ππππππππ: πππππππ π ππ ππππππ πππππ ππ..... 19
πππππ ππππ....
Niliinuka na kulipia soda upesi kisha kumshika mkono mke wa Amiri ili turudi nyumbani.. nilianza kuhisi kuchanganyikiwa baada ya kumuona Monika..
Tulitembea hadi tukafika nyumbani.. mke wa Amir hakuelewa kama kuna kitu nimeona ila alijua ni matani yangu tu kwasababu mda mwingi tulikuwa tukitaniana sana..
Kesho yake asubuhi nikiwa naelekea kazini nilipitia njia ileile na kuitaza ile nyumba kwa umakini sana.. kweli ilikuwa ni nyumba ya kifahari sana..
Nilipita haraka na kwenda zangu kazini.. niliendelea na majukumu yangu ya maabara kama kupima magonjwa kwa baadhi ya watu ambao afya zao hazikuwa sawa, nilifanya kazi zangu huku nina msongo mkubwa sana wa mawazo.. nilihisi hata ningeweza kuwapa wagonjwa majibu tofauti na maradhi yao..
Niliomba ruhusa na kuamua kurudi nyumbani asubuhi ile.. nilifika na kuingia chumbani kujipumzisha.. Mke wa Amiri pia alikuwa ndani kwake kalala nadhani kwasababu alikuwa ni mjamzito kwahiyo mda mwingi alikuwa ni kulala tu..
Niliifikiria sana ile nyumba.. "kwahiyo kama magari ya kifahari huwa yanaingia mule ndani na Monika yupo mule inamaana monika sasa ni mfanya biashara pia.. haiwezekani monika kuwa msichana wa kazi za ndani.... huu ni mkanda mzima wa wale wauzaji wa madawa kuanzia kule dodoma.. inaonekana ni mkanda mrefu sana na kuna wafuasi wakubwa nyuma yao wakiwemo wanasiasa wakubwa.
Nilibaki chumbani nikiwaza... hili kundi ndio linaua watu bila hatia hasa wasichana wenzangu na kuwaharibu..
inamaana monika sasa ni msichana wa kazi za ndani.? hapana hili suala nalipinga. Martha alikufa.. alafu bado nina deni la kwenda kutoa taarifa kwao akina martha.. nitafanyaje mimi jamani.. mbona likiisha tatizo linakuja tatizo lingine..?? nilianza kukumbuka na matukio yote ya dodoma ambayo nilianza kuyasahau.. sikumpenda monika kwasababu hakuwa na msimamo na alianza ubinafsi wa kufanya mambo bila kunambia ukweli
machozi yalianza kunitoka na kujikuta naanza kuipoteza tena furaha niliyokuwa nayo.
Macho yalikuwa mekundu sana na sura yangu ilikuwa imejaa hasira..
Baada ya muda alikuja mke wa amiri na kuingia ndani kwangu.. nilijifanya nimelala na kutulia kimya..
"huyu kiumbe sialiniambia anaenda kazini au hamna kazi leo kaamua arudi kulala
Aliongea mke wa amiri kwa matani..
Nilijichekesha na kumwambia.."rafikiangu alishaingia.. mimi nitaenda mchana kumsaidia kidogo..
" poa shosti wewe lala kwa raha zako ngoja nikupikie chai ya karafuu na tangawizi ujing'ate. mimi ndio mtanga bana.. wasomi hamuwezi kujua mambo kama haya..
Unadhani kwanini Amiri akanioa mimi akawaacha wasomi wenzie.??
aliniuliza mke wa amiri..
"Sijui kwanini...
Tunafundwa sisi.. unadhani ni kama wasomi hata mapenzi hamjui.. mkilala kitandani kama magogo.. sisi tunapiga mauno asikwambie mtu..
Mke wa amiri alizidi kujisifia pale ndani kwangu..
"haya shost mmeshinda kapike chai.. uuhhh utaaanza kujisifia hapa hadi usingizi uniishe.. Kakuoa wewe kwasababu hujui matumizi ya hela.. hakutaka hasara za kijinga.. unadhani mwanaume gani anaetaka mwanamke asiejua hata aina za vyakula vyakumlisha mwanae.. wewe na ushamba wako ukijifungua unaweza ukaanza kumlisha mtoto makande maana wapare tunawajua ushamba wenu....
""hahahhahhahha. tulizidi kuchambana mule ndani mwishoe na mimi nikaamka tukapika chai na kunywa mimi na shostiangu....
***
***
TURUDI DODOMA.
"Mambo shost.. Mimi naitwa Lilian na rafikiangu anaitwa irene.. Tunafanya kazi na kampuni ya Pedi ya Freestyle..
ilikuwa ni sauti ya binti mmoja kwenye saluni ya eliza..
" karibuni sana.. nashukuru kuja kwenu pia.. sijui naweza kuwasaidia nini.??
Aliongea eliza..
"kama haupo bize sana kuna mazungumzo ya biashara naomba tukayaongee pembeni tusije kuwasumbua wateja wako..
Bila shaka twendeni basi pembeni pale kwenye baraza..
Aliongea Eliza kisha kunawa mikono yake na kuahirisha kumsuka mteja aliekuwa anamsuka kisha kutoka njee kuongea na wageni wake...
"Dada samahani.. sisi ni wafanya biashara wakubwa.. lakini ni biashara ya siri sana.. tunasafirisha madawa mikoa mbalimbali na ofisi yetu ipo dar es salam..
Tumekuja hapa tumeelekezwa kuwa kuna mgonjwa unae yupo mahututi na siyo mtu wa kupona kulingana na maradhi aliyo nayo..
Tunamuomba huyo mgonjwa atusaidie kusafirisha madawa kwenda dar es salam kisha tutakulipa fedha nyingi tu..
"Haaa.. hembu tulieni.. mnatumia mwili wake kusafirisha vipi hizo dawa.??
"Tulia dada usipanic.. nakuomba utuuzie huyu mgonjwa tutakupa Milioni thelathini.. nakuomba ukae utafakari.. chukua hizi namba ukiwa tayari utujuze.. tunashida sana.. pia hii siri asijue mtu. ikijulikana tunakuua..
wale wasichana waliongea na kuongozana kuelekea kwenye garu.. wakati wanapanda gari mmoja tisheti yake ilifunuka kidogo Eliza akaona bastola...
Eliza aliogopa sana na kubaki na rundo la mawazo... aliingia ndani na kumalizia kumsuka mteja wake.. alivyomaliza alifunga salumi yake na kurudi nyumbani..
Alifika na kuingia hadi kwenye chumba cha mgonjwa wake ambaye alikuwa mahututi sana.. hatu aliyo fikia Arafa ilikuwa ni wakujisaidia ndani hata kutembea ilikuwa kazi sana kwake
"Hivi kuliko kukaa na mgonjwa wa kuniletea shida miaka yote hii si bora nipate hizo hela nikuze biashara zangu kuliko kuendelea kukaa nae.. na hata akinifia hapa nitamzika wapi.???
Eliza aliwaza lakini baadae alimua kumuuza tu..
Alituma ujumbe na kuwaambia wale wasichana waje kumchukua Arafa..
Bila kuchelewa zilikuja gari mbili moja ilikuwa ni ambulance ya wagonjwa...
walishuka wasichana wawili na mkaka mmoja ambae alikuwa na sura iliyojaa makovu makubwa..
"Nic ingia kampe hela zake.. alafu usiku tuwatume vijana wamvamie wamuue kisha wachukue hela..
'aliongea binti mmoja akimwambia yule kaka mwenye makovu kichwa kizima..
Nic aliingia na begi lenye fedha na kumkabidhi Eliza.. waliingia vijana watatu na kumbebe Arafa kisha kumpakia kwenye ambulance..
Walimpeleka hadi kwenye kambi yao na kumpasua tumbo kisha kumwekea mapakti ya madawa ya kulevya..
walipanga pakti zaidi ya thelathini na kumshona vizuri kisha kumpakia kwenye Ambulance na safari yakwenda dar es salam ilianza wakiongozwa na nic..
mwendo ulikuwa mkali sana.. askari walikuwa wakiogopa sana kusimamisha ambulance wakiamini inaenda kuwahisha wagonjwa hospitali ya taifa...
***
***
DAR ES SALAM...
Mchana wa siku hiyo nilirudi na kuendelea na kazi zangu hospitalini hadi saa kumi na mbili jioni ndio nikatoka..
Jua ndio lilikuwa linaanza kuzama lakini bado hapajaingia giza...
Nilitembea na kupita mitaa ya lile jumba kama kawaida yangu na kutembea taratibu sana baada ya kufika maeneo yale...
Nikiwa bado nashangaa niliona Ambulance imepita pembeni yangu na kusimama kwenye geti la ile nyumba... niligeuka ili nione nini kinaendelea pale lakini niliona kioo cha lile gari limeshushwa..
Nilizidi kuangalia lile gari lakini niliona mtu katoa kichwa chake na kuniangalia kwa mda kidogo..
Nilimwangalia kwa makini na kumuona ni nic japokuwa Sura yake ilikuwa imeharibiwa kwa kupigwa.. nadhani ni zile mawe nilizompiga porini..
Nilishtuka sana na kushika mdomo.. niligeuka haraka na kuanza kukimbia huku naangalia nyuma..
Nic pia alishuka haraka na kuanza kunifuata. nilifika sehemu na kuanza kupita chochoro kuelekea nyumbani lakini bado nic alinifuata..
ITAENDELEA...
No comments: