Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA SABA (07).




Riwaya:THE TRUE LOVE.

SEHEMU YA SABA (07).
Maneno hayo aliyasema Wanjera mara baada tu ya mama yake kutokea pale mlangoni na kudai kwamba ana njaa,Sasa mama Imma kusikia kwamba tayari chakula kimeshawekwa mezani alifurahi sana akaanza kuzipiga hatua kuisogelea ile meza akafika na kuketi kwenye kile kiti cha mwisho.Kwa bahati mbaya upande huo ndiko ambako kile chakula chenye sumu kiliwekwa,ina maana Wanjera alijua kama mama yake ataenda kukaa hapo? Mimi sijui acha tuone.Basi mama Imma kabla hajaanza kula aliomba maji ya kunywa akasogezewa na Wanjera nae akayanywa hapo hapo....baadae alinawishwa tayari kabisa kwa kuanza kula.Dakika moja aliitumia kwa kukiombea kile chakula,alisali akamaliza....Sasa ile anakamata kijiko aanze kula.Mara simu yake kule chumbani ilianza kuita,Wanjera akamuomba mama yake amfuatie simu hiyo mama Imma akamwambia aache tu ataifuata mwenyewe.Mama huyo alisimama haraka akaingia huko chumbani na kwenda kuipokea akakuta kumbe anayempigia hiyo simu ni mwanae mpendwa Imma.Bila kusita wala kujihoji maswali yasiyokuwa na msingi aliipokea na kuiweka sikioni."Haloo mwanangu kulikoni?"...."Mama nakuomba uje hapa nyumbani kwangu muda huu huu kuna jambo moja la mhimu sana limetokea".Imma aliongea na kisha kuikata simu yake....akamuacha mamaye katika wakati mgumu mno huku akibaki kujiuliza ni kipi kimetokea au ni kipi kimempata kijana huyo.Alitoka sebuleni akiwa na unyonge kiasi na mudi ya kula ikatoweka kabisa."Mama mbona unaonekana kama haupo sawa nini kimekupata?" Wanjera aliuliza baada ya kumuona mama yake akiwa katika ile hali ya unyonge."Imma amenipigia simu akidai kule nyumbani kwake kuna shida imempata hivyo amenisihi niende huko muda huu huu". Aliongea mama Imma huku akianza kuusogelea mlango wa kutokea nje....Wanjera alikasirika sana akajua kwa hapo lengo lake limebuma,,alianza kumsihi mamaye ale kwanza ndo aende lakini mama Imma wala hakukubali."Mama si ule kwanza ndo uende jamani? Ina maana unataka kwenda huko ukiwa na njaa?" Alisema Wanjera."Hapana Wanje,nikianza kula nitachelewa na Imma hatonielewa,Acha niende tu". Aliongea mama Imma na kwa hapo hakuwa na muda wa kuendelea kubaki pale,aliondoka mara Moja akafunga safari ya kuelekea nyumbani kwa mwanae Imma.....umbali kutoka kwake hadi huko kwa Imma ulikuwa si mrefu sana kwani kwa haraka haraka unaweza kutumia dakika kumi tu au kumi na tano unafika.Basi mama huyo alitembea kwa mwendo wa kukimbia kimbia akawa amefika huko huku akitumia dakika nane tu."Hahahaha!! Mama karibu!!" Hilo lilikuwa ni neno la kwanza la kijana Imma mara baada ya kumuona mama yake akiingia humo ndani maana ule mlango wa kuingilia haukuwa umefungwa .Mama Imma alikuwa akihema sana muda huo mapigo ya moyo wake yakienda mbio maana alijua labda kuna kitu kibaya au cha kushtuza kimetokea."Mama kaa mbona umesimama?" Aliuliza Imma baada ya kumuona mama yake amesimama tu."Nitakaaje mwanangu ili hali umenishtua,niambie kuna nini au ni jambo gani hilo?" Aliuliza mama Imma huku akiwa bado amesimama."Mama wala usiwaze sana,nimekuita tuje tule pamoja kwani leo nimeandaa chakula kitamu sana mama naamini utakipenda". Aliongea Imma ,mama yake akashusha pumzi kana kwamba amepumzika baada ya kufukuzwa vya kutosha na jitu la ajabu,kwa hapo alikubali na akawa amekaa lakini akabaki akitabasamu tu huku akimkodolea macho mwanae ."Ina maana mwanangu hicho ndo ulichoniitia daah,Imma wakati mwingine punguza utani,utakuja kuniuwa mama yako mi nilijua labda kuna kitu kibaya kimekupata". Aliongea mama Imma,Imma mwenyewe akawa anacheka tu bila ya wasiwasi."Nisamehe mama,unajua kama ningekupigia simu na kukuambia kuna chakula kitamu nimekipika usingekubali kuja hapa na ndio maana nikatumia sentensi ile kukushawishi uje". Aliongea Imma ."Kwa hapo mwanangu umenishinda tabia,ila na sisi kule tulikuwa tunajipanga kula na mpaka sasa ninapozungumza na wewe kuna chakula nimekiacha mezani".Alisema mama Imma."Huko utakula kesho naomba kwa leo ule chakula nilichokipika kwa mikono yangu mwenyewe".Imma alimshawishi mama yake mpaka akakubali hatimaye kile chakula ambacho Imma alikiandaa wakaanza kula wote.Wakati wakiendelea kula,mama Imma alimtazama kijana wake kama mara tatu hivi mpaka Imma akashtuka."Mama mbona unaniangalia sana?" Aliuliza Imma maana ile haikuwa kawaida ya mamaye kumtazama kiasi kile."Mwanangu mi nataka nikuulize swali moja tu".Alisema mama Imma."Swali gani mama,unaweza kuniuliza nami nipo tayari kulijibu". Aliongea Imma."Hivi mwanangu umeshapata mchumba kweli mpaka muda huu? Maana kwa sasa una umri wa miaka ishirini na tisa na hata kwa bahati mbaya sijawahi kukuona ukiwa na mchumba wala kunipa taarifa yoyote kuhusiana na hilo".Alisema mama Imma,Imma akajikuna kidogo kichwani na kwenye zile ndevu zake kiasi baadae akakohoa na kumtazama mama yake."Bado mama sijapata,ila naamini Mungu atanisaidia tu nitampata yule aliyeumbwa kwa ajili yangu sitaki nikuletee mkwe ambaye atakusumbua mama yangu".Alisema Imma.Kule nyumbani kwa Mr Ludovic,chumbani kwa Recho,macho ya binti huyo yalikuwa hayatulii,binti macho yake alikuwa akiyaangaza huku na huko akiombea masaa yaende haraka haraka....utimie ule muda ambao aliupanga ili akakifanye kile ambacho alikitarajia.Alichoka kujilaza pale kitandani akashuka na kuzipiga hatua chache akaenda na kukaa kwenye kiti chake cha plastic kilichokuwa kimeegemea ukutani.Aliitazama saa yake ya mkononi akatikisa kichwa baadae akaitazama na ile saa ya ukutani akakuta bado ni saa mbili na nusu tu na kwa muda huo walikuwa wameshamaliza kula chakula cha usiku.Recho alisimama akatembea kwa kunyata akaufikia mlango wa chumba chake na kisha kuufungua taratibu akatoka na kuurudishia pole pole.Alitembea kwa mwendo wake ule ule wa kunyata akakifikia chumba kimoja hivi,akajing'ata mdomoni akawa anaunyanyua taratibu mkono wake wa kulia ili aufungue mlango wa chumba hicho.Alihesabu kimoyo moyo kama mara tano hivi baadae akaufungua ule mlango akaingia moja kwa moja ndani .Humo aliona mfuko mkubwa aina ya ile mifuko ya Shangazi Ukerewe,akausogelea kwa umakini sana mfuko huo akaufikia na kuanza kuufungua.Humo aliona kuna mabunda mengi sana ya dora,,,akatabas
amu akayaangaza macho kulia,kushoto .Hapo hapo akatoa mabunda saba ya zile dora akatoka nayo huku akiwa ameyaficha vizuri.....aliu
rudishia ule mlango akakimbia kimya kimya hadi chumbani kwake na kujifungia humo.Dakika tano tu,Mr Ludovic alionekana akitokelezea kwenye ule mlango wa chumba chake huku mkononi kwenye ule mkono wake wa kushoto akiwa na kufuli akaanza kutembea kukifuata kile chumba akakifikia , akaufungua ule mlango na kisha kuurudishia tena.Alipoufunga vizuri alipigilizia na kufuli akaondoka zake.Sasa Recho baada ya kuyabwaga kitandani yale mabunda ya noti alicheka kimoyo moyo akaanza kuzihesabu pesa hizo akakuta ni kiasi cha Dora elfu thelasini na tano za Kimarekani.Alizipanga vizuri kisha akazitia kwenye begi lake akamaliza na kukaa kitandani."Imma,,,,Imma nitaingia na slogan gani kwa huyu kijana? Hapa mjini kila mmoja ananijua kwamba mimi ni nani,na isitoshe nimeshalala na wanaume ishirini hadi nafikisha huu umri ila hakuna hata mmoja ambaye alinitamkia kunioa.....kwa sasa hii miaka yangu ishirini na nane inavyozidi kwenda kasi nisipoangalia nitazeekea nyumbani,,,sasa nitajibebisha kwa Imma kwa kadri niwezavyo ili anioe yeye bila kujali kule nyuma nilikuwa nikimchukuliaje,ikishindikana sana,nitatumia pesa kumpata".Alijisemesha Recho,kisha akawa amejilaza kitandani na kujifunika shuka papo hapo.
Kwa upande wa Mama Imma baada ya kumaliza kupata kile chakula na mwanae,alisimama akamwambia kijana wake ni muda sasa wa yeye kurejea nyumbani maana dakika zilikuwa zikisogea na usiku nao ulikuwa ukizidi kuwa mrefu.Imma alikubali kiroho Safi lakini wakati wa kutoka ulipowadia alimsindikiza mama yake kwa gari hadi nyumbani kwake akawa amemfikisha salama.Waliagana kwa mara nyingine tena na wakawa wametakiana usiku mwema.....Imma aliondoka pale bila kuingia ndani ya ile nyumba ya mama yake na mama Imma nae akawa ameingia ndani.Alipoingia humo ndani alimkuta Wanjera amekaa chini kwenye marumaru huku akionekana dhahiri kuchukizwa sana na kile kitendo cha mama yake kukataa kula chakula."Wanje? Wanje?.....Wanjera??" Aliita mama Imma lakini Wanjera hakuitika akajifanya kama hasikii."Wanjera si nakuita ina maana hunisikii?" Aliuliza mama Imma na hapo sasa Wanjera ndo akaekiti kuitika."Abe mama" aliitika huku akiyageuza na kuyarembua kidogo macho yake."Mtoto unamwangalia tu,amelala hapo,huoni kuna mbu?" Aliuliza mama Imma Wanjera akanyanyuka na kumbeba mwanae akaingia nae chumbani kule alipokuwa akilala.Mama Imma nae akaingia chumbani.Wanjera kule chumbani hakukaa,alipomlaza tu mwanae alitoka hadi sebuleni .Akaanza kumuita mama yake huku akiamini kwa mara hii atakubali tu kula kile chakula maana bado pale mezani hakuwa amekiondoa.Mama Imma baada ya kuitwa alitoka kwenda kumsikiliza binti yake huyo kuona kama kuna shida au ana jambo la kumwambia."Mama ina maana ndo umekataa kabisa kula si ule mama?" Alisema Wanje,mama yake akamkazia macho."Samahani Wanjera,nilipoenda nyumbani kwa Kaka yako Imma ile nafika tu nilikuta akimalizia kutenga chakula,akaning'ang'aniza nile nikawa sina namna ilinibidi nikubali tu,hivyo kwa sasa nimeshiba sina njaa mwanangu". Aliongea Mama Imma."Sawa mama ila...ila...Okey haina shida mama ,mie nikutakie usiku mwema".Alisema Wanjera ,mama yake akarudi tena kule chumbani kwake.Pale sebuleni Wanjera alibaki amesimama mithili ya nguzo akazungumza zunguka baadae akaichukua ile sahani yenye chakula cha sumu akatoka nayo na kwenda kukimwaga mbali kile chakula.Alirudi akakaa kwa muda pale sebuleni,kimoyo moyo akajiongelesha "Mhu!! Si nipo nae hapa hapa,lengo langu bado halijafa litatimia tu".Alimaliza akasimama na kuelekea chumbani.Turudi nyumbani kwa Mzee Ludovic....
*******************
Recho akiwa amejiegesha pale kitandani alichoka kulala bila mafanikio maana kwa siku hiyo usingizi ulikuwa umemgomea.Alilitupilia mbali shuka lake pamoja na uwepo wa baridi mishale hiyo ya saa tatu na robo za usiku akakaa kitandani baadae akasimama na kuitengeneza vizuri nguo yake ya ndani.Alikaa kidogo akasimama tena.....mara hii aliivua hiyo nguo akawa mtupu kwa upande wa chini kwa juu akabakiwa na kijiblauzi cheupe ambacho kilikuwa ni chepesi sana na kilikiacha nje kitovu chake.Alichukua kanga moja akaishikilia,ak
aanza kuyazungusha macho yake....alipoona mawazo yake yametiki,aliivua na ile blauzi akawa mtupu moja kwa moja.Aligeuka akayatazama makalio yake makubwa akacheka na kisha kujifunika ile kanga akamaliza na kutoka nje ya chumba chake,alitembea hatua chache tu akasimama ikaonekana kuna kitu amekisahau.Alirudi haraka chumbani akatoka akiwa ameshikilia funguo za gari,,,gari ile ambayo alinunuliwa na baba yake Mzee Ludovic.Alitoka haraka akafika nje akamfuata mlinzi wa geti na kumsihi afungue geti."Sasa dada,usiku wote huu unataka kwenda wapi?" Aliuliza yule mlinzi akaambulia matusi ya aibu akatulia.Ikambidi afungue geti tu,muda huo Recho tayari alikuwa ameshapanda ndani ya gari yake kuelekea nyumbani kwa Imma maana alikuwa amefuatilia na kupajua pale anapoishi kijana huyo.
ITAENDELEA.................................................



No comments: