SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {22}





SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {22}


           Endelea.........

NGOMANI!! NGOMANI!!
haya! wasi wasi waanza kumkumba kwa mara nyingine Faraja, licha ya kuwa tayari alishaokoka kutoka kwenye ulimwengu ule wa majini, siku hiyo akiwa kwenye sherehe za kuwakaribisha wanaowania kumgombea binti mtemi nae akiwa mmoja wao, basi usiku huo ulikuwa wa wasi wasi kwa Faraja baada ya kuona mabinti wawili wageni waliomshitua sana, mmoja alicheza zile ngoma kama jini na mwingine ndio kabisaa alimfata na kumuuliza unanikumbuka?? Faraja alisema hapana sikukumbuki lakini binti yule alimvuta mkono kisha akamwambia "Njoo huku utanikumbuka tu" ni nani huyo binti???

ENDELEA NAYO......

"Maswali mengi yaliuzunguka moyo wangu, kila nilipomtizama binti yule sikuweza kabisa kumfananisha na binti yeyote wa pale kijijini, binti yule alikuwa mrembo aliongea kwa vituo na mapozi ya aina yake, weupe wake asili kabisa ulioteleza na nyuma umbo lake zuri liliojaa kiasi miguu na mwendo wake anapotembea utajua wazi binti yule sio wa kawaida, alinivuta tukatoka pembeni yani faragha sehemu ambayo sauti za ngoma zilisikika kwa mbali nyuma ya nyumba moja hivi ya udongo na makuti, tulifikia hapo na kuweka kituo kisha moyo wangu ukafunguka kutaka kumjua vizuri binti huyo aliejiamini kunitoa kule ngomani na kunileta faragha "ah! Bado sijakuelewa mrembo ulichokipanga juu yangu" niliongea huku nikimtizama binti yule, "naitwa Zubeda nzugu" alianza kwa kujitambulisha "sijakuuliza jina lako nambie umenijuaje na tulishaonana wapi?" nilimtupia maswali mfululizo kisha nikakaa kimya kumsikiliza "mh! wee nae hata jina hutaki niseme jamani! sawa sio mbaya, hukumbuki siku zilee muda mrefu umepita lakini katika sherehe za mavuno?" aliuliza Zubeda na kunifanya nifikirie jambo la miaka kadhaa iliopita "yap! yap! nimekumbuka, mhu! ilikuaje sasa?" nikamuuliza tena "Tukipiga mvinyo kwa pamoja tukala nyama pamoja, tukabadirishana mate yani kiufupi siku ile ulinipa penzi ambalo kila mara huwa na kukumbuka kwa ujemedari wako ulivyoweza kunimudu kunikidhia haja hadi nilipo ridhika" aliongea Zubeda kwa kujiamini sana tena akinipapasa papasa sehemu mbali mbali,.. "mmhuu!! mmhu!! bado hujanielewesha vizuri kwaiyo tulifanya tendo la ndoa mimi na wewe??" nilimuuliza tena huku nikiipangua mikono yake aitoe kwenye mwili wangu,. "ndio tena ulinibiringisha sana usiku ule" "mimi huyu?" nilimuuliza kwa mkazo "ndio ni wewe jamani Faraja" aliongea Zubeda na kunitaja jina jambo lililoulipua moyo wangu kisha ukaanza kudunda kwa kasi, "hapana itakuwa umemlenga mtu tofauti na sio mimi kabisa, mi sijawahi kufanya tendo la ndoa  na binti wa kijiji hiki huenda umenifananisha" niliongea na kumtoka binti yule, lakini Zubeda hakuonyesha kabisa kuridhika na majibu yangu licha ya kuwa aliniacha niondoke tu lakini moyoni mwake alijisemea "siwezi kukubali mwanaume mzuri kama wewe unaniacha hivi hivi, malkia Zinduna utanisamehe bure kama mara ya kwanza niliweza kumteka safari hii simleti huko" mawazo yalipamba moto hadi nikahisi ubongo unatokota kulingana na maneno ya binti yule Zubeda alieongea kwa kujiamini huku akiwa hana chembe chembe ya aibu "daah!! mabinti wengine hawa kashindwa kutafuta mtu mwingine mpaka ananipaparukia mimi??" nilijisemea na kurudi ngomani nikamtazame yule binti mwingine, lakini nilipofika sikumuona nilijitahidi kumuangaza huku na kule kwenye kila kikundi cha ngoma nilizunguka lakini sikumuona binti yule. "dah! tayari ameshaondoka muda huu huu tu hata sijamaliza dakika tano??" nilijiuliza mwenyewe na baadae nilijaribu kuwauliza watu hasa wale waliopiga ngoma karibu nae lakini walidai hawakuona mtu aliekuwa anacheza, kila mtu niliemgusia kumuuliza habari hiyo na kuwaelekeza kuhusu binti huyo hakuna majibu yeyote niliyoyapata zaidi ya kuonekana mburura!
      ★★★★★★★★★★★★

Baada ya ngoma kuisha sikuweza kurudi nyumbani nilibaki huko huko hadi pale ilipotimu saa moja kamili za asubuhi, firimbi nyingi zilipigwa na watu wote waliohudhuria waliamka na kusogea kwenye makazi ya mtemi kupata maelezo kuhusu shindano, "ahsanteni kwa wote mliohudhuria mashindano haya na nipende kuwapongeza sana, kila mwaka nimekuwa nikimtoa binti yangu mmoja kwa shujaa ataeweza kushinda shindano hili, leo nitawaruhusu mashujaa wote mjiandae kumshindania binti yangu Mum,, hivyo kwa kila shujaa afanye mazoezi yake ya mwisho pamoja na kuandaa siraha zake zote zikae sawa kwani huko muendako kuna wanyama wakari, pamoja na binadamu wanaokula nyama za binadamu wenzie" kama kawaida ya shindano letu inatakiwa abaki mtu mmoja pekee ataeweza kuwashinda wenzake wote, na huyo ndiye ataekuwa shujaa ataemuoa binti yangu" sauti ya mtemi ilipaa kabisa na kumuingia kila shujaa aliejitokeza pale, na kila mtu aliweka matumaini ya kung'oa dodo kwenye nyumba ya mtemi, binti mrembo mtoto wa kumi na mbili katika uzazi wa mtemi mhango kwa mke wake wa sita, mashujaa walishangalia kwa kupiga ngao zao kwa mapanga na wengine wakionyesha ujemedari wao kwa kuyatingisha matiti ya vifua vyao vikubwa vilivyojaa, mi sikuwa na presha hata kidogo licha ya kuwa mwili wangu haukulingana na miili yao lakini niliiamini sana Pete kuwa ndio ngao ya kuwashinda majitu yale yenye miili mikubwa kama majayanti, kwa kuniona mdogo mdogo walipita na kunisonkora wengine waliniahidi kunibaka, tukiwa huko yote hiyo nikatika sehemu ya kuivuruga saikorojia yangu, "Mmh! hamnijui nyie" nilijisemea kimoyo moyo huku nikiwazarau vikari wote walionidharau na kunihisi mi nidhaifu..

usiku tena ulitanda wengi wakawa wamepumzika wakijiandaa kwa ajiri ya shindano, na wengine walikuwa nje wakibadirishana mawazo mawili matatu, wengine nao walikuwa huko wakichoma nyama zilizowindwa maporini kiufupi kijiji kile kiliitwa kijiji cha wawindaji kilichotulia sana na asilimia kubwa ya uendeshaji wa maisha kwa kijiji kile waliamini sana uwindaji tofauti na kijiji chetu tulichoamini uvuvi sana pamoja na ukurima, kwa kuwa sikuwa na kampani yeyote Bulicheka na Leki,. wao walikuwa Busy kwenye vyumba vya wanawake, hivyo nilikaa peke yangu tu nikisubiri kesho shindano lifike, lakini ghafra nikiwa nimeketi kwenye viti vya mbao vilivyochongwa kwa ustadi, moyo wangu ulishtuka na mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi nilihisi hata damu haizunguki kwani hofu niliokuwa nayo ilikuwa kubwa kupitiliza kwa kitu kile nilichokiona kikija mbele yangu, "ZI...ZI..NDUNA???" nilijiuliza huku domo likitetemeka kwa hofu,

-HATUPOI HATUBOI-

Kimemleta nini tena zinduna duniani??
        me sijui we cha kufanya wewe toa maoni yako kisha subiri kesho tuujue ukweli,,,

       ITAENDELEA,,,,,,,,,,,,,,,,,



No comments: