Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA SITA (06).




Riwaya:THE TRUE LOVE.

SEHEMU YA SITA (06).
Gari ilitembea kama umbali wa kilomita moja hivi maana kutoka eneo lile alilokuwa akiishi Mzee Ludovic pamoja na familia yake haikuwa mbali sana.Hivyo baada ya kufika,dereva wao alisimamisha gari,mzee Ludovic na mkewe wakaanza kushuka.Alishuka kwanza mkewe na Mzee akafuata....Waliposhuka hawakuwa na muda wa kupoteza walianza kuzipiga hatua za mwendo wa taratibu kuingia kwenye kumbi kubwa ya hospitali ile ya Taifa kabla hawajaenda kukata kona ili wanyooshe moja kwa moja hadi kwenye chumba cha reception kwani ingewapasa waende kwanza huko kabla hawajaelekezwa cha kufanya na utaratibu mzima ulikuwa ni huo yaani kabla hujaonana na Daktari ni lazima uanzie Reception.Basi walifanikiwa kuingia ndani ya ukumbi mkubwa wa hospitali wakaona watu kadha wa kadha wakiwa wamekaa huku wengine wakiwa wamesimama kusubiria foleni kubwa iliyokuwepo eneo la mapokezi.Kutokana na heshima yao hawakujipanga kwenye hiyo foleni walinyoosha hadi kwenye dirisha la mapokezi wakatoa vya kutoa hasa vitu mhimu baadae wakaelekezwa cha kufanya.Waliambiwa waende kwenye chumba namba mbili.....wakafanya hivyo wakawa wameelekea kwenye chumba hicho,walifika wakabisha hodi wakaruhusiwa kuingia ndani.....kwa bahati nzuri wakati wanaingia,daktari waliyemkuta humo alikuwa akimalizana na mtu mmoja tu.Wakatakiwa wakae kwanza wasubiri yule mtu atimiziwe shida zake.....ndani ya dakika tatu tu yule mgonjwa alihudumiwa na kutimiziwa shida zake akawa ametoka."Mzee shikamoo karibu".Alisema Daktari huyo aliyekuwa akionekana ni kijana sana,Mzee Ludovic alitabasamu kwanza kabla hajamjibu "Marahaba bwana,habari za kazi?" Alijibu Mzee Ludovic."Ah! Za kazi Mzee wangu ni nzuri kabisa namshukuru Mungu".Alisema Dokta ."Naomba nikuhudumie Mzee wangu,sijui unashida gani?" Aliuliza Daktari na hapo ndipo Mzee Ludovic alipoanza kuielekezea shida yake,aliielezea ikaeleweka na Dokta kwa kumshauri tu akamuelekeza kwa kwenda,,,, akamwambia ni vyema akapate vipimo haraka iwezekanavyo na itamlazimu akamuone kwanza Daktari mkuu ambaye kwa muda huo alikuwa akifanya mambo kadhaa ndani ya Maabara.Waliongozana hadi huko,sasa baada ya kubisha hodi na kuruhusiwa kuingia hata kidogo hawakukaa kuyaamini macho yao kwa hicho walichokuwa wakikiona humo.....Walimuona Imma mwenyewe akiwa ndani ya mavazi ya kidaktari,Mzee mzima akashindwa afanye je akabaki akitokwa na Machozi tu.....hapo hapo alimtazama Imma usoni akayagandisha sana macho yake mwisho akaanza kuyakumbukia maneno ya kejeli aliyokuwa akimfanyia kijana huyo kwa kumuona kama mtu asiye na thamani yoyote dunia bila kujua kama hii dunia ni lidandalindanda,leo umelala maskini kesho umeamka tajiri."Baba Recho,mimi nilikuambia kwamba katika hii dunia si vizuri kumdharau mtu kwa muonekano wake eti kisa ni maskini amezaliwa na maskini.....Mungu ni wa ajabu sana baba Jack!!! Maana hata huyo unayemuona ni maskini leo kesho utashangaa kumuona akiendesha gari la thamani,,,mwanangu Imma siamini kama umefikia katika hatua hii,ina maana kumbe wewe ndiye Daktari wetu mkuu wa hospitali ya Taifa? Ama hakika kila binadamu katika hii dunia Mungu kamweka kwa kusudi lake".Alisema mama Recho,Mzee Ludovic akabaki akigugumia kwa kilio tu maana alijiona muda huo huo kama yeye ni mkosaji tena hastahili kuzibeba kabisa zile heshima ambazo anazipata."Mama wala usijali,baba mimi zamani sana nimeshamsamehe na nimeshayasahau yote,cha msingi hebu ngoja nimpime tu baadae akatibiwe tena nitawasihi na madaktari wangu wafanye hima kumhudumia vizuri ili apone na kurudia katika hali yake ya kawaida,usihofu mama,baba nampenda sana". Aliongea Imma,kisha akaanza kumfanyia checkup mzee akamaliza na kisha kumuita yule Daktari wa mwanzo aende nae wodini kwa ajili ya matibabu zaidi.Jioni yake Mzee Ludovic alipona na hakusumbuliwa tena na maumivu na kwa vile afya yake haikuwa na mashaka..... aliruhusiwa muda huo huo kurudi nyumbani.Wakiwa ndani ya nyumba yao,huku Recho nae akiwemo hapo sebuleni pamoja na Jack aliyekuwa akiwaza muda wote kwenda nyumbani kwa mama Imma,kuna mazungumzo ya hisia sana yalizuka ndani ya hiyo sebule ."Mama Recho,kumbe kijana Imma siku hizi ndo ameshakuwa Daktari mkuu wa hospitali ya Taifa daah! Nilikosea sana kumdharau".Alisema Mzee Ludovic muda huo akikuna kichwa bila ya kumtazama mkewe usoni."Ndo hivyo baba Recho,Imma ndo hivyo tena na ndio maana Mimi nikakuambia siku zote usimdharau mtu usiyemjua ". Aliongea mama Recho,Recho mapigo yake ya moyo yakawa yanaenda haraka haraka "Samahani mama ina maana Imma siku hizi amekuwa Daktari?" Aliuliza Recho huku akiwa haamini amini,Jack yeye alikuwa akiwachora tu na ongea yake kwa huo muda lilikuwa ni tabasamu lake basi yeye hakuwa na neno kwani tangia zamani alikuwa akimthamini sana Imma ina maana kama ni kumpenda alimpenda tangiepo tena hivyo hivyo pamoja na umaskini wake."Ndio Recho tena Imma wa sasa ukimuona huwezi amini kabisa,Imma amekuwa ni bonge la handsome amenawiri ,makovu yake ya hapa na pale hayapo tena".Maneno ya mama huyo yaliuteka sana moyo wa Recho kiasi kwamba wivu nao ukawa unauteka pole pole moyo wake .Recho alikuwa ni binti wa nyumbani tu na tangia amalize masomo yake ya kidato cha nne na kufeli kuendelea mbele kwa muda wote huo hakuwa na mchumba wala mpenzi na hata dalili tu za kwamba atakuja kuolewa hakuwa nazo.Kule nyuma wale wote aliokuwa amewahi kuwa na mahusiano nao ya kimapenzi hakuna hata mmoja ambaye alitamani kumuoa wote walimtumia tu kama chombo cha starehe baadae wakambwaga,hivyo na umri wake wa miaka ishirini na nane neno ndoa lilikuwa likimsumbua sana huku akiomba kila aina ya sala ampate mchumba wa kumuoa hata kama hana pesa masuala ya pesa atayashughulikia mwenyewe.Hivyo hiyo ikawa fulsa kwake kuanza kujibebisha kwa Imma kuona kama ataokota dhahabu barabarani."Daah!! Mama natamani sana nimuone Imma ili hayo maneno unayoniambia niyaamini,sijui nitamuonea wapi tu!!" Alisema Recho huku akijifanya kujisahaulisha kwa yote aliyokuwa akimfanyia Imma kipindi akiwa katika hali tete."Au nyumbani kwao nitamuona hebu niambie basi mama?" Alisema kwa mara nyingine tena akamfanya mama yake acheke huku akijipiga piga kifuani."Recho wewe si ndiye uliyekuwa ukimchukia Imma pamoja na mama yake eti kisa wanakaa ndani ya nyumba ya makuti,sasa leo kiko wapi au umeshayasahau hayo?" Aliuliza mama yake."Mama hayo yameshapita,unajua siyo kwamba Imma nilikuwa nikimchukia Imma wala sikuwa nikimchukia kabisa,sema nini kwa muda huo zile nguo alizokuwa akizivaa zilikuwa zikinikera sana,Imma alikuwa ni bonge la handsome tokea zamani sema hakuwa na matunzo tu na mambo ya bustani yalimfanya achoke sana.By the way nikimuona ni lazima nianze kwanza kwa kumuomba msamaha maana binadamu huwa tunakosea".Alisema Recho,mara mlango ukasikika ukigongwa,Akanyanyuka Jack kwenda kuufungua.Alitokelezea rafiki yake na Jack aliyekuwa akiitwa Minza "Waoo Minza karibu".Alisema Jack huku akimsogelea rafiki yake huyo na kisha kumkumbatia,baadae akaongozana nae hadi kwenye masofa."Wee Minza hivi kwa sasa umefikisha miaka mingapi maana kipindi hicho ulikuwa kadogo kadogo sasa umekuwa mmama na shepu yako". Aliongea mama Recho,macho ya kila mtu yakamgeukia binti huyo."Kawaida tu mama,kwa sasa nina miaka kumi na tisa,ndo kwanza nipo kidato cha nne".Alisema Minza,binti mwenye shepu mithili ya nyigu na makalio ya maana tu.
"Sasa mama Recho mimi natamani tupange siku kijana Imma pamoja na mama yake tumuite hapa ili tuje tuzungumze vizuri unajua siku ile baada ya kumuona niliumia sana? Yaani nililia nikajisemea kweli dunia iachwe tu iwe dunia,,mpaka muda huu nimejifunza na kijana Imma sitokuja kumchukia tena ,na hapa itakuwa kama kwao".Alisema Mzee Ludovic wakapanga siku ya kumuita Imma pale kwao mwisho wakakubaliana kwa pamoja siku ya juma pili wamuite.Maongezi yao yalimalizika kila mmoja akatoka kwenda kuendelea na shughuli zake.Jack na rafikiye Minza walitoka lakini ile wanajiandaa kutoka nje ya geti,Racho aliwakimbilia huku akiwaita wakasimama kumngoja."Jack nikuambie kitu?" Aliuliza Recho huku akijichekesha."
Niambie tu dada".Alijibu Jack."Hivi wewe na Imma bado tu mnauendeleza ule urafiki wenu mliokuwa mkiufanya zamani au?" Alisema Recho."Ndio dada".Jack alipojibu tu hivyo,Recho aliukunja uso wake japo Jack hakumgundua."Da
da kwa nini umeuliza hivyo?" Jack nae akamuuliza."Nilitaka kujua tu wala usiwaze mdogo wangu basi mnaweza kuendelea na safari yenu".Alisema Recho na hapo hapo Jack na Minza wakaondoka na safari yao ikawa ni ya kuelekea nyumbani kwa mama Imma.Huko walitembea kwa miguu wakawa wamefika baada ya dakika ishirini kupita ....wakamkuta Wanjera akiosha vyombo huku akiimba nyimbo moja ya Bahati Bukuku isemayo Dunia haina huruma,,,,Wimbo wake aliusitisha baada ya kuwaona hao mabinti."Waah! Jack karibu,yaani umenishtua hatariii".Alisema Wanjera na muda huo huo akanyanyuka na kufuata viti ndani akatoka navyo na kuwaletea nao wakakaa."Ehe Jack za tangu juzi?" Aliuliza Wanjera huku akijikuna shingoni ."Nzuri tu,hivi mama yupo au?" Aliuliza Jack baada ya kumjibu Wanjera."Mh? Mama siku hizi mmmmh!! Hayupo wala,kwa muda huu ameenda kwenye kikao cha kina mama mtaa wa pili". Alidanganya Wanjera lakini ukweli ni kwamba mama yake alikuwa yumo ndani na kwa muda huo alikuwa amepumzika tu."Aha!! Sawa ila bila shaka nitamsubiri maana nina tamani kumuona".Alisema Jack."Hapana Jack wala usijisumbue sana mama utamuona siku nyingine kwa sasa hawezi kurudi mapema anaweza kurudi usiku". Aliongea Wanjera ,Jack akakubali tu akawa amesimama na rafiki yake wakaagana na Wanjera ili waondoke.Walipo
ondoka,Wanjera aliung'ata mdomo wake kwa hasira."Mama!! Mama!! Nyoko nyoko!! Nani mama yake hapa? Halafu hichi kibinti kinapenda sana shobo ngoja ipo siku nitakuja kukikomesha tu". Alijiongelesha Wanjera akanyamaza na kuendelea na kazi yake.Aliviosha vyombo akawa amevimaliza.Giza lilipoanza kuingia alianza kuandaa chakula cha usiku.....lakini wakati akiandaa chakula hicho kuna wazo baya sana lilimuijia kichwani mwake,,,Wanjera aliitizama ile nyumba nzuri ya kulia,nyumba ya kifahali ya mama yake aliyokuwa amejengewa na mwanae Imma pamoja na duka kubwa la jumla jumla,akaitazama na ile nyumba ya kushoto ya wapangaji akasema hapana,ni muda sasa wa kufanya mpango kumuua mama yake kwa namna yoyote ile ili zile mali ziwe zake kwani aliamini Kaka yake Imma yeye anajitolesheza kwa kila kitu hivyo hawezi kurudi nyuma na kuzitaka zile mali.Aliandaa chakula akamaliza ,akachukua sahani tatu,moja akaiwekea chakula kisha akaingia ndani haraka akatoka na kijimfuko cha sumu,sumu kali ambayo aliitumia kumuulia yule kijana Sabo baada ya kumshtukia na kukimbilia mbali kabla hajarudi tena mjini hapo.
*************************
Alitoka akiwa amekibeba kile kijimfuko akaja nacho hadi jikoni,,, aliyaangaza macho yake huku na huko akaona yupo salama hakuna anayemuona.Haraka haraka alikifungua kile kijimfuko akachota ile sumu kwa kutumia kijiko akaitia moja kwa moja ndani ya ile sahani ya chakula akaichanganya vizuri ikachanyanyikana kwani ilikuwa ni nyeupe.Baada ya kuhakikisha hiyo sumu imeenea pote bila kujulikana,alimalizia kwa kuzipakulia chakula zile sahani zingine.Alitabasamu akaamini huo ndo utakuwa mwisho wa maisha ya mama yake atamfuata babaye kule alipo.Alisimama akakificha vizuri kile kijimfuko baadae zile sahani kwa pamoja akazitia kwenye sahani kubwa akaondoka nazo kuelekea ndani.Kwa muda huo mama yake alikuwa bado amepumzika kitandani kule chumbani kwake na yule mwanae nae pia alikuwa amelala.Wanjera alipoona mambo yamekaa sawa alienda karibu na mlango wa mama yake kumwamsha.....Mama Imma aliamka na akadai ana njaa sana."Mama tena umeamkia pazuri chakula kipo tayari karibu".
ITAENDELEA......................................



No comments: