π’πˆπŒπ”π‹πˆπ™πˆ: ππˆπ“π€πŠπ”π…π€ 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ππ†π” 𝐄𝐏..... 𝟏𝟎




π’πŽππ†π€ ππ€π˜πŽ...

nilikumbuka na zile ndoto nilizokuwa nikiota na kuhisi huenda mwanamke mwenye kuhitaji msaada wangu ni mama yangu mzazi..

Nilifika kwenye ile saluni na kuingia ndani..

"Habari zenu..
 nilisalimia wasichana waliomo mule ndani..
wawili wakiwa wanasukwa na mmoja akiwa kwenye kochi nadhani aljkuwa kwenye foleni akisuburi waliopo watoke..

'salama shost karibu sana...

"Samahani nimemkuta eliza.??

Niliuliza swali na kugeuka nyuma kuangalia wakati huo Monica ndio alikuwa anaingia saluni kwasababu nilivyokimbia nilimwacha mbali kiasi..

' ndio huyo hapo kakaaa..

alijibu binti mmoja..

"Samahani dada.. unamfahamu Arafa Abdull.??

kuna mama anaitwa arafa aliwahi kuja huku dodoma miaka kama 15 hivi iliyo pita..
sijui kama unamfaham dada...

' 'mmmmhhb hapana mrembo sijamuona..
mwenyewe unavyoniona nina miaka 22..  miaka 15 nyuma nilikuwa darasa la kwanza shuleya msingi..
sasa nitamjua vipi huyo Arafa jamani.??
Utakuwa umenifananisha dada...
au aliyekuelekeza alikosea..

"Sawa samahani.....  nilimjibu nakuondoka nikiamini kwelinilikosea kwasababu ya umri wa eliza nilie mkuta mule..

***

Tuliendelea kuzunguka mjini na baadae kwenda skwea..

Tulichagua baadhi ya mitumba na kuanza safari ya kirudi stendi ya daladala JAMATINI ili tupande gari kurudi chuo..

Tukiwa tunavuka barabara jioni ile kwenye barabara kubwa...

Nilisikia kishindo cha gari kama kimegonga kitu nyuma yangu....

"Umeua jamaniiiii.. uuuuuwiiiii...... Kaua jamani........

Nilisikia kelele za watu na kunifanya nigeuke nyuma haraka...

nilishtuka sana kumuona Monika yupo chini anavuja dam mdomoni na puani...

watu kutoka stendi walianza kumiminika kuelekea ajali ilipotokea..
kulikuwa na umbali mdogo tu kutoka tulipo hadi stendi ya JAMATINI..

Nilijikuta nasisimka kwa kuchanganyikiwa..
sikujua naanzia wapi kulia..
sikuamini kama mtu niliekuwa napiga nae story sasaivi yupo chini...

watu walikusanyika na kuizuia gari iliyomgonga monica..

niliwahi kuchukua vitu vya rafikiangu monika na kuweka kwenye begi langu...

Mtu alie mgonga monika alikaa tu kwenye gari lake nadhani aliogopa kutoka kwaajili ya uwingi wa watu asije jeruhiwa..

Lakini baada ya sekunde kadhaa baadae niliona mlango wa lile gari linafunguliwa na kushuka Mtu mmoja alie valia Mabuti makubwa meusi na Mavazi ya kijeshi..

Watu baada ya kuona vile walirudi nyuma haraka kwa kumuogopa yule jamaa...

yule mwanajeshi alisogea karibu na monika na kumpima akagundua bado mapigo yake ya moyo yanadunda.

Aliniangalia na kunipa sim yake nimshikie..

aliinama na kumbeba monika kisha kumpakia kwenye gari lake...

aliniambia kwa ishara nipande kwenye gari kisha safari ya kwenda hospitali ikaanza...

tulitembea umbali mdogo tu na kuingia hospitali ya AGHAKAN...

Monika alipokelewa na kuanza kupewa huduma ya kwanza..

mimi na yule mwanajeshi tulikuwa tumekaa tu njee kwenye benchi kumsubiri daktari..
Hakuna mtu aliekuwa na hamu ya kuongea na mwenzie kwa muda ule....


***

"Shkamoo dada...... (ilikuwa ni sauti ya kike ikiongea kwenye simu ya Eliza mara tu baada ya eliza kupokea)

Marahaba wewe nani jamani mimi nipo na kazi mbona mnasumbua.???  aliongea Eliza kwa ukali..

" ni mimi Naomi.. msichana wako wa kazi... nilikuwa nakwambia kuwa dada Arafa kazidiwa na anaongea tu vitu visivyo eleweka muda wote anataja jina lako na jina la HAJRA sijui ndio nani huyo...

Eliza baada ya kusikia hivyo alikata sim haraka na kunawa mikono kisha kumwachia msaidizi wake amsaidie kumsuka mteja..

"Shosti.. sinilikwambia kuna mgonjwa namuuguza pale kwangu.??

nasikia kazidiwa sana na ananiita...
acha nichukue tax nimkimbize hospitali...

" Pole shosti.. mpeleke hospitali ya AGHAKAN ndio huwa wanatoa huduma ya haraka... tafadhali wahi dada Eliza..

Eliza alitoka na kuchukua tax hadi kwake....

walisaidia kumpakia Arafa kwenye gari na Safari ya kwenda Aghakan ilianza..

Njia nzima  Arafa alikuwa akiita tu jina la Mwanae..

"HAJRA mwanangu.. utakuwa salama.. utakuwa salama hajra....
 (Arafa alikuwa akiongea tu mwenyewe..)

walifika hospitali na kumshusha kisha kumpakia kwenye kitanda cha matairi kumpeleka wodini..

" Hajraaa.... utakuwa sawa mwanangu... Hajraaaa utakuwa salama maisha yako yote....

Alizidi kuongea Arafa akiwa anaingizwa ndani ya wodi....!!!!

ITAENDELEA....






No comments: