SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {21}




SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {21}

           Endelea...........

"Vita ilikuwa vita usiku ule anga zima lilichafukwa kwa mafataki mazito aliyoyaachia malkia Zinduna kumzuia suleyha asimtoe nje ya ulimwengu wa majini Faraja, na kwa bahati mbaya katika harakati za suleyha kuyatetea maisha ya Faraja alijikuta akiumia vikari, kitu cha mwisho ambacho hatukijua ni kwamba suleyha alikufa au hakufa? maana mwishoni kabisa tuliona Faraja akitabasamu..

ENDELEA NAYO........

Jicho liligeuka na kuwa na chembe chembe za furaha baada ya kuiona Pete ikianza kuutoa mwanga wake, na haraka nikasimama na kuiendea pale nilipoitupa naliiokota huku nikizidi kuikazia macho, haikupita muda mwanga ule uliambaa na kwenda moja kwa moja ulipo mwili wa suleyha kisha ukamzunguka mwili mzima  ule mwanga na ndani ya muda mfupi suleyha alifungua macho "suleyha??? umepona????" niliuliza kwa furaha kubwa baada ya kumuona suleyha akiamka na kukaa kabisa tena akiwa na nguvu zile zile kama mwanzo "tumeshatoka kwa Malkia Zinduna??" aliuliza suleyha punde baada ya kuzinduka "hapana bado usiku huu umetung'ang'ania tukiwa maeneo haya ila hawezi kutufata tena nimeweka uzio mkubwa" nilimjibu suleyha "hapana tuondoke muda wa ule mwezi mwekundu umekaribia" suleyha alisimama tena nae seif aliunga mkono jitihada zetu nae akasimama "utaweza kunibeba tena??" nilimuuliza "yeaah!! mi nipo poa we njoo upande twende" suleyha alinijibu huku akinitizama kwa jicho la mapenzi haraka niliiva pete yangu tena kisha nikamdandia suleyha "fumba macho" suleyha aliongea nami nikafata kama vile alivyotaka, nilifumba macho na suleyha alianza kukimbia kwa kasi kama kimbunga na mwisho tulifika sehemu ya ajabu ambayo ilikuwa ukuta wake ni maji matupu yaliyokuwa yamesimama wima kana kwamba yamepangwa kwa mawe, "huu ndio mpaka wenyewe sasa na hapa ndio kati kati kabisa ya bahari ambapo meri za binadamu zikiuvuka huu mpaka basi hupinduka na damu na mifupa ya wanadamu huwa kama sadaka kwa majini na chakula, suleyha alitolea maelezo mafupi ukuta ule wa maji uliokuwa mrefu hakuna kifani "lakini maji hayapandi mrima vipi tena maji kusimama wima hivi?" nilimuuliza suleyha bado ni katika harakati za kutaka kunyambua ukweli "Ni maajabu ya mungu Faraja" "eeeh!! na wewe unamjua mungu??" nilimuuliza "yap!! kwani hata sisi tumeumbwa na mungu kwa moto, malaika wao wameumbwa kwa nuru na nyie wanaadam mmeumbwa kwa udongo wa siku arobaini kisha mwenyezi mungu akawapulizia roho ndani ya siku arobaini mwanaadamu alizinduliwa kutoka katika wafu baada ya mungu kutumia maneno 'kun faya kun' akimaanisha 'kuwa na muda huo kitu kinakuwa' alisema suleyha "tumeshavuka vikakwazo huko hebu nambie kwa hiyo kati ya jini na binadamu ni nani alieanza kuumbwa??" nilimtupia swali suleyha "malaika ndio alieanza kuumbwa na wa mwisho ni binadamu" "inamaana unataka kusema binadmu ndio wamwisho kuumbwa na mwenyezi mungu?" nilimuuliza tena "ndio kwani wakati anaumbwa adam mungu tayari alikuwa ameaiumba dunia na kila kitu kilichomo sema alimpa uwezo mkubwa wa utambuzi mwanadamu kuliko hata malaika kitendo kilichomfanya ibilisi apinge jambo lile na alikataa katu katu kumsujudia mwanaadamu kisa yeye aliumbwa kabla yake" "suleyha unanipendeza sana kwaiyo nyie majini mna dini moja??" "nilimuuliza tena "tunazo dini kulingana na dini nyingi zilizopo duniani nao majini wanamubudu mungu nakumuogopa pia" alisema suleyha akijibu kila swali  nililomuuliza mpaka tukasahau kama tunatakiwa kutoka, "lakini usije ukafikiria na katika majini pia wapo wanaozikaidi amri za mungu" suleyha aliongeza neno, nilitizama kisha nikamuuliza tena "wakoje hao?" "aah!! tuondoke bwana nafikiri tunamajukumu mengi story huku majini itakupotezea muda tu" suleyha alikatisha na pale aliniomba nipande mgongoni anivushe kwenye ukuta ule wa maji, kwa kweli safari nzima ukiwa na suleyha huwezi kujutia kamwe! alinisafirisha salama usalimini na kunitoa nchi kavu kabisa pwani ya bahari ile "haya kinjia cha kwenda kwetu kile pale twende" niliongea huku nikimshika mkono anifate lakini suleyha alitingisha kichwa na kukataa kisha akasema "mimi ni nusu jini nusu binadamu hivyo kwa kipindi hiki siwezi kuishi na wewe wacha zipite hizi siku saba za muandamo wa mwezi hakika nitarudi kwako mpenzi wangu" suleyha aliongea. licha ya kuwa maneno yake yalinikatisha tamaa lakini sikuwa na budi ya kuendelea kumlazimisha kwani tayari nilishaelewa maana ya muandamo wa huo mwezi mwekundu "lakini ujue ni hatari kwako kwani malkia alikigundua" nilimkumbusha "hapana malkia nikiwa vile hawezi nijua kabisa hivyo we kapumzike usiku huu alafu kesho usiku nitakuwa nakuja kukutembelea, alisema suleyha kisha tukakumbatiana kwa muda mrefu na baadae suleyha aliniachia busu kali mdomoni likabaki kama ukumbusho huku yeye nikimpungia mkono kwa mbaliiii akikimbia juu ya maji kurudi kwenye utawala wao,
       ★★★★★★★★★★★★

Maisha yangu yaliendelea kwa amani sana, marafiki zangu hawakuamini kabisa kisanga nilichowasimulia nilichokutana nacho huko katika maisha ya kijini, wao walisema ni hadithi za kutunga hakuna maisha kwa kiumbe yeyote ndani ya maji tena Leki, ndio alionekana mbishi kabisa.
sikuitaka tena kazi ya uvuvi kwani nilijua yawezekana siku moja ?Malkia Zinduna ataniita kwenye ulimwengu ule, muda ulipita sasa miezi kadha wa kadha tokea nitoke kwenye ulimwengu ule sasa mimi ndio nilikuwa doni kijiji kizima kwa kutumia thamani zile za majini, siku moja usiku nikiwa nimelala ndoto ya ajabu ilinisumbua nilijikuta nikiweweseka usiku kucha mpaka inapofika alfajiri, nilijiuliza sana kwanini ndoto ile inanisumbua sumbua kila siku "au yawezekana kivuli cha malkia bado kipo nami? maana miezi sasa imekatika lakini ndoto za kule kuhusiana na ule utawala bado zinaniijia" nilihisi huenda yakawa mawazo tu hivyo niliishia kuyapuuza,,,,

Siku moja pale kijijini lilipigwa parapanda mtu mmoja wa pembe alipita akitangaza mashindano ya ngumi ya kumuwania mtoto wa mtemi, ambae atafanikiwa kushinda katika majaribio basi ataweza kupewa binti Mum, binti Mtemi hivyo vijiji vyote vya mbali na vya karibu vikatoa majemedari wao wakuweza kuingia kwenye shindano hilo, kwa kua niliona uwezekano wa kurudi kwa suleyha haupo basi niliona ni vyema nami nijiunge kwenye shindano hilo la kumuwania binti Mtemi ambae hata hapo mwanzo kabla ya kukumbwa na ghasia ile tulikuwa na mahusiano ya chini chini, sio mimi pekee ambae nilijiunga hata marafiki zangu wawili Bulicheka na Leki nao walijiunga pia, usiku iliangushwa ng'ombe kubwa zikaandaliwa ngoma za kiasiri za kuwakaribisha wageni waalikwa kwenye shindano hilo, hivyo ngoma zilichezwa sana sana, na utamu wa (ntiki ntiki) kwa kina dada waliponogewa kucheza walivua nguo zao na kucheza bila kuvaa nguo, ila kama akitokea mtu kumpenda msichana aliecheza vizuri basi humchukua na kwenda naye, mimi sikuwa mtumiaji wa pombe na sikupenda sana nyama hivyo katika sherehe hizo nilikuwa mzungukaji tu nikiangalia mabinti wale wakivinyonga viuno vyao huku matiti yakiwa nje, nikiwa katika kikundi kimoja cha wacheza ngoma nikizubaa ghafra Pete yangu ilianza kudunda tena, tena kwa kasi tofauti na siku zote nilishtuka kwani alama pekee ya hatari nilioigundua kupitia pete ile nikutweta, nilianza kuangaza huku na kule kuona labda kuna kitu kibaya kipo kati kati ya watu wote waliohudhuria pale, katika kuzungusha zungusha macho niliona kuna mdada mmoja akiwa anacheza ngoma kwa style ya namna yake kabisa tofuti na midundo ya ngoma inavyoenda, alizungusha kichwa chake kulia na kushoto huku akichanganya juu na chini kiufupi alicheza kama mtu aliepandisha majini, nilianza kuzipiga hatua taratibu kumsogelea binti yule alienishtua huku macho yangu yakiulekeza umakini wote kwa yule binti ghafra kuna dada tena akaja nakunipushi kidogo nilipogeuka kwa hasira nikakutana na tabasam murua kisha binti yule akaniuliza "UNANIKUMBUKA??" aliuliza binti yule ndio kwa mara ya kwanza kabisa namuona alafu ananiuliza kama namkumbuka hiyo ilinishtua sana, kisha nikatoa jibu la kujiamini "Sikukumbuki" nilijibu huku namtizama machoni "Njoo huku utanikumbuka tu" alisema binti yule nakunivuta mkono kunitoa kwenye kundi lile la watu,

 -HATUPOI HATUBOI-

Wewe unafikiri nini hapo kuhusu huyo binti mgeni atakuwa mwema kweli??? na vipi yule anaecheza kimajini au ndio wamerudi nini kumuijia mtu wao???
Ebu changia,,,,, kisha
     -BAKI NA MIMI-
      ITAENDELEA,,,,,,,,,,,,,,



No comments: