UKIWA NA MAMBO HAYA MUMEO ATAKUPENDA SANAA
1. MWENYE HISIA ZA UCHESHI:
Ikiwa
unafurahishwa na utani wake, ni jambo
litakalomvutia sana. Lakini ukiwa mwepesi
wa kuchukia na kukasirika, yumkini
mumeo asivutike nawe. Jitahidi kuwa na
hisia za utani na ucheshi... _
2. MWENYE KUSAMEHE:
Unapoelewa kuwa
mumeo sio mtu mkamilifu na unapokuwa
na uwezo wa kumsamehe kwa dosari
zake, hii itamaanisha kuwa unamiliki
mojawapo ya sifa muhimu sana ambazo
wanaume wanazitaka kwa udi na uvumba.
Ukiwa na mchezo wa kumrukia kwa kila
kosa dogo analolifanya au ukawa na
ukosoaji uliopitiliza, tambua kuwa mumeo
hatakuwa mwenye kukufurahia, hata kama
ni miongoni mwa wale wasiosema.
Niliwahi kumnasihi memba wangu mmoja
wa Ndoa Maridhawa kuwa: “Kama
wamtafuta mume asiyekosea, hutampata
na utaishi bila mume”. _
3. MWENYE ASHIKI:
Mwanamke ambaye sio
romantic huwa hamvutii mwanaume. Ili
mwanaume avutike unatakiwa kumfanya
ahisi raha na uwe mwepesi wa
kumchokoza. Ikiwa unadhani kuwa
mwanaume ndiye tu anayepeswa
kukuchokoza, basi hapo unajitesa na
haitakuwa na faida kwako. Boresha uwezo
wako wa uchokozi na kuwa romantic
utaona namna mumeo atakavyokuwa
akikutamani.
No comments: