π’πˆπŒπ”π‹πˆπ™πˆ: ππˆπ“π€πŠπ”π…π€ 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ππ†π” 𝐄𝐏.....20





π’πŽππ†π€ ππ€π˜πŽ....
Nic pia alishuka haraka na kuanzanza kunifuata.  nilifika sehemu na kuanza kupita chochoro kuelekea nyumbani lakini bado nic alinifuata..

Nilihofia kupita chochoroni sana na kujitokeza mahali kuna mwingiliano kidogo wa watu na endapo atasogea nimpigie kelele za mwizi. jinsi sura yake ilivyokaa lazima watu wangeamini ni mwizi tu...

Niliongeza mwendo na kukata kona upesi kisha kuchungulia nyuma kama bado ananifuata.. niliangalia lakini sikumuona.. nilijiweka sawa na ile nageuka tu mbele nilikutana nae uso kwa uso.. "HAJRA naamini upo salama.. nitakuua nina kupa hii ahadi haya siyo mazingira mazuri kufanya hivyo.. ila nitakufuatilia hadi nijue unapoishi..
Aliongea nic na kugeuka nyuma kuondoka zake..

Nilisimama pale kwa muda nikiwa natetemeka sana.. nilitoka mbio na kwenda kupanda daladala kuelekea Maeneo ya stendi ya  Mawasiliono yote ilikuwa ni kumpoteza maboya ili asijue kama naishi mitaa ile..

Baada ya kukaa kwa muda kama nusu saa hivi nilirudi tena na nilivyoshuka nikapanda boda boda kwenda hadi geto kwangu.. nilifika na kubadili nguo zangu za kazi kisha taratibu nilianza kuelekea kwa Amir ili nikapate chakula cha usiku.

Kabla sijafika kwa Amiri niliona ile Ambulance imepaki njee ya geti la kuingilia kwa amiri.. Nilianza kulia machozi na kutetemeka kwa hofu huenda mtu wa watu anauliwa kisa mimi..

Lakini baada ya mda nilisikia watu wanacheka wakitoka ndani ya geti.. nilijibana kwenye kona na kumuona Amiri na Nic wameshikana mikono wanaelekea kwenye gari na nyuma yao alikuwepo mke wa Amiri.. Walimuaga Nic kisha nic akaondoka..

Kwa hofu nilitulia kidogo na baada ya kuona kumepoa nilienda na kugonga geti.. Nilipokelewa na kuingia hadi sebuleni.. lakini nilikuwa na hofu sana na sikuwa na ujasiri wa kumwangalia Amiri kabisa.. Nilijikuta naanza kumchukia Amiri moja kwa moja....

Tulikula lakini baadae Amiri aligundua ile hali..

"Hajra haupo sawa mamy... au wamekuudhi kazini.?? aliniuliza amiri

Hapanda nilipitia kwa nesi mwenzangu alikuwa anaumwa nikaona nikamtembeleee.. niliongea na kuangalia chini..

" Anaumwa nini.. maana naona hata wewe hauna furaha kabisa leo.. au kuumwa kwa rafiki na wewe umeumia...??

" ndio nawaza hapa kwasababu nitakuwa bize na kazi kuanzia asubuhi hadi usiku bila kupumzika hadi apone..

"usijali toto.. ndio ukubwa huo.. Leo tulikuwa na ugeni hapa kuna Mjomba wangu mtoto wa dada yangu alikuja hapa kunisalimia.. mmepishana kidogo tu.. kwasasa amerudi dodoma.. ni mwanajeshi kule dodoma pia na leo walikuja kumleta Mgonjwa mwanajeshi mwenzao  muhimbili akaona anipitie hapa..

"Anha.... basi anakupenda sana eti..

" Siyo kunipenda tu.. michakato yote ya kwenda jeshini nilimfanyia mimi. nilimsomesha na mahitaji yake yote nilikuwa nikimpatia mimi.. kwasababu dada yangu alipewa mimba na kutelekezwa huko kijijini kwetu.. ikabidi nimsaidie majukumu.. Usije ukawa mzembe na wewe wakakuchezea bana sawa hajra.???

Ndio Mr Amir.. nitakuwa makini hadi Allah anijalie Mume mwema kwangu..

***

Tulimaliza kula kisha mimi nikarudi kwangu.. "Nilikuwa na mawazo sana kuhusu Nic na undugu wake na Mr Amir..

Nilioga na kulala.. Asubuhi niliamka mapema lakini sikwenda kazini.. nilikuwa nikiwaza tu.. Nilishika simu yangu na kumpigia baba kumsalimia.. alifurahi sana kuona nimempigia asubuhi kwasababu sikuzote huwa naongea nae USIKU..

"Mwanangu kipenzi.. Kuna link nitakutumia ujaribu kuiangalia kisha kama utaiweza utanijuza.. inamalipo makubwa pia nimafunzo ya mda wa miezi sita tu nchini URUSI.. wanahitajika watu sita tu.. watatu wakike na watatu wakiume..

Kama utaipenda unijulishe nikufanyie mpango ili uende kuungana nao..
Aliongea baba na kukata sim..

Baba yangu hanaga maneno mengi sana... akimaliza maongezi hana umbea hata kidogo.. kinachofuata ni kukata sim tu..

Niliendelea kuwaza pale kitandani na baada ya mda iliingia ujumbe..
Niliifungua ilikuwa ni link ya kuhitajika vijana sita kwaajili ya kwenda kupata mafunzo ya KIINTELIJENSIA YA USALAMA WA TAIFA kwaajili kuimarisha amani..

"nilishusha pumzi na kucheka tu mwenyewe.. 'kweli mwenye nacho huongezewa...'  Hii link itakuwa wamesambaziana Maboss tu na wafanyakazi wakubwa wa serikali na badala ya kuchagua watu basi wanachukua watoto wao...

Ndio maana unakuta mkuu wa wizara fulani ni mzee fulani na wizara nyingine yupo Mke wake au mwanae... "Hii ndio Africa yetu... Nilikuwa nikiwaza na kujichekea tu mwenyewe..

Mafunzo ya miezi sita tu...

mmmhh haiwezi nishinda.. kwahiyo baada ya hapo mimi nakuwa ni Afisaa..

Nilishika sim na kumtumia baba ujumbe kuwa nipo tayari.. baba mda huo huo alinipigia sim...

"Mwanangu hii ni siri na ikiwezekana hapo kwa Amir waage kuwa kuna tatizo unarudi nyumbani.. kisha wahi Gongolamboto Asubuhi hii uchukue chumba lodge.. na jioni utachuliwa kupelekwa Airpot kwaajili ya kuanza safari..

Tayari nimekusajili na Namba yako ya usajili ni T-3037 ambayo itatumika badala ya jina lako.. mtu yeyote akikuuliza jina usimwambie kwasababu za kiusalama.. utatembea kwa Namba yako tu.. na kule hutoitwa jina.. namba yako ndio jina lako hadi urudi nyumbani..

***

Nilijiandaa na kwenda gongolamboto. baada ya hapo niliwapigia sim Amir na mke wake na kuwaambia ninaenda morogoro baba kaniita kuna tatizo kidogo..

Amiri hakuwa mbishi alikubali na kuniomba niwahi kurudi kwani watanimiss sana..

Nilifika Gongolamboto na kuchukua chumba lodge.. niliingia Dukani na kununua Skin jeans na Tishet za kutosha na makoti kulingana na maelezo niliyopewa kwenye ujumbe na baba.. Nguo zangu za kiislam hazikuwa na nafasi tena kwa kule.. kwani hatukutakiwa kuvaa chochote kichwani..

Nilikula na kupumzika.. saa kumi na moja niliamka na kuoga kisha kuvaa upesi.. Hatukuwa na haja ya hata paspot kwasababu tulikuwa ni Maafisa wa serikali..

Gari ya Serikali ilikuja hadi lodge nilipo na kunipakia na mizigo yangu hadi uwanja wa ndege.. Tulikuwa na chumba maalum tumehifadhiwa.. Baada ya mda waliletwa na wenzangu watano kisha kupakiwa kwenye ndege..

Safari ilianza lakini hakuna alie ongea na mwenzake.. Usiku mzima uliisha tukiwa njiani.. Alfajiri ilifika bado tupo angani na baada ya masaa kama mawili tulitua Nchini URUSI..

Tulipokelewa na wanajeshi sita wakirusi tukiwa chini ya ulinzi mkali sana na kuingizwa kwenye kambi....
Wasichana tulipewa chumba chetu na wavulana chumba chao..

Tuliingia ndani kwetu na kila mmoja kuvua nguo zake kwaajili ya kuoga kutoa uchovu...

Tuliingia bafuni wote watatu kwasababu bafu lilikuwa kubwa sana.. story zilikole mule ndani lakini tukiitana kwa namba tu...

Jina lilikuwa ni siri ya kila mtu..

Nikiwa navaa alikuja mwenzangu mmoja na kunishika Mgongo kisha kuniambi...

"Hajra mambo vipi.??

Nilishtuka sana kuitwa jina langu.. nilimtazama yule msichana kwa mda bila kummaliza.. lakini sura yake haikuwa ngeni sana kwangu..

"Naitwa irene.. miaka kadhaa nyuma tulikuwa wote dodoma..

Nilishtuka sana na kukumbuka ni Yule Irene mke wa Nic ambaye aliwahi kuniteka na kunipeleka kwenye kambi zao kunipa mateso...

Nilianza kutetemeka hadi yule mwenzetu akahisi kuna nini kinaendelea tena pale..

"T-3037 nakuomba usishtuke.. kwasasa nipo kwa amani na tupo kwenye majukum ya Taifa.. tutaongea mengi kwasababu tupo pamoja hapa kwa miezi mingi sana... 'Aliongea irene na kwenda kwenye kitanda chake...

ITAENDELEA....






No comments: