Riwaya:THE TRUE LOVE. . SEHEMU YA NNE (04).




Riwaya:THE TRUE LOVE.
.
SEHEMU YA NNE (04).
Maneno hayo aliyazungumza baba Rachel kama kitishio cha kumkataza mwanae mdogo Jack amuache Imma aende zake lakini Jack hakumuelewa baba yake zaidi alizidi kumshikilia kijana Imma tena akitumia mikono yake miwili .Kitendo hiki kilimkera sana baba huyo akaamua kumsogelea binti yake na kumtoa pale na ndipo Imma aliposimama na kuanza kuondoka bila hata ya kugeuka nyuma kuona kinachoendelea.
Cha kushangaza kasichana hako baada ya kuondolewa na babaye kaliingia ndani na kwenda kujifungia humo kakashinda mchana kutwa bila kula na muda wote huo kalikuwa kakilia tu,Imma japo kwa ule muda mfupi kalimtambua ni kijana mmoja wa kipekee sana na ni zaidi ya ndugu.Basi kwa upande wa Imma aliondoka akarejea kwao kwenda kumfariji mama yake,bado Imma aliamini ipo siku neema itamshukia tu na atafanikiwa na kuwafedhehesha wale wote wanaomdharau na kumuona kama hafai hana manufaa yoyote kwenye jamii.Siku ziliendelea kupita kama kawaida hatimaye miezi miwili ikakatika ,matokeo ya kidato cha sita yalitangazwa na Imma akawa amefanikiwa kufaulu kwa kishindo kwa daraja la juu kabisa yaani division one katika tahasusi yake ya masomo ya Sayansi.Muda wa kijana huyo kwenda masomoni uliwadia pia kwani alikuja kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu kimoja kikubwa sana nchini India kusomea masuala ya udakitari.Na wakati anaondoka kwenda huko aliondoka kimya kimya bila mtu yeyote kujua tofauti na mama yake pekee,dada yake Wanjera ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ameshawatenga na kuhamia nyumbani kwa yule kijana nae hakujua chochote kuhusiana na hilo.Basi Imma akawa ameenda huko na ikatakiwa kukaa kwa muda usiopungua miaka saba kwani alitaka kuunganisha na miaka kabisa ili asomee udakitari bigwa wa masuala ya mifupa.....Katika hayo masomo yake tumaini kubwa lilikuwa ni kwa Mungu kwani aliamini katika yeye hakuna kitu kitakachokuja kushindikana.Huku nyuma,taabu,majonzi na kilio zote zilihamia kwa binti mdogo Jack kila siku na kila muda msichana huyo aliyekuwa ametokea kumpenda sana Imma alikuwa akimsumbua mno mama yake,maswali ya kumuulizia ni wapi Imma anakoishi hayakukoma kiasi kwamba ikaja kufikia hatua mama yake akachoshwa na hilo na kupanga siku moja ampeleke nyumbani kwa kina Imma akamuone kijana huyo labda hatolia tena,mama Rachel aliamini hivyo na hakujua kama Imma kwa muda huo hayupo kwao yupo nchini India kimasomo na hii ilitokana na Imma kuondoka kimya kimya bila kuwaaga.Tangu kipindi kile afukuzwe na baba Rachel pale nyumbani mithili ya mbwa takribani miezi miwili ilipita bila Imma kukanyaga huko hivyo ingekuwa ni vigumu sana kwa yeye kumuaga mama Jack.Basi mama Jack akapanga siku ya kwenda kwa kina Imma na siku yenyewe ikawa ni ya juma pili jioni saa kumi na moja kasoro......alifika huko akiwa ameambatana na bintiye Jack ,binti mdogo kabisa wa miaka kumi na miwili.Walifika wakamkuta mama Imma amekaa mbele ya mlango wa nyumba yake akipepeta mchele kwa ajili ya maandalizi ya kuandaa chakula cha usiku,mama Imma aliwakaribisha vizuri na akawapa viti vya kukaa,kwa muda huo mama huyo alikuwa kashanunua viti vya plastiki hivyo hakukuwa na haja ya kuwatolea viti aina ya vigoda."Mama Rachel karibu sana hapa nyumbani japo umepita muda mrefu tangu tuonane". Yalikuwa ni maneno kutoka kinywani kwa mama Imma akimkaribisha mama Rachel pale kwake."Asante mama Imma,habari za siku nyingi mwenzangu?" Mama Rachel alimsalimia muda huo akimgeukia mwanae na kumtazama akamuona halii wala kutokwa na machozi kama ambavyo alikuwa akifanya,Jack yeye alikuwa bize tu kuyaangaza macho yake huku na huko kuona kama kuna uwezekano wa kijana Imma kutokea maana furaha yake yote iliishia kwake ."Safi tu mama Rachel".Mama Imma alijibu,hapo hapo mama Rachel akaachia tabasamu."Mama shikamoo?" Alisalimia Jack kwa heshima ."Marahaba mwanangu hujambo?" Aliitikia mama Imma huku nae akitabasamu."Sijambo mama,hivi mama Kaka Imma yupo?" Aliuliza Jack na hapo ndipo mama Rachel akadakia."Mwenzangu huyu mtoto amenichosha yaani kila siku amekuwa akinisumbua sana kuniulizia kuhusiana na Kaka yake Imma,sasa nimeamua kabisa kuja nae hapa ili angarau amuone furaha yake irejee maana imekuwa ni kero sana....kwani Imma humu ndani yupo?" Alisema mama Rachel huku akiigeukia nyumba ndogo aliyokuwa akilala Imma.....Sasa alipoigeukia tu,Jack alisimama akausogelea mlango wa nyumba hiyo akasimama mbele yake huku mkono wake wa kushoto akiwa ameuweka shavuni.Swali lile lilimfanya mama Imma atafakari kidogo kwani alianza kuwaza ni kwa namna gani amjibu mama Rachel ukizingatia hakuwahi kumwambia chochote kuhusiana na safari ya mwanae kwenda nchini India masomoni,alipopata pa kuanzia aliamua kuzungumza "Kwanza mama Rachel nipende tu kukuomba samahani kwa kutokutaarifu......Imma alifaulu kwenye ule mtihani wake wa kidato cha Sita na akawa amechaguliwa moja kwa moja kujiunga na masomo nchini India".Alimaliza kuzungumza mama Imma,taarifa hiyo ikamshtua kidogo mama Rachel,Jack kusikia hivyo aliangua kilio cha juu akawa anatapatapa lakini mama Imma akasimama na kumleta karibu yake akawa anambembeleza huku akimpa matumaini kwamba Imma atarudi tena nchini maana hatokaa huko milele."Unasikia mwanangu Jack nyamaza usilie ,Kaka Imma atarudi tu na utamuona tena sawa mtoto mzuri?" Alisema mama Imma akambembeleza sana binti huyo hadi akanyamaza.
Huku hayo yakiendelea,nyumbani kwa baba Rachel mambo yalikuwa si mambo,hii ilitokana na Rachel mwenyewe kutoboa siri kwa kumwambia baba huyo kwamba mama yake hayupo ameelekea nyumbani kwa mama Imma tena bila kutoa taarifa.Mzee mzima alikasirika sana akaapa kumfuata mkewe huko huko na akishampata basi atakiona cha mtema kuni."Rachel,hivi mama yako huwa ana matatizo gani? Ni mara ngapi namuonya kutokukanyaga kwenye miji ya watu wasioleweka ? Sasa ngoja huyu leo atanitambua". Aliongea Mr Ludovic kwa hasira mara baada ya kuambiwa na bintiye kuhusiana na mama yake alipo."Unajua baba hata Mimi mama huwa simuelewi,yaani simuelewi kabisa? Sa anaenda kwa mama Imma kufanyaje? Yule mama kwa ninavyosikia ni mchawi huwa anaroga watu,na cha kushangaza mama ameondoka na Jack akirogwa huyo Jack na jimama hilo sijui itakuaje,jimama jenyewe halina kitu kusema utaenda kuliazima". Aliongea Rachel muda huo akiibana bana pua yake.....binti huyo wa kidato cha nne anayesoma katika shule ya Sekondari ya Nsansi kama alivyo baba yake nae alikuwa na roho mbaya sana ,alimchukia Imma kutokana na umaskini wake akapitiliza hadi akamchukia na mamaye yaani mama Imma na kwa muda huo hakuwa akijua kama Imma yupo India anatafuta Masters ya Udakitari."Rachel nasema hivi acha unachokifanya tumfate mama yako huyo mshenzi huko huko maana nikiendelea kumchekea atatuletea dharau,damu yangu ya pesa kamwe haiwezi kuchanganyana na damu ya kunguni twende". Alisema Mr Ludovic nao wakatoka haraka humo ndani hadi nje wakapanda gari,safari ya kuelekea nyumbani kwa mama Imma ikaanza.Mama Rachel yeye hakujua chochote bali mazungumzo yake na mama Imma yalizidi kuendelea kama kawaida."Mama Imma labda unaweza kuniambia,kijana wetu huko ataenda kukaa kwa muda gani?" Aliuliza mama Rachel ."Imma huko atakaa kwa miaka isiyopungua saba,na ndio maana nimemwambia Jack avumilie tu Kaka yake atarudi na atamletea zawadi maana siku hazigandi". Alijibu mama Imma baadae vicheko vikasikika."Mama nami naapa kutomsahau Kaka Imma na kwa huo muda nitazidi kumkumbuka hadi pale atakapomaliza masomo yake na kurudi tena nyumbani,na nitamngojea kwa ha......?"
********************************
Kabla Jack hajamalizia neno hilo,mara ukasikika mlio wa gari ikija.....gari ilipoonekana tu tayari mama Rachel pamoja na Jack mwenyewe waliitambua vizuri kuwa ndiyo gari ya Mzee wao yaani Mr Ludovic hivyo wakabaki njia panda wakijiuliza imefuata nini pale na ni nani anayeiendesha kwa maana hawakumtambua vizuri aliyemo humo ndani.Basi ile gari ikasogea ikawa imefika karibu kabisa na ule mti mkubwa wa Mkuyu aliokuwa akipenda kupumzikia Imma.Ilipakiwa hapo,wa kwanza kushuka akawa ni Rechel,Mr Ludovic akawa wa mwisho.Walianza kuzipiga hatua kuwasogelea wakawafikia,Rachel alisimama upande wa kushoto kutoka kwa baba yake akabadirisha mapozi kama mara tano hivi , akamtazama mama Imma hapo hapo lile sahani la mchele akalitemea mate ya makohozi akasogea nyuma kidogo.Mama yake alimtazama sana akaishia kutikisa kichwa kwa masikitiko makubwa."Fyuuuuu!!!". Rachel alisonya akayazungusha macho yake na kuyaelekeza kwa mdogo wake Jack aliyekuwa amebaki mdomo wazi,mama Imma nae hakuwa na cha kufanya zaidi ya kuuondoa ule mchele uliokuwa umetemewa mate."Wewe mama Rachel,si nimeshakwambia sitaki niwe nakuona ukikanyaga kwenye nyumba zisizojulikana? Si nimeshakwambia sitaki damu yangu ichanganyane na damu chafu ya kunguni? Sasa leo utanitambua........?".
ITAENDELEA..........................................



No comments: