekea nyumbani kwa mama mmoja tajiri wa mifugo ya ng'ombe na kondoo akafika na kumuita,mama yule akatoka na kumshangaa sana."Ehe nikusaidie nini mama cha kuomba?" Mama yule alimuuliza kwa dharau sana akawa kama amempatia mama Imma kwa asilimia mia na hii ilitokana tu na umaskini aliokuwa nao na si kingine,mama Imma lile swali lilimnyong'onyesha sana akainama kidogo kisha kuanza kuzipiga hatua kuondoka mbele ya mama yule pamoja na kwamba alikuwa amedhamiria kumwambia kama kijana wake amepatwa na matatizo makubwa.Aliondoka huku mikono yake akiwa ameirudishia nyuma akawa anatembea pole pole kumfuata mwanae pale mtini.Kwa bahati nzuri wakati akisogea eneo hilo,kwa mbali alimuona Imma amekaa ,akatabasamu mama wa watu na kuanza kumkimbilia mwanae furaha yake ikiwa imerejea,baada ya kumfikia alikaa chini akamtazama kwa macho ya huruma.Alimtazama sana akaja kugundua michirizi ya machozi machoni kwa mwanae Imma,,,mama huyo aliikamata vizuri kanga yake akamsogelea zaidi na kuanza kuyapangusa machozi hayo.....Naam nani mwingine angeweza kumfariji Imma kama si mama yake pekee? Nimeyasema haya nikiwa na maanisha kijana huyo mpole hakuwa na rafiki yeyote yule na mpaka kipindi hicho cha umri wake wa miaka kumi na tisa bado hakuwahi hata siku moja kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi."Asante mama yangu,najua kama ipo ipo tu". Aliongea Imma kwa sauti ya kwikwi iliyokuwa imekaliwa na kilio hadi mama yake akashindwa kuyazuia machozi yake,machozi yalianza kumtoka na Imma akawa anayaona kwa uzuri .Kijana alijikaza akasimama akamsimamisha na mama yake wakaanza kuondoka pale kuelekea ndani wakafika ndani na kukaa juu ya vigoda vyao ."Mama ina maana baba bado amelala tu hadi muda huu?" Aliuliza Imma ,mama akiwa ametulia akamkazia macho."Ndio naona amelala ila hebu ngoja nikamwamshe ili tuje tule".Alisema mama Imma akasimama na kuingia chumbani kwenda kumwamsha baba Imma.Imma nae akatoka nje kuelekea jikoni,akatoka haraka muda huo akiwa amebeba sufuria ya ugali maana mboga ilikuwa humo humo ndani ya nyumba ,sasa ile anaingia tu alimuona mama yake akitoka chumbani huku akilia kichwa chake akiwa amekiinamisha chini,Imma akapigwa na butwaa kumuona mama yake akilia namna ile akajua huenda kuna kitu kimetokea.
Upande mwingine walionekana Wanjera na yule kijana wakiwa wamekaa kitandani wakicheka huku wakirushiana mito,akasimama Wanjera na kuanza kukisogelea kioo kimoja kikubwa akawa anajitazama sana.Yule kijana pale kitandani alibaki akichekelea tu,ndani ya kichwa chake akapata wazo ."Baby unaonaje ukivua nguo zako zote nianze kukupiga picha?" Aliuliza kijana huyo,Wanjera akatabasamu na kisha kukubali kwa ishara ya kichwa.Bila kujua kijana yule alikuwa na lengo gani kumwambia vile,Wanjera alianza kuvua nguo zake zote hadi akabaki mtupu,kijana akatoa simu yake na kuanza kumpiga picha akamaliza.Baadae zile picha akazitunza ili akishatulia ajue nini cha kufanya.Baada ya mambo hayo kumalizika walirudi kitandani wakaanza kufanya mambo yao,walifanya wakamaliza,wakatoka nje ya chumba kwenda sebuleni kupata chakula maana kijana yule pale nyumbani alikuwa na mfanyakazi wake."Wanjera,nina wazo jingine natamani ulisikie " Alisema kijana huyo,Wanjera akamtazama usoni akamruhusu alitoe wazo hilo ."Sema tu sweet,si unajua ni kwa kijinsi gani ninavyokupenda!!" Alisema Wanjera,kijana akatabasamu,akamrushia jicho furani hivi binti huyo akajikohoza kabla ya kuzungumza "Naomba uache shule nikuoe uwe mke wangu tuyaanze maisha,wewe ni mrembo sana huna haja ya kujisumbua kiasi hicho,acha shule inatosha!! Halafu kule kwenu kwenye kijumba cha mabua sijui cha makuti usikanyage tena unaniaibisha,ut
akaa hapa hapa na tutaishi pamoja,sijui umenielewa?".Ndugu msomaji kitu ambacho hukifahamu kwa kijana huyu kuna jambo alikuwa akilifanya kwa binti huyo na kama atalifanikisha basi itabaki story tu kwamba kulikuwa na binti aitwaye Wanjera.....jambo la kwanza la kumtoa bikra aliyokuwa akiitafuta kwa udi na uvumba alilifanikisha likabaki jambo moja tu.Na kijana huyo mwenye umri wa miaka thelasini alikuwa na mchumba wake ughaibuni na ndiye aliyemfanya awe katika hali ile aliyonayo,hatari sana.Wanjera yeye ndo kwanza hata miaka kumi na nane hakuwa ameifikisha kwani kwa muda wote huo alikuwa na miaka kumi na saba tu."Wewe tena yaani kwa hapo nimekuelewa sana,Sabo unajua katika hii dunia hakuna mwanaume yeyote ninayempenda kwa upendo wa dhati kama ninavyokupenda wewe!! Yaani sijielewi kabisa,kila siku kila muda nazidi kukupenda tu hivyo nipo tayari kwa lolote lile ".Kuna msemo mmoja unasema na huwa unarudiwa rudiwa sana,msemo huo unasema,jambo usilolijua ni kama usiku wa giza.....Wanjera hayo hakuwa anayajua,pesa za yule kijana ukichanganya na kumpenda kijana yule zilimvuruga sana,yaani ukisikia mtu amevurugwa na mapenzi ni huyu binti,yeye hakujali na alikuwa tayari hata kumtukana mama yake kisa anampenda Sabo.Kumbe Sabo mwenyewe alikuwa akimchora tu......Naam ngoja nikudokezee kitu kingine usichokijua.Katika ule mji wa Gilgali kijana Sabo baada ya kuanza harakati za kuyasaka maisha akiwa na umri mdogo wa miaka kumi na nane tu,marehemu baba yake enzi za uhai wake alimuachia urithi wa mali kadha wa kadha lakini akampa masharti mawili mhimu,sharti la kwanza lilikuwa ni kumuunganisha na mama mmoja wa kizungu aliyekuwa akiishi nchini Marekani,mama huyo yeye alikuwa ni tajiri sana na utajiri wake ulikuwa ni wa utata usiosomeka kirahisi na kwa kipindi hicho alikuwa na binti mdogo wa miaka kumi na miwili.Sasa katika huo mkataba ,Sabo alipaswa kila mwisho wa mwaka awasilishe titi la kushoto kwa yule mama na katika maisha yake yote asiowe mwanamke yeyote yule zaidi ya mwanae yaani yule binti......ila kuhusu kuwachezea tu hapo aliruhusiwa.Sharti la pili ili utajiri wake uendelee kukua siku hadi siku ni lazima kila mwishoni mwa mwaka atoe bikra angarau kumi kwa mabinti wadogo,wenye miaka kati ya kumi na mbili hadi kumi na saba.Na kwa muda wote ule,Sabo tayari alikuwa kashatoa bikra zaidi ya mia za mabinti tofauti tofauti na wote kati yao hakuna ambaye alipona waliishia kufa.Sasa Wanjera sijui ......Okey tuachane na hilo.....wawili hao baada ya kukubaliana waliendelea kula wakaja kumaliza ndani ya dakika ishirini hivi.Mara baada ya kumaliza kula walijiandaa watoke ili wakafurahie maisha mbele ya safari.
**************************
Kijana Imma maswali yenye mafumbo magumu na misamiati isiyoteguka ilianza kuzunguka kwa kasi ya ajabu kichwani mwake akashindwa kujua ni kwa nini mama yake analia na amepatwa na nini ama kuna kitu gani kimetokea!! Alitamani amuulize mamae apate kuujua ukweli ila moyo wake ukishirikiana na kinywa ulimsihi kwa woga asifanye hivyo .Alibaki kimya akawa anaishia kumtumbulia macho tu mama yake mpaka mama Imma mwenyewe akaamua kufunguka kuusema ukweli wa nini kimetokea.
ITAENDELEA...........................................

No comments: