SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {28}





SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {28}


             Endelea..........

ILIPOISHIA.......

";Tuliishia pale Faraja alipokuwa akifungishwa ndoa lakini bado mauza uza hayakumuacha yalizidi kumsumbua, mmoja katika wale mabinti wa kumsindikiza binti mtemi aliona akiwa amefanana na suleyha. na binti yule alionekana kumuita huku akiwa anatabasamu

ENDELEA NAYO,,,,,,,,

"Binti yule alizidi kuurubuni moyo wangu nitoke kwenye kiti kile nimfate, taratibu nilianza kujinyanyua ili nimfate binti huyo pasina hiyali yangu kwani akili na mawazo vyote vilivurugika na kuhisi yule ndio suleyha wangu ananipungia mkono, lakini ghafra mzee mfungisha ndoa aliligundua hilo na haraka alinirudisha chini kwa kunisukuma mabegani na nikarudi kukaa kama hapo awali, pindi aliponishika tu! lile wazo na ile taswira ya suleyha vilipotea kabisa na hata nilipomuangalia tena binti yule hakuwa suleyha wala hakuwa anatabasamu bali alitulia tu kushuhudia ndoa hiyo, na hatimae tukafunga ndoa kwa amani kabisa bila hati  hati yoyote wala kizuizi, ngoma za kiasiri zikachezwa kutoka kwenye makabila yote yaliyohudhuria sherehe hiyo, sherehe iliyopambika vizuri kwa baadhi ya watemi kushiriki katika sherehe hiyo, watu wakala na kusaza wengine ilibidi wafungashe vyakula vyao kwenda navyo majumbani mwao haswa!! kwani vyakula vilikuwa vingi na tena bwelele!
        ★★★★★★★★★★★★

Tawala nyingi za kitemi zikaungana, wigo wa kijiji ukatanuka, wakazi wakaongezeka kwa kasi wengine wakivihama vijiji vya jirani na kuhamia kijiji kwetu, kijiji kikawa kikubwa sana tofauti na mwazo, mtemi alifurahia sana na aliona amempa mwanae mtu sahihi kabisa kusimamia na kuendesha tawala hiyo, Asubuhi nyingine tena tulivu ndani ya kijiji cha wawindaji, ilikuwa ni asubuhi ya heka heka kwa wataalamu wa mawindo nami nikiwa mmoja wao kwenye mchezo huo, nilijitahirisha na kuunoa vizuri upanga wangu ukae sawa, pamoja na upinde na mshale wangu alionindalia mke wangu Mum,. muda huo akiwa tayari ni mjamzito wa mimba ndogo, "lakini mume wangu usingeenda huko, yani moyo wangu unakuwa mzito sana kukuruhusu nahisi balaa zito uendako, tizama naona giza mbele yangu mume wangu kwanini usinisikilize tu?!!" tokea jana nilipokuwa najiandaa na mchezo huo mke wangu Mum,. hakuonyesha ushirikiano kikamirifu alikuwa mnyonge muda wote aliongea huku muda huo nikiwa busy kujikarabati tu wala hata nilikuwa sizingatii kile anachokizungumza, "mume wangu unajua penzi letu ndio kwanza linaanza na tena tayari nimekubebea mtoto tumboni mwangu au unataka nibaki mjane? nambie mume wangu unataka mtoto aitwe yatima?" Mum,. aliendelea kuongea kwa uchungu na alipoona siyajari yale anayoyasema alinifata na kunikumbatia kwa nyuma, bado hakuchoka kunisihi "mume wangu nakupenda sana hata kama hutojari kile nilichokwambia sitakula sitalala hadi pale nitapouona uso wako kwani nikuonapo tu ni pona ya moyo wangu, kwa sasa moyo wangu hauna amani tena" alizidi kuongea binti mtemi Mum,. yani mke wangu huku mikono yake ikipita kiunoni mwangu kama mkanda, "Mwanangu atanirithi ushujaa wangu, mke wangu utaitangaza heshima yangu, kifo itakuwa haki yangu, nyama ya moyo wangu itakuwa kafara ya dhambi zangu, nikifa sijapotea bali nitaendelea na maisha mengine kwa mungu, ulidake chozi langu usiliache litaabike, usionyeshe udhaifu wako mbele yangu, kaa kijemedari kuitunza kumbu kumbu yangu, Mum,. nakupenda wewe pekee ndio mwanamke wa maisha yangu" niliongea kwa uchungu mkubwa hadi macho yakashindwa kuhimiri maneno yale yakaanza kudondosha chozi, yakaanza kwa tone kisha yakateremka kama mvua, "mume wangu usilie najua wazi itakuwa safari ya matumaini lakini nitakuombea dua kwa mungu urudi salama, sitaki niitwe mjane mume wangu, nisingependa mwanao asimjue baba ishi kwa ajiri yangu eeh!! mume wangu" Mum,. nae alizidi kuyafukua machungu yake kwani aliamini kwenye safari ile huenda nisirudi tena au nikirudi basi utarudishwa mwili tayari nikiwa marehemu, "jicho lake lisiendelee kumwaga chozi izuie nafsi yako kujilaumu, ufunge moyo wako kwa mapenzi usiruhusu hisia zozote kwa sasa kuyatawala mawazo yako" nilizidi kuongea kijasiri sana maneno ya kishujaa maneno yaliyozidi kunifanya nilie tu, "mume wangu inatosha usiendelee kuongea tafadhari, moyo wangu ni nyama utauchimba kidonda tafadhari nenda na urudi kwa ajiri yangu, mimi nitabaki kukusubiri" Mum,. aliongea nae safari hii aliacha kulia tena nakutoka kifuani kisha akaniangalia kwa macho ya melenge lenge ya machozi, "Niahidi mume wangu utarudi kwa ajiri yangu" alisema Mum,. na kukikunjua kidole chake cha mwisho huku akinitizama, "Ni mipango ya mungu Mum,. ila naahidi nitafanya niwezavyo nirudi kwa ajiri yako" "unaahidi??" "ndio nakuahidi" nilimjibu kisha tukaviunganisha vidole vyetu na huku tukikumbatina kana kwamba hatutaweza kuonana "Chukua zawadi hii ya Pete nakupa kama bahati kwako, kama nitarudi nikiwa salama basi utanirudishia na kama sitafanikiwa kurudi nikiwa hai basi Pete hii uitunze na utampa mwanangu ataezaliwa ikiwa wakiume mvishe mkono wa kulia kidole cha Pete na akiwa wa kike mvishe mkono wa kushoto kidole cha mwisho" nilitoa maagizo hayo kisha nikamkabidhi Pete na kutoka nje ambapo nilikuta msafara wa watu kadhaa walionisubiri, walikuwa sita pekee na sikutaka ulinzi wowote kwani mchezo ule huwa ni mchezo huru haitakiwi kumdhuru mtu labda bahati mbaya tu, Leki mabaunsa watatu, pamoja na mshiriki mwingine walinipokea na tukaanza safari kila mtu aende akawinde wanyama wakubwa yeyote ataefanikiwa kupata mnyama mkubwa katika mawindo yake huyo ndie atakuwa mashindi, tuliondoka na kwenda kwenye msitu waliouita salala, msitu uliosifika kuwa na wanyama wakali wa kila aina na wadudu wenye sumu kali kupitiliza, kwa kuwa kila mtu akiwania kupita njia yake kweli kila mtu alipita njia yake kama ilivyokuwa kwenye shindano la mwanzo, kila nilipopita sikufanikiwa kukutana na mnyama yeyote hadi inatimu saa kumi na mbili jua linapoaanza kuzama na kiza kujongea, nilijipumzisha huku mshale wangu naupinde nikiviweka karibu kabisa kwa usalama zaidi,
        ★★★★★★★★★★★

"OYA ile sumu mmekumbuka kuja nayo sasa! tuifanyie kazi?" "ndio tena hii hapa nimeifunga kwenye pindo" upande wa pili Leki,. anapanga mipango amuangamize Faraja kwa sumu "Na umefanya maamuzi magumu haswa! kumuua rafiki yako sio kitu cha mchezo??" "wacha afe nataka niumiliki utawala" Leki,. aliongea na wale vijana wanne walioungana nia yao wamuuwe Faraja, "Atakuwa wapi kwa sasa??" mmoja aliuliza "Sijui ila amepita mashariki najua nikienda haraka usiku huu huu namteketeza" Leki, aliongea  maneno ya kikatiri kabisa "sawa basi ichanganye au tumpige mshale tulioupaka sumu?" "hapana nipeni mimi nitaifanya kazi hii" Leki,. aliongea kisha wakamkabidhi kichupa hicho kilichofungashiwa sumu, kisha anabadirisha masafa na kupita njia fupi kwani yeye kwenye pori hilo alikuwa mwenyeji njia zote, hivyo haikuwa kazi kabisa kumfikia Faraja. kwa utaalam wa mawindo aliangalia nyayo na hatua zote alizopita Faraja,...!!!

-HATUPOI HATUBOI-
ITAENDELEA....!!!



No comments: