Home
Unlabelled
Mbinu 5 Tofauti Za Kumwomba Mwanamke Namba Ya Simu
Mbinu 5 Tofauti Za Kumwomba Mwanamke Namba Ya Simu
Je umejaribu kutumia mbinu uliyojifunza kuomba namba ya mwanamke lakini hukufaulu? Ama ulifaulu lakini mwanamke amekataa kujibu sms zako?
Well, tumekuja na mbinu mwafaka ambazo zitakufanya wewe upate namba ya mwanamke na aweze kujibu texts zako siku ya pili ambapo utaamua kumtumia meseji.
Wanaume wengi huingiwa na woga ikifikia wakati wa kuomba namba kutoka kwa mwanamke. Haufai kuogopa na jambo hili. Mwanzo nataka nikuonyeshe njia za kumwomba mwanamke namba na pia nikuonyeshe umuhimu wa mbinu moja muhimu ya hizi. [
Mbinu za kumwomba mwanamke namba ya simu.
Hizi ni hatua tano ambazo zitakurahisishia kazi yako.
1. Wajua nataka kwenda, lakini nilikuwa nataka kukujua zaidi. Waonaje nikupigie simu kesho?
Makinika hapa ya kuwa sijasema "nitakupigia simu siku flani" bali nimesema "kesho". Mwambie utampigia simu halafu umuulize umpigie saa ngapi. Njia hii inakupa nafasi ya kujui iwapo amevutiwa na wewe au anakupotezea wakati. [Soma: Hatua za kupata girl friend mpya]
2. "Hey, wajua nataka kwenda lakini nataka kuendeleza maongezi yetu. Waonaje tukutane siku ya ____saa ____?"
Kuweka deti ya siku maalum ni njia nzuri ya kuomba namba kutoka kwa mwanamke. Fahamu ya kuwa umeweka deti yenu sehemu maalum. Hivyo anaweza kuamua kama mtakutana ama kutafuta sehemu nyingine mwafaka. Usitumie maneno kama "wakati mwingine" kwani itaonyesha dalili ya kutojiamini ama kuonesha woga kiasi flani. [
Hizi hapa ni njia za moja kwa moja za kuomba nambari ya mwanamke:
3. "Hivi unatumia simu aina gani?" Atakujibu "Mbona wauliza?" Mjibu "Sababu nlikuwa nataka unipatie namba yako."
4. Mpatie simu yako halafu umwambie "Nataka kwenda lakini waonaje kesho tuendeleze gumzo letu?"
Hii mbinu ya mwisho ni nzuri ya kutumia kumwomba mwanamke namba yake kwa sababu unakwepa kutumia maneno kama: "Naomba namba yako ya simu" [
Hili ni jambo kubwa sana kwa kuwa kawaida mwanamke huandamwa na wanaume wengi asiowapenda ambao wanamuuliza namba zake. Hivyo pindi utakapotumia maneno "Naomba namba yako ya simu" anaweza kukufananisha na wanaume wale wa kawaida asiowapenda ambao kila wakati wanapenda kumwomba namba yake ya simu.
Lakini pindi ambapo utampatia simu yako utakuwa umeashiria mambo mawili: Kwanza atakuwa ameelewa jambo ambalo unataka kutoka kwake bila kutumia maneno "Naomba namba yako ya simu" [
Pili ni kuwa unajenga dhana ya uaminifu kwa akili yake. Kumpatia simu yako mwanamke kunaleta dhana ya uaminifu ambayo ni jambo muhimu kwake. Simu yako ni kifaa chako binafsi na ni faragha yako, lakini pindi ambapo utamruhusu mwanamke kuishika kutaonyesha ya kuwe wewe si mtu mfiche. Mwanzo kulingana na utafiti uliofanywa na wanasaikolojia ni kuwa kupatia simu yako kwa mwingine ni ishara ya uaminifu.
Pia kupatiana simu yako ni kuonyesha kutaka mwenzako akuamini zaidi. So waonaje wewe uitumie mbinu hii ya kuomba namba ya simu kwa njia ya urahisi? [Soma: Mitandao maarufu afrika ya kupata wachumba papo hapo
Mbinu 5 Tofauti Za Kumwomba Mwanamke Namba Ya Simu
Reviewed by RAHA YA MAPENZI
on
February 25, 2020
Rating: 5
No comments: