Simulizi ya kusisimua: SIRI YANGU Sehemu: 5&6




Simulizi ya kusisimua: SIRI YANGU

Sehemu: 5&6



Inaendelea

Amina:"...Baada ya wiki moja nikiwa bado nipo pale hospital majibu yaliletwa kuwa nina mi mi miimba"
Swala hilo lilimshtua sana Rajabu na kuanza kujiuliza moyoni mwake.
Rajabu: "sasa Amina kama alipata mimba kwanini mtoto sijawahi kumuona??".
Ila anona bora asikilize kwanza alfu maswali baadae.
Amina:" Baada ya wiki mbili kumalizika nikaruhusiwa kutoka pale hospital, Maisha yakaanza kuniwia magumu sana mpaka nikawa natamani nirudi nyumbani kwetu nikaendelee kuishi na mama mbaya.
Baada ya Mwaka 1 na miezi 6 hiki kipindi nilikua nisha pata mtoto tena wakiume, Na kipindi hiki niliyaendesha maisha yangu kwa kufanya kazi kakati vihoter vidogovidogo sana. Wengi walijua wazi kua mimi ni kichaa, sababu maisha niliyokua nayo yalidhihilisha wazi kuwa mimi mi kichaa.
Siku moja nikiwa naosha vyombo katikati kihoter kimoja gafla mmiliki wa kile kihoter nakumbuka jina lake alikua anaitwa ( Mama ally), Alianza kutafuta simu yake na kwavile mimi nilikua naosha vyombo kando yake wazi ikasadikika mimi ndiye niliye ichukua.
Mama ally:" we mjinga naomba unirudishie simu yangu taila mkubwa, Shida zako unataka utuletee hapa, tena nakwambiaje lazima ulipe simu yangu malaya mkubwa, Mpumbavu kabisa wewe kwanza ngoja nikuonyeshe
.."
Alichukua mbanio na kunipiga nao kichwani, gafla watu wakajaa pale kama utitili, cha kushangaza watu wale walichukua Maelezo ya yule mama lakini mimi hawakunisikila. Wakaanza kunipiga kama mwizi halisi lakini sikufanya hivyo, aisee niliona maisha siyawezi
Amina:"Hivi mimi nilikuja duniani kufanya nini jamaniiii, mbona kila siku mimi, Hivi wewe mungu hunioni hata huoni magumu ninayopitia jamaniiii nihirumie.
Siku hii nilipatwa na uchungu nikatamani aridhi ipasuke niingie na kisha inifunike kwani walipo kuwa wakinipiga mtoto wangu alikua mgongoni wala sikutaka nimuache kwani nilimpenda sana.
Gafla mbaba mmoja alichukua jiwe kubwa na kulirusha kwa nguvu nilipokuwa nimekaa, cha ajabu jiwe lile lilimpiga mwanangu kichwani hadi kichwa kikapasuka sula lilosababisha apoteze maisha pale pale....."

Itaendelea.






No comments: