Simulizi ya kusisimua: SIRI YANGU Sehemu: 10
Simulizi ya kusisimua: SIRI YANGU
Sehemu: 10
Final chapter
Amina:"....mda huu nilikua kama tahiraa kwani maamuzi yangu yalikua hayana mwisho mzuri".
Kesho yake mida ya saa 6:30 tulienda mjini ili nikafanye biashara niliyoichagua.
Siku hiyo ilikua njema kwangu kwani alikuja Kaka mmoja anaitwa (jose) akanichukua, nilionekana mgeni wa mambo hayo akaanza kunidadisi na nikamwambia ukweli juu yangu, akamua kunichukua nikaishi naye kwani nilionekana nina hekima na heshima na kikubwa zaidi ni upole wangu.
Maisha yakaanza nikiwa na jose huku nikimsahau rafiki yangu jack na kumuona hana maana kwa sasa.
Baada ya mwaka mmoja nilipata tena mtoto wa kike kiukweli alikua mzuri sana na tulimuita (Jenipha), upendo ulizidi kutoka kwa mume wangu huku zawadi kibao zilinijia.
Tabu ilinipata na nikaanza kuangaika tena pale mume wangu Jose alipo pata Ajari mbaya ya Gari na kupoteza maisha pale pale, Maumivu yalinitawala zaidi pale msiba ulipo isha kwani ndugu za mume wangu walinitaka niondoke nirudi kwetu kwani hawakua wananijua.
Aisee nilifukuzwa kama Mbwa na sikujua pakwenda wala pakukimbilia, Wazo likanijia nirudi kwa jack nikamuuombe msamaha kwani ndiye msaada pekee uliye baki kwangu.
Nikiwa njiani naelekea kwa rafiki yangu jack, Jenipha nilimbeba mgongoni ila bahati mbaya sikuwa nimemfunga vizuri, Nikiwa kwenye Boda Boda nilishangaa watu wanapiga kelele kuja kushituka daaah Jenipha mwanangu alidondoka mpaka chini na kufa palepale kitendo kilichopelekea watu kuniangushia kipigo kama cha mwizi, sitaisahau siku hiyo.
Polisi walikuja na kunipeleka hadi hospital kuu ya mkao na Matibabu yakaanza juu yangu.
Manurse walinipima na kunihudumua kwa juhudi zote, Majibu yalitoka na nikakutwa nina ugonjwa wa UKIMWI, na cha ajabu aliye nipa Majibu yale alikua ni Dada Anna swala lililonifanya nishtuke sana.
Baada ya mda hali yangu ikiwa imkaa sawa na sikua na hata mia mfukoni nikaamua kutoroka hospital kwani ghalama sikuweza kuzimudu.
Siku ile ile nikaamua kupanda magari yaendayo dar es salaam, Ila nilipo fika morogoro nikashuka nikaenda zangu, na chaajabu kilicho nitokea sikudaiwa hata mia kwenye Bus ile.
Na maisha nikayaendesha mimi mwenyewe mpaka hapa nilipo fika Niko na wewe".
Rajabu: " Amina mbona hukuniambia kama una UKIMWI, umenia Amina".
Amina:" Sikua na lakufanya nilijua utaniacha".
Rajabu akaamua kuondoka ndani na kwenda dukani kununua bidhaa huku mawazo yalikua juu yake, akiwa njiani anaenda dukani gafla ikitokea pikipiki na kumgonga , Rajabu akapoteza maisha pale pale.
Huku Amina aliona amemukosea sana Rajabu na akaamua kusaga chupa na kunywa, Amina naye akapoteza maisha.
MWISHO
No comments: