Hatua Za Kutumia Kumfanya Mwanamke Aingiwe Na Wivu Kwa Manufaa Yako




Kwa nini unafaa kumfanya mwanamke awe na wivu? Wale ambao washawahi kuwafanya wapenzi wao kuwa na wivu wanajua manufaa yake...yanamfanya mwanamke kuwa na uraibu kwako na hatotamani kukuacha uponyoke mikononi mwake hata kwa sekunde moja.

Mahusiano ya kimapenzi ni kama gurudumu la tukuto, ni hisia ambazo zinamwelekeza mwanamke na mwanaume kutangamana pamoja. Mapenzi, uchu, maliwazo, furaha, na hata wivu. Wivu una nafasi muhimu katika mahusiano kwa kuwa inasaidia kuonyesha majukumu na uwakfu katika mahusiano.

Pia wivu unasaidia kuunganisha mapenzi kwa kuwa wanawake wengine hawayaoni manufaa ya mapenzi mpaka ile siku wataona gere wakati ambapo wapenzi wao wanapata atenshen kutoka kwa wanawake wengine.


So utafanyaje hadi umpandishe wivu mwanamke na wala asipoteze maslahi kwako? Relax, nimekurahisia kazi yako kwa kukuandalia hatua hizi sita.

Kumfanya awe na wivu

ONYO: Hatua hizi zina nguvu ya hali ya juu. Zinaweza kumfanya AATHIRIKE kwako. Hivyo zitumia kwa makini na usizitumie vibaya. 

Hatua #1. Kwanza mpe atenshen yako yote
Bila kuonyesha ama kuwa na connection ya mbeleni, hatua hii haitakuwa na maana yeyote.

Hivyo basi unafaa kutenga muda ili uwe naye. Hii ni kuanzia kuwa pamoja, kumpongoza na kumsifu mara kwa mara, kumtabasamia nk ilimradi ajiskie raha akiwa nawe.

Mfanye ajue kuwa yeye ana umuhimu wa hali ya juu kwako (aidha kama rafiki ama mpenzi wako), na jinsi alivyo tofauti na wengine. Lakini hakikisha ya kuwa hauonyeshi matamanio ya kupindukia kwake. Kuwa mkweli kwa kumwelezea jinsi unavyomhisi bila kuvuka mipaka. [
Hii itasaidia kufanya mahusiano yenu yawe ya nguvu na hali ya juu.

Hatua #2. Ongea na wanawake wengine kwa madakika
Hatua hii inafaa ifatwe na umakini kwa sababu mbili kuu:

i. Ukosefu wa usalama -wakati ambapo utakuwa ukiongea na wanawake ili kuonyesha wivu, hakikisha ya kuwa hauvuki mipaka yako ya kuwatongoza kwa kuwa mpenzi wako anaweza kudhania ya kuwa unatabia za kitombi, jambo ambalo linaweza kuleta chuki badala ya mapenzi.

ii. Matumaini ya uongo -pili ni kuwa kwa hao wanawake unaotangamana na kuongea nao hakikisha ya kuwa hauwatongozi. Hii ni kwa sababu unaweza kuwachanganya na fikra za kuwa umewazimia ilhali ni jambo ambalo ni la kupanga tu. 

Hatua #3. Toka out na marafiki zako halafu umwonyeshe jinsi ulienjoy muda wako 
Hii inaonyesha kuwa kando na kuwa unaonyesha maslahi kwake, una mambo yako binafsi ambayo wewe hufanya.

Ongea kuhusu marafiki zako kwa kuwataja majina, mwelezee mambo uliyofanya ukiwa pamoja na marafiki zako nk. Hakikisha ya kuwa unamwonyesha kuwa unaenjoy zaidi kama hayuko nawe.

Hatua #4. Ongea kuhusu wanawake wengine na yeye
Kuongea na yeye kuhusu wanawake wengine ni njia rahisi ya kumfanya mwanamke awe na wivu. Kama imefanywa na umakini, mwanaume anaweza kupata point muhimu.

Mfano wakati ambapo unaongea na mpenzi wako unaweza kusema "Nimependa style ya nywele za Kate, zinamfanya apendeze sana"

Hatua #5. Vuna nishati yako kwa kutumia mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii ni sehemu muhimu ya watu kutangamana na wengine kweupeni. Ni njia murua ya kuonyesha wivu kiasi fulani katika mahusiano. Waweza kumakinika na baadhi ya marafiki zako wa kike wa mitandao hii kwa kulike photo zao na kutoa maoni kwa picha zao. Njia hii itamfanya mwanamke wako kunotice ya kuwa unathamani flani na kukuona muhimu kwa njia flani. [

Hatua #6. Usizidishe mipaka ya hatua tulizoziorodhesha
Wanawake hawapendi wanaume wabatili na ambao ni waongo. 

Kama utakuwa mara kwa mara ukitongoza wanawake, kunyatia wanawake katika mitandao ya kijamii na kumwambia jinsi wanavutia kumliko kunatoa alama za wewe za kuweza kumfanya mpenzi wako apendezwe kwako.

Kama kuna hatua yeyote ambayo imeelezwa hapa ambayo itamfanya mpenzi wako kuanza kulalamika kwa marafiki zake ni bora kumwambia ukweli.

Fahamu ya kuwa wivu kiasi kidogo ni vizuri...lakini ukipitisha kiwango chake utaharibu.




No comments: