SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {20}





             Endelea,,,,,,,,,,,,,,,

"Haya kizaa zaa chazua kizaa zaa!! tuliishia ambapo suleyha alipotaka kujidhihirisha mbele ya Faraja kuwa ana mapenzi ya kweli kwa kutaka kumrudisha duniani mbele ya malkia Zinduna,

ENDELEA NAYO.......

"alafu kingine unachotakiwa kuzingatia usigeuke nyuma kabisa au kuchungulia sawa??" alinisisitiza suleyha, nilimkumbatia kwa nguvu upande wake wa mbele nae akazitikisa mbawa zake kubwa mara mbili nakutoa upepo mkali uliwasukuma mbali wale walinzi waliokuwa pale nje ya geti wakitaka kutuzuia kisha suleyha akaanza kuambaa ambaa huku nyuma Malkia Zinduna hakukubari kushindwa hivyo nae alitoa ule mruzi wake wakumuita farasi seif, na pale pale seif alitokea lakini malkia alipompanda kumuamuru seif atufate seif aligoma na kumrusha pembeni malkia Zinduna, malkia alinyanyuka huku akiwa amejawa hasira na kuchomoa mabawa nae pia kisha akaruka kwa spidi huku safari hii uzuri wake wote ulipotea na likaja umbile lake harisi la ndege wa kijini, umbile ambalo kwa kawaida ukiliona kama unaugonjwa wa presha unaweza kuanguka na kufa! kivumbi na jasho katika anga la sayari ile ya majini baada ya malkia kuanza kutoa vimbora kwa kutumia mdomo wake huku macho na mikono yake vikiwaka moto, jitihada zilibaki kwa suleyha kuhakikisha si dhuriki kwa mafataki yale mazito ya moto yaliyokuwa yakitumwa na malkia Zinduna, "jikingeeee na usitetemeke hautaumiaaa" suleyha aliongea kwa sauti ya juu kutokana na mawimbi mazito ya anga lile, alizidi kuweka uzio kwa kutumia mgongo wake na kukwepa vikali makombora aliyokuwa anayaachia malkia Zinduna upande wa nyuma, niliona suleyha akizidiwa kwani makombora ya Zinduna yalikuja mfululizo, haraka wazo likaniingia kuwa na Pete ni ulinzi tosha kwetu hivyo niliona niiombe msaada Pete hiyo "ili tusafiri salama usalimini lazima wewe Pete leo utende miujizaa" nilisema nakuitazama Pete ile kisha nikachungulia upande wa nyuma alipo malkia Zinduna akiandaa makombora mengine "Pete nakuamuru weka ulinzi kwa suleyha asidhurike kwa chochote" nilisema na ajabu ni kwamba miujiza ya Pete ile ilifanyika muda huo na ukatokea ukuta mzito wa barafu ulioelea elea nakuiziba njia ya malkia Zinduna, hapo tulipata nafasi ya kupumua kwa amani licha ya kuwa suleyha alidhurika kwa baadhi ya makombora aliyoyakingia kupitia mgongo wake yasinifikie,

Tulisafiri angani huku suleyha akiwa hoi bun taabani kwani aliweza kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha anayaokoa maisha yangu hivyo nguvu za kuendelea kupaa zilimuisha, tukiwa juu kabisa suleyha alikosa muelekeo na tukaanza kushuka chini kwa kasi, kabla hatujatua chini Buraqu seif farasi muaminifu kwa malkia Zinduna, farasi wa kike mwenye mabawa alitokea na kutudaka wote wawili kisha akatushusha taratibu mpaka chini, haraka nilishuka na kumshusha suleyha pale juu ya mgongo wa seif kisha nikamlaza na kumtizama kumbe sio mgongo tu ulieumia vikali,  hata moja ya bawa lake lilikuwa limevunjika kabisa, nilimtizama suleyha akiwa hoi akihemea pua moja maskini! "Seif bado sijaiona njia yakufika duniani mbebe tuendelee na safari huko tutapata msaada" nilijikuta nikiongea kwa hasira, seif hakuwa na uwezo wa kuongea zaidi alitikisa kichwa chake ishara yakutaa kuwa hawezi jukumu lile, kisha akakunja miguu na mikono yake akakaa akimtizama suleyha kama binadamu, "Pete nakuomba fanya miujiza yako umponyeshe suleyha tafadhari Pete nakuombaaaaa msaidie suleyha wangu" nilizidisha maombi ya nguvu kuiomba pete itoe ile nguvu yake lakini pete ilionekana kutopokea kabisa yale maombi, nilijikuta nikiangusha kilio kikubwa na zaidi kilichonifanya nilie ni juhudi za suleyha kunitoa mikononi mwa malkia Zinduna kila nilipowaza wema wake basi machozi yalizidi kutiririka kwa wingi, nilikaa nikiwa nimekata tamaa kabisa nisijue kama suleyha atakuwa mzima au amekufa nilika pembeni yake nakukinyanyua kichwa chake nakukiegesha kwenye mapaja yangu huku machozi hakizidi kumdondokea usoni binti suleyha "siamini kama suleyha ndio umeondoka hivi nakuniacha peke yangu, mi nilizani tutaishi maisha ya raha duniani tukiwa pamoja? nilifikiri wewe ndio utakuwa mke wangu sasa ukifa nitaishije? tafadhari suleyha fumbua hata kinywa basi unijibu" niliongea kwa uchungu huku machozi yakiendelea kuchuruzika kwa wingi, taratibu umbile lile kubwa la binti suleyha lilianza kubadirika nakurudi katika hali yake ile ya kawaida, utulivu wake ulionyesha wazi hawezi kuamka tena kuendelea na safari, yeye sasa ataungana na wenzie kibao walioko mwenye tumbo la ardhi, nililia sana aseee sikuyaamini macho yangu kama kweli ndio hivi nampoteza suleyha, farasi seif aliemuasi Malkia Zinduna nae aliionyesha huzuni yake, pale pale kwenye ule mchanga mweupe alianza kuchimba shimo kwa ajiri ya kumhifadhi jemedari huyo alieyatoa sadaka maisha yake kunitetea mwanadamu, "hii itakuwa hadithi yenye huzuni kubwa moyoni mwangu kumpoteza shujaa wa mapenzi kama huyu, hii ni hadithi itayonitoa machozi kila mara niikumbukapo, suleyha ndio kichwa cha habari cha hadithi hii" maneno ya simanzi yalizidi kujipanga kichwani kila sekunde iliokatika mbele yangu, niliona hata ile pete haina maana tena hivyo niliivua na kuitupa pembeni kwa hasira kwa kushindwa kuyaokoa maisha ya suleyha lakini baada yakuitupa kuna kitu kilinishtua na pale pale nikafuta machozi nakusimama haraka huku nikitabasamu..

 -HATUPOI HATUBOI-

We unafikiri nini kilicho mfanya faraja atabasamu tena???

Endelea kutoa maoni yako katika Simulizi hii Kali kuliko zote,.. kisha....
    -BAKI NA MIMI-

         ITAENDELEA...........



No comments: