SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {30}




SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {30}


             (MWISHO)

Maisha ya kijana Faraja yaliingia mashakani baada ya kupotea akiwa katika shughuri yake ya uvuvi, jambo lililompelekea aibukie katika ulimwengu wa majini ambapo alikutana na vitu vingi vya thamani ikiwepo jumba kubwa kabisa lililopambwa kwa madini na mawe yaliyoitwa lulu,  kwa mara ya kwanza Faraja anakutana na jini mwenye sura ya binadamu jini yule anampokea kwa bashasha kubwa na kumpeleka kwenye himaya ya malkia wa majini Zinduna, baadae Malkia anatoa  tangazo la kuolewa na Faraja hapo ndipo yakaibuka makundi ya kulipinga hilo, inshu inakuwa ngumu kila siku ikipangwa ndoa mambo yanaingiliana na ndoa ile inashindwa kukamilika, nje ya hapo Faraja pia anajikuta akimpenda mtumishi wake jini suleyha jambo lililoleta mtafaruku mkubwa na hatimae malkia Zinduna anagundua na kumuhamisha suleyha ili wasiwe karibu na Faraja tena, muda ukayoyoma, Faraja akaanza kuhisi mambo tofauti kwa malkia Zinduna hivyo akaanza kumpeleleza na ndipo anafanikiwa kumjua Zinduna sio jini wa kawaida, Faraja akafanya mpango wa kutoroka kurudi katika dunia yake kupitia mikono ya suleyha pamoja na Pete aliopewa zawadi na malkia Zinduna huyo Malkia Zinduna, huku nyuma ameshajua siri kuwa Zinduna ndio aliewaua wazazi wake, hatimae Faraja akafanikiwa kutoroka na kutoka nje kabisa ya ulimwengu ule akiwa na Seif farasi aliemuasi malkia Zinduna pamoja na suleyha mpenzi wake, mwisho suleyha anakataa kuishi duniani kwa kuwa yeye ni jini na Faraja ni binadamu, wanaachana hivyo suleyha akirudi ujinini na Faraja akirudi na kuendelea kuishi maisha  yake ya kawaida duniani, alikubali kukiacha cheo cha ufalme kwenye sayari ile aje aishi maisha aliyoyazoea, muda mrefu ukapita nae suleyha hakurudi ndipo Faraja alipoamua kujiunga na shindano baada ya kusikia mualiko huo, aliingia kwenye shindano hilo la kumuwania binti mtemi, na kukuta njemba za miraba saba zikiwemo shindanoni, mwisho wa yote anafanikiwa kuwashinda kwa kumponyesha mtemi, lakini upande wa Malkia Zinduna nae alizidi kutumia mbinu za kuwatuma majini wake ili wamrejeshe Faraja kwenye himaya yake lakini inashindikana kabisa Pete inakuwa msaada mkubwa kwa Faraja, inafikia sehemu Faraja anakumbana na vitimbwi tofauti tofauti lakini pete inakuwa ngao, hatimae vita ikatangazwa na malkia Zinduna lakini walipovamia kijiji majini wale walikuta tayari kijiji kikiwa na ulinzi hivyo wanarudi kujipanga upya kwa mashambulizi, mwisho rafiki aonekana kuingiwa na tamaa lakini baada ya maneno yenye sumu kutoka kwenye kinywa laini cha Faraja rafiki akili makosa yake na hatimae SULEYHA anafika kwa mama mjamzito mke wa Faraja uku Faraja akiwa bado msituni...

ENDELEA NAYO,,,,,,,,,,

"Moyo wa binti ulitaharuki uoga ukamtawala kwani hakuwahi kuona binti alieng'aa kama yule, alianguka chini na kuaanza kujivuta kwa makalio hadi pale alipofika kikomo ukutani macho yalimtoka koma akizani sasa ni wakati wa kufa kwake, "usiogope binti mtemi mimi ni mwema sana kwako" suleyha aliongea huku akiupunguza urefu kwa kuchuchumaa na kumtizama binti mtemi aliye kuwa amekwama hata maneno kushindwa kuyatoa kwa hofu, "mimi ndio niliemuokoa Faraja kumtoa kwenye dunia yetu ya majini" suleyha alizidi kuongea huku macho yake yote yakilitazama tumbo la binti mtemi, "Ila nisamehe mimi sina hatia nisamehee"  binti mtemi aliongea kwa uoga sana huku jasho la uoga na ngozi ilitoa vipele, "Hauna hatia binti mtemi sema nimekuja kukupa hongera kwa kumbebea shujaa wangu kitoto, na mtoto huyu ni mtoto wa miujiza ni mtoto ataezaliwa na nguvu nyingi za ajabu, na mtoto huyu atakuwa mtetezi kwa wanyonge, atapambana na nguvu za wachawi, majini wachafu, maruhani na mapepo wote wabaya" suleyha aliongea na kulishika tumbo la binti mtemi na kuzipenyeza nguvu zake, kisha akanyanyuka na kusema "Najua unayo mengi yakujiuliza kuhusu mimi muda hautoshi kubaki duniani narudi kwenye dunia yangu ila chochote ulichokiona na kukisikia tafadhari usimwambie Faraja kuwa nilikuja hapa, ifanye iwe siri yako usithubutu kabisa kumwambia" suleyha aliongea kisha akaondoka zake tayari akiwa amepenyeza nguvu zake katika tumbo la binti mtemi,
    ★★★★★★★★★★★★
"Tupumzike hapa rafiki yangu na kesho alfajiri tutarudi ngomeni" nilimwambia Leki na tukapumzika pale, usiku mandoto ya ajabu yalizidi kunisumbua tu, kucha niliweweseka sana jasho zilinitiririka hata radha ya usingizi sikuipata kabisa, kiukweri hali ile ilikuwa ikiniumiza sana moyo nilijiuliza hali hiyo itaisha lini maana mauza uza yamekuwa mauza uza kwangu kila uchao, Asubuhi hiyo baada ya kulala tongo macho tulianza safari ya kurudi kijijini kwa mwendo wa taratibu sana tukipiga story za hapa na pale hadi tulipofika kijijini kwetu, walitupokea kwa shangwe kama ilivyokawaida yao licha ya kuwa hatukufanikiwa kupata kidigi digi chochote, "MUME WANGUUUUU" Mum Queen,. alifurahi sana kuniona nikirudi nikiwa mzima sina hata kovu kwani tokea jana hakuyafumba macho yake kabisa, alikuja anakimbia nami nilimfata nikikimbia na kuutupa mshale huko, "Sikulala usiku kucha nilikesha kukusubiri tu wewe mume wangu" Mum Queen aliongea baada ya kuwa ametua kifuani, "Nami nilijua wazi umeteseka ila pole mungu kanirudisha tena kwako" niliongea kwa furaha iliopitiliza, "sasa hapa moyo wangu umetulia tuli kama kichanga kilichopata nono" aliongea Mum Queen jambo lilionifanya nicheke, "Acha utoto nawe huoni wanakutazama??" nilimuuliza kiutani "acha watizame kwani nani asiejua na kupenda?" Mum Queen, alitania tena "kila macho yamekuwa shahidi juu ya mapenzi yetu na umeonyesha mfano bora kwa wenzio NAKUPENDA SANA MKE WANGU" niliongea "nakupenda pia laazizi kipenzi cha moyo wangu" alijibu Mum Queen, kiririii riiiii riiiii!!!! vikifatia vigere gere kibao kwa kina mama,
 ★★★★★★★★★★★★
Mapenzi yetu yalistawi vizuri kwa kila mtu kumjari mpenzi wake, vitisho vya Malkia Zinduna havikuendelea tena, muda ulipita siku zikasonga miezi ikakatika na sasa yametimia!, jioni moja hivi Mum Queen,  anapata uchungu, haraka haraka jitahada zinafanyika za kumchukua kumpeleka kwa mkunga  mmoja aliekuwepo karibu sana na hiyama yetu, tulimfikisha na haraka aliingizwa ndani kwa ajiri ya zoezi zima la kuzalishwa, nilibaki nje na Leki.  tukizunguka zunguka kusubiri uzao huo, mwezi nao ukazidi kuachia mwanga wake mkali, mara sauti ya kitoto kichangaaa ikapenya masikioni mwangu ikilia Ahghaaa na tayari niligundua dume limezaliwa tulipongezana sana na Leki,  kwa kufanikiwa kumpata shababi mwingine, tulibaki nje kusubiri maelezo ya mkunga na baada ya muda tuliruhusiwa kuingia kumuona mtoto, "hongera  sana sana mama" nilimpa hongera mke wangu kwa kufanikiwa kujifungua salama "la kiume au la kike??" nilimtania tena, "kama wewe" nae alijibu kwa sauti ya chini, moja kwa moja nilimuangalia mtoto mtoto nae aliponiona alitabasamu kisha akaita BABA, mshituko mkubwa ukanikuta hakuna alieamini kitu kile mtoto wa masaa kadhaa kucheka na kuongea??? hii ilikuwa mpya hakuna alietarajia lile kuliona na kulisikia,...

   .!!!....MWISHO......!!!!

Tukutane katika season  Nyingine tukiaacha hii ya Malkia Zinduna (malkia vwa majini),..

Pia nikushukuru wewe uliekuwa nami bega kwa bega toka mwanzo hadi mwisho wa kigongo hiki cha kusisimua,
AHSANTENI SANA!! NA TULIPOWAKOSEA MTUSAMEHE BURE,,,
NASI NI BINAADAM, NA  ATUJAKAMILIKA,,,,,,,,,,
ila tu usitoke kwenye Group lako hili pendwa la Mafunzo kwa njia ya Hadithi kamatia hapo hapo twendwe pamoja,,,,,,,,
#HASH TAG,,, YETU NI:-
Dr. Tupe raha kwa mafunzo elekezi ya Simulizi,..pia Ujumbe wetu Kama Bodi ya Ulimwengu wa Simulizi,;
##################
KAMA Ukiamka kesho mzima basi Chukua Tsh. 5000/= kanunue Mchi wa Sabuni, Dawa za Meno, Na Miswaki, Mafuta ya kujipaka. Nenda Gereza lililo karibu Na wewe Muombe Askari kwamba Unataka kutoa kwa Wafungwa (3) au (4) Ambao hajawai kutembelewa Na Ndugu zao kabisa.
Askari Atawaita, Then Wagawie kipande kimoja kimoja Na Zile Dawa za Meno, Nenda vivyo hivyo Gereza la Wanawake Nunua Na Pedi, Wagawie ambao hawajawahi kutembelewa Na Ndugu,,,.
Fanya hivyo kwa Wagonjwa walioko Hosptalini ambao hawajawahi kutembelewa Na ndugu Na kupewa mahitaji, hakika jambo hili Utaona  ni dogo ila ni kubwa kwa Mungu aliye tuumba,,,....
Usidhani kila jambo ni kupiga Magoti Na kuswali tu, au Kudiriki kila siku Swala Tano Laashaa,... Mambo mengine kwa mungu yanaitaji Funguo mbali mbali Ndiyo maana Una Swali mwaka mzima Ukiomba mambo yako yakuendee Vizuri ila unaona Mambo hayaendi Vizuri,. Kufuli ya Solex Ina funguo zake, Kufuli ya Wohu, in a funguo zake, Usikariri funguo moja tu,..
Majibu ya Maombi yako (Dua) zako Sometimes yapo kwenye funguo za waliofungwa Magerezani huko wawe Na hatia ama wasiwe Na hatia, Ama funguo zako zipo kwa  Wagonjwa Mahospitali, Wajene, Na Mayatima,.
Ndugu Mwana Ulimwengu wa Simulizi Fungua mambo yako Mwaka 2020 Na funguo sahihi ili uone Majibu ya Mungu wetu, hakika Utastajabu,,,,,,,,,
Nawatakia Kheri ya Mwaka 2020,,...
         ASANTE,,,,,,,,,,,,,,



No comments: