Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA NANE (08).





Binti huyo ikambidi usiku huo huo aanze safari ya kwenda kwa Imma na alikuwa na mpango kabambe kichwani mwake....kubwa zaidi ambalo lilimfanya akate shauri ya kwenda huko lilikuwa ni kwenda kumtega Imma ili ikiwezekana akafanye nae mapenzi lengo lake litimie.Hakupot
eza muda,aliiendesha gari yake akawa ametoka nje ya geti la nyumba yao tayari kabisa kwa kuinyoosha barabara ile iendayo nyumbani kwa kijana Imma.Aliikamata barabara hiyo akawa anadrive kwa speed sana,baadae kama kwenye saa tatu na dakika arobaini na tano hivi yaani saa nne kasoro robo alifika nyumbani kwa Imma,akaipaki pembeni ile gari na akaanza kushuka.Alishuka akasimama pembeni akawa anajitazama kwenye viganja vya mikono yake.Aliyaangaza macho huku na huko akaanza kuzipiga hatua kuelekea kunako mlango wa chumba kile ambacho aliamini Imma huwa analala.Aliufikia huo mlango akasimama akaanza kujihoji aanze vipi kuugonga mlango huo.Alijaribu kuunyoosha mkono wake wa kulia akausogeza ili agonge lakini akasita,alijiuliza kwa mara nyingine tena baadae akajisemea potelea mbali acha nianze kuugonga tu huo mlango lolote na liwe.Alianza kuugonga,akaugonga kama mara tatu hivi,dakika tano baadae mule ndani akaonekana Imma akiusogelea mlango huo kwa ajili ya kuufungua.Alipoufungua kwa vile alikuwa na mawenge ya usingizi hakumtambua huyo binti."Wewe ni nani na kwa nini unanigongea usiku wote huu?" Aliuliza Imma huku akijipangusa machoni....Recho alianza kujichekesha chekesha mara ajigeuze geuza kwa namna ile apendayo."Kaka Imma mimi ni Recho nimekuja hapa nikiwa na matatizo makubwa sana naomba unisaidie". Aliongea binti huyo kwa sauti ya kudeka."Recho !! Recho wa wapi?" Imma alimuuliza tena."Recho wa kwa Mzee Ludovic dada ake na Jack".Jibu hilo likawa kama limemfumbua macho Imma na hapo ndipo alipomtambua msichana huyo,kabla hakuwa amemtazama vizuri ila baada ya kumtazama aligundua binti alikuwa amejifunga kanga moja na kwa jinsi ambavyo alionekana ilionyesha dhahiri alikuwa ni mtupu,Recho hakungoja Imma aongee neno lolote alianza kumsogelea kijana Imma,lakini Imma mwenyewe akawa anamkwepa kijanja."Sasa binti ujue sikuelewi,kama vipi tuonane kesho". Aliongea Imma akaingia ndani na kuufunga mlango akamuacha Recho pale nje akitapatapa asijue aamue nini au afanye nini."Shiiti nitakupata tu hata kwa bao la mkono". Alijisemesha mara hii akiirusha rusha mikono yake akatoka pale alipokuwa amesimamia akaanza kuifuata gari yake akaifikia na kupanda moja kwa moja akaondoka kurejea kwao.Kulipopambazuka,tayari ilikuwa ni siku ya juma tano,asubuhi na mapema....Recho aliamka akiwa na mawazo chungu nzima akiwaza ni mbinu gani aitumie ili ampate Imma amuoe awe mume wake.Aliwaza mambo mengi mno mwisho akapata wazo la kwenda kwa mganga wa kienyeji kuangaliwa.Hakungoja wala hakumshirikisha mtu yeyote yule asubuhi hiyo hiyo alifunga safari ya kuelekea kwa mganga mmoja wa kienyeji aliyekuwa akijulikana kwa jina moja la Sagora,alifika huko saa mbili na nusu,kwa bahati nzuri kama mawazo yake yalivyokuwa yakimtuma alimkuta huyo mganga tena akiwa kikazi zaidi kwenye ngome yake ya kuagulia."Hahahaha!! Huuuuuhuuuuhu!! Karibu sana binti kwa mganga Sagora mtu mtakatifu wa himaya ya watu wa ukoo wa Tabori,hapa umefika na kama umefika basi jua shida yako imeshatatuliwaa!!".Mganga Sagora alimkaribisha kwa mbwembwe za ajabu mpaka Recho akaamini tatizo lake litatatuliwa."A
sante mganga,tawile kabisa najua shida yangu bila shaka itatatuliwa". Aliongea Recho huku macho yake akiwa ameyageuzia pembeni hakuwa akimtazama mganga Sagora."Una zawadi gani kwa mganga binti,bila shaka jina lako wewe unaitwa Mwanajimi au siyo au kama sivyo jina lako utakuwa unaitwa Chero au siyo binti hahahaha!!" Aliongea mganga huku akimkazia macho makali Recho."Hapana mganga jina langu siyo Mwanajimi au Chero,jina langu ni Recho naishi mtaa wa tatu wa Tabori". Aliongea Recho mganga kama kawaida yake akacheka."Sawa binti naomba unieleze,nielezee,,hahahaha!! Nieleze shida yako binti ila kabla hujaanza kuieleza shida yako hiyo naomba utie dora kadhaa ndani ya hiki chungu,hahahaha!! Lidandalile binti,safari lindandalile huhuhuhu!! Mtukufu mganga Sagora,mtu wa watu hahaha!! Tia dora kadhaa kwenye hicho chungu,uache huo moshi unaozuka maana hiyo ndo barabara ya mababu wanakujaa!! Wanakuja kuitatua shida yako".Alisema mganga Sagora,Recho akaanza kujisachi.Upande mwingine kule nyumbani kwa kina Recho,Jack nae aliamka asubuhi ile....hakuwa na muda wa kunywa chai wala nini,baada tu ya kumaliza kuoga alipanga safari ya kwenda hospitalini kumsalimia Imma maana Usiku kucha hakulala kwa ajili yake,alikuwa akimuwaza sana kijana Imma,na isitoshe alimuota,moja ya ndoto ambayo aliiota Jack usiku wa kuamkia siku hiyo ni ndoa,harusi kubwa ya kifahali akiwa na anafunga ndoa na Imma na katika hiyo ndoto kuna mambo mengine mazuri zaidi yalijitokeza.Basi alipokuwa tayari alichagua gauni moja zuri sana la kuvutia akalivaa ,akavaa na viatu vya maana akawa amekamilika kila idara.Jack ,siku ya juma mosi ambayo ndiyo ilikuwa siku yake ya appointment na Imma aliiona ikichelewa mno hivyo katika siku hiyo ya juma tano aliona ni bora akaonane na Imma tu,hata salamu kwake itakuwa na maana kubwa sana.Kitu ambacho hukifahamu kwa msichana huyu mrembo mwenye rangi ya chungwa,ngozi nyororo na umbo la kumtoa nyoka pangoni alikuwa ni bikra yaani hakuwa ameshiriki tendo la ndoa na mwanaume yeyote yule,yeye tangia akiwa mdogo baada ya kukutana na Imma kwa mara ya kwanza kama Kaka yake baada ya ule moyo wa upekee aliouonyesha Imma hasa kule bustanini,binti alimpenda mazima kijana huyo na akaapa kumtunuku penzi pindi atakapokuwa mtu mzima.....hivyo katika kipindi hicho chote,Jack aliamua kujitunza na kuutunza mwili wake kwa ajili ya Imma.Alimpenda Imma pamoja na mama yake kama ambavyo alikuwa akijipenda mwenyewe.Basi mambo yote yalikaa sawa ,binti akachukua mkoba wake akatia na ua moja jekundu ambalo alilichuma kwenye moja ya bustani yao ya maua....alitoka mule chumbani kwake,kama kawaida yake akamuaga mamaye ambaye alikuwa bado hajaenda kazini akatoka na kuianza safari ya kuelekea kazini kwenda kumuona Imma kule hospitalini alipokuwa akifanyia kazi.Alichukua bajaji ya kumwahisha haraka maana kwa upande wake babaye hakuwa amemnunulia usafiri kama ambavyo alimfanyia dada ake Recho.Bajaji ilimbeba safari ikaanza mara Moja,,,muda mfupi baada ya dakika zipatazo kumi na tano kukatika alifika huko,,,alishuka akatua ndani ya maeneo ya hospitali hiyo ya Taifa.Akaanza kutembea haraka haraka,sasa kwa bahati mbaya hakuwa akiifahamu ofisi ya Imma hivyo ikambidi aulizie ili aelekezwe.Alimfuata muuguzi mmoja wa kike.
"Samahani dada,hivi unaweza kunielekeza ofisi ya Dokta Emmanuel William ilipo?" Aliuliza Jack,yule muuguzi akamkazia macho ya dharau."Sina muda mchafu wa kukuelekeza ofisi ya Dokta Imma ilipo,hata hivyo sidhani kama utafanikiwa kuonana na Daktari mkubwa kama huyo yupo bize". Aliongea yule muuguzi kisha akaondoka zake na kumuacha Jack akiwa amesimama kama nguzo.Jack alimtazama sana muuguzi huyo akaishia kutikisa kichwa chake baadae akaondoka hapo na kwenda moja kwa moja eneo la mapokezi,,alifika huko akakutana na foleni ndefu sana ya watu waliokuwa wakisubiria huduma.Alisimama kwa mbali akahisi uchovu ikampasa akakae kwenye moja ya mabenchi ya pale Reception.Alikaa hapo kama dakika saba hivi,baadae akaonekana Daktari mmoja akija ,Jack akasimama na kumfuata."Samahani Dokta!" Alisema Jack kwa upole."Bila samahani binti".Dokta aliitikia huku akisimama."Shikamoo?" Alisalimia Jack maana ule umri wa Dokta pamoja na umri wake haukuwa ukilingana."Marahaba binti vipi?" Aliitikia Dokta kisha akamuuliza ."Naomba unielekeze ofisi ya Dokta Emmanuel William ilipo maana nina shida nae". Aliongea Jack,Dokta huyo akamtazama kwa mshangao."Dokta Imma? Binti unafahamiana na Dokta huyo? Maana huwa hapendi kuonana na watu hovyo hovyo isitoshe ni Daktari mkuu wa hii hospitali hivyo kumuona mpaka uwe na shida ya maana,okey haina haja naomba unifuate". Aliongea Daktari huyo kisha akaanza kuondoka huku Jack akimfuata kwa nyuma.Daktari huyo alinyoosha hadi ofisini kwake akafika na kuufungua mlango."Binti mbona una sita sita hivyo ingia usiogope". Aliongea Dokta ,Jack akawa anaogopa ogopa kuingia mwisho akaingia akaruhusiwa kukaa.Daktari huyo alianza kumtazama sana Jack,na akaonekana dhahiri shahiri ameshamtamani maana kiukweli binti huyo kwa ule muonekano wake,mwanaume yeyote rijali ni lazima udenda ungemtoka tu."Kwanza binti pole na safari" Aliongea Dokta huyo ."Asante,ila Dokta mbona hunielekezi ofisi ya Dokta Imma ilipo?" Aliuliza Jack,Dokta yule akacheka kidogo."Dada usijali nitakuelekeza tu ila naomba uniambie huyo Dokta ni nani yako?" Aliuliza Daktari kwa sauti ya chini."Ni mchumba wangu na nina mpenda sana".Alijibu Jack bila kuuma ulimi wala kusema kwamba Imma ni Kaka yake kama wengi wanavyofanya."Ahaa!! Sawa,ila dada ni vizuri ila nakuhurumia sana". Aliongea Dokta huyo muda huo akitikisa tikisa kichwa chake."Dokta una nihurumia kwa kipi sasa?" Aliuliza Jack."Huyo Imma hadi muda huu naongea na wewe hana nguvu za kiume,unajua sisi madaktari huwa tuna...tuna...tuna program maalumu ya checkup yaani ya kuchunguzwa miili yetu na afya zetu kabla hatujawatibu wengine na majibu hutolewa hadharani kwa madaktari wote huku tukipaswa kutunziana siri.Hivyo mimi nimeamua kukudokezea siri ya Dokta Imma japo ni kosa kisheria". Aliongea Daktari huyo.
*************************
Turudi kwa upande wa Recho....baada ya binti huyo kujisachi alitoa noti kadhaa za dora akazihesabu,jumla ya noti hizo ikawa ni kiasi cha dora elfu tano za kimarekani akazitia ndani ya kile chungu cha mganga Sagora."Hahahahaha!! Lindandalile binti,Hahahaha!! Na wachawi ee baba,wako wapi ee baba!! Hahahahaha!! Sasa binti mizimu imeshakuruhusu uiseme shida yakoo!! Mizimu ya mababu imekuruhusu zungumza shida yako bintii!!". Aliongea Mganga Sagora huku akiinyanyua fimbo moja iliyokuwa ikitokwa na moshi mzito."Mganga natafuta mume wa kunioa,ni miaka mingi sana nateseka,siolewi na sijui tatizo ni nini ,sijui ni mikosi sijui !! Miaka ya nyuma nimewahi kuwa na mahusiano na wanaume wapatao ishirini,nililala nao lakini kati ya hao wote hakuna hata mmoja ambaye alinitamkia ataja kunioa!! Sasa nimechoka kukaa nyumbani maana umri wangu unaenda nitazeekea kwetu na nitaaibika,nitachekwa mimi!!.Sasa mganga naomba unisaidie nipate mume". Aliongea Recho."Hahahahaha!! Huhuhuhu!! Lindandalile binti!! Sasa naomba umchague huyo mume ambaye unataka akuoe". Aliongea yule mganga."Kuna kijana mmoja anaitwa Imma Daktari mkuu wa hospitali ya Taifa natamani sana huyo awe mume wangu".
ITAENDELEA...............................................



No comments: