Simulizi ya kusisimua: SIRI YANGU Sehemu ya: 7 & 8






Simulizi ya kusisimua: SIRI YANGU

Sehemu ya: 7 & 8



Inaendelea

Amina:"...Swala lilosababisha apoteze maisha pale pale. Polisi walikuja na kunichukua haraka nikawa nimefkishwa hospital kuu ya sengerema lakini madaktari waliomba nipelekwe hospital ya mkoa  iitwayo Bugando hospital ipo mwanza mjini.
Safari ilianza nikiwa katika Gari la wagonjwa, huku hali yangu ilikua mbaya sana .
Baada ya mwendo wa kama nusu saa  nilishangaa kichwani napimepigwa na chuka kizito, Gari nililokuemo lilipata ajari mbaya  sana watu wote walipoteza maisha Ila mm tyu ndiye niliye nisulika kifo katika ajari ile.
Matibabu yakaanza juu yangu nikiwa pale Bugando hospital.
 Baada ya miezi 6 nikaanza kurudi katika hali yangu ya kawaida, nakatika hospital ile alitokea nurse mmoja akawa amenizoea sana nikamwambia maisha yangu ya nyuma huruma ikamjaa akalipa gharama zote nilizo tumia hospitalini pale na akanipeleka kwake ili tuishi wote.
Kiukweli mpaka Leo hii sijui mwanangu alizikwa au raah kiufupi sina taarifa yyte ya kumhusu mwanangu.
Jina la nurse yule alikua anaitwa ( Anna) na alikua anaishi na mume wake na kiukweli walinipenda wote kama ndugu yao wa karibu.
Dada Anna akanifungulia kiduka cha M-pesa nikawa nafanya kazi pale, Japokua sikuwahi  kutumia simu ila ilifkia sehemu nikazoea.
Nakumbuka maisha yangu yaliniendea kombo siku moja na hiyo siku ilinifanya niwa nahangaika mpka Leo hii, Siku hiyo dada Anna alienda kazini kwake usiku kwani hiyo siku alipagwa kuingia kazini usiku kama unavyo jua manurse wanavyo fanya kazi zao.
Shemiji aliita usku ule sebuleni na kuniambia
Shemeji:" Kaitesi hivi unajua wewe ni mzuri kushinda dada yako".
Amina:"Acha hizo bwana shemeji nipo napika nambie haraka umeniitia nini??".
Shemeji: "Usikilize  mrembo mimi nimetokea kukupenda kuliko hata huyo dada yako na ntakupa utakacho sawa mama".
Amina:"Mie namuogopa dada Anna kwanza wewe ni shemeji nakuheshimu jamani".
Shemeji:" ukinikubalia ntakupangishia nyumba yako mwenyew na tutaishi wote na dada yako hatajua chochote au utamwambia??".
Amina:" aah. Aaaah mimi nao naogopa dada akijuuu" kabla sijamaliza shemeji akanishika mkono na kunivuta akanilaza kwenye koshi alilokua amekaa, Sikuweza kujizuia kwani tamaa ilinikamata moyoni mwangu, shemeji akiwa pale juu yangu gafla mlango ulisukumwa kwa nguvu daaah alikua ni dada Anna aliye ingia.
Dada Anna:" haaaaah nini hicho Kaitesi unafanya nini na mume wangu si nakuuliza wewe malaya, mume wangu munafanya niniiiiii?".
Shemeji: "Yaani huyu Kaitesi ni malaya amenikuta nimekaa akanza kunishika shika gafla akanikaba anilaze nikawa nakataa lakini hukunielewa nikataka nimpige na wew ukafika, huyu ni malaya mkubwa".
Dada Anna:" Nyamazaa wewe sio wa kunifanyia hivi, Ulikosa nini kwanguuuuu.
........"

Itaendelea






No comments: