SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {29}




SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {29}


             Endelea.........

"Tamaa ya madaraka yamuingia rafiki wadhati wa Faraja, Leki,. ageuka adui mbele ya Faraja msituni amsaka ampe sumu afe ili arudi akitawale kiti cha kitemi hali ya kuwa mtemi alimuchia madaraka yote Faraja, siku hio pia ilikuwa ni siku ya mateso kwa Faraja kwani moyo wake ulikuwa ukihisi safari yake ya mwisho imefika,

ENDELEA NAYO.......
"Akimaliza kumuuwa tunamuuwa na yeye, tena tumfatilieni tuone anaishia wapi kama kweri ataweza kumuuwa mwenzie" wale mabaunsa nao kumbe walikuwa na wazo lile lile iwapo Leki,. atafanikiwa kumuua Faraja, nao wamuuwe Leki,.. ili wao ndio wataenda kupindua utawala na wao ndio watawale enzi hiyo, "Ni wazo zuri wacheni tumfatilie tuone kama atakunywa ile sumu" waliongea na kukubaliana kwa pamoja kisha wakanyanyuka na kuanza kumfatilia Leki,. kwa kila hatua,

Leki,. alizidi kuchanja mbuga kwenye kiza kile, huku akizidi kuzifatilia nyayo za miguu ya Faraja popote alipopita tena uzuri ardhi ilikuwa imeloana kufatia mvua kubwa ilionyesha siku mbili mfululizo hapo nyuma, kwa utaalamu wake wa kusoma nyayo alizidi kufatilia tu mpaka pale alipofika na kumkuta Faraja akiwa ameketi kama vile vile akili yake ilivyolenga, ndio hivyo alivyomkuta Faraja akiwa ameegamia mti akiota moto, nilishtuka baada ya choko choko za majani yaliyomakavu nilijua ni myama hivyo haraka nilichukua upinde na mshale wangu na kuviweta tayari kukabiliana na mnyama huyo, nilikuja kushtuka kumuona aliekuja pale sio mnyama bali alikuwa ni Leki,, "Mmmh!! Leki,. wewe hukupita njia ya magharibi?" nilimuuliza Leki,. huku nikiutoa mshale wangu na kuurudisha ulipokuwa mwanzo, "Anha!! niliona vyema nije niungane nawewe huku tunywe kwa pamoja kama marafiki wapenzi wa kufa na kuzikana" Leki,. aliongea huku akikitoa kibuyu chake alichojaza maji ya kunywa na kukikaliza chini, "Safari ya maisha ni safari ndefu sana rafiki yangu, mpaka kuitwa mtu mzima sio shughuri ndogo, kwani utavivuka vikwazo vya namna tofauti tofauti kwenye ukuaji, lakini hata kama utavuka vikwazo hivyo pia, lakini siku moja ikumbukwe utakufa tu, na wewe kwenye dunia hii itabaki historia yako tu alikuwepo mtu fulani aliyekuwa mwema au mbaya kama tunavyosoma vitabu vya kale vya watu walioisumbua dunia" niliongea huku nikitupia tupia tuvipande tudogo twa mawe kwenye ule moto niliouwasha "una maana gani kusema hayo Faraja?" Leki,. aliniuliza huku akinitizama machoni,
"Maana zipo nyingi rafiki yangu kipenzi ila hesabu tu hakuna marefu yasiyo na ncha, hata kama utakuwa mwamba kiasi gani lakini ipo siku utavunja chungu na pua yako italamba udongo tu" niliongea tena kwa hisia sana nikiyatizama macho ya Leki,. vile yalivyoonyesha wasiwasi, "Lakini leo naona hauko sawa Faraja eti kuna nini kinachokusumbua, maana leo umekuwa wakuongea mafumbo mafumbo tu" Leki,. aliuliza na kukisogeza kile kibuyu kando na yeye akasogea karibu nakutua panga zake kisha akakaa  na kunitizama kwa makini, nilimtizama sana kisha tena nikavunja ukimya na kuendelea kuongea  "Rafiki yangu sikufichi leo nachukia majini, majini leo wamenifanya niishi kwa tabu na kunipa mikosi mingine nisiyoitarajia majini hawa wamenipa hasira za mara kwa mara, tazama uso wangu umechakaa kwa huzuni na hauvutii tena kama zamani, Malkia Zinduna na kulaani kabisa kwa kuwauwa wazazi wangu, alafu bado unanisumbua na mimi kama vipi nichukue mimi na uiache familia yangu ikiwa salama, kama ni roho yangu nakupa zawadi ichukue basi uiache familia yangu najua nimeacha kiumbe mdogo tumboni asie na hatia kama kuniuwa basi niuwe mimi na iache familia yangu Zinduna" nilianza kuongea maneno yaliyomshitua Leki,, na kuniona labda nimepandwa na wazimu "Faraja uko sawa wewe??" Leki,. aliendelea kuuliza kwa mshangao, "Ndio mi nipo sawa" nilimjibu na muda huo nafsi ya Leki,. ilianza kujutia jambo lile alilopanga kulitekeleza, "daah!! kumbe nafsi yangu ilitaka kunidanganya kufanya maamuzi ya kishenzi sasa maamuzi ambayo yangenifanya niwe na mashaka muda wote, maneno yake mazito yameifumbua akili yangu ni kweli kabisa Faraja una mke na tayari umeshapanda mbegu ya shujaa kwenye tumbo la mama yule, nitakuwa mtu gani nilijaa uchu kiasi hiki, na kwanini moyo wangu ulikubali kushaurika eti nimuue Faraja hapana hapana, hapana kabisa" nafsi ya Leki,. ilizidi kumsuta hata akatingisha kichwa huku machozi yakimtoka, kisha akaitoa sauti yake iliyotawaliwa na kigugumizi cha kilio, "Nisamehe bure rafiki yangu" Leki,. aliongea na kukifungua kinywa chake na kuachia mwano mkubwa nilistaajabu sana kitu alichokifanya Leki,. ndipo nikamuuliza "Leki,. nikusamehe kwa kipi tena na kwanini ulie?" nilimuuliza Leki,. aliye kuwa kainama tu akilia "rafiki yangu mi nimkosefu wa aina yake" "una maana gani Leki,. kuongea maneno hayo?" nilimuuliza huku nikimpiga piga mgongoni kwa mkono wa kushoto taratibu, "dah! rafiki yangu umenitoa kwenye shimo la ujinga wa mataminio yasiyo na maana kisa binti mtemi, najua ulikuwa hujui hili ngoja leo niliweke wazi,  muda mrefu nilikuwa na uhusiano wa kificho na Mum,, tuliyaendesha mapenzi yetu kwa kificho sana ili tusigundurike kwa baba ake kwani ilikuwa hatari upande wangu, hata zile samaki tulizokuwa tukigawana nilikuwa nikizikata mafungu mawili moja kwa mama nalingine nalipeleka kwa Mum,. tabia yangu ya kupenda wanawake ilimshinda binti yule mwenye mapenzi ya kweli hakuweza kuivumilia kabisa, alinikanya mara kadha lakini sikumtii kabisa jambo lililonipelekea tuachane na tokea tumeachana binti yule ameonyesha msimamo wake hataki kabisa turudiane kwani tabia yangu yote anaitambua kuwa mabinti vigori gori ndio kilevi changu, Nilikubari kuja kushiriki mashindano yale ili nishinde niwe mume wake kwa njia hiyo lakini baada ya shindano kuingia dosari alama ya ushindi ilinipotea moyoni mwangu, hivyo tokea ilipotangazwa ndoa yenu nilijitenga nawe na hapo mawazo mengine yakanza kunitawala likiwepo moja la kukuuwa nimrithi mke wako, lakini ulivyosema maneno hayo moyo wangu umeumia sana tena sana kuona kama nitakuuwa na mtoto akazaliwa bila baba asee imeniuma sana rafiki yangu, nisamehe sana tena sana ikibidi unipe adhabu yeyote chungu," Leki,. aliongea na kuzidi kumwaga machozi kama mtoto, "Haustahiri adhabu Leki,. kuyajutia maamuzi yako pia ni adhabu tosha kwa moyo wako, mimi sina neno rafiki yangu kimoyo kwatu bila kinyongo nasema nakupenda wala usijutie maamuzi yako tena usijione mnyonge tena najua mapenzi ni kitu kibaya na ndio kitu kinachonifanya niteseke hadi sasa na Zinduna, Malkia Zinduna pia aliwauwa wazazi wangu kisa mapenzi hivyo hivyo kwa hiyo Leki,. mimi sikushangai kabisa, wewe ni rafiki yangu bado" niliongea huku nikimkumbatia Leki,. kana kwamba hakukuwa na jambo nililolisikia, Leki,. alilia tu bila mpaka, "siumeona sasa niliwaambia wale hawawezi kuuwana wapige mshale wote tuwauwe" wale jamaa waliokuwa wamejificha pembeni waliona tukio lile hilo walisemezana wawapige mishale lakini sijui kiliwaingia nini baadae nakusitisha zoezi lile kisha wakaondoka pale nakuwaacha marafiki waliopendana,

#UPANDE_WA_PILI,,,,
Mum,. aliendelea kusubiri tu nje kama mumewe atarudi muda huo, "Malkia ungeingia ndani sasa usiku huu unataabika hapa nje bure, mumeo atakuja tu" mlinzi wa Mum Queen,. alimpa neno baada ya kuona muda umekwenda nae Mum Queen,. hajachoka kumsubiri mumewe, "acha nitaabike tu, sijui hari aliyonayo mume wangu unafikiri napata raha gani sasa kukaa ndani?" Mum Queen,. alimtupia swali yule mlinzi aliemuuliza hapo mwanzo "Lakini atarudi tu," yule mlinzi nae alimpa moyo binti mtemi asikate tamaa, lakini baada ya muda aliingia ndani na kukaa kwenye kiti huku mlango akiuacha wazi na macho yake yote yakielekea njia aliyopita mumewe kuona kama atatokezea, kwani mlango wa nyumba hiyo ulitazama sana na njia ile aliyopita mumewe,  lakini ghafra akiwa bado anatizama nje alimuona binti mmoja mrembo mweupe mrefu alievalia gauni lake jeupe refu na kichwani akiwa ametinga kidani cha kimalkia, binti yule alionekana kuja taratibu kabisa tena kwa mwendo wa madaha, binti mtemi aliogopa sana kumuona binti huyo wa ajabu aliye kuwa aking'ara sura yake, "we..! we..! ni nani??" aliuliza baada ya kuingia binti yule ndani pasina kizuizi kwa walinzi "SULEYHAAA" alijibiwa ..!!

Suleyha amerudi kwa Kheri au kwa shari? tukutane saa Tatu katika hitimisho la SIMULIZI HII..

NITATUMA FINAL EPISODE HIVYO USIKOSE  KESHO MAPEMA,,,,,,, Kumbuka Ewe Mwana Simulizi kutuma Mchango wako wa Manunuzi ya Mb. Katika Bodi ya Simulizi ndiyo inasababisha kukuletea Vitu vikubwa sana Na kukupatia Simulizi zenye Mafundisho mema Na mazuri sana. TAFADHARI Ebu Leo jaribu kutuma Sent hiyo ni 1000/=tu inakuwezesha Mwezi mmoja kupata vitu vikubwa sana, Karibu,,...

 -HATUPOI HATUBOI-

Onyesha upendo kwa Kutoa Maoni Na Mtazamo wako:-

          ITAENDELEA,,,,,,,,,,,



No comments: