SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {24}
SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {24}
Endelea...........
"Vita kali yaibuka msituni Faraja anakutana na kiumbe asiye wa kawaida kiumbe yule anadai kuitaka Pete kisha analivua gamba la ubinadamu anakuwa kiumbe mmoja wa ajabu nani ni nani mi ndio refaaa!!
ENDELEA NAYO......
Kiumbe kile kilizidi kujiseti na kuyatoa mamiba makubwa makubwa juu kwenye alama za uti wa mgongo, huku domo na mikono yake ikibadirika na kuwa kiumbe kikubwa tofauti na awali mkia wake uliongezeka na kuwa mrefu tena mnene, huku domo lake lilokuwa wazi likizidi kuangusha udende, "khaaaaaaa!!" liliunguruma kwa sauti nzito iliotoa upepo mkari ulionisukuma pembeni kwa nguvu, niliamka na kukikitizama kiumbe kile vile kililivyozidi kubadirika, lilikuwa jitu kubwa jeusi lenye makucha marefu pamoja na ulimi wake uliojigawa upande wa mbele kama ulimi wa nyoka, liliurusha ulimi wake na kuanza kunivuta kwa nguvu kunisogeza karibu nami nilijitahidi nisiweze kuingia kwenye domo la kiumne yule "iyaaaaaaah" nilitoa mwano wa nguvu huku nikiwa nimeshikilia miti midogo miwili ili kiumbe kisinivutie kwenye domo lake lililowazi "KRAAAAAA" liliunguruma kisha likatingisha kichwa chake kitendo kilichonifanya nishindwe kuhimiri na kuiachia ile miti miwili nalo kwa kutumia ulimi lilinirusha mbali, "anha sawa" niliamka kwa ghadhabu kubwa baada ya kuona kiumbe kile kimedhamiria sasa kufanya kweli, nilimungalia wakati anasogea taratibu kisha nikauinua mkono wenye Pete juu na kuliandaa kombora kubwa ambalo wazi likimpiga hawezi kupona, lakini kabla sijaliamuru kombora lile waliibuka watu wawili waliokuwa mamevaa nguo zao za ngozi ya chui na mikoba midogo, huku watu wale walionyesha kuwa ni wazee, walipofika walianza kumzuga kiumbe yule mmoja akiwa upande wa nyuma na mwingine alikuwa upande wa mbele huku akiwa ameshika kimshare kidogo alichokuwa amekiweka sawa shida ikiwa ni tageti tu, yule aliyeko upande wa nyuma alimpa ishara kwa kichwa sasa waweza kufanya walichotaka kufanya nae yule wa mbele alipoona ishara ile alimlenga kiumbe yule kwenye kifua chake ambako kulionekana kuna duara liliokuwa linawaka waka, hivyo mzee yule aliutumia upinde na mshale wake, alifyatua na kile kimchale kikatua pale pale alipokadiria kufika, lilipiga sana kelele kiumbe lile na taratibu nguvu zake zilienda zinapungua na kuanguka chini kama mzigo, kisha lile umbile la kutisha likaanza kutoka na likarudi umbire lake la kibinadam "Ni mwanangu huyu ametuhangaisha sana kumtafuta hatimae tumempata" mzee yule alieurusha ule mshale aliongea kunipa history "alikuwaje mpaka imempata hali hii??" nilimuuliza mzee yule "ni stori ndefu sana mwanangu wewe acha tu dunia hii!!" alisema kwa kukatisha, kisha mzee yule wakisaidizana na yule mwingine wakamfunga binti yao kwa kamba ngumu miguuni na mikononi pamoja na kumfungia kikengere shingoni mwake, tafsiri ya haraka kengere ile yaonekana kuwa kizuizi kwa binti yule ili asiweze kubadirika hivyo ndivyo nilivyofikiri, wazeee wale walimbeba binti yao na kusepa huku nyuma nikipata nafasi ya kushusha pumzi kisha nikarudi nikikoka moto na kuendelea kuota, nilipitiwa usingizi mzito na ndani ya usingizi ilipita ndoto, ndoto iliokuwa ikinionyesha Malkia Zinduna akiitumia ile damu yangu alioichanganya na damu yake siku ile kufufua wafu ili waje wanitese tena kwa kuamuru "namtaka Faraja arudi kwangu yeye ndio mfalme wangu" nilishtuka ikiwa ni asubuhi tayari kumeshapambazuka "hiii ndoto ina maana gani? ina maana Malkia Zinduna bado ananitaka nirudi kwake?? ila hapana haya ni mandoto ya asubuhi asubuhi tu sio ya kuyazingatia" nilisema na kudharau kisha nikabeba kibuyu changu niendelee na safari, "fuuuuuuh!! fuuuu!! fuuuuu!!!" ni sauti ya pembe iliokuwa ikipulizwa kama kuna tatizo kwenye nyumba ya mtemi niliposikia sauti ile ikijirudia nilijua iko shida nyumbani kwa mtemi ila kwa vile nilikuwa bado sijaifikia check point niliona vyemaa nirejee kwenye jumba la mtemi nikaone kama kuna tatizo, na haikuwa mimi tu niliesikia sauti ile ya pembe na mlio wa ngoma, kumbe hata na wenzangu wote walisikia hivyo wote tulikutana kwenye jumba la mtemi na kusitisha shindano kwa muda,
Tulimkuta mtemi akiwa na hali mbaya ghafra tu, na wanakijiji wengi walikuwa wamerundikana kwenye nyumba ya mtemi wao, hali haionyeshi matumaini kabisa ya mtemi yule kupona, waliitwa waganga wengi walioaminika kuja kumpa matibabu mtemi lakini wote jitihada zao zilidunda kwenye ukuta wa chuma, hadi inafikia usiku hali ya mzee inazidi kuwa mbaya, na ni siku moja tu lakini ajabu mtemi tayari makucha ya vidole vyake yalianza kunyofoka nyofoka kana kwamba ukivitazama vidole utafikiri ni mtu alieshambuliwa na wadudu, "hii! hii hii nayo mpya yani asubuhi tu ya leo alikuwa mzima kabisa kufikia saa nne akaanguka, kufikia tena usiku mtu ameanza kuharibika hivi jaman??" "nae afe tu alikuwa mchawi mno" "hapana bwana uchawi vipi wewe mama ntulu si amekusaidia sana shida nyingi ulikuwa unakuja kumlilia leo unasema afe? eti alikuwa mchawi kweli binadamu hamna wema" mashallah wanawake wakijiji kile walijaaliwa midomo, badala ya kushauriana kutafuta dawa au mtu wa kumsaidia mtemi wao waliongea mambo ya upuuzi niliwasikitikia sana wanawake wale wasiojielewa wao wanadhani shida ni ya mtemi na familia yake tu bila kujua shida niya kila mtu haichagui haibagui, walizozona sana wanawake wale watatu mmoja alionyesha kupinga maneno yao wale wawili walimtolea matusi sana "wewe ndio unajiona mwema, utaishia kulalia ngozi hivyo hivyo nyie ndio wachawi wale wale tu kwendaaaaa hiloooo huna jipyaaaaa" walimsokomeza kwa maneno mabaya binti yule,
nikiwa nimejipumzisha nikifikiria namna ya kumsaidia mtemi "najua Pete hii inauwezo mkubwa wa kutenda maajabu yoyote lakini je watanichukuliaje hawa wanakijiji??" nilijiuliza mwenyewe kisha nakujijibu mwenyewe "nafanya liwalo acha liwe kumpoteza mtu na uwezo wa kumsaidia upo nitakuwa naitumia akili vibaya Pete hii itakuwa msaada kwa jamii na sio kuiteketeza jamii" niliongea kwa ujasiri moyo ukavimba uchu wa kwenda kutoa msaada kwa mtemi, moja kwa moja niliwapiga vikumbo wote walioziba ziba njia ili niingie ndani lakini kufika mlangoni mijemba ilinizuia nisipite "nataka kumsaidia mtemi niruhusuni nipite" niliongea kwa sauti, watu walicheka sana hawakudhani kama naweza kusema hivyo mbele yao "unawazimu hivi wewe kweli ni timamu??" mlinzi mmoja aliuliza kwa kebehi "huyo chizii huyoo" "hahhahah hivi si vituko eti! ndio huyu wa kumsaidia mtemi??" kila mtu alionyesha dharau kwa maneno tofauti tofauti ya dharau..
Upande wa pili Malkia Zinduna nae anakusanya jeshi la majini kisha anasema "NAKUIJIA FARAJA KITI CHAKO KINAKUSUBIRI"
-HATUPOI HATUBOI-
Ni mwendo wa mchaka mchaka
ITAENDELEA,,,,,,,,,,,,
No comments: