SIMULIZI__ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {27}





SIMULIZI__ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {27}


             Endelea,,,,,,,,,,,,,,,

HOFU!! HOFU! HOFU YATANDA...
HOfu kubwa yawatanda wanakijiji wote juu ya ujio wa majeshi ya majini, walishindwa namna gani wanaweza kuwadhibiti majini hao, anaibuka mzee na kutoa dawa itayokuwa kinga watu wasidhurike na majini hao, huku nako Leki,. amkana  Faraja kwanini anaiogopa pete??

ENDELEA NAYO........
..maneno ya Leki,. yananifanya niingiwe na mashaka makubwa kwanini jambo la kuiogopa Pete ile ilikuwa ni kwa majini pekee sasa iweje leo Leki, mwanaadamu aiogope Pete? nilijiuliza sana huku nikimtizama Leki alivyohangaika kujificha macho yake asiione ile Pete, nami nilipoona udhaifu huo niliutumia vyema ili nimnase alie ndani ya Leki, nilisogea taratibu huku Pete nikiifanya kama taa au tochi kwa kummulika Leki, "NIACHEEEE NIACHEEEE NAUMIAAAA AAAGHHHH!!!" ghafla sauti ya Leki ilibadirika na kuwa kama simba mwenye njaa, tayari nalipata jibu kuwa Leki ameingiliwa na pande la jini, "nilijua tu mtakuwa ni nyie ndo maana rafiki yangu Leki anakwepa dawa kumbe mpo kichwani mwake?? haya tokeni haraka nammuache salama bila kumdhuru" niliongea kwa uchungu huku machozi yakinidondoka kwani kwa jinsi jini yule alivyomkaba Leki nilizidi kumwonea huruma, "Toka pole pole na urudi kwenu" niliongea huku nikimkaribia zaidi Leki, pale alipoanguka, tena kwa tahadhari kubwa, "wewe makata, kisimba subiani, maimuna jini mari, bahari, zanjia, lucifuge, santanachi, baal, agarept, marbes, muachie mwili wa kijana huyu taratibu na mrudi kwenu mlipotoka" niliongea kwa kijasiri ili niyanusuru maisha ya rafiki yangu kipenzi, "HATUTOKI KAMWEEE!! sauti za kujirudia rudia zilitoka kwa Leki "anhaaa mna viburi si ndio ngojeeni niwasambalatishe" niliongea kwa hasira na kufungua kile kibuyu niwamwagie yale maji niwaangamize kabisa, lakini kabla sijatenda kumbe yule mzee aliniona na alikuja haraka nakunizuia nisifanye kile kitendo, "Hawa ni hatari ukicheza utampoteza rafiki yako" alisema mzee yule kisha akauingiza mkono wake kweye kile kimkoba na kutoka na dawa ile ya kinga kisha akakipakaa kidole chake cha shahada kisha akamsogelea Leki, pale alipoanguka na kumshika kichwani pindi alipomshika tu Leki,. aliamka kama mtu alipigwa na shoti na kuanza kujirusha rusha huku akipiga kelele nyingi, kelele zake zilipaa na kuwaita wanakijiji na ndani ya dakika chache wanakijiji walisogea kuhushudia movie iliokuwa inaendelea pale, mzee yule aliendelea kufanya utaalamu wake ili amdhibiti Leki,. kwa kadiri awezavyo, lakini nguvu ya jini yule ilionekana kumshinda mzee, kwani ilikuwa kubwa hata zaidi hata waliposogea wale mabaunsa waliokuwa kwenye shindano ili kutoa msaada wote walirushwa kando na kuambulia kulamba vumbi tu, waliamka kwa ghadhabu ili warudi wajaribu tena lakini babu aliwazuia, kisha akasema "kijana huyu jini ana nguvu zaidi na inaonekana alikuwepo nae kwa muda mrefu sana hivyo tutumie akili sana kumtoa na sio nguvu kama tunavyodhania" mzee aliongea kwa sauti ya chini huku muda huo wanakijiji wakiwa wamehaha wasijue wanaweza kutoaje msaada ili kumponya Leki, tulikaa kimya kiasi kisha mzee akasema tena "hatuna njia nyingine zaidi ya hii itatubidi tuitumie tu" aliongea huku akinionyesha ishara nikifungue kibuyu "unahakika haitamdhuru?" nilimuuliza kwani tayari moyo wangu ulikuwa umezungukwa na hofu, "Kuna njia mbili hatujui ni ipi atayopitia" mzee alisema nilimtizama sana vile ambavyo macho yake yalikosa kujiamini, "Mmh!" niliguna huku nikijiuliza nifungue au nisifungue, na hapo yakanijia mawazo ya nyuma kidogo nilipokuwa kule kwenye ulimwengu wa majini "haya ni maji ya chemi chemi ya uzima na kifo, ni mazuri kutibu maradhi ya tumbo na vingine lakini pia yaweza kuwa sumu kwa mtu alie na majini, pia maji haya unaweza kumtimua jini alie kichwani ukitumia maji haya haya" "Mmh!! suleyha kwaiyo nikiyanywa sinitakufa sasa?" "Hapana sio sumu ila yakikutana na madudu tumboni huwa yanageuka na kuwa tiba au sumu" ni maneno ya suleyha yaliyonijia kichwani siku ile tulipotoka matembezi kwa wizi kwenye jengo lile la dhahabu la malkia Zinduna na kwenda kwenye chemchemi moja hivi iliotoa maji ya baridi huku chemchemi ile nakumbuka suleyha alinambia ni chemi chemi takatifu ya uhai na kifo, baada ya kukumbuka nilijua wasi kwa vile kibuyu kile alikileta Suleyha lazima atakuwa amechota maji kwenye chemi chemi ile tena nikiambatanisha na maneno yake siku ile kwamba ninywe nitapata nguvu tayari nililijenga jibu papo hapo "mmh!! sawa kuna kitu nimekumbuka tuyatumie haya haya maji yatamtibu" niliongea kisha nikatabasamu kwani kumbukumbu ile ilinifanya nione alama ya ushindi ikiunyemelea moto wangu, nikayafungua na kumkabidhi yule mzee kisha mzee yule akamzunguka Leki,. na kuanza kumwagia kichwani huku akimpiga pole pole na ile fimbo yake "kama wewe makata, toka sasa, kama wewe mahaba toka sasa na umuachie kijana huyu, kama wewe ni kisimba toka sasa" mzee yule aliongea mneno yale kisha akapitisha maneno yake ya kikabila ambayo sikuyaelewa hata kidogo, macho yote ya kila mmoja aliekusanyika pale yalimtoka kusubiri na kuona majibu ya  mzee anachokifanya, Leki, alizidi kubiringita (kugaa gaa) chini kisha ndani ya muda mfupi akaamka na kuketi kitako akiwa amekunja miguu yake, mzee hakusita bado aliendeleea kufanya maombi yake ya nguvu, taratibu anga lilianza kubadirika na kurudi katika hali yake ya kawaida, huku nako Leki,. jini lile likimtoka na kumuacha akiwa hoi, watu wa kijiji walipoona utulivu kwa Leki, walishangilia kwani waliona wamepata waokozi wawili wataoileta amani kwenye kijiji hicho pasina ncha ya upanga,

UPANDE WA PILI.......
"sheeeeeenzi kabisa wahabi anatuzuia sisi kufanya yetu wakati muda mrefu tumemfungia huku?? subiri atakiona cha moto" malkia Zinduna alifoka baada ya kuona kila analolifanya anazidiwa binadamu wawili wanaonekana kuwashinda nguvu licha ya kuwa malkia Zinduna ana nguvu nyingi za kijini, "malkia tutajitahidi kwa uwezo wetu wote kuwadhibiti hao binadamu" jini mmoja katika walinzi wake aliongea kumfariji "Daah! wale binadamu wanauwezo wa hatari sijui nguvu hizi wametolea wapi??"
"Hata mi nashangaa wamekuwa na nguvu nyingi kutushinda hata sisi??"
"itakuwa kuna jini anaevujisha siri wamejipanga sasa safari hii, naona wameweka ulinzi sasa kwa wale wanaadamu hawawezi kuingilika kirahisi tena wanaulinzi mkubwa sana mtukufu malkia" majini walizidi kupanga mikakati mbadala ya kuishindwa nguvu ya binadam walionekana kuvichanganya vichwa vyao, "ZINDUNA HAJAWAHI KUSHINDWA bado nitarudi tu kuhakikisha nairudisha Pete yangu pamoja na Faraja wangu haiwezekani! nimuache hivi hivi, kwanza Zubeda yuko wapi?" malkia Zinduna aliuliza wote wakakaa kimya, "NAULIZA ZUBEDA YUKO WAPI??" malkia aliuliza tena kwa ukali, ndipo mmoja akajitokeza na kusema, "malkia Zubeda amekwamia duniani" "Na yeye???" malkia akang'aka "ndio mtukufu malkia" "hii vita haita isha milele na huyu binadamu atajutia kile alichokianzisha" malkia alisema kwa hasira mpaka macho yake yakabadirika nakuwa meusi,

#ILIPITA_WIKI_NZIMA tokea tuishinde ile vita ya majini nae Leki, akiwa safi na afya njema kabisa, kwa mujibu wa makubaliano shindano halikuendelea tena kwani, mtemi alikata moja kwa moja na kunipa jiko, siku hiyo vilialikwa vijiji vingi vya jirani vije vishuhudie harusi hiyo iliyokuwa imefana kwa cheleko cheleko na ndelemo, bwana harusi nilikuwa ndani nikisubiria muda ufike niende kukabidhiwa  langu jiko, na baada ya muda kupita niliongozwa njia kwenda kufugishwa ndoa, mfungishaji alianza kwa matambiko maalumu ya kimila kama ilivyo tamaduni yao kisha tukakalishwa kwenye viti viwili walivyoita vita vya mizimu kisha mzee wa kimila akaanza kufungisha ndoa, akiwa anaendelea na maombi kisha ahitimishe kwa kutupa viapo vya ndoa, katika kugeuka geuka kwangu nilishtuka baada ya kuona kuna binti aliefanana kabisa na suleyha akiwa katika wale mabinti wanaomsindikiza binti mtemi wa akiwa wameshika vile viungo vidogo kwa ajiri ya kumwagia mwagia mchele baada ya ndoa,  "suleyha?" niliita  nae alinitizama huku akitabasamu kisha akanionyesha ishara ya kuniita, nilijikuta moyo na akili nikishindwa kuviongoza na taratibu nilianza kuamka kumfuata binti yule  aliefanana na suleyha,

ITAENDELEA....!!



No comments: