SIMULIZI___ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {26}




SIMULIZI___ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {26}


              Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,,

"Pete ya Faraja yatoa ishara ya ujio wa malkia wa majini kisha Faraja anajikuta akiropoka mbele ya familia ya mtemi "WANAKUJA" nae mtemi anarudisha swali kwa faraja "WANAKUJA!! WAKINA NANI??"

ENDELEA NAYO......

"Swali la mtemi lilinifanya nigundue kuwa nilikosea kuropoka kwani ningeifanya kuwa siri yangu, "UMESEMA WANAKUJA!! WAKINA NANI??" mtemi alirudia swali lake la awali akitaka ufafanuzi wa ndani kwa kile nilichokisema, nilimtizama mtemi kwa nusu dakika kisha nikatingisha kichwa na kusema "Ni vitaaa nzito mtemi wewe unafikiri utaweza kupambana na majini??" nilimuuliza na wote wakashtushwa na swali hilo, wakaniangalia kwa pamoja "wewe majini!! ulishaona wapi mtu akapigana na majini hivi wewe unawazimu??" mke mmoja wa mtemi aliongea kwa kung'aka hadi mtemi ilibidi aingilie kati kumzuia mke wake mwenye Mdomo mdomo, "we nae uwe unapunguza mdomo, kalomo lomo tu siunasubiri kwanza mtu aeleze wewe haraka yako nini?" mtemi aliweka hali sawa kisha akanigeukia "unaweza endelea! na kwanini unasema ni vita dhidi ya majini?" mtemi aliniuliza kistaarabu tena akikaa makini kunisikiliza, "Ni malkia wa majini ndio anaenihitaji mimi, kwani ni muda mrefu umepita alinipa kiapo cha damu kumuoa lakini baada ya kumgundua si mwema anataka kunitumia nilimtoroka na kurudishwa duniani na jini mwingine anaeitwa suleyha, nilizani suleyha nitapofika duniani nitamuoa kutokana na ahadi tuliowekeana huko lakini suleyha aliponitoa kwenye ulimwengu ule alisema haitawezekana kwa kuwa yeye ni nusu binadamu nusu jini hivyo kuna mambo yangeniponza akiwa nami, lakini pia nje ya hilo siku ananifikisha duniani ni siku tuliiziba njia ya malkia kwa ukuta mzito wa barafu lakini sijui alifanyaje na kuizibua njia hiyo sasa amerudi kuniijia, namjua wazi Malkia Zinduna anawivu sana hivyo hatoweza kukubali miezi yote hiyo nilipotoka huko niendelee kuishi duniani" niliongea huku macho yote yakiishia kuitazama Pete ilivyokuwa inawaka nakudunda dunda "Kwa hiyo huyo malkia anakupenda si ndio?" "ndio mheshimiwa mtemi" "kwani hakuna njia ya kumdhibiti asiendeleee kukufata??" mtemi aliuliza "Nipo njia panda mtemi sijui namna gani naweza kumdhibiti jini huyu kwani ni jini aliewaondosha wazazi wangu pia kisa wivu wake wa mapenzi na sasa amerudi kunisumbua na mimi??" niliongea "mh! inasikitisha!, kwa hiyo na wazazi wako waliuwawa na jini huyu huyu sijui nani umemsema! hapo!" mtemi aliuliza "Zinduna na ndie malkia wa majini" nilimjibu kisha ukapita ukimya kiasi wote wakiwa wameinamisha vichwa chini kufikiria tu kwani jambo lile ni zito, "yani nafikiria njia ya kukusaidia lakini nakosa hata cha kusema, kwani! natamani wewe ndio uje kuwa mtemi baada yangu umuoe Mum,.sasa huyu jini si atakusumbua??" mtemi aliuliza "Dhahiri shaqiri! haitawezekana hilo najua kama aliweza kumuuwa mama yangu ataweza kumuua na mke wangu hivyo tutafute namna ya kumdhibiti kwanza Malkia Zinduna" niliongea "daah!! nisamehe mwanangu kwa kukuita mwenda wazimu sikujua kama kuna mambo mazito uliyobeba, asee kweli nakakanya kalomo 'naufunga mdomo'" aliongea mama yule "basi sawa tusipoteze muda zoezi hili tulifanye mapema kama itawezekana" mtemi aliongea na kutuomba wote tusimame tumfate, tulisimama tukatoka nje sijui mtemi alikuwa anatupeleka wapi, Hatujafika popote tulimkuta yule yule mzee alienisaidia usiku wa jana akiwa amesimama nje ya chumba cha mtemi huku akiwa kashikilia kile kifimbo chake, "Na huyu mzee vipi?" mtemi aliuliza "Huyu mzee namkumbuka  alinisaidia kupita pale mlangoni baada ya walinzi kunizuia" nilimjibu huku wote tukikatisha safari na kumtizama mzee yule, "Ni wawapi?!" mtemi aliuliza tena "Sifahamu maana leo ndio siku yangu ya kwanza kumuona sijui hata katokea wapi?" nilimjibu "mh! hawa watakuwa omba omba tuachane nae sie tuendelee na safari yetu" mtemi aliongea na kutuamuru tuendelee na safari tuache yule mzee akiwa amesimama pale pale, "Hakuna sehemu ya kwenda kumdhibiti jini huyo" sauti ya mzee yule ilisikika baada tu yakuwa tumemvuka na kumtegea mgongo, tulishtuka kwa pamoja tukageuka kumtizama mzee yule, "wewe nani kakufahamisha hilo??" mtemi aliuliza ni mshangao tena sana kwa kila mtu mzee yule amejuaje kuhusu hilo, tulianza kurudi alipo yule mzee ili tumsikilize zaidi huenda mungu katuletea msaada kwa njia hiyo, "Mzee samahani umejuaje jambo hili?" nilimuuliza baada yakuwa tumemfikia, alikaa kimya kiasi na muda huo anga lote lilianza kubadirika na kuonyeaha miale ya ajabu huku harufu za marashi nazo zikitawala kila upande "nfu! nfuuu! mh! mbona nasikia..!" mwanamke mmoja miongoni mwa wake wa watemi alitaka kuropoka lakini mzee yule alimuwahi na kumkatisha kwa ukali asimalizie kauli yake "NYAMAZA!! na usije siku nyingine kusikia harufu ya marashi ukauliza au kuongea hawa viumbe ni hatari akisikia umeyavuta marashi yake ataweza kukudhuru Ukome! narudia tena ukome! na ukome! tabia hiyo" mzee yule alirudia neno ukome! mara tatu kwa kuonyesha msisitizo wa jambo hilo, "lakini mzee tokea muda ule sijakuelewa wewe ni nani na nini unataka kutoka kwetu?" nilimuuliza mzee yule, "Utanijua muda ukifika kijana wangu kwa sasa sio muda wa kutaka kujua mimi ni nani" aliongea "Wewe mchawi eeh!! au ni malaika? we jini au msukule, mbona sikuelewi elewi" mtemi aliongea "Piga kengere pulizeni pembe nataka kuwapa kinga kwanza ya kumzuia jini huyu" yule mzee aliongea, kitu ambacho nilikuja kukigundua kuwa karibu na mzee yule ni kinga tosha kwani muda wote tuliosimama Pete yangu haikulia wala kudunda dunda ilikuwa imetulia tuli lakini alipotoka mzee yule ilianza tena kudunda "We! mng'oso nenda kapige ngoma ya wito wa dharura haraka huenda huyu mzee anachokitu cha kutusaidia na atalitatua tatizo hili, na kijana wangu utapata msaada, ukiona mtu anakushika basi jitahidi nawe kushikamana nae" mtemi aliongea huku akijipepea kwa kipepeo chake..

PUUMM! PUUUM! PUMMMMM!!
Sauti nzito ya ngoma ya kijiji iliwashtua watu kuwatoa katika ile hali ya sherehe na shangwe kwa kusikia wito wa ngoma ile, wengine walikuwa wamelewa chakali lakini waliposikia muito ule walijua kuna shida ya muhimu kwani sio kawaida ya mara kwa mara kupigwa kwa ngoma ile, kusikia sauti ya ngoma ile ni hadi liwepo jambo la muhimu sana na tena liwe na chata ya hatari, hivyo wote walijongea na ndani ya dakika tano wakawa wamejazana kwa mtemi, "poleni kwa kuwakatisha na starehe zenu, jamani sie sote tupo katika hali mbaya kwa sasa hebu tazameni anga ilivyo badirika na kuwa ya ajabu" alisema yule mzee na wote wakaangalia juu "mmmh!! mmmh!! mmmmhuu!!" ikazuka miguno kati yao na wengi wao hawakuiona hali ile kabla kutokana na ubize wa sherehe, "macho yenu shahidi masikio yenu yasikaidi, hio ni ishara ya ujio mkubwa wa majini" mzee yule bado aliendelea kuongea masikio na umakini kwa wanakijiji wote waliyatega kisawa sawa kusikiliza hotuba hiyo mpya ya kushtua, "msiogope, wala msifadhaike nipo hapa kuhakikisha jeshi hilo la majini haliangamizi damu yoyote isiyo na hatia" mzee aliongea kisha akauingiza mkono wake kwenye kimkoba chake nakutoka na kibuyu kimoja alikinyoosha juu kisha akasema "hii ni tibaa mbadala haina shaka tutaitumia kwa kila mtu kuipaka kwenye usawa wa utosi wake kwanzia watoto wadogo hadi wazee" aliongea mzee, baada ya maongezi ya lisaa limoja kila mtu alipata alichokipata wakudharau walidharau wakutii walitii, aliwakusanya wanakijiji wote na uzuri wa kijiji kile kilikuwa hakina wakazi wengi hivyo haikuwa kazi kubwa kuwapaka dawa ile ilioko kwenye mfumo wa mafuta mepesi  kama maji, "kwanini Leki,. hutaki kupaka mafuta yale ya ulinzi??" nilimuendea Leki, baada ya kumuona akiwa pembeni hajishuhurishi na maswala ya kupakwa dawa "Wewe inakuhusu nini?! Usinifate fate bwana wewe vipi??" Leki, alinijibu kifupi, nilishtuka kwani tokea tumeujenga urafiki wetu haijawahi kutokea Leki,. au mimi kumjibu vibaya, au kutukanana lakini leo Leki, ananijibu kwa hasira tena akiwa amekunja ngozi ya uso wake yaani ndita, "Leki, unatatizo?? au kuna kitu nimekukwaza labda!! sema! funguka rafiki yangu sio kunikunjia ndita" nilimuuliza Leki kwa upole kwani ni rafiki niliempenda sana kutokana na mengi aliowahi kunitendea, "we vipi mbona unanifata fata kama ni urafiki ushakufa jua hilo" alisema Leki,. "mh! mbona ghafra sana rafiki yangu umebadirika hivi?" sikuchoka bado niliendelea kumuuliza "oyaa!! fanya yako basi huelewi!" Leki, alijibu kwa jazba na kunisukuma nikaanguka pembeni nae Leki akawa anatoka kama hanijui, niliamka tena na kwenda kumshika mkono huku nikiwa nimepiga magoti "unajua Leki, wewe ni kama ndugu yangu na hivi nafanya mpango nikimuoa mtoto wa mtemi nikupe nafasi uwe mlinzi wangu" niliongea matarajio yangu ya baadae, Leki, alionyesha kuelewa na kuanza kuniangalia alipotupia macho mkono niliovaa Pete alishtuka na kufyatua mkono wake kwa haraka kama risasi kisha akasogea mbali kabisa na mimi, tena akionyesha hofu kisha akasema;. "USINISOGELEE"

 ITAENDELEAA,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,



No comments: