SIMULIZI___ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {25}





SIMULIZI___ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {25}

               Endelea..........

"Mabwanaaa leo ni siku njema kwetu wote mliokusanyika hapa nyote mnisikilize kwa makini, lakini kabla ya yote nawashukuru kwa kupokea na kutiii wito wangu, leo nitawatuma duniani muende mkaitafute Pete kwa kijana Faraja na muilete hapa pamoja na huyo kijana, kwa kile alichokifanya kutotii sheria na kuniacha lazima akijutie kwa mateso makali, nawaamuru nendeni sasa duniani mkailete Pete nendeni" Sauti ya radi ya malkia Zinduna akiliamuru jeshi kubwa la majini liingie kwenye sayari ya dunia lije liichukue Pete pamoja na Faraja wamrudishe kwenye ulimwengu ule ambao anatambulika kama mfalme, kisha baada ya kupokea maagizo yote jeshi lile tiifu la malkia Zinduna liliondoka kwa kuruka kuja duniani,

ENDELEA NAYO......

"Bado walizidi kunitia simanzi wanakijiji wale kwa kuonyesha ugumu wa namna yake, kutoshindwa kunielewa na kunijua mimi ni nani "jamani mngenielewa tu tafadharini mimi najua dawa ya kumtibu mtemi acheni kutia kelele zisizo na maana, maisha ya mtemi yako hatarini na hamna kati yenu anaewaza kutafuta dawa si wapo waganga wenu wamekuja kumtibu wameshindwa sasa nipeni nafasi nimtibu mtemi nyie nipeni tu nafasi mtaona" niliongea kwa uchungu huku nikiwa nimewageukia wale wananchi washenzi wenye fikra potofu, "lakini haiwezekanai juzi tu hapa ulikuwa unapiga kelele mwenyewe leo wewe ndio uweze kumtibu mtemi?? hii miujiza sasa imeshuka kutoka mbinguni yani washindwe waganga vingunge wewe kapuku usiejulikana ndio uweze hahahaha hizi sasa ni ndoto, aki ya mama nakuapia ukiweza kumtibu mtemi nakupa hekari kumi za shamba langu na mimi nitabaki na mbili peke" jamaa mmoja aliongea kwa majigambo akijiamini kwa asilimia mia katika kile alichoongea kuwa sina uwezo wa kumtibu mtemi, "Kwanza nyie ndio wachawi wenyewe apigweeeee apigweeee!!!!" mmoja katika wajinga alianzisha maneno yaliyochafua utulivu uliokuwapo mwanzo sasa zikawa pande mbili za kupinga na kukubali, wapo walioanza kurusha mawe kunidhuru lakini walinzi kwa hilo walisimama kidete na kunikinga kwa ngao zao ngumu, "Jamani hebu tusikilizane" mzee mmoja aliingilia kati choko choko lile la vurugu, wote walipomuona walitulia na kurudi katika utulivu wao wa awali kisha wakayatega masikio yao vizuri kumsikiliza mzee yule "kupigizana kelele wakati wa shida ya pamoja kama familia ni matumizi mabaya ya akili, badala mkae mtafute njia ya kumponyesha mtemi mnakaa kupigizana kelele, je yule aliejitolea kumsaidia atakua majinuni au nyie ndio majinuni?" aliwauliza mzee yule alieonekana sio wa kijiji kile kwani uvaaji wake hata lafudhi ya maneno yake hayakufanana na wao, mzee alivalia kikoi huku mkononi mwake akiwa na kifimbo kimoja kilichochongwa kwa mti na kupakwa rangi huku kichwani mwake akiwa na kikofia aina ya tunga,  wote kimya hakuna hata mmoja alienyanyua domo lake kutoa maneno yake ya shombo, "kaomba nafasi mpeni msimdharau mtu msiye mju je kama ni malaika wa mungu ameagizwa nyie mtajueje kwa mara nyingine msije mkamuhukumu mtu msiyemjua chimbuko lake" mzee yule aliongea kwa kuonyesha mkazo kwa jambo analolisema kana kwamba ni mtu anaenijua vizuri, moyoni niliweka tiki kwa maneno ya busara ya mzee yule, mioyo yenye nyama na mishipa yake iliozungusha damu ilikubali kulainika kwa maneno yale ya busara ya kikongwe yule heshima ilishika mkondo na wale walinzi waliiitoa mikuki yao na kuniruhusu kuingia ndani, moja kwa zote nilifika kilipochumba cha mtemi na kukuta akiwa na hali mbaya miguu ya mzee yule ilikuwa imejaa sana huku vidole na makucha zake vyote vikiwa vimekatika, kiufupi waliekuwepo mule ndani ni watu wenye mioyo migumu kama chuma, "Faraja tafadhari msaidie baba yangu niko chini ya miguu yako" Mum,.. binti mtemi alianza kwa kulia tu huku akijiburuza chini ya miguu yangu kuniomba msaada, "nipo kwa ajiri yako Mum,. usiogope atapona kwa uwezo wa mungu" niliongea huku nikimtizama mtemi akihema kwa shida, "naombeni wote mnipishe" niliongea wote wakashtuka, "Naombeni wote mnipishe hili ni jambo kubwa sana hivyo ningependa wote mkae pembeni mniachie mimi swala hili" niliongea na safari hii sikuongea kiupole kama vile nilivyo maisha yangu yote, "Haiwezekani bwana tukupishe unataka umuuwe?? au," mmoja wa wanawake katika wake wa mtemi alikataa "Narudia tena naombeni mnipishe kwani mtemi ameingiwa na jini baya na jini huyu akitoka kwa nyie mlioko vichwa wazi atawaingia kupitia utosini na kuivuruga akili yako" niliongea na kuwapa maelezo kidogo walishtuka na hapo kila mtu alijigusa kichwa chake na kukutana na nywele za mabutu hivyo wote walitoka nje haraka "Atakuwa mchawi huyu kijana eti majini amejuaje kama ni jini yule??" bado wakina mama wale waliendelea kuteta kwa sauti,

Walipoondoka tu nilimuomba mlinzi arudishie kidogo mlango ule wa matete kisha shuhuri nibaki nayo mwenyewe ndani, nilijikuta akili ikiniangiza kufungua kibuyu nilichopewa zawadi na suleyha, haraka nilikifungua na kukutana na kimimika aina ya maji kisha nikaanza kumnyunyizia matone kidogo kidogo mwili wa mtemi, kila tone lilipotua lilileta athari kwenye mwili wa mtemi kwani ilikua kama asidi vile, "AAAAAAH!!! AAAAAGH!!" sauti nzito aliitoa mtemi iliokuwa ndani yake kisha akaanza kujinyonga nyonga huku akisema "WANAKUJA!! WANAKUJA!! BADO HUJAISHINDA VITAA" sauti ile nzito ilisikika "wewe ni nani? Na nani amekutuma?" "hiihiiiii hiiihii" mara sauti ikawa inabadirika na kuja sauti ya kike mara ya kitoto kisha ikarudi ile sauti ya mwanzo "NATOKA BAHARI SABA" "Mmhuu!! kimekuleta nini duniani kwenye mwili wa mzee huyu??" nililiuliza jini lile liliokuwa tayari limeuamsha mwili wa mtemi na kukaa likiwa limekunja miguu "HAHAHAHAHAH" badala ya kunijibu jini lile lilicheka "Unanicheka sasa Nakuteketeza sasa hivi kama hutosema?? shida yako na nani aliekutuma??" niliongea huku nikiipapasa ile pete inipe nguvu za kumkabiri jini yule, bado lilibaki kimya tu na likaanza kumnyonga mtemi huku likisimama na kujipigiza ukutani, niliona nikiendelea kuliuliza litamuua mtemi na nitapata kesi pale pale nililisogelea na kumshika kichwa kwani baba alishawahi kuniambia mtu mwenye majini hapendi kushikwa kichwani akishikwa yatatibuka au kutulia hivyo niliwahi na kumshika kichwa "RUDI ULIPOTOKA UWAMBIE DUNIANI SASA KUNA MTETEZI MWAMBIE ALIEKUTUMA JINI SASA HANA NAFASI" Niliongea kisha nikammwagie yale maji nusu huku nikilikemea vikari kupitia nguvu ya Pete jini lile liliogopa na kuondoka kabisa ajabu ni kwamba lilivyotoka tu mwili wa mtemi ulirudi na kuwa sawa kama hapo awali lakini mtemi ndio akawa amepoteza fahamu,

nilitoka na kuwapa taarifa walinzi na walinzi walipoingia ndani walimkuta mtemi ameamka, shangwe na vigere gere vikapigwa huku wakinishangilia kama shujaa wa kihistoria licha yakuwa kuna wengine hawakufurahia kitendo kile, usiku huo huo ilikuwa siku ya mkesha wa shangwe kwa wanakijiji wote, ngoma zilianza kupigwa pale pale nyumbani kwa mtemi huku wengine wakiwasha moto halaka na kuanza kuchoma nyama, nikiwa ndani na binti mtemi pamoja na wake zake mtemi pamoja na mtemi mwenyewe tukibadirishana mawazo huku wakiniuliza niliwezaje wejaze kujua ilihari vingunge walishindwa? kabla ya sijatoa ufafanuzi Pete ilianza kudunda dunda na leo ikatoa ile sauti yake "Ntiti ntiti ntiti" "WANAKUJA" niliongea huku nikitizama Pete " WANAKUJA!!! WAKINA NANI???" mtemi aliuliza kwa mshituko...

       -HATUPOI HATUBOI-

           Itaendelea.......!!!!



No comments: