Simulizi ya kusisimua: SIRI YANGU Sehemu ya 01
Simulizi ya kusisimua: SIRI YANGU
Sehemu ya 01
" Rajabu niache sitaki mazoea na wewe na sitaki hata kukuona machoni mwangu " Amina alisema hayo huku machozi yakibubujika mashavuni mwake. Rajabu alijibu " Amina hivi ni kitu gani kinacho sababisha uchukue maamuzi hayo mpenzi wangu ". Wakati huu sasa Amina aliamua kuongea kwa sauti tena ya juu " Sio kwamba sikupendi na sikuitaji kuna mambo yananianda na ni Siri yanguuu!! " Amina alijishtukia amemwambia Rajabu kitu ambacho hajutegemea. Rajabu :" Nakuomba Amina wangu niambie ni Nini kinacho kusumbua huenda tukakitafutia mwisho wake, Tafadhari usinifiche. " Suluhisho pekee ni kuachana ba wewe, Rajabu naogopa Sana sababu nikikwambia lazima ni ni niii " Rajabu akadakia " ufanye Nini niambie " Sasa Amina kwa hasira alisema " Ondoka mbele yangu, Tokaaaaa!! "
Rajabu: " Amina mimi siendi popote pale sababu nakupenda na nipo radhi kwa lolote lile " Maumivu yalimujaa Amina huku machozi yakibubujika kama chemichemi kutoka ndani ya macho yake.
Amina aliulazimisha moyo wake "Sasa liwalo na liwe lazima nimwambie Rajabu Siri niliyoitunza kwa miaka 13 iliyo pita"
Amina: " Rajabu nakwambia siri hii Ila jua nikisha maliza kukwambia lazima ni niii nifee!!" Rajabu hakutaka kuwa mdhaifu na kuonyesha ungangali wake " Amina huwezi kufa nitakulinda ". Amina alianzaa kutoa Siri yake na akasahau kuwa Siri yake ndo uzima wake ila kwa sababu mapenzi kiza kinene hakuweza kujizuia.
Amina: " Rajabu mimi jina langu halisi naitwa (Kaitesi), Nimzaliwa wa mwanza wilaya ya sengerema na wala si nilivyo kwambia mwanzo , Nisamehe kwa kukudangnya kwa hilo " Sasa Amina kwa jina tunalolijua ambaye kwa sasa ni Kaitesi alikaa Kimya ili aweze kuvuta pumzi na kisha akaendelea kutoa Siri yake nzito
Amina" Wakati nilipo kuwa na miaka 8, Nakumbuka siku moja usiku sana nilitoka nje nikielekea chooni gafla mikamuona mama yangu mzazi akiwa amevaa mavazi ya ajabu yakiwa na rangi nyeusi yote, huku shingoni akiwa amevaa kibuyu kikubwa sana. Sikuweza kujizuia nikapiga kelele kwa sauti ya juu sana huku nikikimvia kurudi ndani, nilipo fika mlangoni nilishangaa mlango unajifunga wenyewe na nikajibamiza kwenye ule mlango palepale nikapoteza fahamu." Amina alilia sana huku kwikwi ikiambataba na kikohozi vilimjaa, machozi hayakukauka hata kidogo, ilikua nafasi ya Rajabu kumtuliza Amina wake.
Rajabu: pole mpenzi wangu, acha kulia jamani mie pia najisikia vibaya.
Amina: Asubuhi ilipo fika nilijikuta nimelala mapajani mwa mama yangu ..........."
No comments: