SIMULIZI:- >ZINDUNA, (malkia wa majini) SEHEMU YA {17}
SIMULIZI:- >ZINDUNA, (malkia wa majini)
SEHEMU YA {17}
Endelea......
ILIPOISHIA......
"Tuliishia pale ambapo Faraja alipozinduka usiku na ile pete ikimuonyesha njia na kubahatika kuona kwenye chumba alichoishi mama yake kuwa ni mauza uza matupu,
ENDELEA NAYO......
Moyo ulipatwa na hofu kubwa huku macho nayo yakizidi kutizama viumbe wale waliokuwa busy wakicheza,.. moyoni nilijiuliza "ina maana kweli yule jini alisema ukweli eti? afu nikajifanya kumkatalia?" nilijiuliza huku nikizidi kuwatizama niliona wazi ile sio sehemu salama kuendelea kubaki kuwaangalia kwani tayari moyoni mwangu nilikuwa nimeshapata jibu kuwa ule ulikuwa ni mtego wa malkia Zinduna na wala sio mama,
Asubuhi ilifika huku nikiwa juu juu nisietulia kila nilipojaribu kufanya hili niliona haliendi kufatia tukio zima la usiku lililonivuruga zaidi akili, aliingia yule jini alienyonyesha kuujua ukweli kuhusu yule jini mwenye sura kama ya mama, akiwa anaitua chai mezani niliona ndio nafasi nzuri kumbana anambie ukweli kwani zile hasira zote za jana niliona hazina maana tena "Mheshimiwa" alinita baada ya kuona nimemvuta bila ridhaa yake na kumbana ukutani huku nikimtizama machoni "Ndio, na leo sitaki uniite mfalme nataka unambie ukweli wote kuhusu yule mama jana nilikuwa na hasira tu hivyo sikuweza kunyumbua chochote sema tu kwa usalama wako" niliongea huku nikimbana mikono yake "leo ndio umeujua ukweli??" aliuliza "sitaki kujua hayo nambie tu ukweli unajua nini kuhusu yule mwanamke aliekushtua jana?" nilirudia swali langu na safari hii nilitishia kwa kumkazia macho, "kiukweli yule sio mama yako, Malkia Zinduna ni malkia wetu na ndio anaetawala miaka yote malkia wetu anauwezo wa kufufua wafu hata kuwatoa duniani na kuwaleta huku pia malkia Zinduna ndio anaetoa utajiri kwa wote binadamu wanaomuomba ila kwa wale wanaompinga malkia ni mwenye roho mbaya sana huwa anawauwa bila huruma, na huyo mama nilivyomgusa nilipata maono kuwa sio binadamu bali ni jini mbaya wa makaburini aliekutwika nae, alafu kingine cha haraka ambacho ningependa nikushauri fanya haraka kuondoka kwenye ulimwengu huu kabla mwezi mchanga mwekundu hujachomoza zingatia karenda na muda wa mwezi kwani kila utokezapo mwezi haya maumbo yote ya ubinadamu hupotea na hubaki na maumbile yetu ya asiri tukibaki vile hatuna akili tena za kumtambua binadamu hivyo utakufa, Faraja hakuna jini asiekujua huku kila jini anakujua kulingana na karama tuliopewa na mungu ya kuona mambo mengi ya sasa baadae hata mwezi au mwaka huko mbele hivyo nikingalia maisha yako nauona mwisho mbaya iwapo utaendelea kudumu katika sayari hii" jini yule aliongea maneno mengi na mazito yaliyonifanya ninyong'onyee kabisa kisha nikamuuliza tena "bado siku ngapi kuchomoka kwa huo mwezi mpevu mwekundu??" nilimuuliza "kwa kweli bado sijayajua majira vizuri ila ipo karibu" alinijibu "na vipi kuhusu kutoka naweza kutoka hata sasa hivi??" nilimuuliza huku nikimuachia mikono yake nae akajitengeneza vizuri gauni lake na kusema "kwa sasa hivi haitawezekana kutokana na ulinzi mkali uliopo kwenye milango yakutoka na kuingilia zoezi hili kama ungeweza ungelifanya majira ya saa mbili usiku au asubuhi ndio majini wengi huwa katika dini zao wakifanya ibada" alijibu "anha!! sawa nimekuelewa waweza kuondoka sasa ikiwa nitakuwa na shida nitakujulisha" "sawa mfalme wangu niite Nuriath" alijitambulisha jini yule kisha akatoka na kuniacha nikizunguuka ndani ya chumba kile, kiukweli kwa maneno ya Nuriath nilikiona chumba kidogo nikitamani hata nitoe mabwa kama suleyha nipae,
UPANDE WA PILI WA SHILINGI..
"jamani hilo jambo naona tuliache yule binadamu kaisha tushinda ujanja kwa sasa hatuwezi kumdhibiti tena kutokana na ulinzi alionao" sauti ya kiongozi wa wale majini waliopinga alitoa sababu iliochafua hari ya kikao chao "hapana hawezi kutushinda nguvu maruhani siye tuna nguvu nyingi tunapaa tunauwezo wa kumungamiza hata sasa hivi Atatushindaje?" mwingine nae alitoa hoja yake "Ni kweli alichokisema baba kuwa tumuache kwa kuwa tumeshatumia njia nyingi zimeshindikana mkumbuke siku chache hapo mbele ni mwandamo wa mwezi mwekundu hivyo hana sehemu atayoishi binadamu huyo atakufa tu" waliendelea kusema wakirumbana kwa hoja mwisho wa yote waliamua jambo moja la kumuacha Faraja na shabaha yao kubwa walilenga siku ya mwandamo wa mwezi mwekundu ndio itakuwa siku sahihi ya kumuangamiza, walicheka sana na kugonga mvinyo kwa pamoja wakisherehekea wakiamini kabisa mwisho wa Faraja umefika,
Baada ya masaa kadhaa kuketi na kufikiria njia nzuri moyo wangu ulipata aibu kubwa sana kwani ni siku chache tu ambayo nilimwambia suleyha nimefanya maamuzi ya kubaki kwenye ulimwengu ule nikichanganya na maneno ya jini Nuriath wallah nilihisi akili kuchanganyikiwa, nilinyanyuka na kuchungulia ulinzi kwanza ulivyokaa kisha nikajua idadi ya walinzi waliopo nje ya chumba changu pamoja na wale wanaofanya doria nilichunguza yote nakujua muda wa kubadirishana windo licha yakuwa wao hawakulitambua hilo waliponiona natoka toka walihisi huenda napata upepo tu hawakujua kama ndio nilikuwa naisoma ramani nzuri ili muda ukiwadia nitoke vizuri kwenda kwa suleyha ili anitoe kwenye jengo hilo, kwani jini pekee aliejua jengo hilo kwa ufasaha ni suleyha pekee na ndo maana malkia Zinduna baada ya kugundua kama kunachembe chembe za mahusiano alimuhamisha haraka ili asije kurubunika kunitoa nje ya ulimwengu ule na kunirudisha duniani, baada ya kuyachora vizuri mazingira niliona sasa ni muda wakukaa kusubiria muda tu ufike ili usiku nimfate suleyha anitoe kwenye jengo lile, nilirudi na kukaa kitandani ghafra nikiwa pale alikuja mjumbe alietoka kwa malkia Zinduna na kunipa wito kuwa nahitajika kwa malkia Zinduna sasa niliona huu ndio muda muafaka wakupoteza muda kwa malkia hivyo nilijiandaa vizuri na kupendeza kama mfalme kisha nikaongozana na walinzi wanne tu safari hii sikutaka ulinzi mkubwa kunifata fata, moja kwa moja tulifika chumbani kwa malkia niliwaacha walinzi nje wanisubirie nami nikazama chumbani ambapo nilimkuta malkia Zinduna akiwa amejilaza kitandani huku akiwa amevalia nguo zake nyepesi nguo ambazo ziliuchora vizuri mwili wake, nilipoingia tu moyo ulishtuka baada ya kumuona malkia alipokuwa amejilaza kitandani na mapaja yake yote yakiwa nje, misuri yote ili simama nilijikuta ikisimama bila ridhaa yangu sikuwaza kitu kingine tena zaidi niliwaza kumsogelea malkia Zinduna akanitekeleze Matamanio yangu aliniita kwa kidole kimoja nami taratibu niliitika na kusogea kitandani kwake kulipokuwa kumepambwa vizuri huku chumba kizima kikienea harufu za ubani pamoja na marashi makari "Nimekuita mfalme wangu unipe haja ya moyo wangu kama malkia, Hakika Mwili wangu nimeitunza kwa muda mrefu nikiamini kabisa wewe ndio utakuja kunionyesha Dunia nyingine, nionyeshe utaalamu uliofanya siku ile Faraja najua wewe unajua sana kushiriki tendo la ndoa ile siku nilikuona ulivyoshiriki na wale wewe hujui tu moyo wangu nikiasi gani ulilitamani hili?" malkia alisema huku akijipambua kavazi kake kepesi kalikoficha mwili wake tu na huku sehemu nyingine kukiwa wazi "hebu tizama mwili wangu Aujawahi kuguswa na kiumbe yoyote nimeutunza kwa ajiri yako tu uje nikufurahishe vile unavyotaka, nimeihifdhi Ujana wangu wewe ndio uje ulitoe kasha lake, mwili wangu huwa unasisimka kabisa kila nikifiria ule utaalamu wako" alisema malkia siku hio alinishangaza kabisa kwa kuongea maneno yaliyonishinikiza kuwaza Tendo la Ndoa tu na muda wote akiongea Malkia Zinduna,. Mwili wangu ulikuwa unasisimuka,.. "sawa malkia mi nipo kwa ajiri yako" nilisema kisha nikaanza kulivua jola kubwa niliokuwa nimelivaa na kubaki mtupu huku nikiendelea kuutizama mwili wa malkia Uliokuwa wazi Ukinisubiria kutekeleza lile aliloliitaji lakini kabla hata sijaanza chochote malkia alisema "ah!! ah!! usinishike na hiyo pete ivue kwanza iweke pembeni" alisema malkia..
*ANA MAANA GANI??@
Inakuwaje tena malkia Zinduna pete ni yake kwanini aiogope? na vipi kama Faraja ataivua pete?? usikose muendelezo wake,
#HATUPOI___HATUBOI
Itaendelea.........
No comments: