SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {23}




SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {23}


           Endelea...........

"Moyo wa Faraja unapata mshituko mkubwa wa ghafra baada ya macho yake kukutana ana kwa ana na malkia Zinduna, anapata hofu Faraja na hajui nini afanye amkimbie au amsubilie afike??

ENDELEA NAYO.......

Bado macho ya hofu yalizidi kumtizama binti yule aliekuja kwa mwendo wa taratibu sana huku mkononi akiwa na kisahani kidogo nilipokikazia macho kisani kile hakikuwa tofauti kabisa na visahani nilivyoviona katika ulimwengu ule wa majini ambavyo vilitumika sana kuwekea ubani, nilijikuta kijasho chembamba kikianza kunichuruzika huku nikiyatoa macho kodo, "zi..zi..nduna" niliongea kwa hofu huku mdomo ukitetemeka na meno yakigongana "nisamehe malkia nisamehe bure" niliongea kwa sauti huku nikirudi kinyume nyume kwa uoga, "Faraja unatatizo gani?" sauti ya binti aliekuja upande wangu ilinitoa wenge na kunitoa kutoka kwenye dimbwi lile la hofu na mashaka, nilimtizama binti yule aliekuja pale na tayari muda huo nilikuwa nimeshaanguka chini "eti nae anawania kumuoa binti mtemi si vituko hivi mtu wakupiga kelele mwenyewe atakuwa mzima kweli huyu??" sauti za kebehi zilisikika kwa baadhi ya kina mama walionizunguka muda mchache wakishangalia movie niliolicheza ndani ya muda mfupi, "hheheheheheheh aluuuuuuu!!!" wanawake wale wenye dharau walitoa sauti za vicheko huku wakipigana viganja kisha wakatawanyika na kuniacha nikiwa bado namtumbulia macho yule binti aliekuja kwa mfano wa Zinduna "vipi mbona unaogopa?" aliuliza binti yule, sikumjibu chochote zaidi nilitingisha kichwa kuashiria hakuna kitu nikasema " Mmh! sawa kama hutaki kusema, naitwa Zureha nimetumwa na binti mtemi nikuletee hiki kinywaji amesema ukinywa utapata nguvu za kufanya kazi vizuri" alisema binti yule aliejitambulisha kwa jina la Zureha "nenda mwambie amesema hataki kutumia kinywaji chochote kwa sasa yuko sawa" nilimjibu huku nikijinyanyua na kurudi juu ya kiti nilipokuwa nimeketi mwanzo kabla ya kukumbana na ile ghasia "Ila ni kizuri kwa afya yako itumie utapata nguvu" alisema Zureha "SIIITAKIII na utoke hapa" nilimjibu kwa hasira kwani alichokiongea niliona kinanichanganya tu, "sawa mimi naiacha hapa ukitaka kunywa kunywa, ukitaka kuimwaga imwage ni wewe sasa na maamuzi yako" alisema Zureha kisha akanyanyuka nakuondoka zake, pindi alipotoka tu Zureha ulipita upepo mdogo sana puani mwangu ulioambatana na harufu ya marashi na nilipovuta vizuri niligundua ni marashi pendwa kwa suleyha, licha ya kuwa katika ule utawala wa majini kulikuwa na aina tofauti tofauti ya marashi lakini marashi pekee niliyoyakariri ni marashi aliyokuwa akijifukisha suleyha, "suleyhaa" nilishtuka na kuita kisha nikaanza kuangaza kila pande kama nitamuona Zureha nimuulize lakini sikufanikiwa kumuona kabisa, nikijaribu hata kutoka kumfatilia lakini wapi! nilienda hadi kwa mtemi na kuwauliza walinzi kuhusu mtumishi wa binti mtemi anaeitwa Zureha lakini walisema hawamjui, tena walisema katika kijiji hicho hawajawahi kusikia jina la namna hiyo, nikajikuta moyo wangu ulijilaumu kumuondoa mapema binti yule bila kujua kama ndiye suleyha alikuja kunisabahi, kweli hasira hasara!, nilirudi hadi pale nilipokuwa nimeketi mwanzo na kukikuta kibuyu ambacho alikuja nacho Zureha huku kichwani nikijitahidi kuyaoanisha majina yale mawili "#Suleyha Zureha, nikisema Suleyha na Zureha hazina tofauti, Suleyha ndio Zureha hapana! Suleyha Zuleyha napata jina kamili Zureha ni kweli ni Suleyha" hatimae nilipata jibu la pamoja na kushindwa kuyazuia machozi yangu kwani umepita muda mrefu sana bila mawasiliano yoyote na Suleyha leo kaja nimefanya ujinga hadi kaondoka sijamtambua lakini kwanini Suleyha unifanyie hivyo siungejitambulisha tu?? kwanini umekuja kwa umbile tofauti Suleyha??" nilijikuta nikilia bila mipaka hadi kila mtu alinishangaa na wengine walihisi nimedata kwa shindano, "niliendelea kulia tu huku nikikumbatia kile kibuyu nilichopewa na Suleyha, "Suleyhaaa njoo basi mpenzi wangu ujue wazi unautesa moyo wangu? lakini kwanini hukunambia mapema Suleyha?? nimekukumbuka suleyha wangu nimekukumbuka sana tena sana, sikujua yote kama ni wewe umekuja kunitembelea aaah!! Suleyhaaaa Suleyhaaaaaaaaaa" nililia sana na machozi hayakuvuja machoni pekee bali hata moyo ulisurubika vikali kumpoteza Suleyha kizembe namna ile,
"kaheuka huyo muacheni jamani" wakina mama wenye midomo kama ya mbete nao hawakukosa la kusema,

KOKORIKOOOOOOOOOOO!!!
Ni sauti ya kuku dume ilioashiria kukucha kwa siku nyingine ndio ilitufanya tuzinduke alfajiri hiyo, hivyo tuliamka na wote tukakutana kwa mtemi na kutupa neno la mwisho ambalo alisema "nawatakia kila la kheri kwenye hayo mashindano yenu" kisha kila mtu alifurahi kuruhusiwa kwa shindano hilo la kufa kupona, huku walionyesha shangwe kabisa ni wale mabaunsa wakapiga ngao zao kwa mapanga yao kisha tukatoka kila mtu na njia yake kilichonishtua zaidi ni upande wa Bulicheka na Leki,,,.. wao waliungana njia na wale mabaunsa wenye miili mikubwa kama majayanti, yote sikujari mie nilipita kwa njia yangu peke yangu nia nifike (check point) ambapo shindano ndio litapoanzia, tokea asubuhi nilikuwa nimeshaweka vituo sita hadi usiku unafika bado nilikuwa sijaifikia check point hivyo niliona vyema nitafute sehemu nijiegeshe kwanza alafu niendelee na safari, nilikusanya matawi makavu yaliyoanguka kutoka mitini kisha nikachukua mawe meusi mawili na kuyagongesha zikatokea cheche na cheche zile zilipotua kwenye matawi makavu yaliwaka na hapo nikachochea kuni kidogo lengo nipate joto la ufukuto, baada ya kuhakikisha kuni zimeshika kisawa sawa nilikaa pembeni na kuanza kupata joto kwani pori lile lilikuwa kubwa na lenye miti mirefu na mikubwa hivyo baridi ilikuwa kali sana, wakati bado naendelea kuota moto nyuma ya mti mmoja mkubwa uliopo mbele yangu nilisikia sauti ya binti akilia kwa kuomba msaada nilijua utakuwa mtego hivyo nilijiweka sawa kusubiri na kuona kama kuna hatari yeyote inayonisogelea lakini bada ya kukaa dakika chache nilikumbuka kwenye mchezo ule hakuna binti hivyo niliona vyema niende kumsikiliza binti huyo, kwa hatua za taratibu na umakini wa macho nilitizama mti ule ambapo ndio sauti ya bint yule ilitokea "wewe kwenye misitu hii ya hatari na usiku kiasi hiki unatafuta nini??" nilimuuliza binti yule aliekuwa amejikumbatia huku akiwa amekaa uchi wa mnyama" hakujibu wala hakunyanyua sura yake zaidi aliendelea kulia tu, niliona nguo zake pale chini zilizoonyesha kuraruriwa kisha nikazichukua na kumfunika wakati bado namfunika binti yule akinyanyua sura yake nakusema "NAITAKA PETE" kisha likanirarua kwa kucha likaruka kama nyani nakukaa kabisa kama nyani kisha yakamchomoka manyoya mwili mzima na tayari likabadirika na kuwa likiumbe la ajabu, "anha!! unaitaka Pete? njoo uchukue" nilisema bila uoga na kuliita kimadharau...

Hiyo vita hapo kati ya mimi na Kiumbe huyo sijui Na nani ata Shinda? Sasa wewe hakikisha,,,,

Baki Na Mimi.....

SIPOI WA ATUBOI

           Itaendelea,,,,,,,,,,,,,



No comments: