π’πˆπŒπ”π‹πˆπ™πˆ: ππˆπ“π€πŠπ”π…π€ 𝐍𝐀 ππˆπŠπˆπ‘π€ π˜π€ππ†π” 𝐄𝐏..... 18





π’πŽππ†π€ ππ€π˜πŽ....
"Hajraa!!!! aliongea mkuu wa mkoa na kutoa sim yake mfukoni kumpigia baba..
walikuwa wakifahamiana na baba kwasababu baba alikuwa ni mwanasheri kwenye mahakama ya rufaa ya mkoa wa Morogoro pia..

Simu iliita hadi ikakata bila mafanikio.. nadhani baba alikuwa bize na majukumu yake.. Mkuu wa mkoa alikata sim na kuja kunisogelea.. "Hajra mwanangu umekumbwa na nini.? jana jioni nilikuwa na baba yako kabla sijaja huku.. aliniambia upo unasoma chuo huku.. leo nakuona kwenye hali hii..
Tulijitahidi kukupigia sim lakini ulikuwa haupokei.. nilichukua namba zako na leo asubuhi nilikupigia pia hazikuwa zinapatikana kabisa..
aliongea mkuu wa mkoa na kuchchumaa chini kunishika mabega..

"Umemuona Martha alivyokuwa.??.. Martha amekufa... Monica nae akamchukua nic wangu akadhani amenikomoa.. nic mwenyewe nishamuua na monika sijui atatoka na nani sasaivi..
niliongea kwa umakini huku namwangalia mkuu wa mkoa bila kupepesa macho..

" unatatizo Hajra.. Aliongea mkuu wa mkoa na kuwaita askari wawili pembeni..
baada ya muda niliona wale askiri wakirudi na kunishika kisha kunipakia kwenye gari..

Askari mmoja alitoka njee na baada ya muda alikuja na binti mmoja ambae nilikuwa nimelingana nae urefu na mwili pia.. yule binti alikuwa na kibegi kidogo kakivaa..
walipanda gari na kuanza kuondoka kuelekea mjini.. nilikuwa nikilia tu baada ya kwenda mbali na mkuu wa mkoa..

Tulifika mjini na kukata kona.. tuliingia kwenye gest Fulani iliyoandikwa KATO guest House.. walichukua chumba wale askari na kuniingiza ndani mimi na yule binti..

"Shost.. mkuu wa mkoa kasema hivi.?? anaingia kwenye kikao na akitoka eti mnaenda nae  morogoro.. kasema kuwa hawezi kuongozana na wewe kama haujaoga.?? kaniambia nikuogeshe na kuna hizi nguo zangu mpya alihisi zitakutosha akazinunua ili uvae upendeze sawa mamy.??
Aliongea yule bint na kuniangalia kwa hofu.. nadhani alihisi huenda ningempiga labda..

Niliitika na kuvua nguo kisha kuongozana nae kwenda bafuni.. Alifungulia maji na kuniogesha vizuri kisha nikatoa haja kubwa na ndogo na kuvalishwa vizuri baada ya hapo tulitoka.. tulipitia mgahawani tukapata supu kisha safari ya kwenda CHUO CHA MIPANGO kulipokuwa na mkutano wa wakuu wa mikoa ikaanza..

Nilikuwa nikitabasam tu mwenyewe njia nzima.. nikiona hata mti nilikuwa nikihisi kucheka.. kila nikimwangalia yule dada pia nilicheka sana.. Kichwani nilikuwa nikijihisi kama mtu alie lewa lakini nilikuwa salama salimini..

Tulifika mipango na kupaki gari njee. baada ya masaa mawili mkuu wa mkoa alitoka kwenye kikao.. na safari ya kurudi morogoro ilianza..

Hadi saa tisa jioni tulikuwa nyumbani.. mama alinipokea ila alishangaa sana kuniona sina hata kitambaa kichwani.. alishtuka sana kwasababu siyo taratibu zetu kutembe nywele zikiwa nje kwa mtoto wa kike..

"Amekumbwa na nini mwanangu.??
aliongea mama kwa mshtuko na kuja kunikumbatia.. hisia ziliniingia hadi machozi yakaanza kunitoka...
niliingizwa ndani kisha baba akapigiwa simu na marahii aliipokea.. alielezwa na baada ya muda alikuja nyumbani..

Walikaa wakiwa wananishangaa vituko vyangu kama kung'ata gauni na kulia kama wanyama mbalimbali..
Lakini mda wote nilikuwa nikiongea maneno haha kwa kujirudia.. "monika anadhani kanikomoa kumbe kajikomoa mwenyewe.. ngoja apasuliwe tumbo."

"Kuna tatizo gani kwa monika.??
baba aliniuliza..

'monika alitoka na nic.. alafu nic mwenyewe ameshakufa porini nilimpiga heee... baba hata wewe ungemhurumia.. eti alitaka kunibaka mimi..
Niliongea na kucheka huku nauma kucha..

Mkuu wa mkoa alisikitika sana na kumuita baba pembeni...

"Jamaangu.. huyu mtoto hajawa chizi.. nadhani ni matatizo ya kisaikolojia tu nahisi kuna matatizo yalimkabili chuo.. sasa nakuomba aende dar es salam kuna mdogo wangu wakike ana mume ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salam ni mtaalamu sana wa masuala ya saikolojia na nirahisi sana kugundua na ataweza kumrudisha kwenye hali yake ya mwanzo..
Mkuu wa mkoa alimwambia baba..

Baba hakubisha kwasababu hali yangu kweli ilikuwa ni mbaya sana.. Mkuu wa mkoa alimpigia sim shemeji yake ambaye ni mme wa mdogo wake na kumwambia hali yangu..

Jamaa alikubali na kesho yake asubuhi nilisafirishwa kwenda dar es salam..



Tulifika dar nikiwa na mkuu wa mkoa akanikabidhi kisha yeye kurudi morogoro kuendelea na majukumu yake... Dar na moro hapakuwa na umbali sana.. ni masaa kama manne tu ukiwa na gari binafsi..

Nilipokelewa vyema na mke wa Dr Amiri ambaye alikuwa ni daktari wa kufikia kiwanngo fulani cha elimu.. wasomi watakuwa wanaelewa.. mtu akifikia ngazi ya PHD huwa anatunukiwa jina la daktari kwa kipindi hicho alikuwa akitafuta nafasi ya kuitwa Profesa tu..

Japo nilikuwa na michezo ya kitoto lakini jambo zuri na baya nilikuwa ninatambua.. mtu akinigombeza nilikuwa natambua kuwa nimefanya kosa.. hivyo ilikuwa ni rahisi kukaa na mke wa Amiri hadi mume wake alivyorudi jioni..

"Unaitwa nani binti... aliniuliza Dr amiri

Baba yangu anaitwa Husein.. mama yangu Arafa alafu mimi ni Hajraaaa.. Nilimjibu na kucheka..

" safi sana kumbe unaakili mdogoangu... "aliongea amiri na kucheka yeye na mke wake. mimi pia nilianza kucheka sana baada ya kusifiwa huku najipigapiga kifua kumaanisha mimi ndio jemedari nimeweza..

" Lakini kaka.. Monika ni mbaya sana.. Mke wa nic ni mbayaa sana na nic pia ni mbaya sana.. usikubali wawe rafiki zako. wakija hapa wafukuze sawa..??

Sawa.. sintawaruhusu.. kwani walikufanya nini.?? aliuliza amir

" Nimesahau.. kwanza nasikia njaa.. nikila nitakumbuka. mniache nilale kwanza nina usingizi.. au niwekeeni katuni nimewamiss.. au niende chuoni.. ujue mimi ni Mtaalamu wa maabara eti..
Niliongea mambo karibu kumi kwa mara moja hadi mke wa amiri akacheka na kuingia ndani kwake...

"Mke wangu.. nakuomba huyu binti usije kumuacha ukitaka kutoka..

pia mjiandae muda huu tutoke out tukaleni hoteli..

"Amiri alikuwa akijitahidi kunifanyia mambo mengi na michezo mingi ili nisahau yaliyonitokea..

***

Siku zilizidi kwenda.. wiki ilipita na baadae mwezi mzima uliisha na hali yangu ilikiwa sawa kabisa

***

Nilifanyiwa mpango wa kuhamishwa chuo kikuu cha dar es salam kuendelea na masomo yangu kwasababu nilichokuwa nakisomea kilikuwemo kwenye chu kikuu cha dar es salam pia..

sikuwa na changamoto sana nikiwa UDSM kwasababu nilikuwa nikiishi kwa Amiri.. Mke wa amiri alinipenda na kuniheshim sana kwa upole wangu na elimu niliyokuwa nayo kwasababu yeye hakusoma kabisa zaidi ya elimu ya msingi tu.. japokuwa aliolewa na mume msomi mwenye elimu ya juu sana..

Nadhani Amir pia alimpenda sana mke wake kwaajili ya upole alio kuwa nao..

Maisha ya nyumbani kwa Amir yalinivutia sana.. amani ya ile nyumba niliipenda sana hadi namaliza chuo hapakuwahi kutokea mkwaruzano wowote..

Nilipata kazi kwenye hospitali ya binafsi iliyokuwa jirani tu na nyumbani kwa amiri ili angalau nipate fedha kidogo ya vocha...

Niliendea kukaa pale lakini baadae niliamua kupangisha chumba changu binafsi jirani na kwao ili kuwapa nafasi mtu na mke wake wawe huru na kazi za ndani..

niliondoka pale lakini chakula na mengine yote ilikuwa ni nyumbani kwa amiri kwangu nilikuwa nikienda kulala tu

Maisha yangu yalikuwa yaamani japo mda wote mke wa Amiri alikuwa akishinda kwangu na yote ilikuwa ni urafiki wetu.. Amiri pia alifurahia mke wake kuwa na rafiki kama mimi kwasababu alijiridhisha sana na tabia yangu..



Siku moja jioni mimi na mke wa amiri tulitoka na kwenda sokoni kununua vyakula.. Tulinunua vyakutosha na kupanda daladala kurudi nyumbani.. tulifika na kushuka kisha kuanza kuingia chochoro kueleka nyumbani..

Tulifika mahali tumechoka sana.. Tuliona kuna duka dogo chini ya mti umbali fulani kutoka nyumbani..
"Shosti tukakae pale tupate hata peps baridi kupunguza joto.. nilimwambia mke wa amiri..

Tulienda na kukaa kisha kuagiza soda.. muuzaji wa pale alikuwa ni mchaga.." Mimi huwa napenda sana kusikia lafudhi ya kichaga.. kwahiyo nilikuwa nikimuuliza maswali mengi ili niweze tu kumsikia akiongea...

"Mchaga.. ile nyumba pale ndiyo kwako.?? maana nyie wachaga huenda unaduka dogo hapa kumbe mnayo majumba ya gorofa huko kwenu..
niliongea na kucheka kisha kumwangalia mchaga

"weeeehhh dada unaongea nini.. ile nyumba usiitaje tena... Mtaani tunaiita JUMBA la UASHERATI yaani pale ukiingia tu lazima upate hamu ya mapenzi.. hasa kwa msichana..
Mama wa ile nyumba hana mume.. kwahiyo kijana wa getini huwa anafaidi sana.. na sasa anae msichana wa kazi pia huwa anatiwa sana.. hawajui kuna nini ila sisi watu wa njee ndio tunajua mule kuna mapepo ya ngono. msicha wa kazi hadi mimi nimeshamtia.. Wakikaa kidogo tu wanaanza kuwashwa.. kwahiyo msukuma huwa anachoka na kuniita mimi... aliongea mchaga

"Kwani mama wa hiyo nyumba anajishughulisha na nini.?
Nilimuongezea swali lingine..

" weee kazi yake siwezi kusema.. huyu mama ni katili sana.. magari ya kifahari huwa yanaingia humu ndani mida ya saa moja jioni..
Hembu ngoja kwanza.. naona msicha wa kazi wanakuja na msukuma huku.. wasije kusikia tunaongelea nyumba yao...

Tulinyamaza kimya hadi msukuma mlinzi wa getini na msichana wa kazi walivyofika dukani..

"We mchaga lete maji kubwa mbili.. huoni nimekuja na mrembo hapa...
Msukuma aliongea na kucheka..

Lakini wakiwa wanaongea mimi nilikuwa bize kumtazama yule binti alieongozana na msukuma.. nilimwangalia kama namfananisha hivi.. sikukumbuka niliwahi kumuona wapi..
Nilianza kuvuta kumbukumbu nyuma na kubaini ni rafikiangu MONIKA..

Kwa haraka nilishusha Nikabu niliyoivaa na kubakiza macho tu ila uso mzima ulizibwa.. niliendelea kumwangalia yule mwanamke hadi kujiridhisha ni monika kweli..

Niliinuka na kulipia soda upesi kisha kumshika mkono mke wa Amiri ili turudi nyumbani.. nilianza kuhisi kuchanganyikiwa baada ya kumuona Monika

ITAENDELEA...







No comments: