Riwaya:THE TRUE LOVE. 05
Riwaya:THE TRUE LOVE.
SEHEMU YA TANO (05).
Bila huruma Mr Ludovic alimfuata kwa kasi mkewe pale alipokuwa amekaa akachomoa mkanda wake wa suruali akamkamata mama Rachel na kuanza kumpiga huku akimwambia atangulie hadi kwenye gari .Mama Rachel wala hakulia alijikaza tu japokuwa ni maumivu makali alikuwa akiyapata......Kitendo kile cha mama huyo kupigwa kilimfurahisha sana Rachel hadi akafikia hatua ya kuanza kumcheka mama yake akimchukulia kama ni mtu wa kawaida tu kwake.Hivyo mama Rachel hakujali aliamini mumewe bado yupo gizani akija kufumbuliwa macho atajua hicho anachokifanya siyo kizuri na hakifai katika jamii yoyote ile.Jack yeye na utoto wake aliumizwa na kitendo hicho akabaki akiungulia moyoni na kujiapiza hata siku moja akija kuwa mtu mzima hatokaa amuache baba yake kumkemea katika tabia hiyo isiyofaa hata kama atakutwa tayari ameshazeeka alijiapiza ni lazima atamkumbusha tu.Basi mama Rachel akiwa na masikitiko makubwa alitangulia hadi kwenye gari akapanda,Jack nae akamfuata kwa nyuma akapanda,Rachel nae akafanya hivyo hivyo na wa mwisho kupanda ndani ya gari hiyo alikuwa ni baba Jack....Baadae wakaanza kuondoka kuelekea nyumbani kwao.Walimuacha mama Imma eneo hilo akiwa peke yake ,,,alikaa kidogo kisha akasimama na kuingia ndani.Siku hiyo ilimalizika ikaingia siku nyingine ambayo ilikuwa ni siku ya jumatatu,,,watu kama kawaida waliendelea na shughuli zao huku wanafunzi wakielekea mashuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo .Kuanzia kipindi hicho ,Jack alikata shauri ya kumweka Imma katika kumbukumbu zake hadi pale atakapoonekana tena ndani ya huo mji.Alijituma katika masomo akawa anamsikiliza kila mwalimu darasani ili nae hapo baadae aje ayafaidi matunda ya elimu.Zilipita siku mbili tu,Jack akaondoka kinyemela pale kwao na kufunga safari ya kuelekea nyumbani kwa mama Imma....Ilikuwa ni siku moja tulivu sana ya Alhamis jioni saa kumi alipoondoka na kwenda huko.Alifika akamkuta mama Imma akiosha vyombo akaenda na kusimama mbele yake akawa anatabasamu huku akimtazama mama huyo kwa macho ya upendo kwani imani yake kwake ilikuwa ni kubwa mno,mama mzaa chema.Kuna kipindi msichana huyo mbali na kuwa na miaka kumi na miwili tu alikuwa akijiapiza hatokuja kuolewa na mwanaume yeyote yule zaidi ya Imma ."Mama shikamoo?" Alipoona amechoka kusimama alianza kwa kumsalimia mama Imma,mama Imma nae akashtuka kwani kipindi anaosha vyombo vyake hakujua kama mbele yake kuna mtu amesimama akimtazama.Alipoisikia tu hiyo sauti aliunyanyua uso wake juu akamuona Jack amesimama akashangaa,,aliyaangaza macho yake huku na huko kuona kama kuna mtu amekuja nae lakini hakuona kitu.Alibaki kimya kidogo baadae akaitikia japo kwa sauti ya chini "Marahaba mwanangu hujambo?" Aliitikia na kumfanya Jack amsogelee zaidi."Sijambo mama ila nimemmisi Kaka Imma,ningekuwa na simu ungenipa namba zake nimpigie ila basi tu".Alisema msichana huyo mdogo mwenye hekima za utu uzima."Hahaha!! Una mambo wewe,Imma anaendelea vizuri kabisa kwa hilo wala usihofu ila unaonaje ukija kuwa mkwe wangu hahaha". Aliongea mama Imma kwa mtindo wa kumtania Jack lakini hayo maneno yalipojipenyeza masikioni mwa msichana huyo yalimpaisha kutoka katika sayari ya dunia na kumpeleka sayari nyingine kabisa....Sayari ya raha na furaha ya ajabu.Jack alimkodolea macho mama huyo huku kidole chake cha mwisho akiwa amekiweka mdomoni..... alimkodolea sana kisha akatembea kama hatua tatu hivi akaja kusimama karibu na mlango."Mama kama kuna picha ya Kaka Imma naomba unipatie ili niwe natembea nayo ndani ya begi langu hasa nikiwa naelekea shuleni". Aliongea Jack mama Imma akamtazama usoni akacheka na kuikung'uta mikono yake iliyokuwa na mapovu ya sabuni pamoja na mchanga."Eti ee,usijali picha utaipata unataka nikupe picha ya aina gani?" Aliuliza mama Imma,Jack akayazungusha macho yake na kujitazama kiunoni."Nipe picha yoyote tu nitaipenda maana sijaona mtu aliyenijali kama Kaka Imma".Alijibu Jack na hapo ndipo mama Emma aliponyanyuka na kuingia ndani.Humo ndani alimaliza dakika tatu tu akatoka na picha mbili akampa Jack na kumfanya afurahi mno akahisi kama anamuona kijana huyo.Sasa pamoja na kupewa picha hizo lakini msichana huyo wala hakuonyesha dalili zozote za kuondoka pale ikaonekana kama kuna kitu bado anakihitaji."Jack nikuletee kiti ukae?" Aliuliza mama Imma,Jack akakataa."Hapana mama,ila....ila?" Alishindwa kuimalizia sentensi yake hiyo."Ila...ila nini sasa mwanangu?" Mama Imma alimuuliza Jack akawa hana jibu la papo kwa hapo akawa anatafakari kwanza."Mama naomba nikuambie kitu kama hutojali" Alisema Jack mama Imma akamruhusu"ongea tu mwanangu mie hapa nakusikiliza".A
lisema."Naomba niwe naishi hapa hapa hadi pale Kaka Imma atakaporudi maana pale nyumbani kila nikilala au nikikaa mawazo yangu ni kumwaza yeye tu na nikijaribu kuyatupilia mbali mawazo hayo huwa naishia kushindwa tu mama angu tafadhari maana Kaka Imma nampenda sana sijui ni kwa nini tu sijazaliwa nae tumbo moja".Alisema binti huyo kwa sauti moja ya upole sana hadi mama Imma mwenyewe akamhurumia lakini akashindwa kupata jibu la kumpa maana alimfahamu vilivyo baba yake kwamba siyo mtu wa masihara kabisa."Mwanangu hebu yatizame macho yangu,,,unaona nini?" Aliuliza mama Imma."Sioni kitu mama" Alijibu Jack."Ni kweli mwanangu ningekuwa na uwezo ningekuruhusu ukae ila huo uwezo sina macho yangu yanakutazama kwa huruma sana ,baba yako mimi na mwanangu Imma hatupendi na hapendi hata kutusikia hivyo akisikia kwamba unaishi kwangu atakuja na kuniangamiza au kunifunga". Aliongea mama Imma lakini Jack wala hakumuelewa alikataa hata kuondoka akasema lolote na liwe na nyumbani kwao harudi.....Mama Imma alimsihi sana tena kwa kumbembeleza lakini Jack hakumsikiliza mwisho mama Imma akaamua kumuacha tu.Jack alikaa hapo hadi giza likaanza kuingia....Mama Imma alitoa mchele wakawa wanasaidizana kuuchambua kwa ajili ya maandalizi ya chakula cha usiku.Huku hayo yakiendelea pale nyumbani kwa kina Jack,zilizuka taarifa za kwamba binti huyo amepotea.Mama Rachel alizongwa sana kuhusiana na wapi Jack ameelekea lakini mwenyewe akabaki na jibu lake moja tu la kwamba hajui ni wapi binti huyo ameelekea.Walit
umwa watu waende wakamtafute wakazunguka kwenye kumbi mbalimbali lakini wala hawakumpata wakarudi wakiwa hawana kitu wakatoa taarifa kwa baba Rachel."Boss binti haonekani,tumejaribu kuzunguka sehemu nyingi hasa kwenye kumbi mbalimbali lakini hatujampata,hivyo boss kama utaona inafaa basi nakuomba tukatoe taarifa kwenye vyombo vya usalama kuhusiana na binti yako".Sasa wakati kijana huyo akiyaongea hayo.....kwa mbali Jack alionekana akiingia mida hiyo ya saa mbili akawaacha midomo wazi watu hao,nyumbani kwa kina Imma....Mama Imma kama alichezwa na machale hivi akaamua kuutumia uwezo wake wote kumsihi binti huyo arudi kwao kwani endapo Mzee Ludovic angegundua kwamba mwanae yupo huko basi yangetokea matatizo makubwa sana.Baada ya Jack kuonekana pale,Mr Ludovic hakumwazibu binti huyo ila akatoa amri kali ya kwamba Jack asiwe anatoka ndani ya hilo geti na kila akitoka kwenda shuleni akirudi tu awe na mlinzi wa kumchunga na kumfuatilia popote pale.Kuna kijana mmoja aitwaye Luka ndiye aliyechaguliwa kuwa mlinzi wa kumchunga Jack mithili ya ng'ombe asiende popote pale.Jack nae alikubali tu lakini kiapo chake kuhusiana na Imma kikabaki kuwa pale pale kwamba hatatokea mwanaume yeyote wa kumuoa yeye akikua na kuwa mtu mzima zaidi ya Imma na hii ilitokana na mapenzi ya dhati yaliyokuwa yamechipuka moyoni mwa kasichana hako.Basi Jack akawa anaendelea na masomo yake na siku nazo zikawa zinapita,,,miezi ilipita na miaka nayo ikawa inakatika kama ilivyo ada.
MIAKA KUMI BAADAE(TEN YEARS LATER).......
Imma kwa kipindi hicho alikuwa tayari kashamaliza masomo yake na kurudi tena nchini.Aliajiriwa kama Daktari Mkuu wa hospital ya taifa ya nchi ya Gilgali na maisha yake pamoja na yale ya mamaye yakabadirika.Pale kwao zile nyumba za makuti hazikuwepo tena.....Imma alizibomoa zote akajenga nyumba nzuri za maana na kwa muda huo alikuwa akimiliki gari ya kifahali aina ya Hammer watu wakastaajabu mno.Pale mtaani kwao kipindi cha nyuma hakukuwa na mtu wa kukanyaga pale lakini kipindi hicho watu walianza kuhudhuria nyumbani kwa mama Imma huku wakipishana mithili ya watu waendao sokoni.Pia kipindi hicho Jack alikuwa kashahitimu masomo yake ya kidato cha sita na alikuwa akijiandaa kwenda chuo kikuu.Ilikuwa ni siku ya juma mosi saa nne za asubuhi Imma alienda kwao kumsalimia mama yake,,,sasa baada ya kufika pale na kuipaki gari yake pembeni,aliposhuka tu hakuyaamini macho yake hata kidogo.Pale nyumbani alimuona dada ake Wanjera akiwa amechakaa sana muda huo akiwa na mtoto wa miaka mitano hivi akashangaa na kuishia kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu,ila kitu kingine kilichokuja kumfariji ni kumuona Jack maeneo hayo akiwa amekaa kwa kumkumbatia mamaye.Sasa Wanjera alipomuona Kaka yake,kijana amenawiri si Imma yule wa zamani heshima ilimrudi akasimama na kwenda kumpigia magoti."Kaka naomba unisamehe sana kwa yote ya nyuma niliyokutendea kwani dunia imeshanifunza,nisamehe Kaka tuyaanze maisha mapya,nimalizie tu kwa kukusalimia shikamoo Kaka?" Wanjera hata siku moja hakuwahi kumsalimia Kaka yake kwa salamu ya shikamoo lakini siku hiyo shikamoo aliitoa kiroho Safi."Dada ni siku nyingi sana mimi nimeshakusamehe kwani hukuwa na subira na hukuwa ukijua ulitendalo,ila nataka nijue huyu mtoto ni wako au ni wa nani?" Aliuliza Imma,Wanjera akainama kidogo."Ndio huyu ni mjomba wako Kaka,anaitwa Bahati kwani wakati namzaa nilimzaa kwa bahati ".Alisema Wanjera huku machozi yakianza kumlenga lenga."Una maana gani kuyasema hayo maneno?" Aliuliza Imma."Acha tu Kaka hii ni story ndefu sana iliyojaa milima na mabonde".Alisema Wanjera baadae akasalimiana na mamaye pamoja na Jack.Baada ya salamu hizo kumalizika,Jack alimsihi Imma watoke pembeni wakazungumze...
..walielekea kwenye chemba moja wakaenda kusimama hapo."Hebu niambie sasa mchumba!!" Aliongea Imma akilitumia neno mchumba kama kumtania Jack,japo msichana huyo kigori alilichukua na kulitia kama lilivyo moyoni mwake."Juma mosi utakuwa na nafasi nikutoe out?" Aliuliza Jack,Imma akatabasamu kabla ya kumjibu,alimalizia kwa kumkazia macho binti huyo japo binti kuna aibu furani hivi ilikuwa ikiyagubika macho yake."Juma mosi bila shaka,tena nitafurahi sana Jack,mchumbaa!! Mchumbaa!!" Aliimba namna hiyo Imma Jack akabaki akicheka tu.Msichana huyo kama ni kuumbika alikuwa ameumbika na tunda lake alilitunza kwa ajili ya Imma kwani ile zawadi kubwa ya kumkabidhi Imma bikra yake haikukwepeka .Wote waliokuwa wakimtaka kimapenzi enzi zile akisoma kidato na hata mtaani hakuna hata mmoja ambaye alimkubali wote aliwakataa,moyoni akabaki na Imma pamoja na kwamba kwa kipindi hicho alikuwa mbali na upeo wa macho yake.Walielewana baadae wakarudi tena hadi pale kwa mama pamoja na Wanjera,waliongea mengineyo hadi jioni wakamaliza na kuagana,Imma akaelekea kwake,Jack nae kwao ,Mama Imma pamoja na Wanjera wakabaki pale nyumbani.Siku moja ilipita yaani siku ya juma pili.
******************************
Siku ya juma tatu ikafika........Siku hiyo Mzee Ludovic aliamka vibaya sana kwani kuna maumivu kadhaa ya mbavu pamoja na tumbo yalikuwa yakimsumbua mno.Jack kwa upande wake hakuwahi kumwambia kama Imma amesharudi na ni Daktari Mkuu wa hospital ya taifa,wala mamaye hakuwa na hiyo taarifa kwani ni miaka na miaka Mr Ludovic alikuwa ameshawapiga marufuku kutoka mule ndani bila sababu maalumu.Sasa siku hiyo Mzee akaamka vibaya,alimuita mkewe na kumwambia amsindikize kwenda hospitalini,mama Rachel akakubali wakaondoka wote kwenda huko,na safari yao ilikuwa ni ya kuelekea hospital kuu ya taifa kule ambapo Imma anafanyia kazi.
ITAENDELEA.........................................

No comments: