Simulizi ya kusisimua:SIRI YANGU Sehemu: 04





Simulizi ya kusisimua:SIRI YANGU

Sehemu: 04


Inaendelea

Amina:".....daaah kumbe mama alikua ndani mda wote na alifikaje bila mimi kujua??"
Mama:"unataka nikiwa narudi nyumbani kwangu niwe nakutaafu ety Kaitesi sasa nimerudi mwanangu"
Nilijiuliza kimoyo moyo 
Amina:"Inamaana mama anasikia kila kitu nacho fikiria??".
Mama alidakia kwa sauti ya ukali
Mama:"sio kusikia tu na kukuelewa nakuelewa vizuri sana"
Nilikaa kimya kidogo na nikaamua kumpa taarifa Mama juu ya kifo cha Baba lakini mama akanijibu
Mama:"Usinisumbue maana unaweza ukamfta Baba yako mda si mrefu".
Gafla kundi kubwa la watu walionekana wakija nyumbani wakiwa wamembeba Baba yangu. Mama alivyo waona akaanguka chini huku akitupa kanga alizo kua amezivaa akisema
Mama:"Jamaniiii mume wangu umeniacha pekee yangu ntaishi vipi mimi, Mbona umeniacha mpweke usinifanyie hivyo mwenzako bado nakupenda, Ona unaniachia Kaitesi ntamulea vipi mimi uwii uu aaah,  ungetuaga basi Baba"
Kwakweli mama alilia na akaonekana mtu ambaye alimhitaji sana Baba lakini mimi nilijua tu kua Mama anaigiza.
Majirani na viongozi wa kijiji alijaribu kumtuliza Mama lakini hawakuweza.
Mazishi yalifanyika siku hiyohiyo na Baada ya siku 3 watu wote waliondoka pale nyumbani.
Nakumbuka siku moja sema ukweli siku hii sitaisahau hata kidogo.
Siku hii nilijua wazi mama hayupo nyumbani na atachelewa kurudi, Nikaingia chumbani kwa Mama huku wasiwasi ikiwa na mimi, Nilipofika nilimkuta Baba akiwa amekaa kitandani, Na alionekana kama mtu ambaye ni punguani kwani alilia na kutoa mabovu kila mda.
Ile nataka kugeuka nitoke chumbani kwa Mama, Kumbe mama alishafika zamani kasimama nyuma yangu.
Mama:"Naona umekua mkubwa, unaingia chumbani kwangu bila ruhusa yangu, ngoja nikuonyeshe kua mimi ni nani".
Mama alinishika mkono na kunipeleka hadi jikoni akachukua sufuria tupu na kulipasha kwenye moto kusha akawa ananichoma nalo mapajani, mgongoni na sehemu zangu za si siii siriii.
Amina sasa alishindwa kuendelea kutoa Siri hiyo akawa ananila tu.
Rajabu akaamua kumtuliza mpenzi wake kwa maneno yenye ujasiri huku yeye naye mashavuni pake palilowa machozi likini alimtuliza mwenzake hivyohivyo.
Amina:" Baada ya kumaliza kunichoma akaanza kunipiga na fimbo kwenye yale majeraha aliyonichoma na sufuria lile la moto.........."

Itaendelea kesho






No comments: