SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {16}




SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {16}


           Endelea.......

ILIPOISHIA......

"Tuliishia pale ambapo Faraja alipofanikiwa kumuona mama yake na kuruhusiwa na malkia Zinduna kutoka nae kule chini na Faraja moja kwa moja aliona vyema ampeleke kwenye chumba chake ampe hifadhi kwa kuwa chumba chake nikikubwa na tena kina vyumba vinne kwa  ndani yake, lakini alipomfikisha mmoja katika  wale  majini mtumishi wake baada ya kuushika mwili wa mama huyo alishtuka sana kama mtu aliepigwa shoti na kuutoa mkono wake haraka kisha akaonekana kupigwa butwaa lakini alipotezea Faraja asijue hilo,

ENDELEA..
..wewe mbona umeshtuka hivyo shida nini?" ilibidi nimuulize baada ya kuona vile alivyoutoa mkono wake haraka "ha.! ha..! hapana mfalme hakuna kitu mi..! mi..! niko sa. sawa" jini yule aliongea kwa kitete kikubwa hadi maneno yake yakawa yanatoka yakiwa nusu nusu nilimtizama kwa muda mchache lakini ile hofu yake ilinifanya nishtuke kidogo licha ya kuwa nilimuacha ampeleke mama akamuonyeshe chumba chake atachokuwa anapumzika,
         ★★★★★★★★★★★★
Mchana wote nilikuwa nafuraha tu kwa kuona tayari nimefanikiwa kumpata mama akiwa hai, huku wazo la kumfikiria baba likiwa halipo kabisa kichwani mwangu, upande mwingine wa akili uliwaza nimtoroke malkia Zinduna nirudi duniani lakini pia nikifikiria maisha ninayoishi kwenye ulimwengu ule basi hata radha ya kuifikiria dunia yangu inapotea kabisa, nikiwa nimejilaza kitandani mchana huo wazo likanijia kisha baada ya kuona ni wazo zuri nilitabasamu na badae nikaamkaa bila kuomba usaidizi wa mfanyakazi niliamua kubadirisha nguo zangu za kifalme, nakuvaa nguo za kawaida tu na kuchukua mkoti mmoja mweusi mrefu ulioburuza mpaka chini tena uzuri wa mkoti ule ulikuwa na kofia kubwa kabisa iliokifunika kichwa kizima, niliva kisha nikatoka kwa wizi kwa kupitia mlango wa nyuma wa chumba changu ili walinzi wasijue kama nimetoka ndani, laiti kama wangelijua wasingeweza kuniruhusu nitoke kufatia amri ya malkia Zinduna, hivyo nilitoka kwa siri sana, kwa makisio ya jua lenye mwanga hafifu wa dunia hiyo nilihisi itakuwa saa kumi na moja hivyo nilitaka nizurure kwa muda wa nusu saa pekee kisha nirejee ndani ya mjengo, baada yakutoka tu nje nilianza kwa kuzungukia maeneo ambayo sikuwahi kufika lakini kila kona niliopita nilishtuka baada ya kuwa nakuona kuna mtu alifanana sana na malkia Zinduna akiwa amesimama akinitizama kwa jicho kali, mwanzo niliona ni mawazo tu huenda ile hofu ndio inayonisumbua lakini baada ya jambo lile kunirudia zaidi ya mara mbili lilinitisha sasa nikahisi kabisa huenda malkia Zinduna ananifatilia kwa kila hatua nitayoipiga, hivyo niliamua nirudi mjengoni na hakuna kitu nilichokipata nje, kwa kutumia njia ile ile niliyotokea ndio na hivyo niliitumia kirudia na hata nilipoingia chumbani mwangu hakuna mlinzi alienishtukia, nilikaa kitandani kwa muda lakini hapo wazo likanijia nimuite yule kijakazi nimuulize kilichomshitua asubuhi ni nini "kuna mtu hapo??" niliuliza kwa sauti kali, kwani nilijua wazi kwa pale nje hawezi kukosekana kijakazi yeyote, na wote walikuwa wakisimama kwa nje kuingia ndani hadi awe na kazi maalumu itayomfanya awepo ndani, alijitokeza kijakazi mmoja na kusimama karibu kabisa na mlango kisha kwa utiifu aliinamisha shingo yake "nimeitika wito wako eeh!! mtukufu mfalme" kijakazi yule alisema, "mwenzako yuko wapi??" niliuliza kwa maana majini hawa ni wageni hata majina yao sikuyahifadhi kichwani, "wapo nje mfalme" alijibu "muite yule mrefu mwembamba" niliendelea kusema "napokea na kutii amri yako eeh!! mtukufu mfalme" alisema binti yule kisha akatoka, muda huo huo aliingia yule binti mwingine ambae asubuhi alionekana kushtushwa na jambo lakini hakutaka kuliweka wazi alilimezea ndani kwa ndani "nimeitika wito wako mfalme wangu" alisema huku akitizama chini "hebu sogea karibu kwanza" niliongea huku nikitafuta pozi zuri lakukaa kitandani ili nimuulize vizuri "hivi unajua adhabu itayokupata kwa kumdanganya mfalme wako?" nilianza kwa kumuuliza swali kwanza lililomshtua aliinua shingo yake nakunitizama kisha akajibu "ndio mfalme natambua hilo" alijibu "anha! kumbe unaijua unaweza kuniambia ni  adhabu ipi?" nilimuuliza tena "nikukatwa kichwa mbele ya halaiki na mwili hutupwa kwenye kisima cha damu" naye alijibu "safi sana! binti mzuri sana wewe, kama unaujua ukweli wowote kuhusu mama hebu nambie na ichunge ulimi wako usije kukuponza, we nambie ukweli tu wala sitoweza kukuumiza iwapo utanambia kila kitu" niliongea kisha nikanyamaza kidogo na baadae nikaendelea "Kwanini ulipomgusa yule mwanamke ulishtuka sana na ukautoa mkono wako haraka??" nilimuuliza na kumtazama  sana huku moyo ukiwa na hamu yakutaka kusikia jibu lake, "kwa kiapo nilichokura mfalme wangu nikupokea amri zako pamoja nakutii hivyo nisingependa kuonyesha utovu wa nidhamu mbele yako" alisema kijakazi yule mwenye upole asilia tokea siku ile nianze kumuona hakuwahi kuonyesha kiburi au chembe chembe ya dharau, juu ya kwamba kiongozi wake ni binadamu yeye niwakupokea na kutii kile atachokisikia kutoka kwangu, "ndio useme sasa" nilimkazia pale pale ambapo bado alionekana kusua sua mdomo wake kuwa mzito kuongea "nakwambia kila kitu mfalme wangu" alisema kisha akanyanyua shingo yake aanze kusema kile kikichompelekea kuutoa mkono kwa mshituko asubuhi pindi alipomgusa tu mama "yule si..!!" kabla hajafungua ukurasa wa kuumimina ukweli gafra alitoka ndani haraka mama na kusimama kwenye mlango wa chumba chake huku akimtizama binti yule kwa jicho baya,  nae binti yule baada ya kumuona alipata kigugumizi cha gafra na kushindwa kuendelea kuongea alianza kutetemeka tu "vipi tena mbona husemi?" nilimuuliza kwa mshangao kwani nilikuwa nimeshaifungua milango ya fahamu kusikiliza huo ukweli wake lakini baada ya kumuona na hari ile ilibidi nisimame nimsogelee pale aliposimama, nilimfikia binti mikono ikiwa inamtetemeka kiasi kwamba ukimuangalia utafikri ni mtu alievishwa viroba vya barafu wakati wa baridi nilimkumbatia kwanza ili nimpunguzie uoga kwa kiasi "waweza sema kama unaogopa asisikie" niliongea huku nikiwa nimemkumbatia "Hu.. huu.. si. si.. oo.. ma..! ma ya..ya.! ko" aliikamilisha sentensi yake kwa ugumu hivyo hivyo huku meno yake yakigongana gongana, nilishtuka na kumsukuma kwa nguvu binti yule "nini wewe???" nilimuuliza huku nikimtizama kwa hasira, binti hakunijibu zaidi aliendelea kumtizama mama pale aliposimama mlangoni na kisha mama alirudi chumbani bila kuongea neno lolote,  pindi alipotoka tu ndio na yule binti akapata nafasi yakuongea vizuri "ukweli kabisa yule sio mama yako nakuapia yule sio mama yako" alisema binti yule "Funga mdomo wewe" niliongea kwa ukari kwa maana maneno aliyoyasema yalinichanganya tu "kweli mfalme wangu" aliendelea kusema huku akiwa amepiga magoti na kuinamisha shingo yake "TOKA HAPA!!" niliongea kwa hasira kana kwamba hata nilitamani nimrukie nimdhuru kwa maneno yake yaliyojaa mauzi "sawa mfalme napokea na kutii amri yako ila zingatia mfalme wangu upo kwenye hatari sana zin..." "NIMESEMA TOKA NJE SITAKI KUSIKIA UPUUZI TENA UNAOUONGEA" nilimkatisha binti yule baada ya kuona anazidi kunifukunyua hasira zilizopo ndani kabisa, "WALINZI NJOONI HARAKA MUITOE HII TAKA TAKA HAPA" niliwaita walinzi nao walinzi hawakupoteza muda waliingia ndani haraka na kumbeba mzega mzega kumtoa nje, licha ya kuwa nilikuwa na hasira lakini maneno machache ya yule binti yalinipa fumbo kubwa, ubongo wangu ninao uamini kwa kufikiria haraka nilijikuta ukishindwa kuyatafsiri maneno ya yule binti mwisho niliona hayana maana "mshenzi kabisa amekosa yakusema anamsakizia mama yangu eti sio mtu kwa hiyo ni nani? n'ka! ningejua hata nisingemuuliza" nililaani vikari kitendo cha kumuuliza binti yule kisha nikajitupia kitandani,
  ★★★★★★★★★★★★★
Masaa kadhaa yalipita tokea yule binti aondoke na kuniacha na mawazo, na sasa ilikuwa ni usiku totoro, usiku ambao hakuna shughuri yeyote inayofanyika ya kulijenga taifa hilo kubwa la kijini, na kama unavyojua usiku una mambo mengi, nikiwa nimelala kati kati kabisa ya usiku nilishtushwa tena na pete baada ya kuanza kudunda dunda kwa kasi na tena safari hii haikuwa kama siku ile, safari hii ilidunda kwa kasi huku ikitoa kiashiria flani cha sauti kama saa kikilia 'ntiti, ntintii, ntiii' nilishtushwa na sauti hiyo hivyo niliamka na kukaa kuiangalia pete hiyo ya ajabu vile ilivyowaka waka na kuitoa sauti ile ya ajabu "Nimeshazijua  ishara za pete hii hapa kutakuwa na shida hapa ngoja niamke" nilijisemea huku nikisimama kutoka kitandani, ghafra bin vuu!! katika chumba cha mama nilisikia sauti akicheka na mara kama analia, wasi wasi na mashaka vikanitanda na ubongo ukauongoza mwili kukisogelea kitasa cha mlango wa kuingilia kwenye chumba cha mama taratibu nilikinyonga kitasa na kuingia ndani nikiifata ile sauti, nilipoingia tu pete iliacha kutoa ile sauti yake zaidi ilizidi kudunda dunda tu, nilifata sauti ile mpaka kwenye chemba moja ya chumba kile kisha nikajibana kwenye kona ya ukuta huo na kuchungulia nilishtuka baada yakuona viumbe wapatao kumi wote wakiwa na maumbo na sura zao zilizofanana na mama wakicheza cheza huku vifua vyao vikiwa wazi na magamba magamba kama ya mamba na nyuma ya migongo yao zilionekana mikia mirefu,
___
___
___
Haya Malkia Zinduna alitoa pete kama zawadi na  leo ndio inazidi kufanya maajabu kwa Faraja wewe unafikiri atafanyaje hapo??

NYUMBANI KUMENOGA
        #BAKI_NA_MIMI&
       ITAENDELEA...........



No comments: