π’πˆπŒπ”π‹πˆπ™πˆ: ππˆπ“π€πŠπ”π…π€ 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ππ†π” 𝐄𝐏..... 𝟏2






π’πŽππ†π€ ππ€π˜πŽ...
Nilijikuta nalia na machozi yananitoka kama maji..... kwaharaka niliinuka na kukimbia kutoka njee kumtafuta kama hawajafika mbali...

Niliangalia yalipo paki magari lakini sikuona ilipo ile tax..

Kwa haraka nilikimbia hadi mapokezi na kuuliza kama nitapata anwani ya yule mgonjwa alie letwa kwa matatizo ya akili lakini bado ilikuwa ngumu kupatiwa siri za mgonjwa hasa Mwathirika wa gonjwa hili kuu..

Nilijikuta nimeishiwa nguvu na kukaa kwenye bench za mapokezi kwa muda kiasi nikiwa nawaza nini chakufanya...

"Yaarab.. nijalie utulivu wa moyo na nafsi.. nijalie nionane na Mama yangu kabla ya Mauti kumfika..

Niliongea yale maneno mafupi lakini yenye nguvu sana kwa nia dhabiti na machungu yasiyo na kifani...

Nilizidi kuinama pale lakini Ghafla nilijikuta napata nguvu na kuinuka nilipokaa na kwenda hadi wodini nilipo waacha akina Monika..

Tuliandaa utaratibu wa kuondoka pale hospitali hatukutaka kulala  kwa sikuile ili kupunguza gharama..

Nic alienda mapokezi na kulipia gharama za matibabu kwa muda ule mfupi pale hospitali na kupewa baadhi ya dawa za maumivu kwaajili ya Monika..

Monika alikuwa akitembea vizuri kabisa bila tatizo lolote..

Tulipanda gari na kumuomba nic atupeleke tu chuo kwa usiku ule.. niliangalia mda kwenye simu yangu ilikuwa ni saa tatu na nusu usiku..

Tulianza safari hadi majira ya saa nne kasoro tulikuwa chuo.. tuliingia chumbani kwetu na kumuonyesha nic tunapokaa na baadae yeye akaondoka..

Tulioga na kupumzika kwa usiku ule..


Asubuhi nilikuwa wakwanza kuamka....
 nilishuka kitandani nakuona simu ya monika imedondoka chini..
nilijua ni katika kujigeuza kitandani akaangusha bila kujua akiwa amelala...

Nilimuokotea na kuanza kujirushia baadhi ya nyimbo kwasababu nilikuwa nikimuomba mara nyingi ila tulikuwa tukisahau...

niliona mda ule kabla sijafanya chochote nijirushie tu zile nyimbo kutoka kwenye sim ya monika..

"Umeamkaje mpenzi wangu na unaendeleaje kichwa chako.??  jitahidi umeze dawa mrembo wangu ili baadae ukiweza uje mjini kama tulivyoongea.."

ilikuwa ni mesg imeingia kwenye simu ya monika... niliisoma kwa haraka na kuipotezea tu bila kuifungua yote mwanzo mwisho..

Lakini nilikumbuka kuwa monika alikuwa ni single tu kama mimi na amepata wapi mwanaume.???

niliangalia ile jina na kuona imeseviwa husband (mume)...

mmmhh niliguna kidogo na kwenda kwenye list ya majina na kuziangalia zile namba...

Nilikumbuka kama niliwahi kuziona mahali hata kwenye sim yangu namba zile lakini sikujua ni nani kwa haraka...

Nilichukua namba nne za mwisho na kuingiza kwenye sim yangu..

Mmmhhhh.... "Inamaana Nic na monika walikuwa wanajuana.????..
niliwaza na kunyamaza tu kimya na  kuirudisha sim ya monika pale chini kisha mimi nikapanda kitandani kwangu nikiwa bado na mawazo mengine mapya kuhusu Nic na monika wameanza lini mahusianoo...

" Anhaaaa... huenda ikawa mdaule nimekimbia kumwangali mama njee huenda Nic ndio alimtongoza monika...
 Lakini imekuaje tena monika amkubalie mwanaume kwa haraka kiasi kile hadi waitane mume na mke.??..
au monika kusikia Nic anakazi ndio kajirahisisha kwake...
Lakini mbona Nic nae yupo hivi jamani..
mimi nilishaanza kumpenda na upole wake lakini kaamua kuwa na Monika jamani...

Nilijikuta nawaza sana huku nimefumba macho yangu.. moyo ulikuwa ukiniuma sana kuona monika anaukaribu na nic..

***

Baada ya muda nilimuona monika kaamka na kuokota sim yake..
alitulia kwa mda kitandani akiwa anachati kwa dakika kadhaa na baadae akaenda  kuoga...

Nilitulia tu nikijidai nimelala bila kumsemesha...

Alivaa vizuri kisha akameza dawa zake za maumivu na kuja kuniamsha..

"Hajra shostiangu.... mwenzio nimeitwa mjini na shangazi yangu..
siniliwahi kukwambia kuna shangazi yangu ni mwalimu kwenye sekondari ya MIYUJI.??

Ndio shost.. kwahiyo kakuita kwake.??

" Yaah ameniita na alisikia niliumia alafu sikumpa taarifa..
nimechati nae hapa kachukia kweli...
 Weweendelea kupumzika mamaangu..
 sinta chelewa kurudi..

Sawa.. nitakumis Monika wangu....

" mmmhh alafu nmesahau...
 shangazi alivyo mtata na sijaenda siku nyingi anaweza kunizuia nilale kule..
 acha nibebe nguo kadhaa zakubadilisha kesho kama nitalala kule..



Nilihisi kama nachomwa na mkaa wa moto ndani ya moyo wangu baada ya kuona monika ananidanganya Kiasi kile wakati najua fika alikuwa akichati na Nic....

Monika alitoka akiwa ananukia  manukato na amejipodoa vizuri...
Umbo lake fupi kiasi na lililojazia lilikaa vyema kwenye sketi fupi ya batiki aliyo ivaa....

Nilijikuta nalia machozi baada ya kukumbuka nyumba ya Nik ambayo niliitamani alafu leo anaenda kulala rafikiangu kipenzi...

Inamaana kweli Monika na misimamo yake yote leo ndio anaenda kutoa bikira yake ambayo alikuwa akijivunia kusema itakuwa ni mali ya mume wake.???

Hapana siyo kweli.. Monika haendi kwa Nik.. Atakuwa anaenda kwa shangazi yake jamani.!!!!!

Nilizidi kuwaza nikiwa nimejikunja pale kitandani na machozi yakinimiminika vyakutosha..

Niliinuka na kuoga kisha kwenda kutafuta chai Cafe....

***
***
***

Karibu Monika jisikie nyumbani mamaangu... "aliongea nic akimkaribisha monika nyumbani kwake..."

"Daaahhh... nimechoka jamani.. ila kidogo kichwa kimetulia kabisa kwa sasa..  Alijibu monika na kujipigiza kwenye kochi

Ni furaha yangu kuona upo salama Monika wangu... Jana wakati tunaongea nilikuwa nikiogopa sana endapo hajra angewahi kurudi.. lakini nashukuru hakurudi haraka.... aliongea nic na kujisogeza karibu ya monika

" hahahahaha... kumbe ndomaana ulianza na kuchukua namba zangu kwanza...  ila mimi nimependa upole wako tu baby.. (monika aliongea na kujilaza kifuani kwa nic)

hembu inuka bana twende zetu chumbani.. hapa sebuleni panachosha
'Aliongea Nic na kumbeba Monika kama mtoto kumpeleka chumbani kwake...

ITAENDELEA.....






No comments: