SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {19}
SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {19}
Endelea............
"Kitifu tifu ndani ya jengo la kifalme ndani ya utawala wa majini linaibuka baada ya Faraja kutambua yote kuwa Malkia Zinduna alimchezeshea mchezo kwa kumdanganyishia jini kuwa mama yake, na hatimae Faraja alipata hamasa ya kuondoka kwenye jengo lile kwa kupitia kwenye mikono ya suleyha siku hiyo usiku alipomwendea suleyha watoroke hakujua kama siku hiyo walinzi walishtukia hivyo ulinzi uliongezwa kwenye chumba cha suleyha hata kabla hawajatoka lilionekana jeshi kubwa likija maeneo yale Faraja aliogopa na hakujua huo msala wanausave vipi..
ENDELEA NAYO.....
"Kama ulisikia moyo kudunda basi siku hiyo moyo wangu ulidunda nahisi ni mara mia zaidi ya siku zote kila nilipochungulia kidogo nakuwona wale walinzi wakiukaribia mlango basi matumini yalipotea kabisa "sasa tutafanyaje suleyha tayari walinzi wameshagundua mpango wote?" nilimuuliza suleyha huku nikiwa nimehaha sijui nifanyeje, suleyha alinitizama kwa muda mchache kisha akasema "niachie mimi hilo" licha yakunipa moyo lakini bado niliona haitoshi hivyo niliamua kukimbilia kwenye kichemba kimoja kilichokuwa na giza kabisa na kujibana kiasi isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kuniona.. mara pupuu!! pupuuuu!!! sauti za kupigwa kwa mlango zikasikika na aliepiga mlango ilionyesha nikwakiasi gani anauchu na kile anachokitafuta "Nyie nini na masiraha yenu usiku wote huu???" suleyha aliuliza baada ya kuwa amefungua mlango nakutanda mlangoni akiwatizama walinzi wale ambao walikuwa wanatupia macho yao mule chumbani "kuna mtu tunamtafuta" mlinzi mmoja alisema, niliposikia moja kwa moja niligundua tayari mchezo umeungua hivyo nilitega masikio yangu kusikiliza kwa makini "Mtu?? mnawazimu nyie kwaiyo mmeona mimi naishi na mtu hapa?? hivi nyie akili zenu ziko sawa kweli mnajitambua kweli nyie??" suleyha aliwauliza "Kuna binadamu mmoja ameiba tufani ya malkia ile ya dhahabu na mikufu" aliongea jini yule kitendo kilichonifanya niishushe pumzi kwani nilielewa wale sio katika wale walinzi wanaokilinda chumba changu, "washenzi sana nyie kwaiyo mmeona mimi ndio nahifadhi wezi au?? kazi kusumbua sumbua tu nimelala mimi kama mimi na kama mnataka kupekua muingie mpekue si amniamini na humu kuna mabinti wengi waliolala sasa ingieni kama hamna adabu" suleyha alisimamia msimamo wake "Mheshimiwa huyu nikiongozi wa majini wote wa kike alichaguliwa na mtukufu malkia hivyo tunamvunjia heshima kuingia katika chumba chake ambacho hulala na mabinti tu, tufanye mpango tuendelee kupekua sehemu nyingine huyu hausiki" mmoja katika wale majini alitetea "sawa kama utafanikiwa kuona mtu alietofauti basi njoo utupe taarifa" aliongea kamanda yule wa ile oparation kisha wakaondoka, hapo nilipata nafasi ya kupumua nae suleyha alirudi haraka pale nilipojificha "nimechungulia, nimehakikisha wameshaondoka kabisa hivyo fanya upesi tutoke hapa kabla hawajarudi wengine" suleyha aliongea haraka haraka kwa kuhimiza kabisa,
MTAA WA PILI,,,,,,,,,,
"Taarifa zikatoka nje baada ya walinzi waliodumisha ulinzi kwenye chumba changu kubaini sikuwepo ndani hivyo alijitokeza mmoja na kwenda moja kwa moja kwa malkia Zinduna, kumpa taarifa ya kupotea kwangu, nae malkia aliposikia hilo alipata presha na mashaka makubwa huku kubwa zaidi akiiwazia Pete ile aliyonipa kama zawadi maana alijua ni Pete ambayo ingeweza kufanya mageuzi, "PUMBAVU SANA NYIE WALINZI GANI MNAMUACHA MPAKA ANATOROKA MLIKUWA WAPI??" aliuliza malkia baada ya kupokea taarifa hiyo "tusamehe mtukufu mfalme yule mtu ana akili sana katutoroka bila kujua, tusamehe malkia" mlinzi yule alijitetea na kupogi magoti kabisa mbele ya malkia "Najua katumia Pete kutoka, hivyo naombeni haraka mumfatilie anataka kutoroka huyu" malkia Zinduna,.. aliongea kwa hasira hadi macho yake yakabadirika na kuwa yale macho ya paka, "Nitajua tu ulipo Faraja huwezi kunikimbia" malkia Zinduna,.. alisema,. kisha alimuamuru yule mjumbe aende jumba kuu akaipige kengere ya hatari ili awape taarifa wenziwe, kengere ile baada ya kulia kila mlinzi alijiiandaa kwa kazi hiyo maalumu kwa kupenyezeana ujumbe huo wakunisaka haraka, tukiwa ndo tumeanza kutoka sauti ya ile kengere tuliisikia ikipigwa mara nyingi tena mfululuzo "Faraja tuondoke haraka tayari wameshagundua haupo ndani, kengere hiyo inapigwa ya dharura ili majini wote wapate habari kila jini akiisikia atajua ni kengere ya hatari iwapo wote wataupata ujumbe huo kuondoka itakuwa tabu" suleyha aliongea nami sikuwa nanjia ya kumpinga kwa kuwa yeye ndio mwenyeji hakuna jambo asilo liweza, hivyo tuliondoka nakipita njia za chini kwa chini ya jengo ambako sehemu ile haikuwa na walinzi ndio akili pekee alioitumia suleyha ili tuokoe muda wa kutoka kwenye ulimwengu ule, sasa hata matumaini ya kurudi duniani yalianza kuonekana nilijikuta nikifikiria naishia kutoa kicheko kidogo kicheko kilichonipa matumaini ya kurudi nyumbani "Tumebakiza mlango mmoja tu mingine sita yote tumeivuka vizuri, sasa huo mlango wa saba huwa unaulinzi mkali kwa kuwa ndio lango kuu tukifanikiwa kupavuka pale basi utakuwa umeshinda" suleyha aliongea huku akinitazama na tayari muda huo tulikuwa tumeibukia upande wa nje kabisa ya jengo lile la kifalme mbele ya mtalamu wa ramani suleyha, "yote nimekuachia wewe suleyha" niliongea huku nikiangaza usalama wa mazingira yale kwani Pete ilikuwa bado inawaka waka tu, hapo ndipo suleyha aliamua kujitoa kimaso maso kuliko kuendelea kupoteza muda tukisimama alinambia "tunaenda kuvuka pale pale Faraja" "suleyha hamna njia tofuti hiyo si hatari sana?" nilimuuliza "niamini mi kichwa chenye ubongo mia moja" aliongea huku akinitazama nami sikuwa na pingamizi tena maana nilimjua vizuri suleyha ni binti mwenye akili nyingi pamoja na maarifa hivyo mambo yote nilimuachia tu, "mnaenda wapi?" mmoja katika walinzi waliokuwepo lindo siku hiyo aliuliza baada ya kuwa tumeshafika kwenye lango hilo "ni amri ya malkia kuna sehemu ametuagiza" suleyha alijibu huku nami nikiwa nimeinamisha shingo tu isitambulike sura yangu, "usiku hivi au kuna kitu mnaficha??" aliuliza jini yule mwenye mamlaka ya kulinda lango lile kwa usiku ule, maswali yake yaliyonijaza mashaka yalinifanya nijiandae kunuia Pete ili hata nimfanye bubu lakini nilimsubiri kwanza nione hatima yake kama atasumbua zaidi "sasa sikia namtuma mtu kwa malkia sasa hivi akapokee huo ujumbe kama ni kweli" nilishtuka kweli baada ya kusikia nakuona yule mlinzi akiwa atanii na kitu anachokifanya, niliipapasa Pete yangu taratibu huku nikijisemea moyoni kwa kuiomba ituvushe salama kwani huko nyuma kuna wimbi kubwa la majini waliokuwa wanakuja kwa kasi, kwa kupapasa ile Pete ghafra niliona mlinzi akimzuia yule jini mjumbe aliemchagua kwenda kuuliza na badala yake aliamua kuturuhusu kuvuka "mnisamehe bure kwa kutowaamini" aliongea na kuinamisha kichwa kwa adabu, "tuondoke Faraja" alisema suleyha na kunishika mkono tuuvuke mlango huo wa mwisho lakini ghafra tukiwa tunataka kutoka hivi suleyha aruke anirudishe kwanza ile sehemu nikipofikia mwanzo, kwa nyuma yetu tulisikia sauti kali kama radi ikisema "SIMAMAAA" haraka tuligeuza shingo zetu tumtizame huyo aliemuru, tuligeuka taratibu nae hakuwa mwingine alikuwa ni Malkia Zinduna malkia wa majini "Suleyha ni malkia huyo" niliongea kwa uoga huku nikimtizma malkia alivyozidi kusogea kwa kasi na "begi lako liko sawa??" suleyha aliniuliza "ndio" "sawa panda hapa mbele naushikilie vizuri nataka niruke" suleyha aliongea kisha akazichomoa mbawa zake kubwa bila kujari alichosikia kutoka kwa malkia Zinduna, "FARAJA UNANIPENDA??" aliuliza suleyha "NDIO NAKUPENDA" nilimjibu "haya sasa tunaondoka" alisema suleyha nakutingisha mbawa zake tayari kuruka..
-HATUPOI HATUBOI-
Je malkia Zinduna atakubali kuona tunda lake la moyo linaondoka hivi hivi???
Haya Changia kisha,
-BAKI NA MIMI-
ITAENDELEA,,,,,,,,,,,,,,,
No comments: