Chombezo: MPANGAJI Episode: 07






Ilipoishia.......

Nilimuachia kiasi cha shilingi elfu sitini kama shukrani. Na wakati naondoka,kiukweli aliumia sana. Mai alikuwa ananipenda toka moyoni, na ndiyo maana hadi leo ninaye.

Songa nayo sasa..

Nilipofika Dar es Salaam,mambo yalikuwa tofauti sana na nilivyotegemea. Kaka yangu ambaye alikuwa anafanya kazi ya kusafirisha bidhaa nje ya nchi kwa kutumia usafiri wa majini,mara nyingi alikuwa siyo mtu wa kushinda pale.
Na bahati mbaya nyumba tuliyoamia alikuwa amepanga lakini wapangaji wengi walikuwa wanafanya shughuli zao na kurudi usiku. Si hivyo tu! Nyumba ile ilikuwa inajitegemea kwa kila mtu,yaani ilikuwa imeunganika na kutengeneza nyumba moja kubwa.Kila MPANGAJI,nyumba yake ilikuwa ina geti na mlango,choo cha ndani,sebule,vyumba viwili vya kulala na jiko.Kwa kifupi ilikuwa ni kama nyumba ya peke yako.Ilikuwa haina bugudha kama zile za Uswahili zilizotenganishwa na korido.

Ile nyumba ambayo kaka alikuwa anaishi,ziliunganika nyumba tatu,na kwa pembeni yake kulikuwa na nyumba nyingine tatu ambazo zilikuwa hazijaunganika. Zilikuwa zinajitegemea lakini ni nyumba za mtu mmoja aliyempangisha kaka.
Sisi tulikuwa tupo kwenye zile tatu zilizounganika,kama nilivyosema hapo mwanzo. Na nyumba yetu ilikuwa ni ya mwisho kabisa,yaani ndiyo ya tatu katika ule muunganiko.

Baada ya mimi kwenda Dar,ambapo ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza,kaka aliniaga kuwa anapeleka mzigo Afrika Kusini,hivyo hatorudi mapema,atakaa kwa miezi kama miwili. Cha msingi alichonihasa ni kuwaheshimu wapangaji wote,na zaidi nisiwe mzuraraji kwa sababu bado sijaufahamu mji.Pia alinihasa kuhusu kutengeneza marafiki,aliniambia niwe makini nao sana,kwa sababu wengi wa marafiki wa eneo lile la Msasani,walikuwa hawaeleweki.
Kwa kuwa nyumba ilikuwa ina kila kitu,yaani kama movies,zilikuwa za kutosha,nyimbo zilikuwepo,kompyuta ilikuwepo,na mambo yote yanayomvutia kijana,yalikuwepo. Sikuwa na sababu ya kuwa mzururaji.Nikawa mtu wa ndani tu! Kuangalia filamu ndiyo ikawa kazi yangu. Siries mbalimbali nikajifunzia Dar kuziangalia. Kwa kifupi niliweza kukaa ndani kwa masaa karibu ishirini.Nilipotoka nje,basi nilienda kununua chakula na kwa kuwa kulikuwa na kila kitu humo humo ndani,basi nilikaangiza mapocho pocho yangu na kujilia humo humo.
Wale wapangaji waliyokuwa wamepanga pale,walikuwa bize sana,na kuna wengine sikuwahi kuwaona zaidi ya mara tatu hadi wanahama.Hao walikuwa nyumba ya katikati katika ile nyumba niliyokuwa mimi. Wale wapangaji wa katikati,walihama baada ya kumaliza nyumba yao waliyokuwa wanaijenga kitunda.
Baada ya kuhama,pale katikati kukabaki wazi,hivyo nyumba ikazidi kuwa kimya.Kelele zilizosikika ni zangu tena wakati nasikiliza mziki au kucheki muvi.Nilikuwa na kelele sana,na tena nilikuwa nazidi kujifunza mengi sana wakati nipo peke yangu. Ile kompyuta niliyoachiwa,nikawa naitumia kuadownload mambo mbalimbali na kujifunza. Niliweza kudownload programu moja inaitwa FL STUDIO 7,ambayo ilihusika na kutengeneza mapigo ya muziki.
Baada ya kudownload,nikaanza kujifunza kutengeneza mapigo hayo kwenye mitandao mbalimbali hasa youtube. Nilikuwa naangalia video za watu wanaoelekeza kufanya hayo kupitia hiyo youtube.
Hatimaye nikaelewa na ghafla nikaanza kutengeneza mapigo hayo na baada ya kuweza,basi nikaanza kufanyia mazoezi ya kuimba na kuchana . Ikawa ni kelele mtindo mmoja pale napoishi,na kwa kuwa hakuna aliyefatilia maisha ya mwenzake,basi kwangu maisha yakaendelea na full kelele.

Mwezi ukakata tangu nije Dar.Ile tabia ya ukicheche ikawa imepotea kwa muda kutokana na ufinyu wa watoto wa kike kunitembelea pale nyumbani. Wapangaji waliokuwepo pale,wengi walikuwa ni watu wazima na wenye hali fulani ya kutishia amani. Kulikuwa kuna mwanajeshi,ambaye naye alikuwa na mke mwanajeshi,nani akaguse hapo,nife.
Kulikuwa a jamaa mmoja ambaye nilikuwa sielewi anafanya kazi gani.Kutoka kwake ni asubuhi,na kurudi ni saa nane usiku,na alikuwa ana hela balaa. Wanawake sikumuona akiwa nao,na mara nyingi alikuwa hacheki kizembe. Wengine waliishi kama sisi.Yaani kulikuwa na mtu na kaka yake wakiishi zile nyumba zilizojitenga.Wao walikuwa wanaondoka asubuhi na kurudi saa nne usiku.Na walikuwa wanarudi kila mtu na mwanamke wake.Walikuwa wanabadilisha kila siku. Maisha gani hayo,sikutaka hata kuwazoea.Nikazidi kuwa mtu wa movies tu.
Kuna hao wengine walikuwa wanakaa mwanzoni mwa nyumba kabisa ile tuliyo sisi.Hao walikuwa ni Waganda,walikuja na kupanga pale ili wafanye mambo yao. Walikuwa ni dada na kaka.Hao ndiyo walikuwa hawana habari na mtu,walikuwa kivyao vyao. Na kama kawaida,walikutana na Prince Mukuru,mzee wa mapozi.Nilikuwa sina habari nao.

Wale wa katikati waliohama,niliwahi kuwaona mara mbili tu!Siku yakwanza walikuwa wanatoka na mimi natoka,ndiyo nikamuona jamaa mmoja na mke wake ambaye alikuwa kavaa baibui la Kiislam lililofunika kichwa chote na kubakiza macho tu!.Na mara ya pili,waliniita niende kuwaaidia kutoa kabati wakati wanahama.Hata hivyo pia,sikumuona yule dada uso wake.Nikapotezea,japo wale wangeendelea kukaa ndiyo wangekuwa rafiki zangu.
Makelele niliyokuwa nayaendekeza,yakaniponza. Kumbe kitambo wahuni wa eneo lile walikuwa wanamendea mali za watu tunaoishi mle.Na kile kitendo cha wale wapangaji wa katikati kuhama,kikawapa upenyo wao kuzidi kutalii maeneo yetu kwa sababu kampani ilipungua.Nahisi walikuwa wamenipania sana kunifundisha jiji.
Nakumbuka siku hiyo nilikuwa nimekaa ndani nasikiliza muziki kwa sauti ya juu kama kawaida yangu.Wakati nafanya hayo,kumbe nje kulikuwa kuna wapangaji wengine wanahamia ile nyumba ya katikati.Nilipogundua hilo,nilienda kuchungulia kwenye dirisha la chumba changu na kuona wapangaji waliokuwa wanaamia. Kulikuwa na rundo la vijana wakifanya kazi ya kuingiza vitu vya hao wapangaji wapya,hivyo sikuweza kuona sura za wapangaji hao. Nikarudi zangu na kuendelea na shughuli zangu zinazonihusu.

Usiku wa siku hiyo hiyo.Nikaibiwa vifaa vyangu vyote. Kuanzia mziki,TV ndogo iliyokuwa kama ya inchi ishirini na nne lakini flat screen ,deki,decoda ambayo ilkuwa ni ya DSTV na vitu vingi vya ndani hasa vinavyotumia umeme. Uzuri tulikuwa na TV moja kubwa sana ya inchi thelathini na saba,hiyo nadhani walishindwa kuinyanyua niliikuta,kompyuta nilipenda kulala nayo,hivyo nayo ikasalimika.
Hayo yote nilikuja kuyagundua baada ya kuamka asubuhi na kukuta geti la nyumba limewekwa pembeni,kufuli nadhani lilimwagiwa asidi,maana kule kuungua kwake kulinipa mashaka. Moyo uliumia sana,lakini nilikuwa sina jinsi zaidi ya kumpa taarifa kaka ambaye alishukuru MUNGU kwa kuwa nilikuwa mzima.Pia niliwaambia ndugu zangu pamoja na baba kilichotokea.
Kaka akiwa amebakiza siku kumi na tano kurudi,alisema akija tutaenda Kariakoo au Mlimani City kurudisha vilivyoondoka. Nikawa mpole sana na kumsubiria aje. Sikuwa na wazo tena la wale wapangaji walioamia.Akili yangu yote ikawa ni kujiuliza endapo wale jamaa wangenivamia tena na kuja kuchukua vilivyobaki. Niliumia sana kichwa.
Kingine nilichokuja kugundua,ni walinipulizia madawa.Kwani karibu wiki nzima nilikuwa mtu wa usingizi tu!. Baada ya wiki hiyo,ndo nikapata wazo la kwenda kuwaambia wale wapangaji walioamia kuwa wawe makini sana na eneo lile.
Nilitoka na moja kwa moja kwanza nikaelekea dukani na sokoni kwa ajili ya kununua vyakula vya siku ile.Baada ya kurudi,ndipo nikaenda hadi kwenye mlango wa wapangaji hao wapya na kuugonga. Haikuchukua muda sana,mlango ukafunguliwa ma binti mmoja ambaye alikuwa anachungulia bila kuutoa mwili wake nje.
“Habari yako”.Nilianza kumjulia hali baada ya kutoa sura yake nje na mwili ukibaki ndani.
“Safi,mambo vipi?”Alinijibu na kunijulia hali pia.
“Poa. Namuulizia Mama au Baba,kama wapo naomba uniitie”.Nikaenda moja kwa moja kwa kilichonileta.
“Baba hayupo”.Alinijibu yule binti.
“Na mama je?”.
“Mama yupo ndani,kwani unawataka wa nini?”.
“Ahaaa,samahani sijajitambulisha. Mimi ni MPANGAJI wa hapo mlango wa mwisho.Ile siku ile wakati mnaamia mwenzenu nilikuwa naibiwa,ndo maana nimekuja hapa na kuwaomba uniitie wazazi wako ili niwape taarifa za kuwa makini”.
“Haa,uliibiwa?”.Binti yule alihamaki huku anatoka nje na hapo ndipo nilimuona mwili wake. Alikuwa kavaa khanga ambayo iliishia juu ya kifua chake,na yawezekana ndani alikuwa kavaa chupi tu!. Sikumfatilia zaidi ya kuwa makini nisioneshe kama namchunguza.
“Ndiyo,nimeibiwa.Ila naomba umuite mama kwanza ili niongee naye,mimi naenda ndani mara moja kupeleka huu mzigo”.Nilimwambia hivyo na kwa kuwa mlango wangu ulikuwa kwa nyuma,nikatoka pale na kuelekea mlango huo ulipo kwa ajili ya kupeleka bidhaa zangu nilizotoka kununua muda ule,ambazo zilikuwa ni mboga.
Wakati nampa mgongo binti yule,kumbe alikuwa kama haamini kama na mimi ni MPANGAJI wa pale,hivyo alianza kunifatilia kwa nyuma bila mimi kutambua. Nikaingia ndani na kuweka nilichonunua,na hazikupita hata sekunde nikawa nimetoka. Ndipo uso kwa uso nikakutana na yule binti akiwa maeneo ya nyumba yangu. Nilijua ana maana gani,hivyo wala sikuwa na wasi wasi,kwa kuwa kishaamini kuwa mimi nakaa pale,basi atamuita mama yake.
Aliponiona akazuga anageuka na kuanza kutafuta kuni za kuwashia moto. He he heeeeee,uwiiii,jamani kuna watu MUNGU kawapa mambo,duuuh!.
Sikumuona vizuri pale nilipogonga mlango wao,sasa nilikuwa nashuhudia ule mgongo aliokuwa nao. Yule binti alikuwa na makalio hayo,dah! Yaani ni figa ya kibantu kabisa.Kwanza alikuwa ni mweusi wa kung’aa,halafu alikuwa na unene fulani wa kuvutia. Sura yake ilirembeshwa na miwani,huku kichwa chake kikiwa kimekatwa nywele kwa mtindo wa kipanki.Alikuwa ni mzuri “ofukozi”.
Baada ya kuokota vijiti hivyo,ndipo akaanza kuelekea ndani kwao ambapo na mimi nikawa kwa nyuma huku nahesabu ile mitikisiko ya makalio yake ambayo ilikuwa inaonekana sambamba na miguu yake mitamu hata kwa kuiangalia.
***********EPISODE 07 INAENDELEA********



No comments: