CHOMBEZO: MPANGAJI EPISODE: 07 (Inaendelea..)
aliingia ndani na mimi nikabaki nikisubiri pale nje ya mlango wao kwa ajili ya kuonana na mama yake. Haikuchukua hata dakika kadhaa,mama yake naye alitoka huku akiwa roho juu,nahisi alikuwa hivyo baada ya kusikia kuwa mahala pale kuna wezi.
“Eti umeibiwa?”.Lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa mama yule baada ya kukutana na mimi.
Kilichonishangaza hata yeye alitoka kavaa khanga moja na mara nyingi alikuwa anajaribu sana kuifunga vizuri ili isidondoke.
“Ndiyo mama. Waliniibia jana sijui saa ngapi,maana mimi nililala saa sita za usiku kwa sababu nilikuwa naangalia muvi zangu”.Nilimjibu yule mama kistaarabu lakini bado nilikuwa namstaajabu kwa alivyokuwa amevaa.
Mama yule hakuwa mama kama nilivyodhani,alikuwa ni mama kwa sababu alikuwa ana watoto tu!. Lakini kiumri ambao ulitambulishwa na mwili wake,wala hakuwa mkubwa. Alicheza kwenye miaka ishirini na nane hadi thelathini.
“Kwa hiyo wamechukua vitu gani?”.Alinitoa mawazoni mama yule kijana kwa kuniuliza swali hilo.
“Aaah! Ni vibaka tu! Wamebeba vitu vidogo vidogo hivi. Ki-TV,Sabufa,dekoda,pasi na jagi la kuchemshia maji,na tuvitu vitu kama huto”.Nilimjibu mama yule huku yule binti yake akiendelea kunisikiliza kwa makini.
“Hiiii jamani.Sasa na mimi wakiniingilia na kuniibia TV na Redio si ndo wataniua kabisa. Maana mimi bila vile siendi kabisa”.Mama yule alionesha hali ya uwoga kidogo.
“Hawawezi kuja tena. Kwanza ni wajinga tu! Mbona hawakuniingilia mimi nilipokuwa nimelala?Wangekuja tupambane”.Nilitoa shaka huku nikijidai na vinguvu,kumbe hovyoo.
“Basi kaka yangu naomba sana uwe unawaangalia hawa watoto,yaani mimi siyo mkaaji sana hapa nyumbani,hivyo naomba sana uwe unawaangalia. Wakipiga tukelele kidogo,toka na kuwaangalia wana nini”.Mama yule alinipa majukumu mazuri sana,ambayo ni wamama wachache wanaweza kufanya hivyo.
“Sawa mama. Kwani kuna watoto wengine zaidi ya huyu binti?”.Niliongea huku namuangalia yule mtoto wake ambaye muda wote alikuwa anatusikiliza tu!.
“Ndio ninao. Yupo mmoja ambaye sasa yupo likizo,anasoma shule ya msingi,anaitwa Yesaya. Na nina mwingine wa miaka mitatu anaitwa Tumpare na huyu amaitwa Tusegile au Tuse”. Mama yule hadi anamaliza kuitambulisha familia yake,nilishagundua kuwa wale ni Wanyakyusa.
****
:: Fisi kakabidhiwa bucha, Unavyodhani nini kitaendelea hapo? Prince atafanikiwa kumpata Tuse? na itakuwaje mbeleni?
:: Usikose Episode 08....stay updated
No comments: