π’πˆπŒπ”π‹πˆπ™πˆ: ππˆπ“π€πŠπ”π…π€ 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ππ†π” 𝐄𝐏..... 𝟏1






π’πŽππ†π€ ππ€π˜πŽ...
Alizidi kuongea Arafa akiwa anaingizwa ndani ya wodi....!!!!

Ester kwa haraka alienda kwenye chumba cha daktari na kumpa hali halisi..
daktari pia kwa haraka alienda kumkagua na kumchoma sindano ya usingizi na dripu...



Baada ya muda alitoka nesi ambaye alikuwa anamuuguza monika na kutuambia mgonjwa wetu anaendelea vyema sana....

na kwasasa amepumzika hadi baada ya masaa mawili ndio tungeweza kuja kumuona..

Nilifurahi sana.. nilijikuta nina tabasam tu mwenyewe...

yule mwanajeshi pia alikuwa na amani sana.. alinigeukia na kuniangalia kisha kuinuka na kunishika mkono..

Mungu ni Mkubwa dada.. Naomba tuendee kula alafu tumbebee na mgonjwa chakula baada ya masaa mawili nadhani tutakuwa tumerudi..

Tulitoka tunatabasam huku tumeshikana mikono tunaelekea kwenye gari...

"We kaka ujue unaogopesha sana..
niliongea kwa kujiamini kwasababu nilishaanza kumzoea yule mwanajeshi..

Kwanini.? naogopesha na nini tena dada mrembo...?

Nilimwangalia kuanzia kiatu hadi kichwani kwenye kofia aliyoivaa.. nilicheka kidogo nadhani na yeye aligundua...

aaaahhh hizi gwanda hazina shida.. nilikuwa nimetoka kazini mda ule ndio naelekea home na matatizo ndio yakatokea...

"Anha polee..

Asante kama hutojali tupitie kwangu nikabadili nguo kisha tuende kula..

" Bila shaka kakaangu.. kwanza unaitwa nani.???

Naitwa NICSON MWAKYAVALA.. 

"hahahahaaha.. Mtu wa mbeya eti....

'ndio mtu wa mbeya.. Mwakyavala imekustua eti..

" hamna mnakuwaga na majina yakipekee sana..

Tulizidi kupiga story mbili tatu hadi tunafika kwake.

Aliniacha sebuleni kisha yeye akaingia ndani kwake upesi kubadili nguo..

Nyumba ilikuwa nzuri na imepambwa kwa ustadi wa hali ya juu...

Nilikaa kushangaa tu ukubwa wa Screen ya TV iliyo jengewa ukutani vizuri na makochi malaini yenya kubonyea vyema..

Nilipatamani sana kwa yule mwanajeshi..

"waaoohhh Umependeza sana Nic..  nilimwambia yule kaka baada ya kutoka ndani kwake..
yaani ungevaa hivi mda ule wananchi wangekuchangia pale kwasababu walikuwa na hasira na siunajua maeneo ya stendi wanao jaa sana ni Mateja tu na wavuta bangi..

Yah ni kweli.. Mwenyewe nilikuwa natetemeka sana ndio maana unaona baada ya ajali nilichukua mda kidogo kutoka ndani ya gari..

"Oky.. nic naomba tuharakishe kula chakula ili tumuwahi Monica..

Niliongea na kutangulia kuingia kwenye gari kisha nic akafuatia na safari ikaanza...


***

Haya dada Eliza.. mgonjwa wako anasumbuliwa na matatizo ya akili kwenye baadhi ya muda kutokana na maradhi yake..

Tumempa dawa na siyo mda atakuwa sawa unaweza kurudi nae nyumbani...

Aliongea Nesi akimwambia Eliza...

Pia naomba ukamwangalie hadi atakapo amka ili asilete fujo kwa Mgonjwa mwingine aliopo mule ndani..

Kuna mgonjwa alipata ajali kalazwa kwenye wodi moja na mgonjwa wako sawa.. ni chumba namba 9..

Eliza alitikisa kichwa kuashiria ameelewa..
alienda hadi wodini na kumwangalia Arafa ambae ndio alikuwa ni mgonjwa wake...

Baada ya muda fulani Arafa aliamka na kumuona rafikiake Eliza yupo jirani yake.

"Eliza.... Hajra amekuja.??????

Arafa alimuuliza Eliza kama mwanae amefika..

" Arafa naomba twende nyumbani sasa tulikuwa tunasubiri uamke rafikiangu sawa...

Aliongea Eliza na kumshika rafikiake mkono ili watoke....

Wakati huo Monika nae kwenye kitanda cha pembeni ndio alikuwa anapata fahamu.. Alionekana kukereheshwa sana na kelele za Arafa..

"Eliza unanitoa humu ndani wakati Mwanangu hajra hajaja jamani... nakuomba tusubiri hajra ajee jamani Eliza..

Alikuwa akiongea Arafa huku analia..
afya ya arafa ilikuwa imedhoofika sana.. alikuwa amekonda kupita maelezo.. macho yalukuwa yametoka makubwa na makavu kama mtu ambaye anasiku kadhaa hajala chochote..

Kauli ya arafa kusema Anamsubiri mwanae Hajra ilimfanya monika atoe macho kushangaa ni Hajra gani anazungumziwa...

Elizaa akisaidiana na Mdada wake wa kazi walibeba baadhi ya vitu walivyokuja navyo hospitalini

"hembu ona shostiangu unapiga kelele unamsumbua mdada wa watu kalala pale tuliambiwa alipata ajali..
Eliza aliongea kwa upole..

ile kauli ni kama ilimuingia Arafa na kunyamaza kimya kisha kutoka nje ili warudi nyumbani..



Tulifika hotelini na kula haraka kisha kufunga chakula na kwenda hospitalini..

Safari ilikuwa bado ni ndefu kiasi..
na baada ya dakika kadhaa tulifika hospitalini...

"Ona kule Nic. umemuona yule mama alivyo konda..
saile tu aliletwa hapa akiwa anapiga kelele lakini sasaivi ametulia anarudi nyumbani..
Niliongea kwa upole baada yakumuona mama mmoja akipakiwa kwenye tax

Yah hii hospitali ni nzuri na baada ya dakika chache wanaweza mruhusu Monika pia Atoke..

" Jamani nitashukuru akitoka. lakini sasaivi usiku umeingia siutatupeleka chuo.??

Ndio msijali.. hata mkitaka kulala kwangu sawa tu..

Hahahaha nilicheka na kwenda dirishani kwa nesi atuelekeze wodi aliyolazwa monika..

" Mgonjwa wenu yupo Wodi namba 9...
Aliongea ness..

Nilimshika nic mkono na kwaharaka tulingia kwa monika..

Tulimkuta  kakaa kitandani akiwa anatafakari sijui nini...

" Pole sana dada... Sikudhamiria kufanya vile dadaangu..
aliongea nic na kwenda kukaa kitandani karibu na monica..

Usijali kaka ni mambo ya kawaida.. nilipata mshtuko tu na docta kaniambia nipo sawa naweza kutoka..  ila kichwa tu ndio kinaniuma kwa mbali...

Pole shostitooo....  niliongea  huku nacheka....

Yaani Hajra wewe.. ungajua kuna mama aliletwa hapa ndani anamatatizo ya akili..
kila mda alikuwa anasema Hajra Mwanangu..
yaani nilikuwa nacheka nilitamani sana ungekuepo...
nadhani kuna mwanae anaitwa hajra...
 (aliongea monika huku anacheka)

Mmmhhh Mgonjwa gani wewe unaecheka...
Aliletwa na nani huyo mama.??

Kuna mama mmoja anaitwa Eliza nadhani sijui kama sikosei....

"khaaaaaahhh nani unasema wewe Monika..
yaani Eliza kaja hapa hujaniambia...

huyo mama anaitwa Arafa au nani.???  niliongea kwa ukali kidogo..

Ndio nilimsikia Eliza akimwita Arafa.....

" mamma yangu mimi jamani....
Monika unanikose jamni...
tulikuwa wote kule saluni tulipokosea kumtafuta Eliza na ulisikia namuuliza Eliza alafu saivi anakuja mama yangu unamwachia aondoke hapa jamani monica..

Nilijikuta nalia na machozi yananitoka kama maji..... kwaharaka niliinuka na kukimbia kutoka njee kumtafuta kama hawajafika mbali...

ITAENDELEA......

NITAFUTE WHATSAPP 0788294399 NIKUUNGE GROUP



No comments: