Simulizi ya kusisimua:SIRI YA YANGU Sehemu: 2&3
Simulizi ya kusisimua:SIRI YA YANGU
Sehemu: 2&3
Inaendelea
Amina:".....Nililia sana lakini kilio changu kiliyeyuka kama barafu kwenye joto, Hakuna msaada uliojitokeza mbele yangu "
Mama:"Hahahahaha basi inatosha mwacheni atulie"
Watu wale waliniachia na kwa Wakati ule sikuwa na nguvu hata kidogo huku vumbi ikinikamata mwili mzima, Gafla mama akaniambia
Mama:" Nadhani umeona mfano na maana chamoto utakiona endapo ukienda kinyume na mimi".
Nilitamani nimlaani mama lakini sikuweza, Nikaanza kumlaumu mungu wangu
Amina:" mungu mbona uliruhusu mimi kuzaliwa kwenye huu ulimwengu wa ajabu, Ona haya yanayo nikuta, Bora nisinge kuwepo nisaidie basi mungu wangu". Palepale usingizi ukanipitia.
Asubuhi ilipofika nilishangaa kujikuta nipo chumbani kwangu, Sikuwa mchafu kama nilivyo kuwa usiku.
Mama akaniita
Mama:"Kaitesi njoo mwangu unywe uji sawa"
Nilijinyanyua kutoka pale kitandani gafla nilisikia maumivu makali sana swala lililonifanya nipigie kelele kwa sauti ya juu, naamini mama aliisikia kelele ile lakini sikumuona akija kutoa msaada, ila nilisikia tu akisema.
Mama:"wewe mtoto mjinga sana unapiga kelele hivyo je Baba yako akisikia"
Na Wakati huo baba alikua ameshaenda shambani, Nilijikaza hivyo hivyo mpaka nikatoka nje alipo kua amekaa mama na nikaanza kunywa uji ule, Japo uoga ulikua nami mda wote na mama aliligundua hilo akaniambia.
Mama:"Unaogopa nini sasa inamaana kitendo cha Jana ndo unajifanya umeumia sanaaa, wewe ushakua mwanamke mkubwa inabidi uvumilie sawa, mimi natoka naenda shamba nikamsaidie Baba yako kazi Mda si mrefu narudi sawa, Ila ukimaliza kunywa uji huo utembee tembee maumivu yatapungua sawa mwanangu".
Niliitia kwa unyonge na uoga
Amina:"sawa mama ntafanya hivyo ".
Mama akawa ameondoka na nilipo maliza kunywa uji nikaanza kutembea huku na huko lakini ilikua palepale nyumbani, kunasehemu nilipofika nikawa nimejikwaa nikaanguka, sasa hapa nilihisi kama nimechinjwa kwa kisu butu.
Amina:"mamaaaaaaaa njoo unisaidie nakufaaaa, jamaniiii nisaidieni uwiiii aaah, Nifanye nini mimi jamaniiii nani wa kunipa msaada mbona mimi tu kila siku u uu uuh".
Polepole na kwa tahadhari nikawa natambaa kama nyoka aliyejeruhiwa mpaka nikafika mlangoni.
Baada ya kama dakika 2 nikaona mtu anakuja nyumbani akiwa anakimbia sana hadi uoga ukanikama kwa mala nyingne tena, alipofika ananiulza
Mtu:" Wewe mtoto mama yako yupo"
Amina:"Hayupo kwani kuna nini??"
Mtu:" Baba yako amekutwa shambani kwake akiwa amefariki, mama yako akija umpe hizi taarifa."
Nilishidwa la kufanya Wakati huo, na sasa maumivu yalinikamata mwili mzima na moyoni mwangu, Nililia sana huku nikiwaza moyoni.
Amina:"Mama si aliniaga anakwenda shamba na huyu anakuja kumuulizia mama angali katokea shambani alikoenda mama".
Gafla nilisikia sauti ikitokea nyuma yangu moja kwa moja niligundua ni sauti ya mama.
Mama:"Mbwa wewe nani aliensa shamba na nikija kusikia amemwambia mtu jambo hili nakuchinja mpumbavu mkubwa wewe ".
Daaaah kumbeama alikua ndani mda wpte.........
Inaendelea
No comments: