SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {15}





          Endelea.........

ILIPOISHIA.....

"Tuliishia pale ambapo malkia Zinduna akiiushtua moyo wa Faraja kwa kumwambia mama yake yupo hai tena alihakikisha kabisa kwa kusema "mama yako bado anaishi" hivyo moyo wa Faraja ukabaki na maswali mengi,

ENDELEA...
"moyo ulipatwa na ganzi ya gafra kusikia mama yangu yupo hai, moyo ulipata shauku ya kujua mahali mama alipohifadhiwa kwa sasa, moyo ulitamani kusherehekea kusikia hilo lakini baada ya halmashauri ya ubongo kufanya uchunguzi wa haraka mwili ulinywea na kulitazama jicho la malkia Zinduna vile alivyoandaa maneno ya kusema, malkia alinitizama sana machoni mwangu akinisoma kupitia macho yangu kile ninachowaza na baada muda alipata chakuongea alisema "najua hutoamini kuhusu hicho nilichokwambia ila ukweli ni kwamba mama yako anaishi ila nasikitika kukwambia tu anaishi lakini ni katika wafu" alisema huku mboni yake ya macho ikiendelea kuyatizama macho yangu kitendo kilichonifanya nijihisi aibu nakuinamisha shingo yangu, niliinamisha kichwa na kutizama chini kisha nikajitutumua na kuipaza sauti kumuuliza "anaishi alafu katika wafu unamaana gani kusema hivyo??" nilimuuliza, malkia alicheka kidogo utafikiri sio yule aliekuwa analia muda mchache uliopita na safari hii hakuonyesha ishara au dalili ya kuongea kistarabu au kiunyonge kama hapo awali, safari hii alibadirisha hata namna ya uongeaji kabisa aliongea kwa kujimini sana huku akizidi kunitizama kwa jicho kali "Unataka kujua???" aliuliza "ndio nambie wapi yupo mama yangu?" nilimjibu kijasiri huku nikiinua shingo na sikutakata tena kuchengesha au kupepesa macho pembeni,  "anha! ni hilo tu? basi sawa" malkia Zinduna alisimama kisha akanyoosha mkono wake wa kulia ishara niushike ili anivute ninyanyuke pale chini nami nilifanya hivyo kwa kuushika mkono wake, kisha Zinduna alinivuta na nikasimama huku nikimtazama,  baada ya kusimama malkia  alianza kunizunguka taratibu huku akinitekenya kwa kidole chake cha shahada tena kwa hatua za madaha kabisa alizopiga nami nilibaki nimetulia tuli nikimtizama "Faraja ibun Wahab kijana pekee wa mzee Wahab mrisho na bi asia masasi, uliepatikana kwa tabu nyingi, hahaah aaah!! Farajaaa!! hebu nifate ikiwa unataka kuujua ukweli kuhusu mama yako" malkia Zinduna alisema kisha bila kusubiri alitoka nje na kuwakokota walinzi wote waliokuwepo pale nje ya chumba chake wakidumisha ulinzi, nami nilitoka nakumfata nia nijue anakonipeleka ndio alipo mama yangu au kuna namna anayotaka kuifanya ili anipoteze maboya,  "Malkia Zinduna nahisi kuna kitu anakiplan kwangu sio bure, huu ni mchezo kabisa anaucheza maana najua jini hili linaakili sana ya kucheza na akili za watu ila kwangu kakwama, afu kwanza ngoja na mimi nicheze mchezo akicheza  nami nacheza nae hadi kieleweke hawezi kunichezea hivi hivi anataka kujificha ili nisimjue? hapa sasa amechemka" niliongea huku tukiongeza mwendo kwenda huko ambako malkia alisema nitamkuta mama yangu, jengo kubwa kabisa la utawala ule lilojengwa kwa ustadi na wataalamu waliobobea kwenye maswala ya ramani huku likiwa limenakshiwa kwa dhahabu tupu sakafu ya ndani ya jengo lile ilivutia sana kwani kila hatua tuliopiga kuikaribia sehemu hiyo zilioenkana nyayo ziking'aa kwa kila hatu tuliyoikanyaga kwenda mbele au kurudi nyuma, tulifika sehemu moja ni hall tupu kukiwa hamna taa za kung'aa kama sehemu nyingine, huko paliwashwa mishumaa mikubwa iliotundikwa kwenye tunga maalumu zilizowekwa kwenye kuta kwa kupangwa kwa msitari ulionyooka niliyatizama kwa makini mazingira yale sikuweza kuyatafsiri kwa haraka kwani eneo lile sikuwahi kufika kabisa tangu niimgie kwenye jengo hilo la dhahabu "eneo hili linaitwa eneo la upweke" malkia alianza kuzungumza "kwanini liitwe eneo la upweke?" nami nilimuuliza "mtawala wetu wa mwanzo lucifer alipenda sana kuja kutulia maeneo haya akiwa na mawazo yake, na ile sehemu tuliopita kule mwanzo kabisa tukawasha na mishumaa ni sehemu ya kuienzi mila ya kiongozi wetu ambae mara kwa mara alipokuwa akija huku kabla ya kuingia ndani anawasha mishumaa yake miwili anaiweka pale mlangoni" alisema Malkia Zinduna, tulifika sehemu tukasimama na malkia alituomba tumsubiri hadi ataporudi tulimuacha aingie peke yake kwenye chumba hicho ambacho bado sikukielewa ndani kuna nini licha ya macho yangu kujaribu kupepesa kila upande lakini mwanga hafifu wa sehemu hiyo ulinifanya nisigundue chochote kile,  na baada ya muda kama dakika kumi hivi malkia alitoka na kusimama mlangoni mwa chumba kile kisha akafanya ishara ya kuniita kwa kidole, baada yakukiona nilimfata tukaingia kwenye chumba hicho nakuwaacha walinzi wote wakiwa nje ile tumeingia tu mlango mzito wa chuma wa chumba kile ulijifunga hivyo ndani tukabaki mimi na malkia pekee "ndio sehemu gani hii ulionileta mbona inaonekana ni makaburi haya?" nilimuuliza malkia baada yakuona sehemu hiyo ya ndani ikiwa imetapakaa makaburi makubwa yaliyojengwa kwa vioo na yale mawe meupe ya lulu yenye kutoa mwanga mkali nyakati za usiku "nimekuleta kwa makusudi  huku Faraja hii ni kwa sababu ya kukupa heshima zote za mfalme kwani hakuna jini yeyote anaeruhusiwa kuja huku ila wewe nimekupa nafasi hii adhimu kabisa kwa kukujari kukuonyesha nikiasi gani Malkia Zinduna anakuthamini" malkia alisema, vitu ambavyo vilizidi kunichanganya tu nilimtizama kwa hasira huku mkono ukitetemeka "sikuelewi malkia siulisema unanileta kwa mama yangu au?! sasa kwenye haya makaburi ndio anaishi mama yangu au vipi mbona unanichanganya?" nilimuuliza huku nikimtizama kwa jicho kari liliojaa rangi nyekundu kwa hasira "Hapana! hapana! hapana aaah! nimejisahau mfalme wangu hivi kweli ulisema kuhusu mama yako daaah!! sijui nilikuwa nawaza nini??" malkia aliongea kwa kuonyesha dharau dhahiri kabisa wala haihitaji akiri kuyafikiri maneno yake ishara za uongo ndio zilizidi kumtawala Zinduna "sasa fanya hivi geukia huku, enhee!! hivyo hivyo, alafu itaa mara tatu mamaaaa, mamaaaa, maamaaa kokote alipo atakusikia  na atakuja na usigeuke nyuma mpaka mimi nikuruhusu kugeuka umesikia?" alisema malkia " nimekuelewa malkia wangu" nilijibu "haya anza kuita" malkia aliniruhusu nianze kuita kisha yeye kasogea pembeni, nami bila kupoteza wakati nilianza kuita "MAMAAAAAA!!! MAMAAAA!!! MAMAA" Kila neno niliolitoa kumtaja mama ndani ya chumba kile palitingishika kwa mtetemo mzito sana kitendo ambacho mwanzo kilitaka kunikatisha tamaa kama sio malkia kunilazimisha kukamilisha mara tatu najua nisingelimaliza kwa uoga nilioupata, baada ya kumaliza kuita mara zote tatu nilikaa kimya kusubiri maelekezo mengine ya ziada kutoka kwa malkia, "ulimtaka mama, haya geuka umuonea mama yako" alisema malkia, taratibu niliigeuza shingo nimuone mama sikuamini kabisa baada ya kumuona mama akija anatembea pole pole tena sura yake ikionyesha furaha kubwa, nguo zake nyeupe zilizong'aa zilinifanya nimtambue vizuri "mama??" niliita kwa mshangao mkubwa huku nikianza kupiga hatua moja kumfata kule alipotokezea sikujari na wala sikuwa na muda tena wakuanza kujiuliza ametokea wapi zaidi nilifanya kile nachoweza kumlaki mama yangu "siamini mama kama ni wewe kumbe siku zote ulikuwa huku mama??" nilimuuliza punde baada ya kukumbatiana pamoja na kusalimiana "ndio mwanangu nilikosa namna ya kurudi duniani nimekwamia huku" alijibu mama, sauti ya mama ilikuwa imebadirika sana wala haikuwa tena kama ile sauti yake ya mwanzo sauti iliokuwa nyororo nyembamba kama kinanda ukimsikiliza pindi aongeapo, sauti aliokuwa nayo kipindi hiki ilikuwa nzito kama kuna mtu aliendani yake anamzungumzia "turudi nyumbani mama kwa vile nimeshakupata haina haja tena yakubaki hapa" niliongea huku nikimshika mkono kumuongoza njia, haikunidhuru akili wala kunishtua nilivyomuona mama akiwa katika umbo lake zuri lile lile alilokuwa nalo enzi yupo hai duniani kabla yakufa, wala kuchuja kwa rangi yake nyeupe iliokoza hakuna kitu kilichobadirika kwa mama tofuti na sauti tu, "Malkia nikupe shukurani za dhati kabisa kwa kunionyesha mama yangu sina cha kukulipa malkia wangu" niliongea bila kujiuliza ni wapi alipotokea mama au niwapi alipokuwa akiishi zaidi niliona vyema nitamuulizia huko tukiwa tumefika "usijari ila usiseme huna cha kunilipa" malkia alisema nilishtuka kidogo kisha nikasimama vizuri kusikiliza kwa makini anachotaka kukisema "anautaka moyo wangu nini??" haraka moyoni nilijiwazia huku nikimkazia macho malkia Zinduna akishika shika nywele zake za kisogoni "Mkataba wetu ni hadi kifo kitapotutenganisha" alisema malkia huku akichomoa kipini kichwani mwake kilichozibana nywele zake za kisogoni "unamaana gani kusema mkataba wetu ni hadi kifo ni mkataba gani huo??" nilimuuliza "kwa vile umeshampata mama yako jukumu lililopo mbele yako ni ndoa, na katika makubaliano yetu tulikubaliana hivyo" malkia aliongea kisha akanishika kidole changu cha shahada na akachukua kitu flani hivi kililichokuwa ukutani kitu kile kikiwa na uwazi mfano wa bakuri, kisha kwa kutumia ile pini yake alikitoboa kidole changu kidogo tu na damu zikaanza kutoka matone matone na kuzikingia katika kile kibakuri kisha na yeye akatoboa kidole chake na kuikingia damu yake nzito kwenye kile kibakuri, pindi tu damu yake ilivyokutana na damu yangu iliotangulia ulitokea mtetemo usio wa kawaida, ulizuka upepo mdogo ulioleta tafrani ya hapa na pale nakupelekea mishumaa yote kuzima "usiogope Faraja" malkia alisema kisha kuna maneno akayanena na mishumaa yote ikawaka, sikujua nini mana yake kunichukua damu yangu nilihisi huenda ikawa ndio kanuni ya huo mkataba wake aliousema niliyapotezea yote, tulitoka kwenye chumba kile cha makaburi na kila mtu akarudi chumbani mwake "furaha yangu ilikuwa nikumpata mama yangu tu ndio kitu pekee kilichonifanya nibaki huku hadi leo kwa kuwa mama nishampata sasa haina budi kumuomba suleyha anitoe kwenye ulimwengu huu" nilijisemea huku muda huo nikiuangalia mlango wa chumba changu ambao tayari walinzi kadhaa waliobaki pamoja na wale mabinti wa kijini wakinisubiria kwa heshima, walimpokea mama vizuri mama na kumuingiza kwenye chumba kingine kilichopo ndani ya chumba changu kiufupi vyumba vya jengo lile kwa kila chumba ni sawa na urefu wa uwanja wa mpira hata hivyo kila chumba kina milango
minne minne yenye vyumba kwa ndani hivyo kila chumba kilikuwa kimebeba vyumba vitano ndani yake, mmoja katika wale majini alipomgusa mama alionekana kushtuka na kuutoa mkono wake haraka kana kwamba mtu alieshtulia kwa shoti ya umeme "we vipi mbona hivyo" nilimuuliza baada ya kuliona tukio zima, alikataa kwa kutingisha kichwa kisha akathibitisha kwa ulimi "Hamna kitu mfalme wangu" alijibu nilimtizama sana binti yule aliejibu kwa kuonyesha shaka au kwa namna nyingine kuna kitu ameficha,
     

Ni nini kilichomshitua binti huyo?? na ile damu alioichukua malkia inakazi gani? ukweli Tutakutana hapo kesho ila hakikisha tu unabaki na mimi,..

      Itaendelea.............



No comments: