SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {18}




SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {18}

           Endelea........

ILIPOISHIA...
tuliishia pale ambapo malkia Zinduna alipomuita Faraja kwenye chumba chake nia ampe Huba lakini kilichonistua zaidi ni swala la malkia kumuomba Faraja aivue pete ana maana gani??

ENDELEA NAYO,,,,,,

"Pete hii ni ya ajabu sana iwapo utanigusa nayo nikiwa hivi sina Nguo itanichoma kwa kuwa ni pete yenye uwezo mkubwa, tafadhari Faraja ivue tu" malkia alisema kwa upole huku akifunika macho yake kwa uoga pindi aionapo pete ile, nilibaki kuyastaajabu ya musa kwani pete ile yeye ndio aliitoa kama zawadi na siku anayonipa na kumbuka alinipa akiwa ameishika vizui tu "kwa hiyo bila kuivua hii pete hunipatii Huba?" nilimuuliza huku roho ya tamaa ya Tendo la ndoa ikinilazimisha niivue pete, "ndio kwa sababu pindi tunapokuwa Atuna nguo  tukidiriki tendo la ndoa tunaikosea adabu wewe ivue iweke mbali siye tuendelee" bado malkia alizidi kuongea kwa sauti iliozidi kuushawishi moyo wangu kuivua pete "hii pete inakawaida ya kumulika wabaya yawezekana anania mbaya sio bure huenda ameshagundua mpango wangu wa kutoroka ndio maana ameona anivue pete kiakili sasa na mimi siivui" nilijisemea kimoyo moyo huku nikiamka na kukaa kitandani na kutafuta sababu tofaauti ili tu nisiivue pete "Faraja mbona umekaa tena??" "najihisi kizungu zungu malkia sijui kwanini" nilimjibu huku nikimuonyesha kwa kushika kichwa "mmh!! yani kimeanza sasa hivi tu?"aliuliza tena kwa mshituko huku akiamka na kukaa akiendele kunitizama "nisindikize malkia nikapumzike kwanza sitoweza kuendelea nikiwa na hali hii" niliongea kwa kufanya maigizo kabisa yaliyompelekea Malkia Zinduna kuyaamini kiasi "Mama alinambia jini anauwezo mkubwa wa kuona lakini mimi namfanya kama ninavyotaka kwa sababu nimekaa nao nimegundua tabia zao na madhaifu yao kama uliona kigezo ni kunidanganyia mapenzi ili unitaifishe pete akili yangu imesimama kidete sasa" nilijisemea huku nikiwa nimejilegeza utazani kweli mgonjwa "kinauma sana eeeh!!" malkia Zinduna aliuliza kwa upole  wa kinafiki huku moyoni mwake akijisemea "Umepona!! na sijui unaakili gani wewe kijana najua kuendelea kukuacha na hii pete wakati bado hujaapishwa kuwa mfalme itanigharimu siku moja, hivyo basi nitafanya juu chini pete irudi mikononi mwangu tena" alijisemea malkia kisha akasimama nakuvaa gauni lake lingine hapo ndipo aliita mlinzi mmoja aliepo pale nje ya chumba chake na mlinzi huyo alipoingia  tu malkia alimuomba anisindikize mpaka kwangu licha ya kuwa kuna lugha ambayo waliotumia kuzungumzia kwani sio kila jini alikuwa anakijua kiswahili, jini yule mlinzi alipomaliza kupewa maagizo marefu basi alinishika mkono  Nakuniongoza njia kitendo ambacho nilishtuka ni hiyo ya kupewa mlinzi wa malkia ikiwa na mimi nina ulinzi pia, anyway sikujari nilitoka kwenye chumba chake na kuungana na wale walinzi wangu wannne kurudi chumbani,

nilifika na kujitupia kitandani licha ya kuwa ilikuwa bado ni asubuhi, nilijikuta napitiwa na usingizi, nilikuja kuamka badae sana na kuona saa itakuwa muda umesogea mbele nijaribu kuwatoroka wale majini, lakini nilishtuka baada ya kukuta jini mmoja lenye maumbile ya kiume likiwa limesimama mbele yangu tena likiwa uchi wa mnyama na sio kawaida kwa chumba changu kua na jini wa kiume "wewe ni nani tena?" niliuliza huku mapigo ya moyo yakienda kasi "nimeagizwa na malkia nije nikupe kampani" liliongea jini lile kwa kujirembua kama mwanamke "Eti niini??? kampani?!! kampani gani hiyo aliyokuambia? mi sihitaji kampani bwana" niliongea kwa uoga huku jini lile nalo likizidi kunisogelea kabisa "amesema nikupatie mahaba" "shenziii we si dume tutafanyaje mahaba ya jinsia moja" nilifoka "lakini mi nataka" nalo liliongea huku likianza kupanda kitandani kunisogelea pale nilipofika kikomo kwa kugota ukutani, niliona sasa jini lile limedhamiria kufanya kile lilichotumwa kuja kukifanya, likiwa limebakiza sentimita chache sana kunifikia nafsi ya pete ilianza kutweta na ikautoa mwanga wake ule wa ajabu na kummulika kama jua jini yule alietaka kufanya Mahaba, jini lile lilichomwa vikari na mwanga ule wa ile pete kisha likayeyuka kama vumbi nakuvutiwa ndani kabisa ya ile pete na baada yakuishia ule mwanga ulipotea tena na pete ikazima nilishukuru kwa mara nyingine kwa kunisaidia kisha pale pale nilibandika jina "HII NI PETE YA BAHATI" niliongea na kutandika busu lete ile baada ya lile jaribio kulifuzu nikiokolewa na pete,

 ★★★★★★★★★★★

Kama vile asubuhi nilivyokuwa nimeisoma ramani nzima hivyo ilivyofika usiku niliona sio muda wakulaza damu kwa kuwa malkia ni mweredi angeweza kulitambua swala la kutoroka hivyo niliona nifanye haraka iwezekenavyo niende alipo suleyha ambae ndio niliona mwokozi wangu, Nilipita vizuri tu kwa kuwa nilikuwa nimeshajua mapungufu ya walinzi wale kisha nikanyoosha na floo hadi kilipo chumba cha Suleyha ambacho kilikuwa hakina ulinzi wowote licha ya kuwa alipewa cheo kikubwa kwenye utawala huo "We Faraja kulikoni usiku wote huu??" aliuliza suleyha punde baada ya kunifungulia mlango wake na kuingia ndani "suleyha hatuna muda wakuendelea kusubiri hapa, we cha kufanya nitoroshe usiku huu huu nimechoka kuishi huku" niliongea huku roho ikiwa juu juu "wewe Faraja unahakika hakuna alieshtukia hili??" suleyha aliuliza "Ndio nimewatoroka walinzi hawajaweza kugundua hilo" nilimjibu "sasa sikia chukua hiki kibegi nilikuandalia zawadi ya mawe lulu pamoja na jedi na vito na pete na mikufu mingi ya thamani itayokusaidia huko duniani" alisema suleyha na kunikabidhi kile kibegi kizito chenye mali nyingi "ahsante" niliongea na kukitwika kibegi kile mgongoni "usiseme ahsante bado hatujatoka" suleyha alisema, muda huo huo Pete nayo ilianza kudunda dunda kama taa ya endiketa hapo nilijua wazi huenda wale walinzi waneshashtukia dili kuwa mule ndani nimeshatoka hivyo watakuwa wananitafuta "Pete imeshanijulisha alama ya hatari hii watakuwa wanakuja upande huu tufanye haraka tuondoke" niliongea huku haraka nikisogea pale mlangoni na kuchungulia kwa nje kama kuna mlinzi yoyoye ataekuwa anakuja kwa upande huo, "chukua mkoti huu uvae weka na kofia ili usigundulike alafu vua na hizo nguo za kifalme isije kuwa rahisi kukamatwa" alisema suleyha na kunikabidhi mkoti mrefu mweusi niliouvaa muda huo huku na kulifunika lile begi "fanya haraka haraka kuna vishindo nimeanza kuvisikia vinakuja upande huu" niliongea, suleyha alifanya haraka kubadirisha nguo zake kisha nae akavaa koti lake, vishindo vizito vilizidi kusikika kujongea upande wetu nayo pete ilizidi kutweta tu kuashiria alama ya hatari inayotusogelea, kwa mara nyingine nilichungulia tena kuangalia usalama, lahaulaaaaah!!!  macho yangu yalikutana na jeshi kubwa la kifalme liliojongea chumba kile huku wakiwa na siraha zao za kivita na cha ajabu zaidi waliongozwa na wale majini saba wenye sura ya mama yangu "mungu wangu wamejuaje kama nipo huku??" nilijiuliza kwa hofu huku haja kubwa na ndogo vikitaka kutoka kwa pamoja,

  -HATUPOI HATUBOI-

Ndio kwanza tunaanza mchezo, vipi suleyha atafanikiwa kuyaokoa maisha ya Faraja na kufanikiwa kumtoa kwenye ulimwengu huo ilihari taarifa imeshavuja???? 

       -BAKI NA MIMI-

ITAENDELEA,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,



No comments: